NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 22 Siku hiyo ni moja ya siku chache katika maisha yangu niliyoshuhudia masaa yakikatika kama upepo. Sikuweza hata kidogo kutuliza akili na angalau ilipotulia niliwaza ni jinsi gani nitaiacha dunia ambayo japo ina machungu kibao ndani yake lakini bado ilikuwa ni tamu na sikutaka kufa kijana hivyo. Nilianza kuwaonea wivu wenzangu ninaowaacha nyuma wakiendelea kufanya kila kitu kwa uhuru, nilijihisi mnyonge na hii yote ilitokana na mimi kujua lini nitakufa. Laiti kama kila mtu aliyekuwepo pale selo angejua atakufa lini nina uhakika wangekuwa wanyonge kama mimi. Ama kweli dunia ni ya wenye uhai, hapa ndiyo nikawaza jinsi nikifa watu wangapi watahuzunika, nikakumbuka jinsi watu wa mochwari watakavyofurahi tena kama maiti yangu itaenda kwenye yule mtu wa mochwari niliyemuandika vibaya kwa kuuza viungo vya maiti, si ndio atanikata hadi sehemu zangu za siri na kuzigawa hata bure. Niliogopa, lakini nilijipa moyo ambao hata hivyo sikudumu dakika hata moja kwa kuwa nilifikiri jinsi ambavyo nitazikwa huku mke wangu akiwa hanitambui kama mimi ni mumewe. Nikiwa katika dimbwi hilo la mawazo, kuna afande mmoja wa kike alikuja na afande mwingine wa kiume hadi pale kwenye dirisha la selo akaita; “Denis!” nilikaa kimya kwa sekunde chache kusikilizia. Huenda kuna mtu mwingine mle ndani alikuwa ana jina kama langu lakini nikaona kimya. Ile sauti ikaita tena, nikaona huu labda ni uhuru wangu sasa, au labda pengine kuna mtu alikuwa ameniwekea dhamana na niliitwa kwa ajili ya kurudi nyumbani. Niliitikia haraka na kusogea pale mlangoni.

at 12:46 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top