Thursday, December 7, 2017

NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 26 Kwa mujibu wa shehe, aliniambia hayo yote aliweza kuyakamilisha ndiyo maana Rabia alionekana mzima na akanionya nisimlaumu kwa lolote, wala nisimkumbushe Jay Love. Akasema; japo Jay Love tulimfunga nyumbani kwangu lakini kwa ile tattoo aliyokuwa nayo Rabia iliweza kumuendesha kama rimoti au rada ndiyo maana hata aliweza kunifunga. Nilimuuliza ule mzimu ulipokwenda, akasema kuwa ni kawaida ya mizimu kama ikiwa imenaswa duniani basi inaweza kukaa siku saba tu na itapotea na itarudishwa kuzimu na malaika anayesimamia roho za wafu huko kuzimu. Swali la muhimu likawa ni je, kweli nina masaa machache kabla ya kufa kama Jay Love alivyonilaani? “Ukweli sijui hata kidogo! Tusubiri kudra za Mwenyezi Mungu,” alinijibu yule shehe na kuondoka zake. Nikarudi ndani, nikakuta Rabia akiwa ameniandalia maji ya moto ya kuoga, akanipeleka hadi chooni na kuniogesha kama mtoto mdogo. Tukiwa tunaoga niliweza kuona ile tattoo niliyoambiwa na shehe, lakini ilisomeka Jay Loveness ikiwa imeongezewa ‘-ness’ mwishoni, nikajua Shehe ndiye alifanya hivyo, nikamtest Rabia nikimuuliza maana ya ile tattoo akaonesha kushangaa eti hakujua kama ilikuwepo mwilini mwake. Nilimtoa wasiwasi na tulielekea chumbani kukumbushia penzi letu, “Ooh Jinsi gani nilimmisi!” Kila kitu kilikuwa kipya, niliona jinsi alivyokuwa na furaha zaidi ya kuwa na mimi kuliko hata siku zote za maisha yetu ya mapenzi. Tuliongea na kupanga mengi, mpaka akalala kifuani kwangu. Maskini alikuwa hajui kama nina masaa machache nitakufa na kumuacha. Lakini hata hivyo nilifurahi kuwa hata kama nikifa nitakuwa nimeacha kila kitu sawa. Sikusahau kuandika urithi wangu wote nikimpatia kwa Rabia najua inahitaji moyo lakini mimi niliamua kufanya hivyo na sitaki maswali. NILIANZA KUHISI JOTO KALI, NIKAFUMBUA MACHO LAKINI NIKAMA VILE SIKUWA NIMEYAFUNGUA KWA KIZA KIZITO CHA SEHEMU NILIYOKUWEPO, KWA MBALI NILIONA MIALE YA MOTO, MASIKIO YANGU YALIYOKUWA NA GANZI SASA YAKAFUNGUKA NIKASIKIA KILIO KIKUBWA MNO

No comments:

Post a Comment