JINSI YA KUPUNGUZA MAJI MAJI KATIKA VIUNGO VYA UZAZI WA MWANAMKE Nina umri wa miaka 28 na nina watoto 2. Tatizo nililonalo sasa ni uke kuwa na majimaji yaani sio mkavu, japo haukuwa mkavu sana hapo awali nilikuwa wa kawaida. Tatizo lilianza mwaka jana baada ya kujifungua mtoto wa pili uke umekuwa na majimaji hata kunifanya nisifurahie tena tendo la ndoa japo mume wangu hajawahi kuongelea jambo hili ila nahisi hata yeye hafurahii kama hapo awali. Naombeni msaada kwa yeyote mwenye kujua dawa ama nini cha kufanya ili uke uwe mkavu ili ninusuru ndoa yangu jamani. USHAURI Umesema uke wako una majimaji na hivyo haufurahii tendo la ndoa, unahisi pia mume wako hafurahii, na hivyo unaomba dawa ili kuinusuru ndoa yako. Kwa kawaida kwa wanawake ambao wameshavunja ungo na bado hawajaingia uzeeni (menopause) ukeni mwao huwa si kukavu,(na kama wakipatwa na ukavu ukeni basi wanahitaji tiba) na umajimaji au unyevunyevu huo ni muhimu sana na unakazi yake maalum, na huzidi vipindi fulani Fulani - nitaeleza. Hata hivyo kwa kuwa wanawake wanatofautiana ni vigumu kusema ni kiasi gani cha umajimaji huo ni wa kawaida na upi umezidi. Hata hivyo namiini mwanamke ambae anahitaji kuvaa pad wakati hayuko kwenye menses hali hiyo inahitaji kuchunguzwa. (Wewe hukusema ni kiasi gani) Kiutalaamu zipo sababu nyingi zinazofanya uke uwe na unyevunyevu, sababu zingine ni za kibaologia (za kimaumbile) na hivyo hazihitaji tiba, zingine zinaletwa na maradhi, na sababu nyinginezo. • kibiologia , hutokea mara baada ya kuvunja ungo, unyevunyevu wake huwa haunuki, hauwashi, haunguuzi na haufanani kabisa na usaha. Unyevunyevu huo huzidi wakati wa msisimko wa ngono, na au wiki ya pili au ya tatu baada ya siku zako, na au kama unatumia baadhi ya dawa za majira nk. • Maradhi: majimaji yake huwa yanaharufu, kama usaha,au ya kijani au kama maziwa yaloganda au kama povupovu. Husababishwa na uambukizo wa trichomonas, fungus, kisonono nk , pia maradhi kama fistula (nasuri), au polyps yaweza sababisha hali hiyo. Pia maradhi kama kisukari yaweza leta hali hiyo. • Sababu nyingine, Douches ( kujipiga bomba ukeni), kusafisha uke kwa sabuni au kemikali nyingine, kuingiza manukato ukeni, kutumia condom (baadhi ya wanawake),kuvaa nguo zinazobana sana na hivyo maeneo hayo kukosa hewa nk. Kwa kuwa sababu ni nyingi nakushauri nenda hospitalini ukachunguzwe kabla hujatumia dawa yoyote kwa sababu huenda ni kawaida au huenda ni maradhi. Na kama ni ugonjwa kila ugonjwa una tiba yake. Na wakati unajiandaa kwenda hospitali nakushauri usifanye douches, usijisafishe ukeni na sabuni au kemikali yoyote, vaa nguo za pamba ambazo hazikubani.

at 9:38 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top