Friday, November 10, 2017

RIWAYA: DAMU YA MWANANGU SEHEMU YA SITA(06) *****ILIPOISHIA****** sauti hiyo aliisikia nyamwela peke yake,,,,akaanza kuingiwa na hofu,,,akageuza singo yake kutazama huku na kule,,lakini hakuweza kumuona mtoto anayetoa sauti hiyo, sauti hiyo ilizidi kuongezeka,,,hatimae ikwa inasikika ndani ya masikio ya Nyamwela! akatimua mbio kurudi nyumbani,,alikimbia mfululizo bila kusimama hatimae akafika nyumbani kwake,,akafungua mlango kwa pupa akaingia ndani!..akapitiliza mpaka chumbani,,,,akakuta mkewe kalala huku anatokwa na damu nyingi shingoni! akamuita huku akimtikisa,,,ghafla akabadilika,,,akaonekana mtoto aliyekatwa kichwa na mikono! Nyamwela akapiga kelele ghafla mtoto huyo akatoweka!!! mke wa Nyamwela akashtushwa na kelele hizo,,akafumbua macho!! TAHARUKI!!!!!! ****ENDELEA**** akastaajabu,,kumuona Nyamwela,,akiukaribia mlango kwa Lengo la kutoka nje ya chumba hicho!! akauliza kwa mshangao!! unamaaniwha nini kupiga mayowe kwa sauti kali kiasi hicho? Nyamwela akabaki kimya huku macho yamemtoka!,, mwili wake uliomekana kutetemeka kwa hofu aliyokuwanayo! kitendo hicho kilimshangaza sana mkewe,,akauliza kwa mara nyingine tena,,"mbona unaonekana kuwa na wasiwasi!? bado Nyamwela hakujibu,,akabaki kimya,, ghafla akahisi harufu ya damu macho yakamtoka! Upande mwingine,,kule kwenye milima ya Nzoka alionekana yule mganga,,akiwa katika ngome yake yake,,akiendelea kutengeneza dawa zake za knowchawi,,kwa ajili ya wateja wake! ghafla akahisi hali tofauti na siku zote!!! akatoka nje ya pango,, akaangaza angaza macho yake huku na kule lakini hakuona kitu chochote!! akazipiga hatua kurudi ndani ya lango,,,ghafla akaona matone ya damu,,yakiwa chini,, akashtuka! punde si punde ikasikika sauti ya mtoto mchanga analia mule ndani ya pango! Mganga akaingiwa na hofu! wakati anatahamaki! akahisi kuishiwa nguvu,,,ghafla kikajitokeza kiwiliwili cha yule.mtoto mchanga! Macho yakamtoka mganga! alipojaribu kutoweka kimiujiza ikashindikana! punde si punde,, akaanza kuhisi harufu kali ya damu mbichi ikinuka kwenye pua zake! baada ya sekunde kadhaa kupita,, kile kiwiliwili cha mtoto huyo kikatoweka kimiujiza! wakati kiwiliwili hicho kinatoweka,, mganga akafa papohapo! ghafla moto mkubwa wa kimiujiza ukazuka na kuchoma ngome hiyo ya mganga... Upande mwingine kule nyumbani kwa Nyamwela pakawa hapakaliki,,aliiona nyumba chungu zaidi ya shubiri! Nyamwela akaonekana akitoka nje ya nyumba,, akizipiga hatua za harakaharaka! Mkewe akashtushwa na jambo hilo! akaamua kumfuata Nyamwela kwa nyuma,,,alipotoka nje ya nyumba akamuona Nyamwela anatimua mbio! hatimae akatokomea kusikojulikana. Baada ya masaa kadhaa kupita,,akaonekana Nyamwela akiwa kaketi chini ya mti,,,akitafakari nini cha kufanya,,akajisemea moyoni,,"mbona mambo yameanza kuwa magumu! najuta kwa unyama nilioufanya! Nyamwela akanyanyuka na kurudi nyumbani ...alipofika akakuta mlango upo wazi,,,akaingia ndani! akastaajabu kuona nguo zimevurugika,,nyingine zimetupwa chini,,,alipoangaza macho yake akaona ujumbe umeandikwa kwenye karatasi! akauwoma ujumbe huo,,,ulikuwa umeandikwa hivi: nimeshindwa kuendelea kuishi katika nyumba hii,,,inamambo ya kimiujiza,,,leo nimeona kaburi Kimjitokeza ndani,,,alafu likatoweka!! nimeamua kurudi nyumbani kwetu! Nyamwela akazidi kuchanganyikiwa,,,macho yakamtoka! punde si punde ikasikika sauti ya mtoto nchanga akilia nje ya nyumba! Nyamwela akaingiwa na hofu,,akazipiga hatua za kunyatia akachungulia dirishani! akastaajabu kuona kaburi pale mbele ya nyumba! wakati anatahamaki! wakaonekana watoto wachanga wengi,,wanafanana,,,wakiwa wamelala kwenye sakafu,,watoto hao wakaanza kulia kwa sauti kali mfululizo,,Nyamwela akatimua mbio kutoka dani ya nyumba,,,alipofungua mlango akastuka kuona lile kaburi alilomzika mwanae aliyemchinja na kumkata viungo pamoja na mkewe Muna,likiwa nje ya mlango! ghafla kaburi hilo likatoweka kimiujiza! wakati anatahamaki,,akaona mwanamke akiwa kajifunika nguo nyeupe akikatiza kuelekea nyuma ya nyumba! Nyamwela akatimua mbio akachungulia nyuma ya nyumba hakumuona tena yule mwanamke! akaamua kuzipiga hatua za kunyatia kurudi upande wa mbele ya nyumba,,,akastaajabu kumuona mwanamke huyo akiishilizia kuingia ndani ya nyumba huku akiwa kambebq mtoto mchanga anavuja damu! Nyamwela akatimua mbio huku akigeuzageuza shingo yake nyuma! alikimbia umbia umbali mrefu,, akahisi kuchoka! akaamua kusimama..... wakati huo ilikuwa ni nyakati za usiku....punde si punde akaonekana yule mwanamke akipita kwa mbali...Nyamwela kaanza kutimua mbio,,ghafla lile kaburi likajitokeza mbele yake! akasita kuendelea kukimbia,,, wakati anatahamaki! ghafla akavutwa na kutumbukia ndani ya kaburi hilo kisha likajifunga! ITAENDELEA..........

No comments:

Post a Comment