SUBIRA YANGU SEHEMU YA 13
Tulikuja kuamka asubuhi huku mimi mwili wote haufai kwa uchovu basi tukaingia bafuni kuoga ili safari ya kurudi nyumani ianze,..
“Baby natamani hata usiondoke jamani tushinde wote tu ndani” frank alinambia huku tukivaa nguo
“Mmh baby hata mimi sema ndo ivo inatupasa kurudi nyumbani” nilimjibu frank tukiendelea kujiandaa na safari ya kurudi nyumbani ikaanza huku kila mmoja akionekana ni mwingi wa furaha
Nilifika nyumbani na kumkuta mama akiwa sebleni na kumsalimia
“Shikamoo mama”
“Marhaba za huko utokako?”mama aliniitikia lakini akiwa mwenye wasi wasi
“Salama tu mama” nilimjibu na kuketi
“Ulienda kwa nani hadi ukaamua kulala nje ya nyumba wakati ulisema utarudi?” mama alinihoji
“Mama bwana nilikua kwenye party sasa nilichelewa kutoka nikaamua kulala huko huko”nilijibu
“Mbona glory jana alikuja kukuulizia ina mana hata yeyey hana taarifa za party”mama aliuliza huku akinikazia macho
“Aah..ye alichoka” nilidanganya
“Endelea tu kunidanganya ila jua mimi ni mtu mzima yote hayo nimeshapitia” mama alinijibu na kuinuka zake akaingia ndani
Siku zikazidi kusogea frank akamaliza chuo pale mlimani jambo ambalo lilinipa huzuni kwani nilijiona ntakua mpweke sana maana nilimzoea sana frank na kumpenda sana na kunijali kwani alinipa mapenzi yale yanayostahili na kunifanya nimsahau kabisaa Joshua..ilifika kipindi akanitambulisha kwa wazazi wake nikawa na fahanika na mim nikamtambulisha kwetu naye akawa anafahamika
Mumgu akamjalia akapata kazi kwenye kampuni ya baba yake na kuanza kujitegemea , na alikua na maisha bora sana, alininunulia gari ya kutembelea nikiwa naenda chuo na mara nyingi nilikua nalala kwake na kunipa mapenzi moto moto ambayo sijawahi kupata kwa wiki alikua ananipeleka out na ku spend sehemu mbali mbali
“Nakupenda sana mume wangu, wewe ndo kila kitu kwangu umenifunza mengi sana kwenye maisha”nilimwambia frank huku tukiwa swimming
Nakupenda pia mke wangu na sitaki kukupoteza kwani maisha bila wewe ni sawa na bure”frank alinijibu huku akinikumbatia na kuhisi faraja ilioje
Nimeandaa party nyumbani kwa wazee mpenzi jioni twende sawa mama”franl alinabia huku akiniangalia machoni
“Party ya nini baby?” nilimuuliza
“Kusherekea uwepo wako kwenye maisha yangu sababu wewe ni mtu muhimu sana”
“Mmh baby sasa ndo ufanye party jamani?”nilimuuliza
“Ndiyo mke wangu” alinijibu huku akitabasamu
Jioni ilifika na kuenda kujiandaa kama alivosema na alikuja kunipitia na kwenda kwenye hiyo party
“Baby naona aibu watu wengi” nilimwambia frank huku tukielekea ndani kwenye tukio
Tulivoinga wegeni wote walisimama na kushangilia hali ile ilinifanya nikose ujasiri kwani mmh sikutegemea kuona watu wengi kiasi kile ..tukakaribishwa na kuketi huku tukiletewa vinywaji huku nikiwaona ndugu zangu wote na kupata faraja ndipo frank akachukua kipaza sauti na kusimama na kuongea “habari zenu ndugu jamaa na marafiki kwa kukusanyika hapa leo ila leo nina kitu nataka kukifanya mbele yenu” frank alitoa kibox kidogo ambacho ndani kulikua na pete ya almasi akaja piga goti mbele yangu na kuniambia “Pls love will u merry me?”…nilijikuta nafurahi kwani sikutegemea kabisa huku nikitokwa na machozi na mimi bila hiyana nikamijibu “yes frenk I do ” watu wote walishangilia kwa vigelegele baada ya hapo tulikumbatiana huku kila mtu akionesha furaha kubwa sana
