Story: Sitaki tena – 07
Ilipoishia..
"Ni..mi..mi.. Ndo
nimemu..uaaaaaaa Peeeeeendo...
Endelea...
Nilijikuta nimeropoka kila kitu
huku kwa ghafla yule mzee
akamuwahi kumshika mke wake
kisha akanigeukia na kuniuliza
tena.,
"Binti ulikuwa unasema?...
Samahani sana sijakusikia vizuri
nilikuwa namuwekea karibu na
mdomo mama yako mfuko aweze
kutapika..."
Aliongea yule mzee bila ya
kuonyesha wasi wasi wowote
kama kuna neno baya ambalo
Levina mimi nimeropoka,
"Nilitaka kukupa mfuko huu hapa
mkubwa nimeona huo mdogo
hautatosha kwa maana mama
anatapika sana.."
Nilimjibu kwa kuzuga huku
macho nimeyaelekezea chini kwa
aibu kubwa niliokuwa nayo pale,
nikajifanya kihere here kwa
kumpa maji yakunywa yule mama
aliyekuwa anatapika ambaye ni
mama yake na Pendo,
Mzee alinishukuru sana kwa
wema wangu japokuwa ukweli
nilibaki nao moyoni,
"Umesema binti unaelekea wapi?"
Aliniuliza yule mzee na kwa mda
ule tulikuwa tukiendelea kupiga
story za kawaida kuhusiana na
maisha njia nzima japo ukweli
kuhusu pendo nilikuwa nao
moyoni.,
"Naelekea Dar es salaam kutafuta
kazi"
"Kazi gani binti yangu?"
"Naenda kutafuta kazi za ndani"
Nilimdanganya sana kuhusu
maisha yangu kwa ujumla na
aliweza kuniamini kwa asilimia
kubwa kuwa natokea Iringa
naelekea Dar kutafuta kazi za
ndani,
Ile roho ya kikatili,ilikuwa
imeshaanza kunikabili kwani
sikuwa hata na huruma ya aina
yoyote..huku tukiwa tumeshasafiri
mwendo wa kama masaa manne
hivyo nikamwambia mzee kwakua
gari ilikuwa inapitia Morogoro
halafu ndo inaenda Dodoma
ilinibidi nimwambie mzee kuwa
tukifika morogoro anishtue kwa
sababu nimeshapasahau
sitapakumbuka vizuri..
* * * *
Ndani ya masaa kama sita huku
kausingizi kakinipitia mzee
alinishtua na kuniambia kuwa
tulikuwa tayari tupo maeneo ya
mzumbe tukikaribia kuingia
morogoro,hivyo niwe tayari
nisilale tena, nilianza kujawa na
furaha isiyotabirika huku furaha
yangu zaidi nikiielekeza katika
mifuko ya ile traki suti niliyokuwa
nimeivaa na kuchomoa zile
karatasi za ramani kisha
nikazing'ang'ania mikononi
mwangu nikisubiri niingie
Morogoro..
***
Hatimaye tukaingia ndani ya
mkoa wa Morogoro,kisha
nikamuaga mzee pale lakini
nilishindwa kumuaga mama
kwakua tayari alikuwa
ameshapitiwa na usingizi.,
"Usijali binti utafanikiwa nakutakia
maisha mema na ubarikiwe upate
kazi na uishi kwa amani huko
uendako.."
Yale maneno hayakuniingia akilini
hata kidogo kwani hayakuwa na
ukweli wa aina yoyote pale ila
nikaamua nimuitikie tu kwa
kumridhisha yule mzee.,
"Ahsante sana mzee na poleni
sana kwa msiba uliowakuta"
Nilimwambia huku nikionesha
tabasamu la huruma la uongo,
nikampa mkono kisha nikamuaga
kuelekea stendi ya upande wa pili
huku yule mzee akiamini kabisa
kuwa nlikuwa naelekea dar
kumbe naweka kwanza kituo..
***
Mda ulikuwa umeshatimia kama
saa nane mchana huku kukiwa na
hali ya uvugu vugu iliyojawa na
baridi lakini siyo kali sana kama la
Iringa kwani manyunyu yalikuwa
yakidondoka taaratibu kuashiria
mvua inataka kunyesha,huku
nikiwa nimejikunyata mikono
yangu niking'ang'ania zile ramani
ndani ya mifuko ya
suruali,niliweza kutoa na
kufungua mojawapo ya ramani
iliyokuwa inaelekeza kwa 'Baba
Ali' huku nikiiongoza
inavyoelekeza..
"Sasa, hapa ndo nimeambiwa
panaitwa 'Boma Road' na ramani
inaelekeza kota hizi hizi... embu
ngoja nimuulizie huyu mtu.."
