Story....... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na moja (11) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp....... 0769673145 Ilipoishia......... Upande wa Nolan yeye alipanga lazima amfundishe adhabu baba yake kwa namna yoyote ile. "Wewe ni baba yangu ndio sikatai, umenitunza vizuri, umenipa elimu ya kutosha Sawa, lakini kwa unyama huu unaotaka kuufanya hakika sitakuacha lazima nitaenda sambamba na wewe." alijisemea Nolan akiwa chumbani kwake akipanga mipango yake. Lakini pia Nolan aliapa kama asipofanikisha ndoa ya Frank na Penina bas atajiua. *********Endelea ******** Nolan alivunja kibubu chake cha kuhifadhia pesa na kugundua pesa iliyopo huko ni ndogo Sana na haitatosha kutimiza mipango aliyoipanga. Nolan aliamua kuwa mwizi wa ghafla kwa ajili tu ya kutimiza anachokitaka. Lakini hata hivyo hakuenda kuiba sehemu nyingine yoyote, aliamua kumuibia baba yake ikiwa ni njia moja wapo ya kumkomesha baba yake. Nolan alikuwa anajua baba yake ana tabia ya kuhifadhi pesa chumbani kwake. Na baada ya Nolan kugundua kuwa baba yake hayupo haraka akaamua kwenda chumbani kwake na kumuibia pesa kiasi cha shilingi million hamsini. Baada ya zoezi hilo, Nolan alichukua kiasi cha fedha kati ya zile alizomuibia baba yake na Kisha zingine akazificha sehemu ambayo mtu mwingine hawezi kuziona. Kisha Nolan akatoka nje na kuchukua gari Lake na kuondoka nyumbani Muda ule ule. * Mzee Joel alitia nanga Katika kikosi kimoja kilichojulikana kwa Jina la the killer (wauaji) Baada ya kufika mzee Joel alielezea shida Zake zilizompwleka pale na Sasa akitaka Frank pamoja na Nolan wauwawe Mara moja. Mzee Joel alitoa picha ya Nolan pamoja na ya Frank na kumkambidhi mkuu wa kikosi kile cha the killer. "mzee tunahitaji pesa kiasi cha shilingi million thelathini ili kuitimiza kazi yako." akaongea mkuu wa kikosi kile kumwambia mzee Joel. "hakuna tatizo kuhusu pesa nyie fanyeni kazi niliyowapa." akaongea mzee Joel. "Sawa kuanzia Sasa kazi imeanza na tutakuletea majibu Muda si mrefu." mkuu yule wa kikosi cha the killer akamwambia mzee Joel. Mzee Joel aliweza kuondoka huku akiwa na uhakika wa Kaz yake kufanyika kwa ufasaha Sasa. Mkuu wa kikosi kile cha the killer aliwateua vijana wanne kwenda kuanza kazi ya kummaliza Nolan na Kisha wengine wanne akawatuma kwa Frank. * Katika hoteli ile ya kifahari Penina na Frank wakiwa wameketi kitandani wakitizama tv, ghafla bila kutarajia walishtukia kumuona Nolan akigonga mlango. "Eeh kaka mbona umekuja bila taarifa?" akauliza Penina kwa mshangao baada ya kufungua mlango. "lazima nije ghafla na taarifa zangu ziwe za ghafla kwasababu nataka nifanye kitu cha kuwafurahisha, na hivi nimekuja kuwaambia mjiandae tuondoke tayari nimeshawakatia tiketi za kwenda South Africa (Afrika kusini)" akaongea Nolan kumwambia Frank na Penina. Zilikuwa taarifa za ghafla kwa kina Penina na Frank, lakini hata hivyo hawakuwa na namna ilibidi waanze kujiandaa kwa ajili ya safari yao waliyoandaliwa na Nolan. * Vijana wanne waliopewa kazi ya kumuangamiza Frank walichunguza wakachunguza na hatimaye wakafinikiwa kupajua nyumbani kwa kina Frank. Na bila kupoteza muda wakavamia nyumbani kwa kina Frank na kuwaweka chini ya ulinzi Wazazi wake Frank pamoja na mdogo wake Frank. Vijana wale wakawaamuru Wazazi wake Frank waseme sehemu alipo Frank la sivyo watawaangamiza. Wazazi wake Frank kwa kuogopa kuuwawa wakajikuta wakitaja sehemu aliyopo Frank. Vijana wale bila kuchelewa waliachana na Wazazi wake Frank wakaingia kwenye gari na kuanza safari ya kuelekea sehemu aliyopo Frank ambapo ni Katika hoteli moja ya kifahari. * Frank pamoja na Penina walimaliza kujiandaa na moja kwa