“Nakupenda sana frank mume wangu..ahsante kwa kunipa heshima hii” nilimjibu huku tukiwa tumekumbatiana huku bado machozi yakiendelea kunitoka
“Nakupenda pia mke wangu wewe ndo kila kitu kwangu,maisha yangu ni bure bila wewe” frank nae alinijibu huku akinibusu kwenye paji la uso, tulianza kucheza muziki huku ndugu na jamaa wakija tukupa hongera kwa jambo lililofanyika usikuu huu mama akaja na kunikumbatia kwa furaha pamoja na baba na kaka joakm.. “hongera sana mwanangu kwa kutupa heshima kwenye familia yetu” mama alinipongeza, frank akatoka na kwenda kuongea na afanyakazi wenzie huku nao wakimpongeza ila mim nikatoka na kwenda toilet sasa nikawa narudi kuelekea kwenye sherehe ila kuna mtu alinishika began a kunifanya nigeuke kuangalia ni nani…moyo ulistuka huku nikitoa macho ya mshangao kwani sikuamini kumouna Joshua akiwa ananiangalia huku macho yakiwa mekundu kama mtu aliekua analia
Sura yake ilionesha inafahamu kila kinachoendelea kati yangu mimi na frank…nikwa bado tunatoleana macho Joshua akavunja ukimya
“Love ndo umefanya nini mpenzi wangu?” aliniuliza kwa upole kabisa ila mimi sikuwa na jibu la kumpa mda ule
“Naomba nijibu love mbona umekaa kimya”
Joshua..ulitaka mimi nifanyaje sasa?”nilimjibu huku nikiumia moyo wangu kwani sikutaka kukumbuka ya nyuma
“Naomba twende sehemu tukaongee mpenzi hapa hutanielewa”Joshua alinambia huku akinishika mkono huku akitaka tuondoke mahali pale
Noo Joshua siwezi kuondoka mhali hapa na unajua fika kua kuna nini kinachoendelea…please siitaji kusikia uongo wako wowote naomba niache “ nilimjibu huku nikitoa mkono wangu kwake na kuondoka zangu
“Love plz nisikilize mama kwanini umeamua kuniumiza kiasi hiki kama glory?” Joshua aliongea kwa upole
“Mimi na wewe nani alimuumiza mwenzie?”nilimuuliza
“Love nisikilize” Joshua aliniomba nimsikilize
“Hapana Joshua sitaki kuongelea mambo yaliyopita “ nilimjibu huku nikiondoka zangu
SUBIRA YANGU SEHEMU YA 14
Niliondoka huku nikiwa na uchungu moyoni mwangu kwani nilianza kukumbuka mambo ya nyuma aliyonitenda Joshua nilijikuta na futa machozi huku nikielekea kwenye sherehe , kumbe frank nae alikua ana nitafuta
“Baby ulienda wapi?” frank aliniuliza
“Nilikua toilet vipi kwani?” na mim nikamuuliza
“Ni muda wa kupumzika saivi na leo una lala kwangu baby” alinambia huku tukienda kuaga wageni na kupanda kwenye gari na kurudi nyumbani kwake ila bado nilikua na mawazo sana lile tukio la kuonana na Joshua lilijirudia akilini mwangu kila saa hadi frank akaona sina raha kabisa
“Vipi mke wangu una tatizo mbona umekua kimya gafla?” aliniuliza huku akiniangalia
“Hapana nimechoka tu baby” nilimjibu kiunyonge….safari iliendelea hadi tukafika kwake huku tukielekea kuoga kutoa uchovu
“Ngoja nikuogeshe malkia wangu maana umechoka sana” alinambia huku akinimwagia maji na kuanza kuniogesha taratibu mpaka alipomaliza nay eye akaoga akaja kitandani
“Ehe nambie kipenzi changu’’ frank alinigeukia huku akianza nipapasa huku nikijua tu anataka mchezo na mimi bila hiyana nikampa haki yake baada mchezo ule ambao ulikua wa kivivu tukalala hadi asubuhi