"Samahani kaka..Sijui
unamfahamu 'Baba Ali'..?"
Nilimuuliza mpita njia niliyeamini
kuwa atanisaidia kumpata mtu
ninayemhtaji.,
"Baba Ali..Baba Ali.. Yeeah,
nimemkumbuka anaishi maeneo
ya paleee juu tena mnene hivii
alikuwa anaishi na mke wake na
watoto lakini sasa hivi anaishi
peke yake?.."
"Ndo huyo huyo..",nilimuitikia tu
huku nikiamini atakuwa ndo huyo
huyo kutokana na maelezo
aliyonipa Gervas.,
"Nyosha na hii barabara ukifika
pale njia panda anza kuhesabu
nyumba ya kwanza mpaka ya tatu
ndo hapo hapo"
"Ok., asante sana.."
Furaha ilinizidia zaidi ya pale
nilipokua naelekezwa sikutaka
hata kugeuka nyuma akili yangu
ikaelekea mpaka kwenye njia
panda na nilipofika kwenye lile
eneo nikaanza kuhesabu nyumba
ya kwanza mpaka ya tatu,
nikaingia ilikuwa ni nyumba
kubwa iliyojaa wapangaji
mbalimbali nilipofika
nikapokelewa na majirani na
kuwaulizia 'Baba Ali' kisha
wakaninyoshea chumba
anachoishi na kuanza kugonga
hodi.,
"Karibu karibu.."
ilisikika sauti yakiume niliyoamini
ndo mwenyewe 'Baba Ali..'
"Wewe ndo baba Ali?"
"Ndo mimi karibu binti"
Niliingia ndani kwake japo alikuwa
na chumba na sebule,ni kweli
sikuona dalili yoyote ya mke wala
watoto ,niliweza kumwelezea
matatizo yangu yote kisa cha mimi
kupelekwa gerezani na wema
wote alionitendea mdogo wake
ambaye ni Gervas,misukosuko
yote hadi nilivyokwenda kwa
Gervas akanipa ramani mpaka
nimefika hapa, aliitikia kuwa
ilikuwa ni kweli alikuwa
akimfahamu Gervas kama ndugu
na alikuwa akiishi na mkewe na
watoto lakini wameshaachana na
kuhusu kuelekea nyumbani kwetu
nisijali kesho yake atanipeleka
mpaka mlangoni kwetu, hivyo
akanizidishia furaha na msisimko
ndani ya mwili wangu zile ramani
zikawa hazina tena maana
kwangu nikampa akazichukuwa
na kuzichanachana kisha akaenda
kuzitupa nje.
Ilikuwa imeshatimia saa tatu za
usiku hivyo akaniandalia maji ya
kuoga nikaenda kuoga niliporudi
nikakuta kashanunua chakula
(chipsi mayai) hivyo tukakaa
mezani na kula,baada ya hapo
akanielekeza chumba
nitakacholala kisha taa zikazimwa
nikamwacha akijilaza kwenye
kochi pale sebuleni..
Ikiwa ni usiku wa manane huku
nikiwa nimejifunika shuka sio zito
sana huku nikiwa nimejikunja kwa
kaubaridi kalichokuwa
kakininyemelea nilianza kuhisi
kama kuna mtu anahema
mgongoni mwangu tena kwa
pumzi ya hali ya juu,nilipaamini
sana pale na pia
nilivyomuheshimu 'Baba Ali'
sikufikiria hata kidogo kama
anaweza kunifanya chochote,
kadri mda ulivyokuwa unaenda
ndivyo nilihisi kama mikono
inapenya katika makwapa yangu
kisha inashika na kutekenya matiti
yangu huku ikiteleza kwa
kunipapasa pasasa ikihamia
taratibu katika sehemu zangu za
siri na kuanza kuzitekenya,
nilishtuka lakini kwa ujasiri
niliokuwa nao sikutaka kupiga
kelele kwanza mpaka nimjue ni
nani anayenifanyia vile, sasa
nikawa napapaswa maeneo ya
mapajani kwangu huku yule mtu
akigeukia upande wa mbele
yangu..
"Kohh..! kohh..! kohh..!"
Nikakohoa kwa nguvu japo yule
mtu ashtuke lakini hakutaka
kuniachia,
"Wewe nani? Naomba uniache..!"
Niliamua kutoa sauti ya juu
kidogo huku nikiwa na hasira kali
na mishipa iliyonitanda
usoni,lakini haikusaidia kwani
kilichofuata nilihisi kama panga au
kisu kikiumana na sakafu kisha
haraka taa ikawashwa..
"Heee Baba Ali..?"
Sikutaka kuamini hata kidogo
kwani ni kweli alikuwa 'Baba Ali'
juu ya kifua changu,
aliyejitambulisha na kunipa hifadhi
hapa kwake ndo alikuwa akitaka
kunibaka..
"Shhh.. Nani Baba Ali..?
Tena ukome siku nyingine kuniita
hivyo,Gervas mie simjui na huyo
'Baba Ali' unayedhania ni mimi
siyo na huko kwenu sikujui
malaya mkubwa we..!"
Yale maneno yalinichoma sana
sikuwa na jinsi kwakuwa alinishikia
panga na kunilazimisha kufanya
atakavyo hivyo akaniingilia
kinyume na maumbile usiku
kuchwa huku akinisababishia
maumivu makali na damu nyingi
kunitoka mwilini mwangu..
Sikuweza kupata usingizi hata
baada
ya kunifanya atakavyo na
kuniacha
pale usiku ule
Kitandani nikiwa sijiwezi,
nilimshuhudia
akichukuwa suruali yake na kutoa
noti
ya shilingi elfu moja na kunipatia..
"We malaya, chukuwa hii
itakusaidia
japo ukapate chai"
Nilijikuta napandwa na hasira
kali,huku
nikihema haraka haraka pale bila
hata
kuongea chochote nikachukua ti
sheti yangu na ile traki suti
nyeupe aliyoniachia Gervas kisha
nikamgeukia
na kumwambia..
"Ahsante sana kwa wema wako
ulionitendea"
Kisha nikatoka nje,kupitia kwenye
kakorido ambapo pembeni
kulikuwa na beseni la vyombo
vichafu vya
majirani kwa bahati nzuri nikaona
kisu
katika vile vyombo hivyo
halmashauri
ya kichwa changu ikafanya kazi
fasta,
nikakichukuwa na kurudi ndani
kwa
kasi ya ajabu na kumkuta 'Baba
Ali' akiwa kainama chini uku
akifunga
kamba za viatu,nikamuwahi kabla
hajageuka na kuinuka na
kumchoma
kisu cha mgongoni kisha
nikakichomoa haraka na
kumuwahi
tena kabla hajapiga kelele na
kumchoma tena maeneo ya
shingoni
kisha nikachukuwa kitambaa na
kumjaza mdomoni ,hivyo
nikamshuhudia 'Baba Ali' akigala
gala
pale chini huku akitoa macho na
mishipa ya shingoni ikimlegea.
Zoezi lililofuata ni kuingia mpaka
chumbani kwake na kutafuta hela
zilipo, nilitumia kama dakika tano
bila
ya mafanikio huku nikishuhudia
kuona
madawa ya kulevya pamoja na
vitambulisho mbalimbali vya watu
tofauti feki hivyo nikagundua
kuwa
'Baba Ali' alikuwa ni jambazi tena
sugu
lililoshindikana tena lilikuwa
likitafutwa, baada ya kutafuta
hela bila
ya mafanikio hatimaye nikazipata
pesa
nyingi sana kwenye kisanduku
alichokuwa amekificha chini ya
kitanda, lakini mimi nilikuwa
nahtaji kama shilingi elfu hamsini
tu hivyo
nikazichomoa,
"Liwalo na liwe..!"
Nilijihisi kama yule stelingi wa
muvi za
kichina 'Jet Li', kwakuwa ilikuwa
usiku
sana kama mida ya saa
kumi,niliweza kutoka pale bila
hata ya kuonana na
majirani wowote haraka haraka
nikafuata ile njia niliokuja nayo na
kuondoka kuelekea msamvu
ambapo
ndipo ilipo stendi ya mabasi ya
mikoani.,
****
Nikiwa tayari nimeshakata tiketi
katika
basi la Abood, safari ya kutoka
Morogoro kuelekea Dar ilianza
na
nilikuwapo ndani ya basi la
kwanza
kabisa lililotoka sa kumi na moja
na
nusu, na tangu nilipoingia katika
basi sikuwa na wasiwasi wowote
kwani
moyo wa kishujaa na kijasiri
ulikuwa
umenitawala, lakini sasa takribani
nusu
ya watu kwenye lile basi walikuwa
wakinishangaa huku
wakiangaliana na
kutikisa vichwa vyao, nilishindwa
kujizuia nikajiangalia juu mpaka
chini..
"Mmmh...! mmmh...!"
Safari hii niliweza kuwah kujiziba
mdomo ili nisiropoke jambo lolote
baya
kwani traki suti yangu yote ilikuwa
imejaa damu huku na mikono
yangu ikitapakaa damu mpaka
sehemu za
usoni kitendo kilichofanya njia
nzima
abiria wanishangae kwa kuwa
vile..
