Simulizi ya maisha. KOSA
Sehemu ya pili
Ilipoishia.
Niliamua kujitoa kuelekea kwenye chumba cha shemeji, ni kiwa na ghadhabu kali, lakini sasa nilipokelewa na mtazamo mwingine.
Naam! unapoamua kufanya jambo lifanye bila kusisita sita maana uwezi jua uwenda kujishauri kwako ndio ikawa unaongeza tatizo badala ya kutatua tatizo.
NA HII NI SEHEMU YA PILI
Mtoko wangu ulikuwa wa kawaida lakini sasa ulikutana na dhahama kali kabisa, maana mwili wa dada ulikuwa upo nje tayari ya chumba chake. Macho yangu yakiweza kuona kile ambacho Shemeji alichokuwa akikifanya kwa dada. Aibu hata kidogo hakuwepo kwa mwanaume, alizidi kumpolomeshea matusi ya nguoni. Na hakuna aliyesalimika katika ukoo wetu. Hakujali uwepo wangu pale, kana kwamba ungemuogopesha, haikuwa hivyo alizidi kuongea kwa ghadhabu sana, na hata ile ghadhabu niliyokuwa nayo ilipoa, nikibaki mtazamaji.
Niliyapima maneno yale yalikuwa yakimtoka, kiukweli shemeji aliongea sana na kwenda mbali kabisa. Huku akishitumu familiya yetu ndio chanzo cha mwanae kushindwa kuongea. Suala lile liliniuma sana, japo kuwa lilikuwa geni masikioni mwangu, maana kwa muda wote sikuwahi kujua chanzo cha ugomvi wao usio kwisha kila siku. Kumbe ilikuwa kwasababu ya mtoto wake kushindwa kuongea.
Ni kweli kabisa yule mtoto mdogo, hakuwa akiongea kabisa, nami sikuwahi kufatiria habari za yule mtoto, na si kuwa na jua juu, ni umri upi sahihi wa mtoto kuanza kuongea. Lakini ninachokumbuka sikuwahi kumsikia akiongea katika siku nilizokaa nae. Na vile sikuwa mtu wa kushinda nyumbani, mambo mengi juu ya yule mtoto si kuwa na yafahamu.
Naam!, maneno ya shemeji yaliniingia sana kwa kiasi kikubwa, lakini ujasiri ulinishika, nikimuendea shemeji na kumtuliza jazba aliyokuwa nayo, alinielewa, kutokana na maneno yangu ya ushawishi, japo nilikuwa na hasira sana, ila sikutaka kuionesha wazi. Kwasababu nilikubali kuwa mtumwa kwake, ili kumnusuru dada yangu.
Kutokana na usiku ulikuwa umeshaenda sana, nilishauri shemeji akapumzike, kisha kesho tuweze kuangalia taratibu za kupata ufumbuzi juu ya suala la mtoto, wakati huo nilimsihi sana dada, achukulie jambo lile kawaida maana hakuna kitu kisicho kuwa na changamoto, na kwenda mbali zaidi kwa kumpatia misemo kadhaa wa kadhaa kuhusu ndoa. Baada ya muda maneno yangu yalimwingia sawa sawa. Hakuwa na kinyongo tena alirudi chumbani kwake kulala. Na mimi nirejea chumbani kwangu.
Nilimeza funda kadhaa za mate kutokana na hasira iliyokuwa imenikaba koo, baada ya yale mafunda ya mate kupita kwenye koo langu, sikuchelewa nilijibwaga kitandani. Kichwa changu kikaingia katika tafakari nzito kuliko hata ile ya awali, jambo lilionekana kuzua jambo. Ghafla taswira ya mpwa wangu ikaja kichwani mwangu. Akinitazama kisha akiachia tabasamu lake la kitoto, kabla ya kuniachia maswali mazito.
Kwa umri alikuwa nao yule mtoto alitakiwa kwa sasa aweze kuyatamka maneno ikibidi hata kwa kukosea, sasa kwanini ashindwe kuongea? Nilijiuliza sana lakini majibu hayakuwepo kabisa. Mwishoe nilianza kumlani Mungu kwa kutupatia mitihani katika maisha kwenye familiya yetu, maana haukuwa mitihani midogo kabisa, ndugu msikilizaji.
Usiku ulikuwa mrefu sana kwa upande wangu, japo nilifanikiwa kuupata usingizi, pasipo mwenyewe kujitegemea. Lakini ulikuwa kama wa manyanyaso. Ndoto za ajabu ajabu ziliutawala ule usingizi wangu. Zikiniachia tafsiri mbaya kana kwamba zilikuwa zinatambua huenda kunajambo baya lilikuwa linakuja kunitokea. Sikuwahi kuamini juu ya ndoto hata siku moja na nilipojua ni ndoto tu nilizipotezea na sikutaka kuzijadili kwenye kichwa changu.
Hatimaye mwanga wa jua ulipenya vizuri nilipokuwa nimekilalia kitanda, hapo sasa mwili wangu ulikuwa umeshakinai. Nilijinyosha nikajitoa kwenye kitanda, taratibu nikaliendea taulo, kisha nikajifunga vizuri kwenye mwili wangu nalo likaa vyema. Taratibu niliubeba mswaki wangu pamoja na sabuni. Na kuelekea bafuni kuoga. Sikuchukua muda sana nililejea chumbani. Nikibadili nguo, pasipo kuwa na wasi wasi. Mara nilisikia mlango wangu ukigongwa. Namna ya ugongwaji ule ulinishitusha kidogo.