Siku hiyo niliamka mapema na kweda home kujiandaa ili niingie chuo,nilimpitia glory nimpe lift hku njiani nikimwadisia yaliyojiri jana
“Mmh glory unajua jana yaliyonikuta?” nilianza kumpa mkanda
“Hapana nini tena best maana hatukuagana hata” glory alikaa vizuri kunisikiliza
“Unaweza kuamini Jana Joshua alikuja kwenye party?” nilimuuliza
Wee Joshua si yuko marekani au Joshua yupi tena?” glory alihamaki
“Joshua huyu huyu unaemjua wewe..jana kaja kwenye party wacha anivute anataka tuongee”
“Hee muongee nini sasa yeye si alikuacha bila taarifa sasa kimemleta nini” glory nae alinambia huku akibetua mdomo kuonesha amekerekwa na kitendo cha Joshua kuja
“Nimemgomea mim kuongea nikasepa zangu maana alilazimisha tutroke tukaongee sehemu nikamwambia hujui kua leo ni siku yangu muhimu?” niliendelea kumwadisia glory kila kitu kuhuasu jana
“Yani josua anachekesha sana,mda wote alikua wapi anasikia unavishwa pete ndo anakuja makubwa haya, wanaume hawa jamani kichefu chefu” glory aliendelea kumlaumu Joshua
“Usikubali love Joshua akuaribie bahati yako maana yeye ulimpa chance kaichezea, waache watu wanaojua kupenda wakuoneshe mapenzi yalivyo matamu, ndo maan mimi nilimbwaga maana angeniumiza moyo wangu tu” glory aliongea sana hukun akionekana kumchukia Joshua kupindukia kwa kitendo alichofanya
Tulifika chuo na kuendelea na masomo kama kawaida hadi ilipotimu mida ya jioni na kuanza kurudi nyumbani nikawa nimeegamia gari huku nikimpigia glory simu tuondoke mara Joshua huyo akaja
“Hee Joshua umefata nini hapa?” nilistuka kwanza maan sikutegemea kumuona pale
Nimekufata wewe mpenzi kwanini umebadilika kiasi hiki mama angu?” Joshua alizidi kutia huruma
“Wewe ndo umenibadilisha” nilimjibu huku nikimtumia glory sms aje tuondoke
“Sasa love kwanini hutaki nikuelezee yaliyotokea wewe unakimbilia kunilaumu tu bila kujua sababu?” Joshua ainambia huku akitaka kuniadisia
Hata ukiniadisia haisaidii chochote Joshua kwani mim ni mchumba wa mtu tayari soon nafunga ndoa so naomba uende tu na usinifate fate maana utanisababishia matatizo kwa mpenzi wangu”nilimjibu
“Kwaiyo love ndo haunipendi tena huna kabisa hisia na mimi?” Joshua alihoji ila sikumjibu
“Pls nambie kama kweli hunipendi ukinitamkia hutaonaura yangu tena au kukusumbua tena” Joshua alinambia hkuk akitaka majibu kutoka kwangu ila sikuweza kujibu chochote nikajikuta naangalia pembeni tu
“Love nakupenda sana kutafuta maisha ndo kumenifanya niwe mbali na wewe, sikuweza kukuaga kwani ingekua ngumu kwako kukubali mim niende, pia sikuweza kuwasiliana na wewe kutokana na mazingira ya kule chuoni ila kila siku lazima nikukumbuke mpenzi wangu na kusoma kwa bidii na kuahidi kurudi kwa aajili yako tuweze kupanga maisha yetu lakin umekosa subira na kuamua kuvishwa pete na mwanaume mwingine…umeumiza sana moyo wangu love lakini bado nakutafuta tu mpenzi wangu tuyaongee haya lakini naonekana na kukera najua hunipendi tena kama zamani love ila jua nakupenda sana na ntakupenda siku zote za maisha yangu nakutakia maisha mema na ndoa njema na frank” Joshua aliongea kwa machozi huku na mimi machozi yalinitoka kwani maneno yake yaliniumiza sana moyo wangu, Joshua aliondoka na kuniacha nalia kwa uchungu mpaka nilikaa chini,
