NILIVYOFANYA INTERVIEW NA LUSIFA 18 Sikujua chochote kuhusu alichofanya Rabia, mpaka nilipofika nyumbani kwangu. Nakumbuka nilipofika tu nilikwenda moja kwa moja kuhakikisha mzimu wa Jay Love kama upo pale chini, kweli niliukuta hali yake ikizidi kuwa mbaya tena saa hiyo wale funza wakionekana kumtafuna zaidi na kutoa harufu kali mle ndani. Hapa ndipo ghafla nilisikia geti langu likigongwa kwa nguvu, nilipofungua nilikutana uso kwa uso na askari polisi si chini ya sita wengine wakiwa kwenye gari yao ya Difenda, Rabia akiwa katikati yao akijitahidi kujificha nisimuone. Sikujua kosa langu ni nini, lakini walinionesha warrant na kuanza kupekua ndani kwangu, katika maongezi waliweza kutambua kama mimi ni mwandishi wa habari ‘paparazi’. Mmoja wao aliyeonesha kuwa msomaji wa kazi zangu aliniambia kuwa kuna taarifa kuwa ninaishi na maiti nyumbani kwangu hivyo walikuja kunikagua. Wakati anazungumza hivyo kuna afande mmoja aliyeingia ndani, alitoka nje mkuku huku ameziba pua na mdomo akawaita wenzake na wote waliingia ndani haraka, nilijua watakuwa wameisikia ile harufu ya mzimu wa Jay Love na walidhania ndiyo haswa maiti wanayoitafuta. Walihangaika sana lakini walishindwa kuona chochote zaidi ya michoro ya ajabu kama vile ile pentagram iliyopo pale chini nyumbani na maandishi ya Kiarabu yaani ile namba 9. Hata hivyo hiyo haikuwa salama yangu badala yake wakanitia pingu na safari ikaishia kituo cha polisi Wazo Hill nikihojiwa kama mtuhumiwa wa mauaji. Itaendelea..

at 1:00 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top