CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA NANE (08) ILIPOISHIA SEHEMU YA SABA: Basi alijikuta mpweke sana na alijikuta anatamani, kuongea na vicent,ili apate kampani na kupoteza muda kidogo. Hata sijui ni kwanini alimuwaza vicent kuwa ndio mtu pekee wa kumtoa upweke. Hata mimi sijui,ila tutajua hivi karibuni. Basi aliingalia simu kwa muda nakujifikiria ampigie au atulie asimpigie. Basi nafsi ya niram ikawa inashindana,moja inamwambia piga nyengine, inamwambia usipige ila akiwa katika mgongano wa kutoa maamuzi nini afanye, gafla akaona kitu moyo ukapiga paaaaah!!! .alishindwa kuamini alichokiita. endelea........ Niram alishindwa kuamini alichokionaa, kwa muda ule kiukweli alitoa macho kama ndubwi, spidi ya moyo kwenda mbio vilizidi kuongezea. Hakuamini kuona mtu aliyekuwa anamuhitaji kwa muda huo ndo alikuwa anampigia.basi alichukua simu yake na kuipokea. "hellow vicent".ilikuwa ni sauti tamu yenye kusisimua mwili.hakika hata vicent alipata kigugumizi cha gafla na wakati yeye ndie aliepiga. "aaaghahg!! Niambie niram umeshindaje kipenzi? ".aliongea vicent kwa sauti ya upole na ya kiume,kiasi niram alijisikia raha sana kuisikiliza. "nipo poa kulikuwa na wageni leo basi kulikuwa na kazi kweli".aliongea niram kwa sauti yake ile nzuri na ya upole, kama ya Madeko hivi. "oooh pole mamy si ungeniita nije nikusaidie".aliongea vicent, kwa utani huku akisubiri jibu. "ahhhhah! Uongo tu ungekuwa kweli wewe".alijichekesha ki kikekike niram huku anabadili mikao ya kukaa pale alipokuwa. "yaap ningekuja kwanini nisije kwa rafiki yangu kumsaidia jamani?".alijiongelesha kama anauliza hivi huku ikiwa sauti fulani inayoonyesha hali ya kujali. Niram alifurahi sanaa kusikia vile. "mmh! Basi nashukuru kwakunijali kipenzi".aliongea niram kwa madeko. "usiliongelee hilo ni wajibu wangu kama rafiki".aliongea vicent. "basi wifi anapata raha sana".aliongea niram huku akitia kijineno cha mtego. "sina mama yangu, bado sijabahatika".aliongea vicent kwa utulivu wa hali ya juu, kwa hakika ungesema kweli mwanaume ndiyo huyu. Alijua sana kuongea na mwanamke na akaelewa. "ooh usijali Mungu atakupa my"aliongea niram. "sawa nashukuru sana na mimi ntajiona ni mwenye bahati".alijibu vicent,basi waliongea mengi sana mpaka walipoagana, kwa maana kesho ilikuwa ni siku ya shule. **** Ilikuwa ni siku ya pili, watu walikuwa na pilikapilika zao kama kawaida. Huku kila mmoja akiwa katika harakati za utafutaji. Magari yakikuwa yanapishana kila wakati. Basi muda huo shuleni niram, alikuwa ni mtu wa tabasamu muda wote,alikuwa kachangamka sana hata marafiki zake wakimshangaa, ila aliyejua tofauti ya niram ni hajra peke yake. Alimtazama kwa muda kisha akamuuliza "vipi dada mbona huko happy hivyo?".aliuliza kwa sauti ya chini hajra, huku wengine wakiwa bize kufanya yao. "mmh kwani nikoje jamani!?".akiuliza niram,huku akiachia tabasamu pana sana usoni mwake. "we mwenyewe ujioni kama upo tofauti leo?".aliongea hajra huku akapachika na swali. "hamna bwana mama jana alinifurahisha sana ".aliongea niram, huku akionyesha kuwa hakuwa akiongopa. "oooh!! Sawa".alijibu hajra, huku anageuka kujumuika na wengine. Niram yeye muda wote alikuwa ni kutabasamu alijishangaa hata kwanini, anajiona ni mwenye amani sana. Basi akachukua kitabu na kuanza kujisomea kwa umakini wa hali ya juu. **** Na huku shuleni kwa akina vicent mambo yalikuwa hatari. Maana suma alikuwa ana mchecheto wa hali ya juu halikuwa kwenye stori za kufa mtu. "basi jana niwaambie si somoe akanipigia bwana unajua nilichokifanya nikamchunia mi nilikuwa na miadi na hadija ye ananiletea kiwingu".akanyamaza kidogo kisha akaendelea. "basi jana nikakutana na hadija weeeeeh!!mtoto fundi mtoto anakata uno kama feniii we acha, yule mtoto balaaa".aliongea suma huku richard na vicent wakiwa wanamuangalia.ila rachard mbavu alikuwa hana kwa kicheko, huku vicent akiwa kutabasamu tu. "umemaliza? ".aliuliza vicent. "daah!huyu kashaanza ulokole wake".aliongea suma. "siyo ulokole uwo ni ushamba, we mwenyewe unaona sifa alafu ukigongewa dada yako unawaka kama pilipili ".aliongea vicent akionyeshwa kuchukizwa na rafiki yake huyo. "yani kwakuwa wewe upendo kwahiyo sisi tusiongee? "alihoji suma, huku kama alishaanza kupaniki hivi maana sura ilichenji. "yani hakuna kusema chochote hapo tabia zako azituvutiii unawazalilisha dada zetu tusikuambie".aliongeara Richard huku amemkazia macho bila chembe ya uoga. "mwambie huyoo huo ni ujinga broo".aliongea tena vicent huku anamtazama. "eeh basi yaishe ,tuongee mengine vipi yule mtoto wa Kihindi nipe stori basi".aliongea tena suma. "aisee suma ukoje mbona hupendeza kuwa mmbea".aliongea richard. "aaah! Kausha mi si nishabadili mada, nauliza mambo mengine".alijitetea suma huku akikaa vizuri kuambiwa yaliyojiri. "hivi unajua kwanini jana nilikukatia simu? Coz lisilokuhusu usilikingie kifua, kila mtu apambane na hali yake mambo ya mahusiano yangu hayakusu"aliongea vicent huku akinyanyuka,na kuanza kutoka nje, richard akamfuata, maana vicent alionyesha kuchukia. Suma akabaki katulia kanywea vibayaaaa, kama kamwagiwa maji.*** Mama vicent alikuwa sebuleni, alikuwa amekaa na mama wa makamo kama yeye kwakweli walionekana ,kama wapo kwenye maongezi mazito, maana vilisikika vicheko vya hali ya juu. Ila gafla wakaacha kucheka macho yote yakageuka kutazama........ Itaendelea.

at 10:37 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top