Nilijivuta nikauwendea mlango, kufungua tu nikapokelewa na sura ya Shemeji, alionekana wazi kabisa hakuwa sawa kabisa katika mtazamo wa kawaida tu.
Sikuonesha tofauti kwa upande wangu, nilipokea ujio wake, na kisha kuanza kuongea nae, hakuwa na jambo jipya sana. Jambo lilikuwa lile lile, sasa hakinihitaji nijiandae haraka maana wao walikuwa tayari wameshajianda ili kuelekea hospitali. Shemeji alikuwa amedhamiria sana ndugu msikilizaji hakuwa na masihara hata kidogo. Nami sikutaka kuleta kipingamizi kutokana na usiku tu mimi ndio nilishauri jambo lile. Nilimuomba shemeji kumalizia kujianda nae alikubali.
Nilijitoama ndani, japo nilikuwa nimemaliza kuvaa kila kitu na sikuwa na hitaji la maana kule chumbani, lakini niliamua kurejea tu chumbani. Hofu ilionekana kuja upande wangu, bila hata kuelewa ilikuwa ikitokea wapi?. Mwili wangu nao hakuchelewa kupata jacho ijapokuwa muda mfupi nilikuwa nimetoka kuoga, lilinivuja kweli. Zilipita kama dakika tano nikiwa mule chumbani, kabla ya kujitoa maana sikuona nini kilichokuwa kinanifanya kuendelea kukaa ndani.
Nilijitoa nje na sasa nilikaribishwa na muonekano wa dada, akiwa amembeba Nasri. Muonekano ambao nao ulianza kunijengea shaka. Dada alionekana ametawalia na hofu kuliko kawaida. Sikujua kama ile hofu inatokea wapi kwa upande wake. Nilimua kumkabili kwa kumpa salamu, alitikia kivivu vivu kuliko kawaida yake, hakuwa yule niliyokuwa nimezoea kabisa, alionekana kuna jambo nzito lipo kwake tofauti na lile.
Tulitoka ndani ya nyumba, na kupokelewa na gari dogo ambalo shemeji alikuwa ameshalianda kwa kumpigia dereva wa tasi ambaye alikuwa akifahamiana nae na mara nyingi huwa anahusika sana katika safari zake. Ilikuwa kawaida ya shemeji japo kipato chake kilikuwa cha kati lakini hakuwa akipendelea kusafiri na daladala.
Ilinibidi mimi nikae mbele shemeji na dada walikaa nyuma. Safari ikaanza ya kutokea pale nyumbani, safari ambayo ilikuwa imetawaliwa na kimya kingi, muungurumo wagari ndio ulikuwa ukifukuza kimya kile, japo ilikuwa asubuhi lakini tulikumbana na foleni njiani, lakini tuliweza kufika katika ile hospitali ambayo nadhani wao walikuwa wakipenda sana kuitumia kutika huduma za kimatibabu, baada ya masaa kama mawili njiani. Tulipokelewa na kukaribishwa kwa ukarimu sana na wauguzi wa pale. Walionekana kumfahamu fika shemeji mimi nikionekana mgeni.
Shemeji sijui alikuwa mtu wa namna gani? Sijui alikuwa akifanya vile kutokomoa au la. Maana baada ya kuenda kumuona na daktari muda mfupi alituacha mimi na dada pale nje, alirejea na kutaka mimi na dada pamoja na yeye, tuelekee kwenye chumba cha daktari. Na mimi sikuwa na hiyana hata kidogo. Nilikubali kulekea ndani ya chumba kile.
Baada ya kufika shemeji ndio alikuwa mzungumzaji mkubwa, katika maungumzo na yule daktari, huku dada kazi yake ikiwa kujibu maswali aliyokuwa akiulizwa daktari, ilikupata maelezo ya uhakika kuhusu hali ya mtoto. Baada ya maelezo ya kutosha daktari, alinitaka mimi nitoke nje kisha abaki na dada na mtoto, pamoja na shemeji. Mimi nilifanya kama vile daktari yule alivyokuwa akisema.
Hakuchukua muda sana dada na shemeji walitoka kwenye chumba cha daktari. Nikiwa sifahamu ni jambo gani lilikuwa limepatikana. Nikiwa nimetulia kimya shemeji alianza kusemeshana na mimi, yakuwa tusubiri majibu ya daktari, huku akisema ‘leo ndio chungu na mbivu zitajulikana’, kisha akirudia lile neno lake la kuita familiya yetu ni washirikina katika hali ya chinichini ambayo hakudhani uwenda mimi nilikuwa nimelisikia neno lile.
Nilitulia kimya, nikimtazama dada nae alinitazama, tuliendelea kutazamana kwa muda kiasi, kabla ya kuitwa kuelekea kwenye chumba cha daktari. Majibu ya jambo lile yalikuwa tayari hadharani.
NDUGU, na kusihi tena katika maisha yako unapotoa maneno yafanyie tathimini kabla ya kuyatamka, maana kwa wakati mwingine maneno yako mwenyewe yanaweza kukugharimu. Na hii ilikuwa sehemu ya pili ya simulizi yetu ya maisha je nini kitaendelea?
No comments:
Post a Comment