πŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊ πŸ’žπŸ’ž_UPOZE MOYO WANGU._πŸ’žπŸ’ž Kutafsiri wazo la kichwa na kuwa neno litamkwalo mdomoni ni rahisi, kuliko kulitafsiri neno litokalo moyoni na kuwa hisia zenye thamani kwa yule atakayelisikia. Asili ya upendo na mapenzi ni amani, wanawake wanapenda kupendwa na wanaume tunapenda kuheshimiwa. Ni muhimu kwamba wanawake wa Kiislam waelewe thamani ya heshima kwa wanaume, wanaume wanafundishwa tangu umri mdogo kwamba wanapaswa kuwa washindi na watunza familia zao. Unaweza kufikiria jinsi gani mwanaume anaumia moyoni hasa ambaye anajitahidi sana kutunza familia yake, kisha mwanamke amuheshimu? Anaweza kukubali na kusema kwamba anakupenda, lakini bila heshima yako, (Heshima ya mwanamke) Mwanaume ni rahisi kujivua upendo huo. Wazo hili juu ya mwanamke kumtii mumewe linathibitisha kwenye quran sura ya 4 aya ya 34 (Surat An-Nisa) "Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhili baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kutii na kujilinda hata katika siri, kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnaogopa unashiza wao, basi wanasihini na muwahame katika vitanda na wapigeni. Watakapowatii msiwatafutie njia. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mtukufu Mkubwa" Mwanaume ni rahisi kubadili mtazamo wa mwanamke kama hutomuonesha upendo kwa vitendo, mwanamke anamchango mkubwa kwenye maendeleo ya familia, mwanamke ndio hukufariji mpaka unafanya kazi ukiwa na furaha. Mwanamke ndio hukuondoshea hasira kwa heshima yake pindi utakapokwazwa kazini, mwanamke ndio pumbazo la nafsi zetu,hupendeza, tunakuwa watanashati kwasababu yao, wake ndio kimbilio pale tunaposhikwa au kuwa na shahawati, wao ndio hutupoza. Wanawake ndio nusu ya dini pindi tutakapowaoa kwa ndoa halali na ya kisheria. Tusiwapende ili watuheshimu na msituheshimu ili mtupende, bali tupendane kutaka radhi za Allah, ili kesho kwakushikamana na kitabu chake na kufuata muongozo wa kipenzi, ya habiby, mbora wa viumbe vyote mtume wetu Muhammad (S.W.S) peace be upon him. Tuweze kukutana tena Jannah Amin. Ewe riziki yangu popote ulipo, nipoze moyo wangu kwa maneno na matendo mzuri, Nipoze moyo wangu kwa kunisomea quran pindi nipandwapo na hasira, Nipoze moyo wangu kwa Aya za mwenyezi mungu pale nitakapoteleza, Mola tujaalie wanaume wote tupate wanawake wema, Mola wajaalie wote waliokuwa kwenye ndoa, ndoa zao zidumu, Mola tujaalie kujiepusha na fitna za sheitwani na uzinifu. Utamu wa ndoa subra, Utamu wa ndoa uvumilivu, Utamu wa ndoa kuelemishana, _Mwana falsafa ndio mtetezi wa wanawake_✍✍ πŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊπŸ’žπŸŒΊ

at 9:33 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top