Glory akaja na kunikuta bado nalia tu huku bado nikiwa chini
“Vipi love unaumwa mbomna unalia mama?” glory aliniuliza kwa mshangao
“Glory naumia sanaaa” niliongea kwa kwikwi huku bado nalia
“Umefanyaje jamani love wangu nambie basi!” glory alinisihi nimweleze
“Glory..joshuua” nilimjibu tena kwa kwikwi zaidi
“Joshua kafanya nini tena jamani?” aliniuliza
SUBIRA YANGU SEHEMU YA 15
“Niambie basi love nijue nakusaidia vip” glory aliendelea kunisi nimwabie kinachonisibu
“Joshua amekuja saivi kuongea na mimi” nilianza kumwelezea glory huku nikiacha kulia lkn bado nilikua na huzuni moyoni mwangu
“Ehe anasemaje?”glory aliniuliza kutaka kujua
“Bado ananipenda na ananihitaji” nilimjibu glory
“Sasa ndo ulie kama umefiwa si anajua wewe ni mchumba wa mtu ama nini?” glory nae akajibu kwa kuonesha kutofurahishwa na kitendo cha Joshua kuja niona
“Anajua lakin kaniadisia kila kitu glory ndo maana najiona nimemkosea sana Joshua jamani” nilimjibu
“Kwaiyo umeamuaje sasa maana na wewe hueleweki upo wapi kusini au kaskazini?”glory alioneshwa kukerwa na mim
“Sijamjibu chochote kwani siwezi kumuacha frank maana amenifanyia mambo mengi sana mazuri” nilimjibu glory huku nikionesha bado moyo wangu upo kwa frank japo nilikua naumia sana moyo wangu
“Basi inuka tuondoke sasa unalia nini sasa kama unampenda frank…mwache aende ye alivoondoka na kukuacha mpweke alitegemea nini” glory aliongea huku akiniinua na kupanda kwenye gari na kurudi nyumbani huku bado nikiwa na mawazo mawazo kichwani mwangu siku hiyo frank alinipigia tutoke out lakini nilikataa kwani sikua sawa kabisa
Zilibaki siku chache tumalize chuo huku arusi ya glory na kaka kim ikikaribia alafu ndo ifate ya kwetu…tulifanya mitihani na kumaliza chuo huku kaka na glory wakafunga ndoa na kuanza maisha yao mapya ya ndoa…kwa kipindi chote hiko sikuona Joshua akinisumbua tena tangu kipindi kile cha mwisho kuonana chuo nikaona yale aliyonambia hata nitafuta tena ilikua kweli basi niliamua kumwelelezea mama kuhusu mimi na Joshua tuliwahi kua na mahusiano na kumweleza kila kitu kwani nilihitaji ushauri wake
“Mwanangu wewe saivi ni mchumba wa mtu na unakaribia kufunga ndoa, mimi nakuomba kama mama yako utilize akili kwani ulikubali kuvishwa pete na frank kwa sababu uliona n mwanaume anaekufaa sasa ukienda kinyume utatutia aibu kwenye familia”mama alinisisitiza sana
“Lakini mama naona kama nimemkosea Joshua sana” nilimwambia mama
“Hatayeye amekukosea sana na uamuzi uliyofanya si mbaya kwani si unampenda frenk?”mama aliniuliza swali ambalo niliona ni gumu kwangu
“Ndiyo mama” nilimjibu
“Basi tulia na mwanaume mmoja ambae ni frank”mama aliniasa huku nikikubali ushari wake kwani zilibaki kama week tufunge ndoa na frank
Siku hiyo nikatoka zangu nikaenda kwa mume wangu mtarajiwa frank nikamsalimie maananilimmisi nikaingia na kukuta viatu vya mwanamke mlangoni mmh nilistuka kidogo na kuingia ndani na kumkuta dada wa kazi sebleni akifanya usafi alivoniona tu alistuka
“Shikamoo dada” akaniamkia
“Marhaba kaka ako yuko wapi?”nilimuuliza lakini hakujibu alikaa kimya tu na kuonesha kuogopa kujibu