Tukiwa tunakaribia kuingia
chalinze,
basi letu likasimamishwa na trafiki
wawili mmojawapo akiwa ni askari
polisi,kwa mara nyingine moyo
ukawa
kama unawaka,nywele
zilinisisimka
huku mdomo ukinitetemeka kisha
nikalitega sikio langu kwa upande
wa
nje kusikia maneno ya kondakta
wa
basi letu akiwa na trafiki.,
"Umesema mmepakiza abiria
wangapi?"
"Sitini na mbili tu"
"Hakuna waliosimama?"
"Hakuna"
"Usiniambie hakuna wacha
nipande
niingie nijionee mwenyewe ndo
uniambie hakuna sawa?"
Maneno hayo yalinifanya nizidi
kulegea
kwani aliyekuwa anaongea na
kondakta alikuwa hajavalia mavasi
meupe bali alivalia mavazi ya kaki
yale
yenyewe ya polisi huku akiwa
kashikilia bunduki akapanda
ndani ya
basi huku akiangaza siti moja
baada ya
nyingine na alipofika kwangu..
"We vipi tena Mmepata ajali
wapi?"
"Hatujapata ajali yoyote huyo
kapanda
basi hivyo hivyo..!"
Aliropoka dereva wa basi huku
akisaidiana na kondakta
wake kunimaliza..
"Haya shuka., shuka upesi
chini.,we
dereva endeleeni na safari yenu"
Nilijikuta nipo mikononi mwa yule
polisi haraka akiniwahi kwa
kunifunga pingu baada
kushushwa chini na
kuacha basi likiendelea na safari..
"Mungu wangu...! Mungu
wangu...!
mbona umeniacha..? Mbona
wanitenda
hivi....!"
Nilijikuta nikiandamwa na mikosi
na kumshushia lawama Mwenyezi
Mungu
alieniumba na kujiona sifai kuishi
katika dunia hii, huku nikiwa chini
ya
ulinzi pale barabarani,Yule askari
polisi
akaniangalia juu mpaka chini
akawa
anatingisha kichwa huku akicheka
kuashiria kama mtu
anayenifahamu
sana..
"Levina..?"
Sikuamini amini kama jina hilo
atakuwa
amelitaja yule askari au
ameambiwa na
mtu kuwa naitwa Levina,nilihisi
kama moyo ukinipasuka
ghafla,hivyo nikawa
sina tena jinsi kwani nikawa
nimeshapatikana, lakini swali
lililoniumiza kichwa ni kwamba
nipo
pale kwa kosa lipi la mauaji?
"maskini isikute baba yake 'Pendo
ndo kamtuma huyu
polisi..? ....Au.,
nilivyomuua 'Baba Ali taarifa
zimemfikia
huyu polisi..?"
Nikiwa bado najiuma uma pale
huku
akili ikiwa haifanyi kazi
kabisa,ghafla
nikamuona yule polisi kabadilika
zaidi ya pale kwani sura yake
ilikunjamana
ghafla huku akinifokea..
"Kwanini umeua Tena..?"
Lile swali lilinifanya nilegee na
kudondoka mpaka chini kwani
nilikuwa sina nguvu tena ya
kusimama huku nikishindwa kujua
kipi cha
kufanya pale chini...
"Au unapenda kwenda tena
gerezani.,
naona safari yako nyingine sasa
imefika..?"
"Hapana nisamehe afande
sijakusudia
nii...l..ii...piii...ti...wa...,tu..na
shetani..?"
Kabla sijamalizia kujitetea
nilishangaa
kuinuliwa kwa kushikwa shati kwa
nguvu kisha kilichofuata ni
kupigwa
vibao na mitama huku
nikishindwa
hata kujizuia kutokana na zile
pingu nilizokuwa nimefungwa
mikononi.,
"Kaka mkubwa, wacha nimpeleke
kituoni Dar huyu mpumbavu ana
kesi
kubwa na nitampigia simu afande
Geofrey aje msaidiane hapa.."
Nilijihisi kama mtu asiye na bahati
hapa duniani,maumivu
aliyonisababishia
'Baba Ali wakati akiniingilia
kinyume na
maumbile ukiongezea maumivu
aliyonisababishia huyu polisi
vilinifanya
niumie sana moyoni,huku mwili
wangu
ukiwa hautamaniki kwa
majeraha..
*******
* * Levina amekamatwa kwa
mauaji
yapi, ya 'Pendo' au 'Baba Ali..?
Inaendelea...
No comments:
Post a Comment