Home → simulizi
→ Simulizi: SAFARI YA MSITU WA SIRI
Sehemu ya kwanza(1)
Baada ya baba yake DAVID kufariki..yapata miezi kumi sasa""" Nyumba yao ilipigwa mnada baada ya mama David kushindwa kulipia deni alilokopa BENKI marehemu mume wake....baada ya nyumba hiyo kupigwa mnada mama David aliamua kwenda kuishi kwenye nyumba ya kupanga,, wakati huo DAVID alikuwa anaumri upoatao miaka mitano",,baada ya kukaa miaka kadhaa alishidwa kumudu kulipia kodi ya nyumba kutokana na kipato chake kuwa kidogo""hivyo hakikuweza kutosheleza kulipia kodi ya nyumba na kutosha mahitaji mengine ikiwemo ada ya kumsomesha David. hivyo mama DAVID alilazimika kurudi kijijini kutokana na ugumu wa maisha huko mjini" ndipo alipoamua kuuza kila kitu cha ndani kwa lengo la kujipatia pesa ambayo itamsaidia kujikimu huko kijijini.
*******
alifanikiwa kuuza vitu hivyo, alipata pesa zipatazo milioni mbili na laki tatu,, walifunga safari kutoka dar es salaam kuelekea igunga mkoani Tabora, mama david alionekana kuwa mnyonge na uso wake ulionekana ni mtu mwenye huzuni,, alikuwa akifikiria sana jinsi ya kwenda kuanzisha maisha mapya tena ya kijijini'' roho ilimuuma sana kutokana alikuwa ameshayazoea maisha ya mjini..pia alimkumbuka marehemu mume wake ambaye ndiye baba wa mtoto wake huyo wa kiume aitwae david,, alikumbuka vitu vingi alivyovifanya na baba David enzi za uhai wake... machozi yalimtoka....David alimuangalia mama yake kwa huruma,, ndipo David aliamua kumfuta machozi mama yake"
mama Daivid alishindwa kujizuia alimtazama mwanae kisha akalia kwa uchungu huku amemkumbatia David...wakati huo David hakuelewa kitu chochote kutokana na umli wake kuwa mdogo..aliona kawaida kwa sababu alizoea kumuona mama yake akilia kila siku" dereva wa basi hilo aliliwasha gari na safari ya kuelekea Igunga ikaanza,,
******
watu (abiria) waliokuwemo ndani ya basi hilo walimtazama kwa nyuso za mshangao mama David kwa sababu alikuwa bado analia..wengiwao walihisi labda kapatwa na msiba hivyo zilisikika sauti za watu tofauti tofauti zikimwambia pole..
mama Davidi alijikaza na kuacha kuendelea kulia.
safari iliendelea na hatimaye wakafika igunga mjini"
gari liliingia stendi kuu na abiria wote wakashuka.
mama david alimchukua mwanae David na kuelekea kwenye gari zinazokwenda kijijjni kwao Igoweko..alilipa nauli na kisha akaingia nda ya gari,,
gari lile lilionekana limechakaa sana kutgokana na ruti za kwenda kwenye kijiji kile kwa sababu kulikuwa hakuna lami.. abiria walipoene kwenye gari safari ilianza...gari lile lilitembea kwa mwendo wa kisuasua...
kutokana na mawazo mama David hakukumbuka hata kununua chakula hatimae David alianza kulia njaa.alimpigapiga mama yake kifuani"
"mama nasikia njaa" mama yake hakumjali ndipo Davidi alipoanza kulia kwa sauti ndipo mama yake alipotahamaki,,kumbe kipindi David anamsemesha mama yake hakusikia kutokana na mawazo aliyokuwanayo kichwani,,akauliza kwa sauti ya upole unalia nini? "nataka kula" alijibu David bahati nzuri abiria aliyekaanaye siti moja alimuonea huruma David kwa sababu ni mtoto, aliamua kumpa mkate na juisi.. vitu vile alinunua kwaajili ya kuwapelekea zawadi watoto wake..."mama David alimtazama mama yule kisha akasema asante Mungu akubariki.. yule mama hakujibu chochote alitabasamu tu..David aliushambulia mkate ule utadhani alikuwa na njaa ya siku mbili..alikula akashiba na baada ya muda kidogo alipitiwa usingizi" mama David alimkumbatia mwanae kisha akatoa kitenge ndani ya pochi yake kisha akamfunika David..
