*💘💘SASA NIMEFAHAMU*💘💘
*💘MANENO YATOAYO MACHOZI💘*
💘"Mama anaongea na mwanawe na kumpa *Usia"*
💘Mwanangu mpenzi:
💘Kuna siku utanikuta uzee, sitafanya mambo yangu kwa akili;
💘Yakitokea hayo nakuomba tafadhali nipe muda na *subira ili unifahamu !!*
💘Pale mikono yangu itakapotetemeka, na chakula changu kikaangukia kifuani pangu, na nisipoweza kuvaa nguo zangu;
💘Jifunge na *kusubiria, na kumbuka miaka imepita nilikuwa nakufunza ambayo leo siwezi kuyafanya!!*
💘Ikiwa leo si maridadi na sina harufu nzuri; usinilaumu.. kumbuka udogoni kwako nikijitahidi sana nikufanye uwe maridadi mwenye harufu nzuri!!
💘Usinicheke utakapoona ujinga wangu na
kutofahamu mambo ya wakati wenu huu, lakini wewe kuwa jicho na akili yangu ili niyapate niliyoyakosa!!
💘Mimi ndiye niliyekufunza adabu na mimi ndiye niliyekufunza vipi ukabiliane na maisha;
*💘Sasa inakuaje leo unanifundisha yaliyo wajibu na yasiyo wajibu?*
💘Usinichoke kwa udhaifu wa kumbukumbu yangu, na uchelewaji wa *maneno yangu na fikra zangu* wakati ninapozungumza nawe, kwani furaha yangu wakati huu ni kuwa pamoja nawe tu!!
*💘Wewe nisaidie tu kupata ninachohitaji;* kwani bado najua ninachotaka!!
💘Miguu yangu ikikataa kunipeleka sehemu ninayotaka kwenda; *nihurumie* na kumbuka kwamba mimi nilikushika sana mkono ili uweze kutembea!!
*💘Usione haya abadan kunishika mkono wangu leo;* kwani kesho utatafuta wa kukushika mkono wako!!
💘Katika umri wangu huu; elewa kuwa mimi siyaelekei maisha kama wewe; lakini kwa ufupi nangojea mauti; kwa hiyo *kuwa pamoja nami wala usinitupe!!*
💘Pale ukikumbuka makosa yangu; jua kuwa mimi nilikuwa sitaki ila maslahi yako!!
💘Na mimi napenda sana unayonifanyia hivi sasa kwa *kunisamehe matelezo yangu na kusitiri aibu zangu..*
*💘💘NAWE MOLA AKUGHUFIRIE NA AKUSTIRI!!💘💘*
💘Bado *vicheko na tabasamu zako vinanipa furaha* kama ulivyokuwa mdogo...
kwa hiyo usininyime suhuba yako!!
💘Nilikuwa nawe wakati *unazaliwa;* kuwa nami pale *nitakapofariki!!*
*💘Maneno bora yaliyopitia katika maisha yangu, na hata nikiyarudia mara elfu moja sichoki kuyasoma..*
"Mola wangu warehemu wazazi wangu kama walivyonilea nilipokuwa mdogo"(Rabbi Arhamu humma kama rabayan swakhira)
*💘MANENO MAZITO KWA MWENYE AKILI💘*
*💘💘SASA NIMEFAHAMU💘💘*
No comments:
Post a Comment