Riwaya : SAFARI YA MSITU WA SIRI SEHEMU YA TATU(3) lakini David hakuwajali wasichana hao..... paul ambae ni mjomba wake david" baada ya kuona David ameshakuwa kijana"aliamua kumfundisha. jinsi ya kuwinda" pia alimpa mbinu za kumnasa mnyama kwa kutumia upinde na mshale....kijijini kwa kinaDavid jamii yao walikuwa wafugaji hivyo hivyo David hakufahamu chochote kuhusu kilimo"" kadri David anavyozidi kukuwa ndivyo alizidi kuwa muwindaji hodari...alitokea kuwa mtu mwenye shabaha sana",, kila aliporusha mshale hakuna mshale uliopotea alihakikisha analenga shabaha yake baraabara...pindi" anapokuwa mawindoni David alikuja kuwa moto wa kuotea mbali kwa uwindaji....mjomba wake alimsifu sana pia alijivunia kuwa mwalimu bora wa David kwenye uwindaji"".....sikumoja mama yake David aliugua ghafla... hivyo walimkimbiza haraka Kwenye kituo cha afya cha kijiji hicho....walimfanyia vipimo ndipo alipogundulika kuwa Anashinikizo la damu ya kupanda(HIGH BLOOD PRESSURE) daktari aliyekuwa zamu siku hiyo alikuja kisha akauliza ndugu wa mgonjwa huyu wako wapi?? David baada ya kusikia hivyo alisimama haraka.. mjomba wake alimzuia kisha akaenda yeye ndipo daktari huyo akamwambia paul maradhi yanayomsibu Dada yake...paul alisikitika sana..kisha daktari akasema lakini hali yake sio mbaya sana tumemwekea Dripu hivyo anaendelea vizuri...hapo nafsi ya Paul ikatulia... ******* wakati huo David akiwa kasimama kwa nje jirani kabisa na mule alimoingia mjomba wake"",huku alikionekana ni mwenye shauku sha kutaka kujua kinachoendelea pia kujua mama yake amepatwa na tatizo gani.. punde alimuona mjomba wake akitoka mule ndani..alimfuata kwa haraka..vipi mjomba" mama anaumwa nini??? anaendeleaje?? daktari kasemaje? hivi kweli mama atapona?? David aliuliza maswali hayo mfululizo... Ndio atapona pia sasa hivi anaendelea vizuri paul alijibu" huku akizipiga hatua za mwendo wa taratibu naweza kumuona:? aliuliza David" hapana yupo kwenye uangalizi wa daktari hivyo tutaruhusiwa kumuona badae... david alibaki kimya. kisha wakaondoka kurudi nyumbani kwaajili ya kuandaa chakula cha mgonjwa.) ****** Baada ya muda kidogo walifika nyumbani",,David alichukua kuni akawasha jiko haraka kisha akaanza kuandaa chakula kwa ajili ya mama yake....wakiti akifanya hivyo pia alikuwa akimuomba Mungu mama yake apone apate afya njema... ******* Paul alimuaga David kuwa anaelekea porini kwaajili ya uwindaji" kisha akaondoka zake kwa lengo la kwenda kutafuta kitoweo. Baada ya chakula kuiva alipakua chakula hicho ilikuwa ni ndizi pamoja na nyama ya swala...kisha akaanza safari ya kuelekea kituo cha Afya kule alipolazwa mama yake...alizipiga hatua kadhaa kisha akakumbuka" hueanda zikahitajika pesa kwaajili ya malipo ya matibabu hivyo basi aliingia chumbani kwa mama yake kisha akaliinua godoro hilo la pamba juu ya kitanda kilichotengenezwa kwa miti. alifanya hivyo kutokana alikuwa akijua mama yake huwa huweka pesa zake mahala hapo",,alitoa kiasi cha shilingi elfu thelathini zilizokuwa na mchanganyiko wa elfu moja moja zikiwemo mia tano mia tano na shilingi elfu mbili mbili...alizichukua pesa zile kisha akaondoka zake kuelekea huko alipolazwa mama yake...alizipiga hatua za haraka haraka na baada ya muda kidogo alifika.. alielekea moja kwa moja kwenye wodi aliyolazwa mama yake...aliingia alikuta mama yake kalala..alipoitazama dripu ilionekana imekaribia kuisha...alimuamsha taratibu kwa kumtikisa...punde mama David aliamka..alifumbua macho na baada ya kumuona Mwanae alitabasamu" wakati huo David alionekana mwenye sura iliyojaa majonzi...kisha akasema unaendelea mama? "nimekuletea chakula ni ndizi na nyama ya swala je utaweza kula kwa wakati huu?? David alimuuliza mama yake"" ndio mwanangu nitakula sasa hivi" kisha akanyanyuka na kukaa kitako.. David akampa chakula mama yake akala mama David alionekana kukifurahia chakula kile kisha akamwambia David unajua kupika,, umepika chakula kitamu sana"" umenikumbusha marehemu baba yako wakati mwingine alikuwa akinisaidia kupika..alikuwa akiingia