Friday, November 10, 2017

OFA OFA OFA. SIMULIZI: JINA LA URITHI SEHEMU YA KUMI NA MBILI(12) ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪ yule mtu akasema,,"mimi ninanguvu za kimiujiza,,na haya niliyaona kabla hayajatokea! nani kati yenu anamkumbuka mwanamke NJILE? wanakijiji wakashtuka! ghafla ikasikika sauti kutoka katikati ya mkusanyiko wa wanakijiji hao ikisema,,"mwanamke yule alizaa mtoto wa ajabu! bila shaka alikuwa ni mchawi,,na tulimfukuza katika kijiji hiki! kabla hajamaliza kuongea sentensi yake...ukasikika mvumo wa upepo uliovuma kwa kasi ya ajabu...upepo huo ulitoa mlio wa kutisha ukitamka maneno haya,,"MIMI NDIYE......... ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪ ghafla sauti hiyo ikanyamaza kwa muda, na ukimya ukatawala!baada ya sekunde kadhaa sauti hiyo iliendelea kusema,,"hakuna atakayeweza kunizuia ,,nitarudi tena siku chache zijazo...ghafla sauti hiyo haikusikika tena na ukimya ukatawala...macho yakawatoka wana kijiji,,kwa sababu aliyekuwa akiongea maneno yale,,hakuonekana kwa macho ya kawaida, wakati huo yule mtu mwenye nguvu za kimiujiza alikuwa tayari ameshagundua kuwa si mwingine bali ni mzimu wa muanzilishi wa ukoo wa Laula,,,mbaya zaidi tayari mzimu huo umeshaingia ndani ya mwili wa Laula...hivyo ni hatari kubwa itatokea ndani ya kijiji hicho. wanakiji waliendelea kuwa na hofu kubwa,,kila mmoja alitamani kutimua mbio,,,,yule mtu mwenye nguvu za kimiujiza aitwae JOGOLO akasema,,"tatizo limeshakuwa kubwa kuliko nilivyotegemea,mambo haya yanasababishwa na mzimu wa Laula,,alifariki takribani miaka mia iliyopita,,tatizo ni jina,,na jina hilo alipewa mmoja kati ya watu wa ukoo wake,,,ni mtoto mdogo wa umri wa miaka kumi sasa naye anaitwa Laula, baaada ya kuongea maneno hayo,,wanakijiji wakashtuka! wakasema maneno yako yanaelekea kuna ukweli ndani yake kwa sababu,ni kweli,,mtoto wa Njile anaitwa Laula na inasadikika mtoto huyo anazo nguvu za kimiujiza... ikasikika sauti ya mwanamke akiongezea kwa kusema,,"tunaomba utusaidie tafadhali tutakupa chochote utakacho. Jogolo akatafakari kwa sekunde kadhaa kisha akasema,,"yahitaji moyo wa ujasiri kuna jambo gumu ndani yake ili kuondoa tatizo hili.. wanakijiji wakatazamana kwa macho ya taharuki.. ghafla akaonekana Jogolo akitazama huku na kule akamuita mmoja kati ya wanakijiji aje pale alipokuwa amesimama yeye...Jogolo akatoa kipande cha nguo nyeusi,,kitambaa hicho kilikuwa kimefungwa mizizi ya mti,,kisha akasema,,"umu ndani ya kitambaa hiki kuna mizizi ya mti maalumu,,,mti huo unaitwa Mfungilwa...mizizi yake huchimbwa usiku wa manane,,na mchimbaji hufanya hivyo akiwa uchi wa mnyama, ni dawa nzuri sana ya kunasa mizimu,,jinamizi na majini,pamoja na viumbe wasio onekana....unapomaliza kuchimba mizizi ya mti huo,,sharti uifunge ndani ya kitambaa cheusi...na siku ya kukifungua kitambaa hicho,,ni lazima binadamu afe ili dawa iweze kufanya kazi,,aliongew maneno hayo akiwa tayari kamkabidhi yule mwanakijiji ile dawa ya kichawi iliyofungwa ndani ya kitambaa cheusi! wanakijiji wakaingiwa na hofu,,ghafla ikasikika sauti ya mwanakijiji mmoja akisema,,"mbona dawa hiyo inamsharti magumu kiasi hicho! kwani hakuna dawa nyingine tofauti na hiyo? Jogolo akasema,,"hakuna namna nyingine,,,na dawa hiyo siruhusiwi kuigusa tena kwa sababu nimeshaitoa mikononi mwangu! mtu huyu niliyemkabidhi,ndiye mwenye jukumu la kuchagua ni nani afe ili kijiji kikombolewe katika janga hili...ukishamchagua mwanakijiji mmoja,,,simama mbele yake..vuo nguo zako zote..kisha fungua kitambaa hicho na ummwagie mtu huyo dawa hiyo. baada ya Jogolo kuongea maneno hayo,wanakijiji wakaanza kurudi nyuma wakisukumana,,kila mmoja aliogopa kufa kwa ajili ya kumkomboa mtu mwingine! hata yule mwanakijiji aliyekabidhiwa dawa hiyo akaanza kuingiwa na hofu,,akajuta kwa nini alikubali kuipokea dawa hiyo kabla hajajua masharti yake!! jasho likaanza kumtoka mfululizo...mwili wake ukitetemeka kwa uwoga! Jogolo akasema,,"usiogope na huu ndio muda muafaka wa kukamilisha jambo hili,, dawa ianze kufanya kazi,,pasipo kufanya hivyo hakuna mwanakijiji atakayebaki hai,,mzimu wa Laula utawamaliza bila huruma! haya endelea kushikilia kitambaa hicho pasipo kukiachilia,,,kaza mikono yako kisha piga hatua kumfuata mtu mmoja yeyote kati ya watu waliokusanyika hapa,, na yeyote utakayemchagua basi atakufa papohapo na dawa itaanza kufanya kazi! wanakiji wakaogopa! ni baada ya kusikia maneno hayo...lakini cha kushangaza,,miguu yao ilikuwa mizito kama wamewekewa gundi,,hakuna aliyeweza kunyanyua mguu kuoneoka eneo hilo! yule mwanakijiji aliyekabidhiwa dawa,,akazipiga hatua huku akiangaza angaza macho yake kumchagua mwanakijiji mmoja! mkusanyiko wa wanakijiji ulikuwa mkubwa,,,kiasi kwamba Jogolo alikuwa amezungukwa na umati huo,, yule mwanakijiji akasita! kuendelea kutembea,,akageuka na kurudi ule upande aliokuwepo mwanzo,,Jogolo hakuwa na wasiwasi,,aliamini huenda ameamua kumchagua mtu kati ya waliokuwa amesimama nyuma ya Jogolo.... lakini mwanakijiji huyo aka,ipiga hatua n akusimama mbele ya jogolo,,akaanza kuvua nguo na kuifungua dawa hiyo....macho yakamtoka Jogolo!! KIZAA ZAA!!!!!!! ITAENDELEA..... 🌸mwendelezo utalipia 1000 Upate hadi mwisho asanten🌸

No comments:

Post a Comment