Home → simulizi
→ NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 23
Tofauti na mawazo yangu wale maafande walinitazama usoni, wakacheka kisha wakaondoka zao wakaniacha nikiwa nimening’inia pale dirishani nikiwa sielewi walichokifuata.
Niliwaona wakipotelea chumba kimoja wapo, lakini macho yangu makali yaliweza kuona mmoja wao akiwa ameshika gazeti lililoandikwa; MWANDISHI AKUTWA NA USHIRIKIN.. (hapa maandishi yaliyofata yalikuwa hayaonekani kwa sababu lile gazeti lilikuwa limekunjwa upande huo, lakini niliweza kujua herufi ya kumalizia hapo ni ‘A’ na kuwa USHIRIKINA na si jingine.
Ukiachilia hayo cha zaidi niliweza kuona lile gazeti likiwa na baadhi ya picha za chumbani kwangu za ile pentagram na maandishi ya Kiarabu, lakini zaidi niliona picha yangu wameiweka kwa ukubwa.
‘Umeshawahi kuona paparazzi anaandikwa?’ Basi siku hiyo na mimi nilikuwa gazetini nikajua fika kuwa kuna vyombo vingine vya habari vilikuwa vinafuatilia sakata langu na wana hamu kweli ya kuniona maana nilikuwa habari ya mjini na kupitia mimi wameuza magazeti kibao.
Hapa nikajiongeza kuwa kumbe wale maafande walikuja kuhakikisha kama kweli ni mimi ndiye niliyeandikwa gazetini na si kunifungulia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: