Home → simulizi
→ Sitaki tena – 08
Ilipoishia..
....uku mwili wangu ukiwa
hautamaniki..
Endelea..
"...Ingia kwenye gari mpumbavu
wee..!"
Aliendelea kunikaripia yule polisi
ambaye sikumfahamu kwa jina
lakini lafudhi aliyokuwa akiongea
ilinifanya niamini kabisa atakuwa
ni muhaya tena yule wa kule
Bukoba ndani ndani
(Vijijini),Tukiwa ndani ya ile gari
aina ya 'One Ten' huku nikiwa
nyuma na askari mmoja na yule
mwingine akiwa anaendesha gari,
Ujasiri wangu feki niliuweka
pembeni hivyo nikawa ni mtu wa
kutoa machozi na kujiuguza
sehemu zilizoonesha kuumizwa
katika mwili wangu,njia nzima
mpaka tunaingia Kibaha nilikuwa
mtulivu bila kusemeshwa kitu
chochote na yule polisi,Tulipofika
maeneo 'Mbezi' yule polisi
akafungua kinywa chake na
kuniuliza,
"Unasikia njaa..?"
"Kimya..!"
"Dereva embu pitia pale 'Mnama
Restaurant' tupate chochote..."
Maswali aliyoniuliza na maongezi
aliyokuwa akiongea na dereva
ndo kati ya vitu vilivyoanza
kuuchanganya ubongo wangu..
"Mbona kabadilika tena huyu
polisi..? Asije kuwa wananifanyia
njama kama Baba Ali..?
Kwanini wameniagizia chakula
kama kweli nina hatia?..sijui
nimuulize kosa langu ni lipi hapa
hapa..?"
Nikiwa bado nimekaa katika kiti
cha mgawaha mmoja pale mbezi
nikiwa mimi na polisi wawili
mmojawapo ndo yule aliyekuwa
akinishikia bunduki na ndo
aliyenifunga pingu,
"Wewe muuaji unakula nini?
"Hapana..., Sili chochot..." kabla
sijamalizia kusema nilishtukia
napigwa na kitako cha bunduki
na yule yule polisi..
"Usitufanye siye wapumbavu,
kuua uue..! Tunakuonea huruma
japo na wewe upate chochote
unatuletea 'usenge' au
umeshazoea maharage ya
Gerezani nini...?"
Nilijikuta nanywea na kuwa
mdogo na kukubali kula chakula
kama walichoagizia wao ambapo
walikuwa wakila wali nyama..
Ndani ya nusu saa nikarudishwa
tena kwenye lile gari lakini safari
hii nilishangaa hawakunifunga
tena pingu mikononi hivyo
nikabaki na maswali mengi sana
kichwani..
* * * *
Mawasiliano ya mimi na wale
askari bado hayakuwa mazuri
kwani hadi tunapita kimara
hakuna hata mmoja
aliyenisemesha zaidi ya yule
mmoja kukaa karibu na mini
nisiweze kutoroka huku mwingne
akiwa dereva ndani ya ile gari...
Mawazo yalitawala sana kichwa
changu huku nikijiona si mtu tena
wa kuonana na mama yangu
wala Gervas..,nikiwa bado niko
kwenye dimbwi la mawazo huku
tukiingia kwenye foleni ya mataa
pale ubungo ghafla macho yangu
yakaamia kwenye gari la pembeni
yetu aina ya 'suzuki' hasira
nilizoshikwa nazo ghafla
ziliwafanya hata abiria waliokuwa
ndani ya daladala ambayo ilikuwa
nyuma ya ile gari niliokuwa
nimeikodolea macho waweze
kunishangaa,hilo sikulijari kabisa
maishani mwangu kwani Levina mi
aibu ilishanitokaga siku nyingi
ukianzia pale shuleni kwa kina
Gervas waliponigalagaza wale
wanafunzi,pia katika basi
nililokuwa nimeshushwa hvyo
ukinishangaa mi ntakuona mtu
wa ajabu sana.,
Akili na mawazo yakiwa bado
ndani ya kale ka suzuki ambapo
macho yangu yalikutana uso kwa
uso na mama ambaye sitakuja
nimsahau hata nife, hakuwa
mwingine bali ni yule mama
aliyenipeleka polisi kwa mara ya
kwanza na ndiyo aliyefanya
maisha yangu yapo hivi mpaka
sasa..,
"lazima nife mimi au wewe"
Nilijisemea kimoyomoyo huku
nikimtolea macho yalioambatana
na mchozi ulioanza kuniteremka
kwa ghadhabu niliyokuwanayo,
kilichofuata ni kuhema haraka
haraka huku pua zangu zikianza
kujaa makamasi kama mtu
aliyepatwa na mafua ya
ghafla..kama kawaida yangu
sikutaka kuchelewesha mda..
