Sunday, January 8, 2017

Pengine kile kitendo cha yeye kuvua nguo na kumuona akiwa uchi ndicho unafikiri umemjuwa sana? Niambie kuhusu ndoto zake, Niambie kuhusu kinachomvunja moyo wake, Kipi anakipenda, Kipi kinachomfanya analia? Niambie kuhusu utoto wake, Niambie hadithi moja kuhusu yeye, Bora hujui... Umeona ngozi yake, Umeshika mwili wake lakini hujampa furaha, Amekuwa kama kitabu Kwani umeshika kasha lake huku ukishindwa kuzijuwa kurasa zake, Maana wewe ulikwenda kama mpitaji kwake ndo maana hukujuwa namna ya kukabiliana na hisia zake, Umemuacha mlimani wala asijue anafikaje kileleni, Umekuwa mkimbizaji usie na mbio japo alikusubiri ili umsogeze kumaliza Mbio lakini ulishindwa na umemfanya ajisikie vibaya Kwani MBIO ZAKE HAZIKUSHINDA kutokana na kuwa aloshindana nae hawezi kumsababisha ashinde.

No comments:

Post a Comment