jikoni wee anapika mahanjumati hatari" David alitabasamu kisha akasema Natamani baba yangu angekuwa Yuhai...punde daktari aliingia na kumjulia hali mama David. ****** Dripu iliisha kisha daktari aliitoa dripu ile", na baada ya masaa manne kupita Mama David aliruhusiwa kwenda nyumbani...waliondoka kuelekea nyumbani. walipo fika nyumbani David alimuaga mama yake kuwa anaenda porini kule alipokuwepo mjomba wake mawindoni...mama David hakuwa na pingamizi alijibu ni sawa...kisha David akaondoka zake kuelekea porini..... alitembea umbali wa kama kilometa nne hivi kisha akafika sehemu ile ambayo paul anapenda kuwinda maeneo hayo aliita mjomba" kwa kupaza sauti..sauti ya David ilisikika vizuri masikio mwa Paulo kutokana na Mwangwi hivyo sauti ilijirudia rudia"" mjomba aliitika kisha David alielekea upande ule ambao sauti ilitokea.. alimuona mjomba wake..Loh! yani leo mawindo magumu yani wanyama hawapatikani eneo hili kabisa tangu nilipokuja sijafanikiwa kuona mnyama hata mmoja..alisema Paul",, walikaa takribani masaa matatu bila kuona mnyama yoyote akitokeza eneo lile.. nabaada ya muda kidogo kupita Paulo aliamua wagawane maeneo. alisema mimi nitaelekea upande ule na wewe utaelekea upande mwingine tujaribu labda tutafanikiwa kuona wanyama.. David aliona wazo hilo ni zuri kisha akafanya kama mjomba wake alivyosema"" ******* David alizipiga hatu kuelekea upande mwingine...alijitahidi kutazama kwa umakini lakini hakuona dalili ya mnyama yoyote kuonekana eneo hilo....aliamua kusonga mbele zaidi pia hakufanikiwa kuona chochote...alikumbuka maneno ya bibi yake enzi za uhai wake alimwambia" ((((katika maisha yako usioende kukata tamaa yakupasa uwe na subira katika kila jambo))) hivyo basi kauli hiyo ilimjenga vyema David kisaikorojia.... alikuwa ni mwenye subira hakukata tamaa mara kwa mbali alimuona mnyama alipotazama kwa makini aligundua kuwa ni Swala...alifurahi sana"" uso wake ulionekana kujawa tabasamu...alinyata kwa hatua za taratibu ili swala yule asimuone...David alinyata unaweza kusema ni mtu mwenye mafunzo ya kininja.....alipo mkaribia alitoa mshale mmoja kwenye (PODO) lililokuwa mgongoni kisha mshale ule akauweka kunako upinde.. kabla hajarisha mshale ule...ghafla swala yule alikimbia na kuelekea mbele zaidi.. David alifadhaika sana hakukata tamaa alimfuta mnyama yule kule alipoelekea....alipoangazaangaza macho alimuona swala yule...David akanyata tena kwa maranyingine tena alipomkaribia swala yule alikimbia na kutokomea porini zaidi....David hakukata tamaa aliamua kuingia katika pori hilo kwaajili ya kumfuatilia swala yule huenda atamuona... ********* Upande wa pili alionekana paul akiendelea kutafuta mawindo lakini hakuna dalili yoyote ya mnyama kutokeza hatimae paul alikata tamaa kisha akaamua kurudi pale walipokuwepo mwanzo.... alikaa katika jiwe moja akimsubiri David arudi huenda atakuwa amefanikiwa kunasa mnyama yoyote"" paul alikuwa akimuamini sana David katika uwindaji na haijawahi kutokea hata sikumoja David kutoka mawindoni bila kurudi na kitoweo..... alimsubiri lakini hakuona dalili ya David kutokeza eneo lile ndipo alipoamua kupaza sauti..alimuita David bila mafanikio yoyote aliamua kwenda kumtafuta ule upande alioelekea David pia hakumuona...alimtafuta pande zote bila mafanikio ya kumuona David... paul alikata tamaa..akajisemea moyoni atarudi tuu wacha mimi nirudi zangu nyumbani... ********** Upande mwingine David aliinekana akizidi kuingia ndani ya pori...." pori lile lilionekana kuwa na msitu wenye miti mikubwa sana..mara ghafla alimuona swala yule,, kwa sasa swala yule hakuwa mbali na pale alipokuwepo David..kisha alivuta unde ule kumlenga swala yule....ile anataka uachia mshale swala alitimua mbio na kutokomea ndani zaidi kunako msitu huo... David alichukia sana....akaamua kuingia ndani zaidi kunako msitu huo....mara ghafla kilipita kiumbe mbele yake kwa kasi ya hajabu akuweza kukitambua kiumbe kile.. Itaendelea....... Asanteni.

at 10:22 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top