"Bunduki kitu gani wacha
anifyatue tu lakini kwa huyu adui
yangu siwezi kamwe kumuacha.."
Nikatoka spidi katika lile gari
nililokuwa huku nikimwacha yule
askari akinilenga huku
akinikimbilia lakini hilo sikulijari
ndani ya sekunde chache nikawa
nshafungua na kuingia kwenye ile
suzuki na ku loki milango yote
tayari kwa kumvagaa yule mama
aliyekuwa akiendesha peke yake
ndani ya kale kagari..,
Nilitumia kucha zangu na meno
kama filamu zile za kutisha
'VAMPIRE' kuisambaratisha
kwanza sura ya yule mama kisha
nikachukuwa mtandio wake
aliokuwa nao amejifunga
mabegani na kuuvingirisha
shingoni mwake tayari kwa
kumnyonga,akiwa bado
anakurupuka na kutapatapa pale
gari zilikuwa tayari zimeruhusiwa
na trafiki na wale polisi niliokuwa
nao tayari niliweza kuwaona
wakiwa nje wanataka kuingia
ndani nilipokuamo,sikujua hata
siku moja kuendesha gari lakini
nilisikia kwa wenzangu tu kuwa
kunakitu kinaitwa gia kipo kama
rungu pia kingine kinaitwa krachi
kipo miguuni, sikulielewa hilo
lakini nilijikuta nimekanyaga chini
bila kujua kama ndo breki au ndo
hiyo krachi kisha nikalishikilia
rungu na kulisogeza kisha
nikashangaa kuona gari ikitoka
tena kwa mwendo wa kasi
pale,nikiwa huku nimekaza ule
mtandio shingoni mwa yule mama
huku upande mmoja nikishikilia
msteringi nilijikuta nimevamia gari
za watu wengine waliokuwa
mbele yangu na kusababisha ajali
mbaya pale huku umati wa watu
ukifurika katika lile eneo
kushuhudia ile ajari.,
Watu walikuwa ni wengi sana
mpaka nikachanganyikiwa
japokuwa nilijihisi mwili wote
haufai kwa maumivu, ile gari
niliokuwa nayo ilikuwa
imeharibika vibaya baada ya mda
mchache nilihisi kuna watu nje
wanavunja vioo vya gari wanataka
kuingia ndani katika kuangalia
vizuri macho yakamwona yule
polisi alionifikisha hapa nilipo..,
"Levina...! Levina...!Jisalimishe
mwenyewe unajitafutia matatizo"
Yale maneno ya yule polisi
aliyokuwa akiniambia,
hayakuniingia akilini mwangu
kabisa niliona kama anampigia
mbuzi gitaa ili acheze.,yule mama
sikujua kama alikuwa amekufa ila
nilimwacha pale akiwa anahema
kwa kasi ya juu huku akiwa
hajitambui wala hajiwezi hata
kunyanyuka,haraka haraka
nikafungua mlango upande wa
nyuma kisha nikatoka spidi huku
nikiuacha umati wa watu ukiwa
haujui nini kinaendelea kutokana
na lile tukio..
Spidi niliyotoka nayo pale huku
watu wachache wakinishangaa si
kwasababu nimeponea
chupuchupu kwenye ile ajali bali
pia waliniona kama mtu
aliyechanganyikiwa kwa jinsi nguo
zangu zilivyokuwa hazitamaniki
kwa uchafu tena ule uliokolea
damu katika ile suruali aina ya
trakisuti ilivyobadilika rangi
nyekundu iliyokuwa imetapakaa
damu na kuwa kama nyeusi
nyeusi,
Sikumuogopa hata mtu nilizidisha
mbio huku nikielekea barabara ya
kwenda mwenge, kelele za
wapiga debe pale ubungo
ziliongeza hisia zaidi ndani ya
kichwa changu kwani kitendo cha
kugeuka nyuma ilikuwa kosa
kubwa sana kwangu kwani
niliamini na kujua tu lazima umati
mkubwa wa watu uwe
unanikimbiza nyuma yangu huku,
nikiwa nasonga mbele haijapita
hata hatua ishirini mara kundi la
watu wengine wakawa tayari
wametanda mbele ya macho
yangu...
* * * *
Baada ya yule polisi kunishika
ndani ya basi akanifunga pingu
baada ya pale akatikisa kichwa
chake kuashiria kuwa
ananifahamu akaniita na jina
"Levina...!"
"kwanini umeua tena?"
