Riwaya: SAFARI YA MSITU WA SIRI
SEHEMU YA PILI(2)
Mama David alipokea kibuyu kile kilichokuwa kimejaa maziwa akachukua vikombe viwili ya bati (bilauli) akamimina maziwa yale kisha akanywa na mwanae david",, David alionekana kuyafurahia maziwa yale hivyo alikunywa akaomba aongezewe tena na tena atimae alikunywa vikombe vitatu....mama David alianza kuongea kilugha na Bibi yake David...walicheka wakafurahi sana lakini ghafla furaha ile ilitoweka baada ya mama david kumpa taarifa za kifo cha mume wake" Bibi yule alihuzunika sana alianza kulia huku akiongea kilugha",, kutokana umri kuwa mkubwa alilia lakini machozi hayakutoka david alimuangalia bibi yake kwa sura ya huruma"" sikuzote mtoto anapoona mtumzima akilia..na yeye huanza kulia pia...wakati huo huo alikuja mjomba wake David ambaye ni mdogo wake mama David...
bibi yule alijaliwa kupata watoto wawili tu..ambaye ni mama david na na mdogo wake wa kiume aitwae PAUL...
Paulo alifurahi sana kumuona dada yake wa pekee ambaye hakumuona yapata miaka kumi na sita sasa...alimkumbatia kwa furaha kisha akambeba David aaaaaahhh Mjomba hakika utakuwa hodari"nitakufundisha kuwinda... Paul ilitoka na David akaelekea nje ya nymba hiyo iliyoezekwa kwa Nyasi kavu.
******
alienda moja kwa moja mpaka shambani huku akiwa bado kambeba David aliufata mti wa maembe kisha akachuma maembe kama manne matano hivi" alimpa embe moja David kisha watoka humo shambani..David alionekana mwenye kuchangamka sana" pia Paul alifurahi sana alicheza na David alichezanae michezo ya kitoto kabisa" ingawa yeye alikuwa ni mtu mzima",, David alionekana kujawa na furaha na uchangamfu wa hali ya juu",,
******
wakati huo mama David alikuwa anaona jinsi David alivyokuwa na furaha anavyocheza na mjomba wake" alitabasam kisha akajisemea moyoni",, hakika umefanana sana na marehemu baba yako, unavyo tembea, unavyocheka, lakini hayupo tena duniani baba yako",, wewe pekee umebaki kuwa furaha yangu nakuombea kwa Mungu ukuwe kwa Afya njema" alipaza sauti mama David akimuita mwanae""daviiiiiiii""
David aligeuka na kumtazama mama yake kisha mama David alinyoosha mikono ishara ya kutaka kumkumbatia mwanae",,kisha David alikimbia nakuelekea kule ndani alipokumo mama yake....waaaa....oooo alisema mama David""
David alimkumbatia mama yake.. na kisha akalipeleka lile embe alilopewa na mjomba wake moja kwa moja mdomoni mwa mama yake...
mama David aling'ata kipande kidogo chaembe kisha akasema asaa....nteee mwanangu".. Davidi alimtazama mama yake na kisha akarudi nje kule alipokuwepo mjomba wake...
******
***BAADA YA MIAKA KUMI NA MOJA KUPITA***
DAVID aliendelea kuwa mkubwa"yapita miaka mingi na sasa ni kijana wa miaka kumi na sita sasa............
ilikuwa ni siku ya ""jumamosi"" david aliamka asubuhi na mapema""kama kawaida yake kisha humsaidia kazi mama yake kama kwenda kuteka maji kisimani, kwenda porini kutafuta kuni..(nk).lakini Asubuhi ya leo hii ilikuwa ni asubuhi ya majonzi kwenye familia yao...Bibi yake David siku hiyo aliamka Yumgonjwa sana hali yake ilikuwa mbaya kupita maelezo ",,kutokana na umri mkubwa aliokuwanao alikuwa hawezi kutembea hivyo alikuwa ni mtu wa kubebwa kupelekwa nje kwa ajili ya kuota jua" na kisha kubebwa tena kurudishwa ndani.