moja wakatoka ndani ya chumba kile na kuelekea mpaka nje ya hoteli ile na kuingia kwenye gari la Nolan. Lakini wakati huo huo vijana wale wanne wa the killer walikuwa tayari wameshawasili kwenye gari lile na waliweza kumuona Frank pamoja na Nolan ambao ndio walikuwa wakiwatafuta wawamalize. Mmoja kati ya vijana wale wanne wa the killer alitoa simu yake na kuwapigia wale vijana wengine wanne waliokuwa wakimtafuta Nolan, na kuwaeleza sehemu aliyoonekana Nolan pamoja na Frank. Vijana wale waliokuwa wakimtafuta Nolan nao walianza safari ya kutoka sehemu nyingine waliyokuwa wakimtafuta Nolan na kushika njia ya kuelekea Katika hotel waliyoelekezwa na wenzao. Wakati huo huo Nolan aliliondoa gari pale hotelini na kuanza safari ya kuelekea Katika uwanja wa ndege. Vijana wale wanne wa the killer nao wakawasha gari Lao na kuanza kuwafuatilia ili waweze kujua wanaelekea wapi na kama ikiwezekana wakaulie huko huko. Safari ikiwa inaendelea, ghafla Nolan aliona gari moja nyekundu ikiwa nyuma na kuitilia mashaka kuwa inawafuatilia. Nolan aliamua kufanya kitu ili apate uhakika kama gari lile linawafuatilia au haliwafuatilii. Nolan alipunguza mwendo wa gari Lao ili lile gari jekundu lililokuwa nyuma yao liwapite. Lakini cha kushangaza gari lile halikuwapita nalo pia lilipunguza mwendo na kwenda taratibu pia. Nolan akaamua kuongeza mwendo wa gari Lao ili kuliacha gari lile, lakini pia gari lile liliongeza mwendo na kuwa Sawa Sawa kabisa na gari la kina Nolan. Nolan hapo Sasa ndio akapata jibu kuwa asilimia Mia moja hilo gari jekundu linawafuatilia vibaya mno. "hawa hawanijui ngoja niwaoneshe mimi ni nani." akajisemea Nolan kimoyo moyo na hapo hapo akaongeza mwendo wa gari Lao ili kuliacha gari lile lililokuwa likiwafuatilia. Wakati huo huo kile kikosi cha pili cha the killer kiliwasili pale hotelini na kuwapigia wenzao simu ambao ni wale wanaowafuatilia wakina Nolan, na kuwatarifu kuwa tayari wameshafika. Kikosi kile cha kwanza kikawapa maelekezo ya sehemu walipo wakiwa bado wanawafuatilia wakina Nolan. Kikosi kile cha pili bila kupoteza Muda nacho kikatoka pale hotelini na kuanza kuwafuatilia wakina Nolan pia. Wakati hayo yote yanaendelea Frank na Penina walikuwa wakicheka na kufurahi kwenye gari bila kufahamu chochote kinachoendelea, na hata Nolan hakutaka kuwaambia chochote kwa kutokutaka kuwavuruga Katika safari yao. Nolan bado alizidi kujaribu kulipoteza gari lile lakini bado hakufanikiwa. Nolan alifika kwenye mataa ya kuongozea magari na baada ya Nolan kuvuka tu kwenye mataa yale, zikawaka taa nyekundu kuashiria magari yaliyokuwa yakitoka upande ule wa kina Nolan yasimame kwa dakika kadhaa. Lakini Nolan wao walikuwa tayari wameshavuka lakini vijana wale wa the killer walikuwa bado hawajavuka hivyo ikawabidi wasimame. Nolan aliweza kugundua kuwa gari lililokuwa likiwafuatilia limesimamishwa kwenye mataa. Lakini Nolan akataka kuwafahamu ni wakina walikuwa wanawafuatilia. Nolan alipaki gari pembeni Kisha akawashusha Frank na Penina na kuwapakiza kwenye tax iliyokuwa pembeni yao, na kuwakabidhi kila kitu kilichostahili kwenye safari yao na kuwataka watangulie na kuanza safari yao. Penina na Frank walishangazwa Sana na maamuzi ya Nolan lakini hata hivyo Nolan hakutaka wamuulize swali lolote, alimwamuru dereva wa tax ile awashe gari na kuondoka. Kisha Nolan naye akaingia kwenye gari yake na kugeuza kuwafuata vijana wale wa the killer na wakati huo walikuwa tayari wameshaungana wote kwa maana ya kikosi kile cha kwanza kilichokuwa kikimtafuta Nolan na kile cha pili kilichokuwa kikimtafuta Frank. ............ Itaendelea

at 6:47 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top