“Wewe si nakuuliza husikii”nilimstua kwani alionekana anafikiria jambo lakini bado hakuonesha kujibu niliamua kutembea kuelekea chumbani kwa frank lkn dada alinizuia nisiende
Wewe vipi una nini kwani” nilimuuliza huku nikizidi kukasirika kwa kitendo cha kunizuia
“Dada usiingie “alinambia na kmpita na kuingia chumbani lakini nilichokiona sikutegemea na wala sikuamini huku machozi taratibu yakinitoka
“Frank!!!!” nilimuita frank na kufanya ashituke na kujitoa mwilini kwa msichana ambae sikumfahamu huku wakiwa watupu
“Love?!!” nay eye aliniita kwa mshangao kwani hakutegemea ningekuja mda ule
Nilitoka chumbani huku nilia na nilia na kuelekea kwenye gari langu huku nikitetemeka kwa kwa hasira na kuanza kufungua gari mara frank akaja haraka na taulo
“Love mke wangu sikiliza nikwambie” frank aliongea huku akiwa ameshikilia taulo lake ambalo hakulifunga vizuri..nilimnasa kibao frank shavuni na kuanza kumpigana nae nae huku nikimpiga mabao na mangumi mfululizo kifuani kwake huku akiwa amesimama huu wima akijaribu kunizuia nisiendelee kufanya vile
“Love pls nakupenda mke wangu” frank akajitetea huku akijaribu kunibana mikono yangu nisiendelee kumpiga
“Malaya wewe” nilimsukuma na kupanga kwenye gari huku nikiondoka kwa spindi huku frank akinifukuzia nyuma, akaanza kunipigia simu nikakata akapiga tena nikazima kabisa simu
Nililia sana njiani na kuona njia yote chungu niliamua kwenda moja kwa moja kwa kaka kim anapoishi yeye na mke wake glory nilivofika tu na nilipomuona glory nikaanza kulia upya huku nikimkumbatia glory jambo ambalo lilimshangaza glory kwani macho yalinivimba si kitoto
“Love una nini tena mama?”glory aliniuliza huku bado nikiwa nimemkumbati tu na kuendelea kulia
“Niambie basi love nijue mwezio unaniacha njia panda “ glory aliniuliza huku akiniketisha kwenye kiti huku akitaka kujua kilicho nisibu
SUBIRA YANGU SEHEMU YA 16
“Glory siamini alichonifanyia frank kabisa” nilimwambia huku nafuta machozi
“Kakufanya nini tena jamani?” glory aliuliza kwa kuhamaki
“Nimemfumania na mwanamke ndani tena kitandani nacho lala mimi na yeye” niliongea kwa uchungu sana
Haa love hapana siamini kama frank anaweza fanya ivo!”glory alistuka huku akionesha kutoamini maneno yangu
“Glory siwezi kukudanganya ukweli ndo huo nimeumia sana sijui nimemkosea nini hadi kuniumiza kiasi hiki” nilimjibu huku bado machozi tu yakiendelea kunitoka
“Sasa itakuaje na zimebaki siku chache mfunge ndoa maandaliz kila kitu tayari na mshaalika watu?” glory aliniuliza huku nae akiwa haelewi elewi
“Mi sitajali kama tumeshaandaa sherehe sijui maukumbi mi na yeye basi sitaki tena ndoa” niliongea kwa hasira
Noo love usifanye umuzi wa haraka haraka kiasi hiko kaeni chini muyamalize!” glory alijaribu kunishauri
“Mmh hapana glory mi siwezi kabisaa..ntapata tabu kwenye ndoa yenyewe kama ndo muuhuni kiasi hiki” niliendelea kugoma
“Sasa wanaume wetu ndo walivyo mama wote sawa ukimuacha huyu utaenda kwa mwingine ukakuta ndo hafai kabisa vumilia tu” bado glory aliendelea kunishauri nisimwache frank
“Sawa ngoja nifikirie maana sitaki kufanya maamuzi yatakayoniumiza moyo wangu” nilimwambia glory huku nikiinuka na kuondoka zangu
