SIMULIZI: JINA LA URITHI SEHEMU YA TISA(09) ⚪⚪⚪ILIPOISHIA⚪⚪⚪ wakati huo huo,,kule kijijini,,waliendelea kusubiri,,punde si punde mganga akashtuka!akahisi harufu isiyoyakawaida akaingiwa na wasiwasi!!! akatimua mbio kukifuata kile chumba akachukua zana zake za kichawi,,akaziweka kando yake kisha akachukua kioo maalumu cha kichawi...akakipaka dawa ili aweze kuona nini kinachoendelea.. wakati huohuo kule upande wa nje,,wanakijiji hawakuwa na mashaka,,,ghafla ikasikika sauti ya mganga akipiga kelele.kule chumbani,,punde si punde mganga akaonekana akitokea ndani ya chumba hicho huku akitimua mbio....wanakijiji wakaingiwa na hofu...mara ghafla giza likatanda!! PATASHIKA!!!! ⚪⚪⚪ENDELEA⚪⚪⚪ Wanakijiji wakaingiwa na hofu kupita kiasi,,hawakuwahi kuona mcha umebadilika kuwa usiku wenye giza totoro! kila mtu akatimua mbio,,pasipo kujua ni wapi wanaelekea! ghafla kikasikika kilio cha mtu akilia kwa sauti ya maumivu makali,,punde si punde giza likatoweka na nuru ikarudi,, huwezi kuamini kilichompata mganga,SAGALI WA SAGALI..alionekana kutokwa na damu mwilini mwake!! upande mwingine,,alionekana Laula akiendelea kutimua mbio,,sasahivi alikuwa tayari katoka eneo la makaburi.. aliendelea kutimua mbio pasipo kusimama....alipohakikisha yupo mbali na eneo la makaburi,,akageuza shingo yake kutaza ule upande wa makaburi...akaona moshi mkubwa,macho yakamtoka! alipotazama kwa makini,,akaona miti inatikisika na kudondoka chini...akaamua kutimua mbio.. alikimbia umbali mrefu mpaka katikati ya mji! akasita kukimbia akaamua kuzipiga hatua za haraka haraka ,,macho yake yakitazama huku na kule,,,uso wake ulionekana kuwa na wasiwasi kupita kiasi,,jambo ambalo liliwafanya watu wamshangae barabarani..Laula hakujali yeye aliendelea kuzipiga hatua pasipokujua ni wapi anakoelekea! upande mwingine,,kule kijijini,alionekana mganga Sagali wa sagali akiwa bado yupo pale chini huku akitokwa na damu nyingi kupita kiasi! hali yake ilikuwa tahabani, fahamu zikarejea,akafumbua macho yake,,akahisi maumivu makali mwili wote! akaangaza macho yake huku na kule,,hakuona mtu yeyote! hakuwepo hata mwanakijiji moja katika eneo hilo! akanyanyuka kwa kujikongoja na kuchukua tunguri zake..akasimama wima akaitazama ile nyumba,,aliyoweka mtego wake wa kichawi,,lakini mambo yakawa ndivyosivyo! Sagali wa Sagali akaingiwa na hasira kupita kiasi...ghafla akaona kitu cha ajabu macho yakamtoka akapiga tunguri zake atoweke kimiujiza katika eneo hilo lakini akawa ameshachelewa,,alipotahamaki mara ghafla!!! Ukaonekana mzimu wa muanzilishi wa ukoo wa Laula....mzimu huo uliamka kutoka makaburini ni baada ya Laula kudondosha lile jino juu ya kaburi hilo! Mzimu huo ukamkamata mganga Sagali wa Sagali na kuondoa uhai wake papohapo....kisha mzimu huo ukatoweka kimiujiza kwenda kumtafuta mrithi wa jina lake!.. wakati huohuo upande mwingine,,alionekana Laula akiwa bado yupo katikati ya mji akirandaranda....akahisi njaa kali lakini akajikaza kutokana hakuwa na pesa ya kununua chakula.... siku ya leo akaamua kuifuata nyumba moja aliyoiona kando ya barabara akiamini huenda akapata msaada wa chakula! alipoikaribia nyumba hiyo akagonga hodi,,,na baada ya sekunde kadhaa mlango ukafunguliwa..Laula akatoa salamu kisha akaeleza shida yake....mtu aliyefungua mlango akamuhurumia Laula akaamua kumkaribisha ndani ya nyumba kwa lengo la kumpa chakula..Laula akazipiga hatua akaingia ndani ya nyumba hiyo! akaketi kwenye sofa,,akisubiri aletewe chakula...yule mtu aliyemkaribisha ndani ya nyumba hiyo akazipiga hatua kuelekea jikoni...akafungua jokofu akatoa chakula na kukiweka jikoni ampikie mtoto Laula. baada ya dakika kadhaa chakula kikawa tayari,,akakiweka kwenye sahani kumpelekea Laula kule sebuleni......kabla ya kupeleka chakula akahisi vitu vinadondoka upande wa chumbani!! akashtuka! akaingiwa na wasiwasi labda mtoto aliyemkaribisha ndani ni mwizi, huenda ndiye ameingia chumbani! akaamua kutoka haraka jikoni na kuelekea upande wa sebuleni... akastaajabu kumkuta Laula akiwa kaketi vilevile kama alivyomuacha mwanzo!!! macho yakamtoka!! Laula akashtuka kumuona mtu huyo akimtazama kwa macho ya msisitizo! akaamua kumuuliza,,"mbona wanitazama? kuna jambo ambalo haliko sawa? yele mtu akaamua kudanganya akasema,,"nilikuwa najaribu kukumbuka jambo fulani,, aliongea hivyo huku akizioiga hatua kurudi upande wa jikoni....alipofika katika korido,,ghafla akasikia tena vitu vikidondoka kule chumbani...sasahivi hata vyombo vilivyokuwa katika kabati la vyombo jikoni,, viligongana na vingine kupasuka...jambo hilo lilimfanya mtu huyo aingiwe na hofu...punde si punde likatokea tetemeko la ardhi na nyumba ikaanza kutikisika....mara ghafla!!!!!!!!! ↔↔↔↔↔ITAENDEA↔↔↔↔↔ Kila msomaji hakikisha una LIKE hadithi hii kuipa nguvu..niirushe kila siku Ungana nami katika sehemu ya 10. wingi wa Like zenu ndizo zitafanya nilete muendelezo kwa wakati.

at 3:49 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top