Mama David alihuzunika sana alisononoka huku machozi yakimtoka...asijue nini cha kufanya"" Davidi aliamua kukimbia mbio kwenda kumtafuta mjomba wake huko porini wakati huo paul ambaye ni mjomba wake David alikuwa porini huko kwaajili ya kuwinda wanyama",, kwaajili ya kitoweo cha jioni
*********
David alimtafuta mjomba wake bila mafanikio yoyote...alikata tamaa na kuamua kurudi nyumbani huku akionekana kuwa mnyonge... alipokaribia maeneo ya nyumbani",,kwa mbali alisikia sauti ya mtu akilia kwa sauti kubwa!",, sauti ile ilisikika dhahili kuwa mtu yule alikuwa akilia kwa uchungu wa hali ya juu...alipoisikiliza kwa makini sauti ile ndipo alipoitambua sauti ile kuwa, ni sauti ya mama yake mzazi...Alitoka mbio unaweza kusema ni mtu anaekimbia mbio za mita mia huku amehaidiwa zawadi nono.alikimbia kwa kasi ya ajabu alipitiliza moja kwa moja ndani",,!!!
David alistahajabu kukuta Bibi yake kaiaga dunia alilia kwa uchungu na kusema kwanini usingenisubiri nirudi angalau uniage!"" nitakuona wapi tena bibi yangu?"" wakati akisema maneno hayo alikuwa kakumbatia maiti ya bibi yake....David alilia sana ,,,""mpaka Mama yake akaanza kumuonea huruma mwanae..alijua wazi kuwa David ameumia sana juu ya kifo cha bibi yake kutokana David alimpenda sana bibi yake kwa sababu alimlea katika maadili mema pia alimfundisha mambo mengi sana ikiwemo ukarimu subira na jinsi ya kuishi na watu vizuri...
kwakweli lilikuwa ni pigo kubwa sana kwa David
*******
Mara punde mjomba wake Davidi akiwa anazipiga hatua jirani kabisa na nyumbani kwao'' mara ghafla akastuka kuona umati wa watu pale nyumbani kwao..huku bado akiwa na shauku ya kutaka kujua kinachoendelea""" alipoangaza macho""",, kwa mbali alimuona Dada yake akilia huku kamkumbatia David" ni kweli ule msemo unaosema "utuuzima dawa" papohapo aligundua kuwa bila shaka Mama yake atakuwa kafariki...roho ilimuuma sana..alikuwa ni mtu hodari mwenye nguvu zaidi kuliko wanaume wote pale kijijini lakini alidondosha machozi...alijikuta analia kwa uchungu wa hali ya juu!! hata yule swala aliye fanikiwa kumnasa huko mawindoni. kwa ajili ya kitoweo cha jioni alimshushu kutoka begani kisha akaangukia magoti huku akilia kwa uchungu usioelezeka. majilani wawili walimfata na kumfariji kisha wakamnyanyua pale chini na kumpeleka nyumbani"
********
Taratibu za mazishi zilifanyika..wakamzika bibi yake David...
kiukweli Davidi alikuwa ni mtu mwenye upweke kila siku"""" hakuwa na furaha hata kidogo..Mama David alimuhurumia sana mwanae lakini hakuna namna huwezi kuilazimisha furaha ikiwa moyoni unamajonzi...
*****
Baada ya miezi minne(4) kupita David aliaza kurudi katika hali yake ya kawaida ya uchangamfu.. lakini mwili wake ulionekana kupungua kutokana muda mwingi alikuwa anawaza juu ya kifo cha bibi yake...mbaya zaidi pale anapokumbuka ucheshi/mafundisho ya maisha pamoja na hadithi za kale alizokuwa akisimuliwa na marehemu bibi yake'''hiyo ilimfanya ashindwe kula chakula vizuri kila siku""" na hatimae mwili wake ulipungua kwa kiasi kikubwa alionekana kukonda....
*********
kijana David alipenda kuutumia muda wake mwingi kudadisi mambo kwa kuwauliza maswali mbalimbali watu waliomzidi umri..hivyo alifahamu mambo mengi zaidi...pia alikuwa nakipaji cha kujua jambo kwa haraka hata kama kaelekezwa bila vitendo" hiyo iliwastahajabisha watu wengi pia
kutokana na nidhamu,,ukarimu,,uchapakazi, unyenyekevu.. tabia nzuri aliyokuwa nayo David ilimfanya watu wote wampende hapo kijijini...
na kwa jinsi alivyokuwa mweupe kwa kufata rangi ya mama yake alionekana handsome na mwenye mvuto...hivyo mabinti wengi wa kijijini hapo walijingonga na kujipitisha pitisha nyumbani kwa kinaDavid kila wakati ilimradi tu",,wamuone david hata kama hakuna jambo la msingi.. walitamani kila mmoja wao amilikiwe na David..
Itaendelea..........
No comments:
Post a Comment