Monday, September 3, 2018

Story...... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi (10) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp...... 0769673145 Ilipoishia...... Baada ya dakika kadhaa Frank na Penina waliwasili nyumbani kwa Frank. Wakashuka kwenye bajaji na kuelekea kwenye nyumba ya kina Frank. Walipoufikia mlango Frank alijificha nyuma ya Penina na kumtaka Penina abishe hodi ili wawafanyie surprise Wazazi wake Frank. ***********Endelea ********* Mlango ulifunguliwa na mama yake Frank na kukutana uso kwa uso na Penina. "ooh mwanangu hujambo?" akauliza mama yake Frank. "sijambo mama shikamoo." akasalimia Penina "marahaba karibu ndani." mama yake Frank akamkaribisha Penina. "Asante mama ila nataka nikufanyie surprise." Penina akamwambia mama yake Frank. "hii ipi tena mwanangu usije ukaniue kwa presha." akaongea mama yake Frank, na Muda huo huo baba yake Frank naye akajitokeza sehemu pale na kuungana na mama yake Frank. Penina alisogea pembeni na hapo hapo Frank akajitokeza mbele ya Wazazi wake. Mama yake Frank alijikuta akishindwa kuongea na kumrukia Frank kwa furaha isiyo na kifani. Frank pamoja na Wazazi waliingia ndani huku wakiwa na furaha tele kwa kumuona tena Frank ambaye alitoweka kwa siku kadhaa. Lakini kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kujua ni nini kilimtokea Frank. Frank ilibidi awaeleze kilichomtokea mwanzo mpaka mwisho. Kila mtu alihuzunika kwa hicho kilichomtokea Frank. Lakini pia Penina aliwaeleza pia kilichomkuta kaka yake Nolan na Mpaka Muda ule kaka yake alikuwa bado yupo hospitalini. Lakini hata hivyo furaha ilirejea upya usoni mwa Penina pamoja na Wazazi wake Frank baada ya kumuona Frank kwa Mara nyingine tena. Frank alienda kuoga na kubadilisha nguo Zake zile zilizochakaa na kuvaa nguo zingine nzuri ambazo ziliendana vizuri na yeye. Frank aliondoka na Penina na kuelekea moja kwa moja mpaka Katika hospital aliyopo Nolan kwa ajili ya kumjulia hali. * Lakini kumbe Katika hospital ile, Nolan baada ya kujua kuwa baba yake ndio alimfanyia mchezo ule. Nolan hakubaki tena pale hospitalini alitoroka bila hata kuruhusiwa na daktari na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwao. Penina na Frank baada ya kufika hospitalini pale. Walistaajabu kuambiwa kuwa Nolan hayupo pale hospitalini na hawajui alipoelekea. Penina na Frank waliondoka na kuelekea nyumbani kwa kina Penina wakihisi labda Nolan ameelekea huko. Na kweli baada ya kufika nyumbani kwa kina Penina walimkuta Nolan akiwa ameketi nje ya geti lao huku akionekana kuwa na mawazo tele. "Nolan vip ndugu yangu mbona mawazo tele?" alikuwa Frank akimuuliza Nolan baada ya kumkaribia. Nolan alinyanyua kichwa chake na hakuamini baada ya kumshuhudia Frank akiwa amesimama mbele ya macho yake akiwa pamoja na Frank. "oooh Frank ni wewe?" akauliza Nolan kama vile haamini, Kisha akanyanyuka na kumkumbatia Frank kwa furaha Sana. "nimefurahi Sana kukuona tena Frank, hakika wewe ndio furaha ya mdogo wangu Penina karibu tena Frank." akaongea Nolan kumuambia Frank. Na hapo hapo Nolan akamtaka Frank amueleze ni nini kilichomkuta mpaka akatoweka Muda wote ule. Frank Bila kusita alimuelezea Nolan mkasa mzima uliomkuta wa kutekwa na watu asiowafahamu. Nolan alimhurumia akampa moyo na kumtaka ajikaze kwasababu wana vita nzito mbele yao. Lakini pia Nolan akawaelezea jinsi baba yake mzee Joel alivyomtumia watu waje wamuue kwasababu ya kutetea penzi La Penina na Frank. "ina maana baba anataka akuue?" Penina akamuuliza Nolan kwa mshangao. "ndio nadhani ndio nia yake kwasababu ameona mimi ndio niliyeamua kusimama na kulitetea penzi lenu." akaongea Nolan kwa huzuni Sana. Penina pia alihuzunika Sana mpaka machozi yakaanza kutiririka usoni mwake baada ya kugundua baba yake ndio alipanga njama ya kummaliza Nolan. "lakini msijali kuweni na amani mimi nawakikishia lazima mtaoana na kuwa mume na mke." akaongea Nolan kwa kujiamini. "tunashukuru kusikia hivyo hata sisi tutakuwa pamoja na wewe kwa lolote lile." akaongea Frank naye kwa kujiamini. "Sasa sikilizeni niwaambie, nataka niwasafirishe muende mkakae nchi nyingine kwa miezi miwili alafu mimi nitabakia hapa Tanzania nikifanya taratibu za nyie kufunga ndoa na kila kitu kikiwa tayari nitawajulisha na mtarejea Tanzania kwa ajili ya kufunga ndoa yenu." akaongea Nolan kumwambia Frank na Penina. Bila kipingamizi chochote Penina na Frank walikubaliana na wazo la Nolan na kilichotakiwa ni kwenda kujiandaa na kuondoka. "ngoja bas nikajiandae Mara moja." akaongea Penina, lakini Nolan akamzuia na kumwambia. "usiingie ndani tena, sitaki uonane na baba kuanzia Sasa kila kitu utakachahitaji nitakutimizia mimi, katafuteni hoteli yoyote mkae hapo mkijianda na kama na pesa au kitu chochote mtaniambia mimi." aliongea Nolan kwa msisitizo. "ok tumekuelewa tupo pamoja." akajibu Frank Kisha wakaondoka pamoja na Penina. Nolan alinyanyuka pale chini akagonga geti na kufunguliwa na mlinzi na bila kusema kitu Nolan akaelekea moja kwa moja mpaka sebuleni ambapo alimkuta baba yake mzee Joel akiwa ameketi huku akionekana kuwa na mawazo. "Niko sambamba na wewe kwa chochote kile utakachokifanya, sitajali kama wewe ni baba yangu au nani wangu lakini nachotaka utambue Frank lazima amuoe Penina." akaongea Nolan kumwambia baba yake Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake bila kusikiliza baba yake atasema nini. "wewe lazima nikuue wewe hata kama mimi ni baba yako huwezi kuniingilia Katika mambo yangu." akajisemea mzee Joel na kutoka nje kwa kasi mpaka kwenye gari Lake. Mlinzi alifungua geti na moja kwa moja mzee Joel akatoka kwa kasi mpaka Katika hospital waliyolazwa wakina Zaza. Mzee Joel alishuka kwa kasi kwenye gari Lake na kuelekea mpaka Katika chumba walicholazwa wakina Zaza. "Zaza mlifanya nini mbona mmeniangusha kias hiki?" akaongea mzee Joel kwa jazba. "mzee Joel yule mwanao ni hatari Sana hebu ona tulivyovunjwa vunjwa." akaongea Zaza huku akionesha jinsi walivyopigwa na Nolan . "ni bora mlivyopigwa kuliko hichi kingine kilichoibuka." akaongea mzee Joel na kushika kiuno. "nini tena mzee wangu?" akahoji Zaza huku akiwa anajinyanyua pale kitandani alipokuwa amelala. "Frank amerudi" akajibu mzee Joel na kuwafanya wakina Zaza washangae. "yaani kwa kweli mmeniangusha Sana alafu isitoshe Nolan ameshaanza kuota mapembe na kama nyie mmemshindwa bas itabidi nitafute wababe wengine zaidi yenu na nyie lazima nitawaua pesa niliyowapa ni nyingi Sana lakini hakuna cha maana mlichokifanya pumbavu nyie. " akaongea mzee Joel kwa hasira Kisha akageuka na kuondoka. * Penina na Frank waliwasili kwenye hoteli moja ya kifahari na kufanya taratibu zote na kuchukua chumba kwenye hoteli Ile na kulipia kukaa hapo kwa siku tatu. Lakini Frank aliwapa taarifa Wazazi wake ya jinsi mipango inavyofanyika hivyo akawataka wasiwe na hofu yoyote kuhusu yeye.* Upande wa Nolan yeye alipanga lazima amfundishe adhabu baba yake kwa namna yoyote ile. "Wewe ni baba yangu ndio sikatai, umenitunza vizuri, umenipa elimu ya kutosha Sawa, lakini kwa unyama huu unaotaka kuufanya hakika sitakuacha lazima nitaenda sambamba na wewe." alijisemea Nolan akiwa chumbani kwake akipanga mipango yake. Lakini pia Nolan aliapa kama asipofanikisha ndoa ya Frank na Penina bas atajiua. ............. Itaendelea

No comments:

Post a Comment