KUNA KITU KIKUBWA SANA CHA KUJIFUNZA KATIKA MKASA HUU
#inasikitisha sana
Mwaka 1993 mwezi wa tatu Mpiga picha maarufu wa Africa kusini aliyejulikana kwa jina la Kervin Carter aliitembelea Nchi ya Sudan Kusini na kufanikiwa kupiga picha ya mtoto aliyeshindwa kuendelea na safari ya kuwafuata wazazi wake waliokuwa wameenda kupokea chakula cha msaada toka UN. Carter alisema alisubiri kwa mda wa dakika zisizo pungua 20 kuona kama tai atarusha mbawa zake kumsogelea mtoto huyo.
Hakujali wala kufikiria kuhusu hatari inayoweza kumsibu mtoto yule dhaifu na mwenye njaa kutoka kwa TAI yule aliekua amemkaribia. Carter Aliendelea na zoezi lake la kupiga picha alipomaliza aliondoka akamuacha mtoto yule na TAI. Mtoto yule alilia sana na kuomboleza kutokana na kiu na njaa kali pamoja na hatari ya TAI nyuma yake ila hakukuwa na mtu wa kumsaidia, alipopoteza fahamu TAI alimla nyama ikawa ndio mwisho wa uhai wake.
Baadaye Carter aliuza picha hii kwenye vyombo vya habari vya NEW YORK na ilianza kuoneshwa kuanzia tarehe 26/03/1993, mamia ya watu waliwasiliana na gazeti lililochapisha habari hii kujua kama mtoto huyo alinusulika kuuliwa na TAI anayeonekana nyuma yake au laa, kwani mwandishi wa bahari hakuweza kutoa tarifa kamili kama mtoto huyo alikuwa na uwezo wa kukabiliana na TAI au laa hivyo mwisho wake haikujulikana japo Carter alikosolewa kwa kuto msaidia mtoto huyo.
Pamoja na hayo yote Carter alitunukiwa tuzo kwa kupiga Picha hii.Lakini hakuweza kuifurahia tuzo hiyo kutokana na kukosa utu ambao ulipelekea kifo cha mtoto huyo akaishia kusema ''kwakweli naomba msamaha kwa kutomuondoa mtoto huyo katika mazingira ya hatari (“I’m really, really sorry I didn’t pick the child up,”)
Baada ya miezi michache alikutwa amejiua kwa msongo wa mawazo yaliyotokana na kukosa utu. Alizithamini pesa atakazopata kwa kuuza habari kwa watu wa New York, hakuishia hapo bado akapewa na tuzo kwa picha hiyo lakini ndani roho yake iliendelea kumkumbusha kuwa hafai kuwa binadamu wa kuigwa katika jamii na wazo pekee lililo mjia baada ya kuona hafai kuwa mmoja wa watu wenye utu aliamua kujiua.
Funzo
Katika kila unalolifanya duniani tanguliza UTU kumbuka dunia ni mapito mali, fedha na vyote vya duniani ni vya muda tu, amani ya moyo wako iendane na upendo na kujali wengine pamoja na kuwasaidia pale inapowezekana.
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
Usisahau ku LIKE
Team Brayton Offical Love
No comments:
Post a Comment