"Au unapenda kwenda gerezani
tena"
Hayo ni kati ya maneno
ninayoweza kuyakumbuka kwani
yalinifanya niishiwe nguvu na
kudondoka mpaka nikapoteza
fahamu,ninachokumbuka
nilishtuka na kushuhudia
nikipepelewa na yule polisi huku
nikiwa kwenye gari ambayo
sikuitambua vizuri kwa nje kwani
alikuwa amenilaza ndani ya lile
gari na mikononi mwangu bado
nilikuwa na pingu hivyo nilipopata
usingizi akaendesha gari mpaka
nakuja kushtuka tumeshafika Dar
na nilikuwa nikiota ndoto tena
matukio ya ajabu ajabu kama lile
la kumuua yule Mama na
kuharibu vibaya lile gari lake pia
kufukuzwa na umati mkubwa wa
watu pale ubungo..
"Mungu wangu kumbe yote yale
ilikuwa ni kama ndoto..!"
Nilijikuta nausemea moyo huku
nikishusha pumzi kubwa..
"Uuhh...! uuhh...!"
Taaratibu nikiendelea kuhema
kwa nguvu na hasira kali.,
"Hapa ni wapi?"
Nilijikuta nikimuuliza swali yule
polisi aliyenitoa kule Chalinze na
ndiye alikuwa amenipakia baada
ya kuzimia pale Chalinze..
"Hupaswi kujua..unapaona pale?"
"Nikakaa kimya.."
Huku nikiona kibao kimeandikwa
mbele yangu.., 'CENTRAL POLICE'
Nilitamani kutoroka pale lakini
nisingeweza kwani mda wote
nilikuwa na pingu mikononi.
"Levina...! Embu niambie ukweli
hizo damu katika hyo suruali
ilikuwaje?"
Nikawa najiuma uma nashindwa
nimpe jibu gani kwani ni kweli
nimeua lakini nikisema ajue
itanigharimu sana maishani
mwangu..
"Afande hizi ni damu za kawaida
tu ambazo nilipitia buchani
kuchukuwa nyama na kupeleka
nyumbani nilipokuwa kule
Morogoro..!"
Nilijikuta namdanganya lakini
kiukweli alionesha kuchekeshwa
na mimi sana mpaka
nikamshangaa..
"Levina acha kunichekesha we
mtoto...,
Mbona kule nilipokushusha
kwenye basi nilikuuliza swali kama
hili na ukaniambia kweli umeua
ila kwa bahati mbaya..?"
"Mi mi...?
Labda utakuwa ulisikia vibaya
afande...."
Nilijitahidi sana kujikaza na
kubadilika lakini yule askari
hakuridhika na majibu yangu,na
kwa safari hii hakuwa mkali wa
kunipiga bali nilimshangaa pia
kwa kuongea na mimi ndipo
akataka kuniambia ukweli sababu
kubwa ya kunichukuwa na
kunileta mpaka maeneo haya
kituo cha polisi endapo tu
nitamjibu maswali yake kikamilifu,
huku tukiwa tumeliangalia lango
la kuingia polisi...
"Sitapenda nikuingize tena pale
polisi najua utateseka sana mpaka
uje kutoka tena mdogo
wangu..,Ila kitu kimoja
ninachotaka kuongea na wewe ni
unipe jibu moja tu ili niweze
kukusaidia..
"Huko ulipotoka umeua?"
"Sijaua na naogopa sana kuua
maishani mwangu..!"
Nilimjibu mara ya pili lakini kwa
sasa nilianza kuonesha
kauoga,kwani nilianza kuingiwa
na hofu huku nikitoka jasho
jembamba mwilini mwangu na
niliamini kabisa ntakuwa
nategwa..
"Mimi nataka kukusaidia Levina
lakini unakuwa mbishi si ndio..?"
Alianza kubadilika yule afande
huku akinikodolea mijicho na
kunionesha ufunguo wa zile
pingu kuwa kama nitakuwa
mkweli atanifungua pingu kisha
nitakuwa huru na salama,kitendo
kile kikanifanya uzalendo uanze
kunishinda na kujikuta namjibu
anavyotaka..
"Ni kweli nimeua lakini si kwa
kukusudia.."
"Umeua..? ..Nani uliyemuua
Levina?"
"B...aa..a..a..b..a.. A...l..i.."
Nilitaja jina kwa kujiuma uma pale
pale yule afande akabadilika
ghafla na kugeuza ile gari kisha
safari ikaanza lakini sikuweza
kujua ni wapi nilipokuwa
napelekwa zaidi ya kushuhudia
akitoka kwa mwendo wa kasi
huku nikiwemo ndani ya lile gari
lake...
***************
* * * Levina anapelekwa wapi?
* * * Je., ukweli gani aliokuwa nao
yule afande...?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: