Friday, November 10, 2017

RIWAYA: DAMU YA MWANANGU SEHEMU YA KUMI(10) *****ILIPOISHIA****** kwa mbali akamuona rafiki yake kipenzi ni yule Matiku...akaamua kuliweka begi lake lililokuwa na zile pesa zote pamoja na nguo zake....akazipiga hatua kutoka ndani ya gari. kumfuata Matiku,,angalau ampe taarifa kuwa ameamua kuhama na kwenda kuanzisha maisha mapya jijini Dar es salaam. Nyamwela akaamua kutimua mbio amuwahi Matiku kabla hajafika mbali! akaamua kupaza sauti kumuita Matiku! Matiku akaitambua sauti ya Nyamwela akageuza shingo yake na kusimama... Nyamwela alipomkaribia Matiku,,,akasikia mngurumo wa gari likiondoka,,,alipogeuza shingo yake kutaza kule lilipokuwepo basi....akashtuka kuona basi hilo likitokomea kwenye barabara ya kuelekea Dar es salaam! Macho yakamtoka! *****ENDELEA***** akatafakari nini cha kufanya,,wazo likamjia, akatimua mbio na kumuacha Matiku akiwa kasimama pale. Nyamwela akakimbia moja kwa moja mpaka kwenye eneo maalumu la kuegesha taxi,,akakodi taxi kisha akamsisitiza dereva aendeshe gari haraka kulifuata basi lililoondoka muda mchache uliopita...dereva huyo akafuata agizo la mteja wake.... kiukweli basi lile lilikwenda kwa mwendo wa kasi...hawakuweza kuliona kwa sababu lilikuwa umbali wa kilomita kadhaa. Dereva akaamua kuuliza,,"kunatatizo gani,,mbona unasisitiza niongeze mwendo hii ni hatari kwa usalama wa maisha yetu.. Nyamwela akadakia na kusema,,"ni bora kufa kuliko nipoteze pesa zangu... Dereva huyo akashtuka akauliza kwa mshangao!! ,,"pesa? kwani ni kiasi gani cha pesa ulichokiacha ndani ya basi hilo? ambacho kinasababisha uhatariwhe uhai wako! Nyamwela akasema,,"ni bora hata zingekuwa milioni tano tatizo ni zaidi ya hizo! Dereva akamtazama Nyamwela kwa macho yq mshangao! kisha akauliza,,"ulikuwa umeketi kwenye kiti namba ngapi? Nyamwela.akatoa tiketi haraka mfukoni mwake..kisha akaitazama,,akasema,,"kiti namba 22.... dereva akaendelea kuuliza maswali,,"uliziweka kwenye nini? Nyamwela akajibu haraka kwenye begi langu jeusi...mbaya zaidi begi hilo nililiweka juu ya kiti hicho! ghafla wazo likamjia dereva huyo,,akajisemea moyoni,"ukisikia zali la mentali ndio hili,,,wacha nifanye jambo. akapunguza mwendo wa gari kisha akalisimamisha,,na kuliegesha kando ya barabara,,akashuka kutoka ndani ya gari! Nyamwela akahisi huenda dereva huyo anakwenda kujisaidia haja ndogo,,, lakini akastaajabu kumuona anaelekea upande wa mbele ya gari,,,punde si punde akafungua boneti ya gari hilo! akarudi ndani ya gari na kusema,,"gari limepata hitirafu..linahitaji matengenezo hivyo safari yetu imeishia hapa! Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa! akasema,,"sasa ndugu,,hapa nilipo sina hata shilingi...nilikuwa nategemea tukilipata basi hilo,,nichukue pesa zangu,,ili niweze kukulioa pesa zako... dereva huyo,,akajisemea moyoni,,"yani ungejua hata sina shida na nauli yako,,mimi nahitaji hizo milioni milioni... alijisemea maneno hayo huku akishuka kutoka ndani ya gari,,, Nyamwela akabaki akimtazama dereva huyo,,,ghafla wazo likamjia,,akajisemea moyoni,,"wacha nifungue mlango nitimue mbio,,naimani hatoweza kunikimbiza.....Nyamwela aliwaza hivyo..huku akiendelea kumtazama dereva huyo,,aliyekuwa upande wa nje ya gari. dereva huyo akajifanya anakwenda kujisaidia haja kubwa,,akazipiga hatua kukifuata kichaka kilichokuwa ndani ya pori dogo uoande wa pili wa barabara... akaingia ndani ya kichaka hicho! Nyamwela akaona huo mdio muda muafaka wa kutimua mbio...akafungua mlango taratibu akatimua mbio na kutokomea porini akajificha nyumba ya mti mkubwa,,akawa anachungulia kule barabarani,,akamuona ye dereva anatokea kichakani na kuingia ndani ya gari,,,,akaliwasha gari hilo akaliondosha kwa mwendo wa kasi! Nyamwela akaonekana akitimua mbio kutokea porini kuja upande wa barabara..alikimbia huki akipiga mayowe,,kuashilia dereva asimamishe gari hilo...lakini akastaajabu kuona dereva huyo anaendelea na safari,,badala ya kurudi alipotoka! Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa...akabaki kasimama katikati ya barabara huku kajishika kichwani! akaamua kuketi chini ya mti uliokuwepo kando ya barabara! akisubiri msaada wa lifti kwenye gari lolote litakalokatiza katika barabara hiyo. ITAENDELEA..........

No comments:

Post a Comment