****
Safari iliendelea gari lilitembea umbali wa kilometa sabini gafla liliharibika... wakati huo ilikuwa majira ya saa mbili usiku...
*******
Dereva na kondakta walilitengeneza gadi hilo na baada ya dakika kadhaa gari liliwaka tena na safari ikaendelea wakati huo abiria wote walikuwa kimya haikusikika sauti ya mtu hata mmoja.
baada ya kilometa kama kumi hivi,, walianza kuingia katika kijiji hicho cha igoweko...na hatimae wakafika...dereva aliliingiza gari stendi ilikuwa yapata saa tano usiku hivyo wale ambao walikuwa wanakwenda maeneo ya karibu na stendi hiyo walishuka...kisha dereva akasema kama kunamtu ambaye anakwenda mbali na maeneo ya hapa stendi anaruhusiwa kulala ndani ya gari kwa sababu ni hatari kutembea usiku kama huu kijijini hapa kunawanyama wakali" alisema deva"
ni kweli kijiji hicho hakuna nyumba ya kulala wageni (guest) hivyo mama Davi na mwanae pamoja na abiria wengine wachache walilala kwenye gari hilo....
kulikuwa na baridi kali sana mama David alimkumbatia mwanae akamfunika na kitenge alipohakikisha kamfunika vyema aliamua kulala...
lakini hakufanikiwa kupata usingizi alikuwa anawaza sana juu ya maisha anayokwenda kuishi" kijijinj hapo..
****
baada ya masaa kadhaa usingizi ulimnyemelea na hatimae akasinzia
palikicha yapata saa moja kasoro asubuhi...mama David alimuamsha mwanae ambae alikuwa bado kalala..kisha wakashuka kutoka ndani ya gari hilo alikuja kondakta akamtolea mabegi yake mawili.. walikuja makuli(wabeba mizigo) huku wakiwa na matoroli yao..."sister niweke au?"alisikika kuli mmoja akisema hivyo ndipo alimuona kuli mmoja aliekuwanae maisha ya utoto kijijini hapo alimkumbuka jina kisha akamuita kwa jina lake "shabani" ndipo kuli yule akaja haraka walisalimiana kisha shabani akaweka mabegi ya mama David kwenye mkokoteni wake...safari ikaanza kuelekea nyumbani kwao mama David..
wakiwa njiani walipiga stori walikumbushana matukio ya utotoni na shabani walicheka kwa furaha ya kuonana kwa mara nyingine tena.. shabani alikuwa mcheshi na muongeaji sana" hivyo basi ilipelekea mama Davidi kutoka katika ile hali ya mawazo
******
hatimaye walifika nyumbani",, Bibi yake David alifurahi sana kumuona mwanae pia alifurahi zaidi kumuona David ambaye ni mjukuu wake aliwakaribisha kwa furaha isiyo kifani.
shabani alishusha mabegi yale kisha akalipwa pesa yake alipewa shilingi elfu tano aliporudisha chenchi mama David akasema usijali hiyo iliyobaki itakusaidia mambo mengine
waliingia ndani kisha bibi yake David alileta kibuyu kikubwa kilichojaa maziwa na kumkabidhi mama David..
ITAENDELEA.......
USIKOSE KUFUATILIA SIMULIZI HII NZURI YA KUSISIMUA NA YA MAAJABU YA KUTISHA NDANI YAKE..
*ASANTE*
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: