Home → simulizi
→ RIWAYA: DAMU YA MWANANGU
SEHEMU YA SABA(07)
*****ILIPOISHIA******
wakati anatahamaki,,akaona mwanamke akiwa kajifunika nguo nyeupe akikatiza kuelekea nyuma ya nyumba! Nyamwela akatimua mbio akachungulia nyuma ya nyumba hakumuona tena yule mwanamke! akaamua kuzipiga hatua za kunyatia kurudi upande wa mbele ya nyumba,,,akastaajabu kumuona mwanamke huyo akiishilizia kuingia ndani ya nyumba huku akiwa kambebq mtoto mchanga anavuja damu!
Nyamwela akatimua mbio huku akigeuzageuza shingo yake nyuma! alikimbia umbia umbali mrefu,, akahisi kuchoka! akaamua kusimama.....
wakati huo ilikuwa ni nyakati za usiku....punde si punde akaonekana yule mwanamke akipita kwa mbali...Nyamwela kaanza kutimua mbio,,ghafla lile kaburi likajitokeza mbele yake! akasita kuendelea kukimbia,,,
wakati anatahamaki! ghafla akavutwa na kutumbukia ndani ya kaburi hilo kisha likajifunga!
****ENDELEA*****
Nyamwela akajikuta ametokezea sehem ya kutisha,,akaangaza angaza macho yake,,lakini hakuitambua sehemu hiyo!
hofu ikazidi kuongezeka,,,akazipigq hatua za kunyatia,,akajificha nyuma ya jiwe kubwa...ghafla akahisi kudondokewa na kitu chq kimiminika akanyanyua uso wake kutazama upande wa juu ya jiwe....akaona damu nyingi zinamwagika kutoka juu ya jiwe kuja upande wa chini,,,akatimua mbio,,,,
alikimbia pasipokujua ni wapi anaelekea! kwa mbali akamuona yule mwanamke aliyemuona kule nyumbani kwake muda mfupi uliopita! lakini mwanamke huyo aonekani sura alikuwa kavalia mavazi meupe,,huku kambeba mtoto mchanga,,aliyekuwa anchuruzika damu yingi upande wa shingoni!
mbaya zaidi,,mwanamke huyo alikuwa anaonekana akiishilizia mguu wa mwisho kuingia katika chumba kilichokuwa na mlango!
punde si punde giza likatawala neo hilo! hofu ikazidi kuongezeka!
Nyamwela akaangaza macho yake kutazama huku na kule,
hakuweza kuona chochote kwa sababu giza lilikuwa totoro!
kwa mbali akaona nuru ya mwanga ukimulika kuja upanda wake,,
macho yakamtoka ! ghafla akamuona yule mganga akiwa kashikilia moyo,,,mganga huyo alikuwa anapumua kwa haraka haraka,,kisha akasema,,umeniponza,,hakika hata wewe huwezi kubaki hai!
baada ya kusema maneno hayo mganga akadondoka chini na kupoteza uhai!
punde si punde ikasikika sauti ya mtoto mchanga akilia mfululizo!
sauti hiyo ilijirudia rudia kutokana na mwangwi...
ghafla giza likatoweka,,na mwanga ukatawala! Nyamwela akashtuka kumuona yule rafiki yake akiwa ameshikilia upanga mkali,,ni yule rafiki yakealiyemchinja kule porini!
wakati anataamaki,,kwa mbali akaonekana Muna akiwa anazipiga hatua kuja upande huo,,,,
ghafla akajitokeza mtoto wa Nyamwela akiwa hana kichwa...mtoto huyo alikuwa kalala chini,,mbele ya Nyamwela!
akatimua mbio!! kabla hajafika mbali,,akahisi harufu kali ya damu inanuka kwenye pua zake! akanyanyua ukono wake kuguza pua zake! akashtuka kuona damu zikimtoka puani,,,punde si punde yule mwanamke,,aliyekuwa kavalia mavazi meupe,akajitokeza kando ya Nyamwela, akiwa kashikilia upanga ,,,akanyanyua upanga huo na kufyeka shingo ya Nyamwela..
Nyamwela akashtuka kutoka usingizini,,kumbe alikuwa anaota ndoto,,usingizini,,,akagusa shingo yake kuhakikisha kama yupo salama! kumbe matukio yote,,ilikuwa ni ndoto!
akanyanyuka haraka kutoka kitandani,,akachukua kiberiti na kuwasha koroboi!akageuza shingo yake kutazama kitandani,,akamuona mkewe akiwa kalala usingizi huku mikono yake akiwa kaiweka juu ya tumbo lake lenye ujauzito!
Nyamwela.akajisemea moyoni,,"ndoto hii inamaanisha nini? mbona sielewi! punde si punde mkewe akadamka,,akastaajabu kumuona mumewe akiwa kasimama kando ya kitanda akimtazama kwa mshangao!
akaamua kumuuliza,,"mbona umesimama hapo?
usiku wote huu!
kabla hajamaliza kuongea, Nyamwela akasema,nimeota ndoto mbaya sana!
wakati huohuo upande mwingine walionekana vijana wawili wakiwa wanatembe barabarani huku wakiimba nyimbo...sauti za vijana hao zilisikika kama sauti ya watu waliozidiwa na ulevi!
mmoja kati ya vijana hao wawili,,akasema,,"huyu bwege analala na pesa ndani wakati sisi tunashida na pesa.
kumbe vijana hao waliiba pesa zilizokuwa Nyumbani kwa Nyamwela! mcha wa leo....hapakuwepo mtu yeyote hivyo waliweza kuingia ndani ya nyumba ya Nyamwela na kuiba pesa hizo.
Ke nyumbani kwa Nyamwela,,alionekana mke wa Nyamwela akisema,,"hiyo ni ndoto tu mume wangu,,cha msingi sali kwa kukemea,,kisha lala..
Nyamwela akamtazama mkewe,,kisha akasema ni jambo jema mke wangu,,wacha nichukue biblia,,,,
akazipiga hatua kuifuata kabati ndogo,,akaifungua ili achukue biblia ,ghafla akashtuka! akauliza kwa sauti ya kukali,,"pesa zangu niliziweka humu ndani ya droo,, ziko wapi?
Muna akamtazama mumewe kwa macho ya mshangao!
kisha akasema,,"ni siku kumi sasa sijafungua hiyo droo,ebu tazama kwa makini,
Nyamwela akasema kwa ukali,,"pesa hizo sio za kwangu,,nilikopa kwa ajili ya kuandaa shamba,,nataka pesa zangu..
Muna akabaki kimya,,
Nyamwela akaingiwa na hasira,,akafungua mlango na kutoka nje ya chumba,,akachukua kisu,,akarudi chumbani,,akamkuta muna kasimama kando ya droo akizitafuta pesa hizo..
alipogeuza shingo yake ,,,mara ghafla!!!!!!!
ITAENDELEA..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: