Home → ushauri
→ MKASA WA KUSISIMUA: WENGI WAMEISAHAU MAANA YA "MAMA, MZAA CHEMA" WANAMLIPA MANYANYASO.
#inasikitisha pole sana mama Venance
Venance baada ya kupata kazi alioa, mke wake alikua mzuri sana wa makabila yale ya mjini, hakika alimteka vilivyo mmewe kimapenzi, kiakili na kumtawala katika kila maamuzi yake. Hicho kilikua chanzo cha Venance kumsahau kabisa mama yake kijijini ambae alikua ni mlemavu wa mguu na mbaya zaidi alikua mjane kwani mme wake yani baba yake Venance alishafariki zamani wakati Venance akiwa mdogo kabisa. Mke wa Venance alimzuia Venance kumleta mama yake mjini ili wakae nae alimwambia, "Huhuhuhuuuu ivi unafikiri unataka umlete huyo mama yako na ulemavu wake akae na nani hapa mimi au nani? Hahahahahaaaaaa usinichekeshe we mwanaume" mbali na kuzuia hilo ila pia hata kiwango cha fedha alichokua Venance akitaka kutuma kijijini kilipitia mikononi mwa mkewe kukaguliwa kwanza na zikionekana nyingi hupunguzwa.
Mama yake Venance aliugua mno, kutokana na ulemavu wake wa mguu ilikua ngumu kusafirishwa kwa usafiri wa kawaida ambao kijijini pale usafiri mkuu ulikua ni malori ndio magari ya abiria, hivyo ndugu wakampigia simu kumuomba aende na gari lake akamsafirishe mama yake kumleta hospitali za mjini kwa ajili ya matibabu. Mke wa Venance alimzuia Venance kwenda, akamwambia acha kuwadekeza ndugu zako wanataka kukupotezea ela zako, watumie 20,000 inatosha wamsafirishe malori yapo tena yanafika hadi hospitali kuu tunampokelea pale.
Ndugu walipokea 20,000 ile wakampakiza kwenye lori wakamsafirisha hadi hospitali kuu. Venance alimuacha mkewe akaenda alipofika Akaambiwa yupo ndani chumba cha daktari, hivyo aliamua kusubiri nje karibu na mlango, alisikia dokta akimwambia mama yake,
"Mama pole sana kwa kuumwa vipimo vinaonyesha una malaria, amoeba, minyoo, presha na upungufu wa damu, magonjwa haya yanatokana na lishe mbovu pamoja na maisha ya shida, je! hauna mtu wa kukusaidia au mtoto?"
Mama yake Venance alilia kwa mda dokta akamtuliza kisha akamuuliza nini kinakuliza mama? Mama Venance akajibu, "Mimi ni mjane, nasikitika mwanangu wa pekee wa kiume niliemsomesha kwa tabu akafanikiwa hanikumbuki tena thamani yangu, amenitelekeza hanijali tena, dokta unavyoona mguu wangu huu ulivunjika kwa ajili ya ajali ya baiskeli siku moja mtoto wangu Venance akiwa mdogo aliugua ghafla hali yake ilikua mbaya sana nikaamua kuchukua baiskeli nikambeba nikamleta hospitali mjini,
Baada ya matibabu wakati twarudi nyumbani tulipata ajali ya baiskeli katika kumzuia mwanangu asiumie ndipo baiskeli iliponizidi nguvu nikavunjika mguu, niliishi kwa shida ila namshukuru Mungu nilifanikiwa kufanya vibarua kulima mashamba ya watu na kukata majani nikamsomesha hadi chuo kikuu, leo amepata kazi hanijali tena, nateseka kijijini watu wananicheka eti nilipoteza mda wangu bure kutunza nyoka asiye jua nini maana ya fadhila."
Dokta alistaajabu akamwambia, "Pole sana mama, Mungu amguse kule alipo akumbuke wema uliomfanyia na namna ulivyomlea"
Maneno yote hayo yalimchoma mno Venance pale nje, aliufungua mlango akaurudishia kwa ndani kisha akapiga magoti huku akilia kwa uchungu, "NAOMBA UNISAMEHE MAMA YANGU, SIJUI NI NINI KIMENIPIGA UPOFU?"
Kabla hajajibiwa kitu kumbe sauti ile ilifika hadi nje, Nje jirani na mlango Wa chumba cha daktari alisikika mkewe Venance akiuliza,"Kuna nini Venance au huyo mama kafa? "
Mama Venance aliitikia akamjibu, "Sijafa na sitarajii kufa, Mungu ndie anaepanga namuachia yeye, nashukuru kwa namna ulivyomteka mwanangu hata hanikumbuki wala kunijali tena ila nakupa neno 1, kama kweli Venance sikumzaa hicho chakula chake unachokula nyumbani kwake kikubariki ila kama sivyo kitakutokea puani".
Mke wa Venance kusikia ivo alisonya, "Mfyuuuuuuuu dua za kuku hizo kamwe hazimpati mwewe." kisha akaondoka,
Venance alimchukua mama yake akasikiliza ushauri wa dokta akaamua kumpangishia kwa siri chumba mjini huku akifanya utaratibu wa kumjengea, haukupita mwaka mke wa Venance alishikwa na Kansa ya damu pamoja na ugonjwa wa moyo kutokana na kula mno vyakula vya mafuta akafa. Venance akamchukua mama yake na kumleta kuishi nae na familia yake ambapo alikua na watoto watatu. Akaoa mke mpya binti jirani yao kule kijijini aliyekuwa akimuuguza mama yake.
Funzo
Haijalishi unaishi na mtu unaempenda kiasi gani ila kamwe thamani ya upendo wako kwa MAMA yako isishuke, yeye ndie muasisi wa maisha yako chini ya jua bila yeye usingeiona leo, huyo anaekushauri umpuuze mama yako hajui uchungu na mateso mama yako aliyopitia katika kukulea hadi hapo ulipokua ukakutana nae ukiwa na meno yako 32, iweje leo akuambie mama yako si kitu???!!!!!.
Kama kweli unampenda mama yako TYPE "HAKUNA KAMA MAMA" kisha SHARE post hii hakika baraka za mama yako zitaambatana nawe daima popote uendapo.
Nakutakia Jumapili Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
Usisahau ku LIKE
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: