🥀🍃JINSI YAKUFUKIZA UDI UKAKAA KWA MUDA MREFU🥀🍃 🥀Anza kwa kufungua madirisha kila ukiamka asubuhi ili kuruhusu hewa chafu kutoka na safi kuingia ndani 🥀Fanya usafi vizuri kama kawaida ya usafi, kufagia, kukunuka vumbi na kudeki 🥀Chukua chetezo chako anza kuchoma habbat sauda katika moto wako ili kufukuza mashetani wabaya ambao nao waishi majumbani kama wanavyoishi binaadam 🥀Baada ya hapo chukua ubani kidogo choma katika kile chetezo. 🥀Hapo malizia kuchoma udi wako na uhakikishe umefunga madirisha ili harufu ibaki ndani, wacha moshi utande ila ukianza kuhisi udi umeisha umebaki moshi tu ondoa moto ule maan moshi wa udi unakuwa umemalizika 🥀Jaribu kufukiza udi akiwa mume hayupo ili moshi usimkere, ama kwa wale wanaokwenda makazini wanaweza kufukiza udi weekend au jioni wakirudi makwao 🥀Usidharau udi ukasema ni mila za waarabu, kumbuka hakuna anayechukia harufu nzuri, harufu nzuri huongeza mapenzi katika nyumba, ukarimu kwa mume na wageni, pia unaongeza Thawabu pale ukifanya jambo jema kwa ajili ya mumeo ni Sunnah. 🥀Hakikisha unatafuta udi mzuri wakuvutia na fukiza angalau wiki mara mbili mpaka tatu utaona mwenyeo nyumba inaanza kuzoea harufu nzuri 🥀PENDA NDOA YAKO, PENDA NYUMBA YAKO🥀

at 3:08 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top