Friday, November 10, 2017

RIWAYA: DAMU YA MWANANGU SEHEMU YA PILI(02) *****ILIPOISHIA****** dirisha linazidi kukatwa akaingiwa na hofu.. akamchukua mwanae akambeba mgongoni..kisha akazipiga hatua za kunyatia akafungua mlango na kutoka nje ya nyumba akatimua mbio.......... wakati Muna anafungua mlango,,,aliurudishia kwa kuusukuma kwangu ukatoa sauti,,, Nyamwela akasikia ,,,akatimua mbio kuwahi mlangoni,,lakini akawa ameshachelewa,, tayari Muna alikuwa ameshatoka nje na anaendelea kutimua mbio.... Nyamwela akasikia vishindo vya mtu anakimbia akagundua kuwa ni Muna,,, Nyamwela kaanza kutimua mbio huku kanyanyua upanga,, kuelekea ule upande aliokimbilia muna!!! TAFLANI!!!! *****ENDELEA****** Muna aliendelea kukimbia akiwa akambebe mwanae mgongoni,, Nyamwela hakufanikiwa kumuona Muna! akaendelea kufanya jitiada za kumtafuta lakini pia hakuweza kumuona,,,kutokana na giza totoro lililokuwa limetanda,,,Muna hakuweza kuonekana kiurahisi,, baada ya masaa kadhaa kupita ,,,Muna akashindwa kuvumilia baridi kalili lililosababishwa na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi. akaamua kuzipiga hatua kurudi nyumbani,,lakini alikuwa kasahau kilichotokea masaa machache yaliyopita,, alipofika nyumbani kwake akaingia na kufunga mlango,,,akamlaza mwanae kitandani kisha naye akajilaza kando yake. ************************** asubuhi palipokucha Muna alidamka mapema,,,akazipiga hatua kuelekea shambani kutafuta chocho angalau apate mlo wa asubuhi....akamuacha mwanae akiwa chumbani,,, hakuwa na wasiwasi kwa sababu shamba halikuwa mbali kutoka usawa wa nyumba yake...akaangazaangaza macho yake huku na kule,,,akafanikiwa kuona uyoga uliokuwa umeota kandokando ya miti ya matunda. akachuma uyoga huo kisha akazipiga hatua kurudi nyumbani,,akakumbuka kuwa hakuna kuni za kupikia,,,akaamua kwenda kutafuta kuni kavu huko porini,,,ghafla akasita kuondoka,,,akaingia ndani ya nyumba akamchukua mwanae ambaye bado alikuwa kalala usingizi,,,akambeba mgongoni akaondoka zake! Upande mwingine alionekana Nyamwela,,akiwa nyumbani kwake,,,uso wake ulionyesha kutokuwa na furaha,,,kwa sababu kila kona anayopita watu wanaomfahamu wanamnyooshea vidole,,wakimsema kuwa ametelekeza familia yake kule kijiji cha tatu,,,mke pamoja na mtoto. siku zilizidi kusonga lakini Nyamwela bado alikuwa na mpango wa kumuua mkewe,,,kwa sababu ni kichaa,,hivyo hakutaka kuendelea kuishinae...kutokana na maneno ya watu kumsema,,akaona ni vyema aiangamize familia yake pamoja na mtoto mchanga,,ili yeye aanze kuishi maisha mapya,, punde si punde mlango ukagongwa,,,Nyamwela akauliza kwa sauti kali,,,wewe nani? ikasikika sauti ikitokea nje ya nyumba ikisema,,mimi rafiki yako Mabula, Nyamwela akanyanyuka na kufungua mlango akamkaribisha ndani. Rube akasema,,nimekuja hapa ninahitaji unisaidie baiskeli yako,,ninasafari kuelekea milima ya NZOKA,, Nyamwela akashtuka,,akauliza kwa mshangao,,unaenda kufanya nini huko? mbona hakuna makazi ya watu maeneo hayo? Rube akasema ,,"nakwenda kwa mganga kutafuta utajiri,nimechoka kuishi maisha haya ya umaskini,,nitazeeka hata sijanunua baskeli,,, Nyamwela akaanza kudadisi kiundani zaidi,,,lakini Rude akasema,,"mengi siyajui kuhusu upatikanaji wa utajiri,,lakini kuna mtu amenielekeza kwa mganga anayetoa utajiri, ndio sababu nimekuja hapa kwako uniazime baiskeli,,ilimradi safari yangu ya kwenda huko iwe rahisi. Nyamwela akajikuta naye anatamani kupata utajiri! akasema,,"hata mimi pia nahitaji,,hivyo ni vyema twende wote. bila kuchelewa safari ya kwenda kwa nganga ikaanza wakaelekea milima ya Nzoka... wakapakizana kwenye baiskeli,,kwa kupokezana kuendesha.. baada ya lisaa limoja wakawa wamefika kwa mganga,,,wakaelezea sida yao,,,bila kuchelewa mganga akanza kupiga tunguli zake,,,,akaanza na Rube,,,akampa masharti magumu ambayo yalimfanya Rube akate tamaa yakuutaka utajiri,,,,aliambiwa atoekafara la wazazi wake wote wawili,,ndipo apate utajiri..ikishindikana basi alete mchanga wa unyayo wa mguu wa mtu yeyote ampendae..kwa upendo ulioshibana. Rube akamwambia mganga kuwa ampe muda akajifikirie kisha atarudi tena,,baada ya kutafakari na kupata maamuzi sahihi. mganga hakuwa na kipingamizi kwa sababu sio lazima ni hiyari. baada ya kumalizana na Rube,,akaendelea na Nyamwela,,,, mganga akasema,,wewe ukitaka kuupata utajiri ni lazima utoe kafara la damu ya mwanao kwa kukata shingo yake pamoja na mikono na miguu yote kisha vilete hapa usiku wa manane ,,hakikisha siku hiyo ni usiku wa kuamkia siku ya jumatano,,,, Nyamwela hakusita akakubali haraka! kitendo hicho kilimshangaza sana Rube,,kwa nini Nyamwela yupo tayari kumtoa kafara mwanae,,hata bila kipingamizi! akamtazama Nyamwela kwa macho ya mshangao,,kisha akajisemea moyoni,,"mganga kasema ikishindikana kutoa kafara wazazi wangu wote wawili,,,basi nilete mchanga wa unyayo wa mtu yeyote nimpendae....wacha nifanye jambo,,ni bora nimtoe mtu asiyekuwa na faida yoyote hapa duniani,,,tena huyuhuyu Nyamwela. mganga akawaruhusu waende,, safari ya kurudi nyumbani ikaanza. ****************************** asubuhi palipokucha Rube akadamka mapema akaelekea kule kijiji cha tatu,,,ni kile kijiji alichokuwa anaishi mwanzo Nyamwela na familia yake,, Rube alnakwenda huko,,kutazama maendeleo ya shamba lake,,,ikamlazimu kuba huko kwa masaa mengi kiasi,,,aking'oa majani yaliyokuwa yamezunguka mazao yake. baada ya masaa matatu kupita akaonekana Nyamwela akiwa,,nyumbani kwake akijiandaa kuelekea kijiji cha tatu ,,kukamilisha masharti ya mganga,,,akachukua upanga na kuuweka vyema ndani ya suruali aliyokuwa kaivaa! ilipofika nyakati saa kumi za jioni,,Nyamwela akawa amefika kijijini hapo,, wakati huo,Muna alikuwa shambani akitafuta mlo wa usiku,mtoto wa Muna alikuwa chumbani kalala usingizi. Nyamwela akazipiga hatua kuifuata nyumba.. kwa mbali akaonekana Rube naye akizipiga hatua kuja nyumbani kwa Muna,,aliona si vyema kuondoka pasipo kumjulia hali mke wa rafiki yake, ghafla akashtuka kumuona Nyamwela anazipiga hatua za kunyemelea kuifuata nyumba ya Muna....akajisemea moyoni,,"huu ndio wakati muafaka wa kuchukua mchanga wa unyayo wa Nyamwela.... Rube akazipiga hatua akaanza kuchota mchanga wa unyayo wa Nyamwela,, wakati huo Nyamwela alikuwa ameukaribia mlango wa kuingia ndani ya nyumba ya Muna,akaangaza angaza macho yake huku na kule,,ili ahaqkikishe hakuna mtu anayeshuhudia au kumuona anaingia ndani ya nyumba hiyo,,, wakati anaangaza angaza macho yake,,akashtuka kumuona Rube akiwa anachota mchanga na kuuweka katika mfuko wa plastiki! Nyamwela akakumbuka kuwa mganga alimwambia Rube kuwa akishindwa kuwatoa wazazi wake kafara basi alete mchanga wa mtu yeypte ampendaye,,kwa upendo ulioshibana! Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa akapaza sauti,,"Rube unafanya nini hapo? Rube akaufunga vyema mfuko uliokuwa na mchanga wa unyayo wa Nyamwela,,akaanza kutimua mbio,,, Nyamwela akaacha kuingia ndani ya nyumba ya Muna akaanza kumkimbiza Rube! ITAENDELEA..........

No comments:

Post a Comment