“Subiri basi unywe hata juice maana umefika tu hata maji hujanywa” glory aliniambiahuku akimwita dada wa kazi aniletee juice
“Hapana wifi yani sina hamu kabisa wacha niende ntakuja siku nyingine, mpe hi bro” nilimwambia na kuondoka zangu na kuelekea nyumbani huku bado nikiwa na huzuni kubwa ila nafika tu nikamkuta mama akiwa na frenk wanaongea, nilshangaa frenk anafata nini mda ule
“Shikamoo mama” nilimuamkia mama na kupitiliza chumbani lakini mama akanizuia
“Wewe love ina maana humuoni mwenzio?” mama aliniuliza kwa mshangao
“Nimemuona” nilijibu kwa mkato
“Kwaiyo?” mama akaniuliza huku akionesha kukereka na tabia yangu
“Tulishaonana tayari” nilimjibu huku nikiwasiwaangalii hata
“Naomba urudi na uketi hapa” mama aliniambia huku akinyooshea kidole kwenye sofa ili nikae..nikaketi huku nikiwa nimekasirika kwani sikutaka kabisa kuonana nae kwa alivonitibua
“Ulikua wapi?” mama aliniuliza
Nilienda kwa bro kim” nilimjibu huku nikiwa nimenuna
“Sasa kwanini mwenzio anakupigia simu hupokei badae ukazima nini tatizo?” mam aliendelea kunihoji
“Anajua mwenyewe tatizo” nilimjibu huku nikimtazama mama
“Ehee frenk kuna tatizo gani mwanangu?” mama alimgeukia frenk na kumuuliza
“Hamna mama tatizo naona tu love amenikasirikia bila sababu!” frenk aliongea uongo jambo ambalo lilinifanya nimpige jicho na kushangaa kwanini anadanganya
“Wewe unasemaje?..hamna tatizo?” nilihamaki
“Ndiyo love hamna tatizo lolote sikuelewi umepatwa na nini” frenk alizii kudanganya na kunifanya azidi kunipa hasira
“Mama frenk ni muongo sana yani anasema hakuna tatizo wakati nimemfuma na mwanamke kitandani” nilimweleza mama
Hee frenk asemayo love ni ya kweli? Mama aliuliza kwa mshangao huku akimkazia macho frank
“Mama hivi mimi naweza kufanya upuuzi kama huo kweli?...”frank aliongea kwa upole na kumfanya mama aanze kuamini namsingizia
“Baba najua huwezi fanya ujinga kama huo” mama alimwambia frenk jambo lilizidi kuniumiza roho yangu
“Love nakupenda sna mke wangu na unajua hilo sijawahi kufikiria kukusaliti ata siku moja na wala sifikirii” frenk aliongea huku akiniangalia na kumuona mnafiki sana ila mimi sikumjibu kitu kwani nilipatwa na hasira tu
“Harusi yetu imekaribia naomba usinitende kiasi hiki” frenk alizidi kujifanya mwema mbele za mama
Wewe frank weweee?” niliinuka na kumnyooshea kidole huku nikwa nimekerekwa sana na uongo wake nikaamua kuondoka zangu chumbani
Mama nakuomba ongea nalove nampenda sana plz mama angu” frenk alimuomba sana
Usijali mwanangu ntaongea nae inaonekana ana hasira sijui nani kamuudhi” mama alimjibu frank na kumruhusu fenk aende atafanyia kazi ombia lake
Frank akaondoka na mama akaja chumbani kwangu na kunikuta nimekaa zangu kitandani huku nikwa na waza
“Wewe love kwani umepatwa na kitu gani hadi umekua hivi lakini..”mama akaja kuketi karibu yangu
“Mama frenk ni Malaya imemfumania kwa macho yangu mawili kwanini nimsingizie mimi?” nilijaribu kumshawishi japo aniamini mimi maana alionekana kua upande wa frank
“Wewe love frank hawezi kufanya ayo mambo, we humuonei ata huruma alivokua analalamika pale” mama alinambia
“Mama mimi ndoa frank basi sitaki tena” nilimwambia mama
“Unasemaje wewe?”mama alihamaki huku akinikazia macho
No comments:
Post a Comment