Simulizi ya maisha. KOSA. πŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌπŸ‘‡πŸΌ Katika maisha kwa namna yoyote ufanyapo jambo ni vyema ulipime mara mbili kabla ujaamua kulifanya, wakati mwingine unaweza kuwa humo ndani ya kosa ambalo kamwe hautakuja kulisahau maana linaweza kukutesa na kujutia katika maisha yako daima. NA HII NI SEHEMU YA KWANZA! Kiupepo kilichokuwa kinatoka katika feni ambalo lilikuwa limelekea sambamba nilipokuwa nimeulaza mwili wangu kutokana na uchovu, niliokuwa nao, ilinifanya nijikunje kama samaki. Wakati huo ule upepo uliendelea kunyanyasa mwili wangu pasipo hata kujua ni jinsi gani nilivyokuwa naumia, lakini nisingeweza kuuzuia maana kulizima feni ambalo lilikuwa likitoa kile kiupepo ingeleta ghasia ya mbu sumbufu ambao wangeleta maumivu makali kwenye mwili wangu, na hata kunisabishia kupata homa. Hali ile ya upepo ndio ilikuwa ikiwafukuza na kuniepusha na mbu wale. Nilivuta shuka ilikuweza kuifukuza baridi lilikuwa likiletwa na upeo ulikuwa unatoka kwenye kifaa kile, lakini shuka alikufanya kukipoteza kibaridi kile. Usingizi sasa haukupata nafasi kama vile awali mwili wangu ilivyokuwa umeupania kutokana na kuokosa kwa muda mrefu. Hapo napo mawazo nayo yakaona ni wakati sasa wa kuanza kunisurubu yakienda sawa na ubaridi ule. Naam! Yalifanikiwa katika hali ya juu na kuniacha na maumivu, kabla ya kuongezeka zaidi katika usiku ule. Ilitokana na vulumai niliokuwa nikilisikia upande wa pili na ubaya haikuwa mara ya kwanza kuisikia hali ile ambayo ilishaanza kujenga mazoea ndani ya kichwani mwangu. Sikuwahi kuipenda hali ile hata kidogo, japo nilishaanza kuizoea katika namna ambayo haikuwa na zuilika. Nilipima uzito wa jambo lile, uthubutu wa kutaka kufanya jambo ukanipotea, nisingeweza kufanya kitu kwa nyakati kama ile. Japo nilikuwa nikiendelea kuzisikia sauti za maamivu ambazo zilikuwa zikimtoka dada yangu. Nilipokumbuka ule ugomvi ulikuwa wa mume na mke, hapo ikawa ngumu mimi kuingilia. Na kwa vile nilikuwa nikimuheshimu sana shemeji, niliona si jambo la busara kuenda kuingilia ugomvi ule katika muda kama ule. Niliendelea kupambana na maumivu makali nikiwa pale kitandani. Na hata kutoa shutuma kali sana dhidi ya Mungu. Kwa nini alikuwa ameifanya maisha yetu katika namna ile, namna ya utegemezi?. Shida ndio iliyonifanya niwe eneo lile na kama isingekuwa shida za maisha ningeendelea kubaki kijijini na nisingefika katika nyumba ile. Na kamwe nisingeweza kuisikia hali ile wakati nipo mbali na pale. Ni kweli shida zilikuwa zimetawala sana kwa upande wetu, kutokana na uwezo mdogo wa familiya yetu. Japo mimi nilikuwa mtu pekee nikitegemewa katika jicho lingine la kuleta ukombozi katika familiya yetu, lakini juhudi zangu ziligonga mwamba. Miaka miwili tu ilikuwa imepita tangia nimalize elimu yangu ya kidato cha nne, huku matokeo yangu ya mtihani wa mwisho ya kishindwa kutolewa kutokana na kushindwa kulipia ada ya mtihani. Elfu hamsini ilikuwa nyingi kwa wakati huo, si mama si baba wote walishindwa kunilipia wangewezaje kunilipia? Miili yao ilikuwa imeshachoka katika mchoko wa kiutu uzima. Mimi pekee ndio nilikuwa ni kila kitu kwao. Katika kuwatafutia chakula na mahitaji mengine. Nani angeweza kufanya vile? Kaka Shukuru, mkubwa lakini akili yake ilikuwa imeshatekwa na mwanamke mmoja uluguruni, hata kujali kama ana wazazi hilo hakuwa akilitambua, thumuni yake kuitoa ilikuwa ngumu, sio kuitoa tu hiyo sura yake kuonekana kwetu pia ilikuwa nadra. Kwa namna yoyote hakuwa upande wetu alishasahau kama yeye ni kaka wa familiya na familiya ilikuwa ikimuhitaji kwa kiasi kikubwa. Utekaji ule wa yule mwanamke, kaka Shukuru hakuwa hakifurukuta hata kidogo. Aah!....achana na kaka Shukuru, huyo ndugu yangu Masumbuko ubishoo mwingi kulima awezi, kijijini kunataka kulima angewezaje kulisha familiya? Yeye amepasaliti nyumbani anashinda mitaani tu. Basi mimi ndio nilikuwa muhanga wa hili, na hata nilipoamua kuja mjini, baada ya kuhadiwa kutafutiwa kazi na Shemeji. Kweli kazi nilikuwa nimeipata lakini sasa sio kazi, tu kila kukicha masikio yangu yamekuwa shahidi mkubwa wa kusikia kile ambacho dada yangu anakipokea. ____________ Nikiwa kitandani pale, taswira ya dada Asha ilinijia, ambaye sasa jina la Asha halikuwa na nafasi tena. Mama Nasri ndio lilikuwa limevaa husika wake. Ni huyo Nasri ambaye kila siku alikuwa akigeuka mtazamaji wa masumbwi ambayo baba na mama yake wakiyavulumisha kila baada ya siku mbili. Lakini kutokana na udogo wake, hakuwa na jinsi alikuwa akilia katika kilio ambacho kwa wakati mwingine kilikosa mbembelezaji, na kosa wa kumahidithia maumivu yale aliyokuwa akiyapata kutokana kile alichokuwa anakiona. Umri wake ulikuwa mdogo sana, mwaka na nusu, hata neno mama lilikuwa likimshinda, sembuse kuwamsimulijia wa kile alichokuwa anakiona. Taswira ya dada sasa ilikuwa imeinijia na kuanza kuninyanyasa, nilikumbuka enzi zile ambazo tulikuwa tukifurahi wote. Tabasamu lake la kitoto lilikuwa halinitoki kwenye kichwa changu. Ndio halikuwa likitoka japo Mungu alikuwa ametunyima utajiri lakini si kutunyima uzuri, nadhani katika wasichana warembo pale kijijini dada yangu alikuwa akishika nafasi ya kwanza, jambo ambalo lilikuwa linanifanya nipate upinzani sana kutoka kwa vijana wengi wa kijijini kile. Nami sikuwa nikikubali dada yangu achukuliwe na watu wa kijiji kile maana nisingeweza kukaa vizuri pale kijijini. Nilihakisha na weka ulinzi wa hali ya juu kana kwamba nilikuwa si ufahamu ule msemo wa mwenye dada hakosi shemeji, lakini kutoka na kuzifahamu tabia za wavulana wengi wa pale kijijini. Nilikuwa nikifahamu wazi huenda dada yangu, angeweza kukumbana na matatizo akiwa na vijana wa kijijini pale. Na hata ilipokuja posa ya dada yangu kuolewa na mwanaume wa mjini, mimi sikuwa na kipingamizi nililidhia kwa moyo mweupe, japo kuna wakati nilikuwa nikishindana na fikra zangu, nakumbuka kabla ya jambo lile, nilimwita dada ya kusema naye, kwa hali ya juu katika mazungumzo ambayo, nilikuwa nihitaji kufahamu fika juu ya mwanaume wake. Japo nilikuwa muoga kugusia alikutana vipi, nikihofia kuingilia mambo ya ndani ya dada, lakini nilijikaza kisabuni nikamkabili dada. Haikuwa kwa lengo baya la hasha katika ule utashi wangu wa kutaka dada yangu awe katika mikono salama. Kutokana na kunihakikisha alikuwa ni mwanaume wa tofauti kuliko nilivyokuwa nikimuhekea dosari. Hatimaye nilikunjua roho yangu, na kulisimamia suala lile kwa hali ya juu. Katika kuenzi ule msemo wa mwalimu wangu moja wa kiswahili ya kuwa kunjua roho tufanye biashara. Nami roho yangu ilikuwa jeupe katika kufanya biashara ile. __________ Niliyakumbuka yote nikiwa kitandani pale, na hapo sasa usingizi hakuwa na nafasi, ubaridi ule endelea kunisurubu, ulinisurubu vya kutosha sauti ya dada nayo haikuwa nyuma safari hii ilizidi kuongezeka kwenye ngoma za masikio yangu na kuleta dhoroba, wazi ilioekana hakikuwa kipigo kidogo ambacho alikuwa anakipata kutoka kwa mwanaume wake, tangu nilipofika pale sasa ilikuwa imezidi. Hisia kali ilinipitia na nilipokumbuka kuwa yule ni ndugu yangu, suala la ushemeji niliweka pembeni, ‘’ni heri ni kose kitu kukilo kumpoteza dada yangu ambaye nilikuwa nikimpigania”. Nilijisemea kimoyo moyo wakati huo mwili wangu hakuwa tena juu ya kitanda. Niliamua kujitoa kuelekea kwenye chumba cha shemeji, ni kiwa na ghadhabu kali, lakini sasa nilipokelewa na mtazamo mwingine. Naam! unapoamua kufanya jambo lifanye bila kusisita sita maana uwezi jua huenda kujishauri kwako ndio ikawa unaongeza tatizo badala ya kutatua tatizo. Na hiii ilikuwa sehemu ya kwanza ya simulizi yetu ya maisha, je nini kitaendele?, Ndio tunarudi tena usikose hapo kesho saa kumi na mbili jioni.

at 5:16 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top