NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 19 Nilihojiwa kwa kina nikitakiwa kueleza mwili wa huyo mtu ninayedaiwa kumuua ulipo kwa sababu walishangaa kusikia harufu kali, lakini kila waliposachi mle ndani hawakuona kitu. Ni wazi kuwa kwa sababu hawakuwa na macho ya kuuona mzimu wa Jay Love kama mimi na yule shehe, mwingine labda ni Rabia. Nikiwa hapo polisi nilivumilia vipigo, na vibano mfululizo nikitakiwa angalau kumtaja niliyemuua, lakini jibu langu lilikuwa moja tu, kwamba sijaua mtu yoyote na kama wakimuona wanifunge kwa hilo. Mtu wa kwanza kuja pale kituoni ili kunihangaikia utaratibu wa dhamana alikuwa ni bosi wangu, Mr. Derick aliyeonekana kuwa na wasiwasi kweli juu ya tukio lililonikuta. Nilizungumza naye kwa muda kidogo kupitia geti la selo kisha akaingia ofisini kwa mkuu wa kituo cha polisi na alipotoka aliondoka zake na wala hakurudi tena. Mtu wa pili alikuwa ni Shehe ambaye alijua ukweli mzima wa tukio naye alifika pale polisi kama bosi wangu, akaingia na kuondoka zake kimyakimya. Usiku uliingia nikalala wakati huo nikiwaza kuwa nimebakiza siku 8 tu za kuishi kwa mujibu wa Jay Love lakini kwa kuwa amelala ufu nyumbani kwangu, sikujua kama bado aliendelea kunihesabia hukohuko ahera au lah! Nikawa sielewi, nikasubiri nini kitatokea nikapitiwa na usingizi.. Itaendelea..

at 1:01 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top