Home → simulizi
→ RIWAYA: DAMU YA MWANANGU
SEHEMU YA MWISHO
*****ILIPOISHIA******
abiria wengine wakadakia na kumuunga mkono abiria aliyesema hivyo akimvuta dereva,,,
dereva huyo akaamua kusimamisha gari na kumfukuza Nyamwela atoke ndani ya gari,,akisema,,"sina uhakika kama unaakili timamu,,yani unanivuta,,wakati naendesha gari,,huoni kuwa unaweza kusababisha ajali? haya toka haraka ndani ya gari.
Nyamwela hakujali akashuka na kutimua mbio kurudi walipotoka...alikimbia kwa kasi,,hatimae akalikaribia lile begi! akaliokota!! macho yakamtoka,,begi hilo lilikuwa tupu,,halikuwa na kitu chochote ndani yake!,,Nyamwela akaanza kulia huku anacheka,,vyote kwa pamoja!!!! alipogeuza shingo yake kulitazama.lile basi,,kama bado limesimama,,,mara ghafla!!!!
TAHARUKI!
*****ENDELEA*****
Nyamwela.akastaajabu kuona basi linatokomea....punde si punde akaona lile gari dogo likiwa linarudi....akasimama kando ya barabara na kupunga mkono ishara ya kumuomba dereva asimamishe gari hilo!
lakini haikuwa kama alivyotegemea,,hakuamini gari hilo lilimpita na kutokomea,,
Nyamwela akaamua kuzipiga hatua,, akalifuata jiwe lililokuwa kando ya barabara ,akapumzika! ghafla akahisi kamuona Muna anakatiza barabarani,,macho yakamtoka,,,alipotazama kwa makini hakumuona tena Muna,,
akaingiwa na hofu,,akaangaza angaza macho yake huku na kule,,hakuona mtu yeyote!
Nyamwela akanyanyuka haraka na kuanza kutimua mbio! kadri alivyozidi kukimbia,,ndivyo harufu ya damu ilizidi kunuka kwenye pua zake,,,akahisi mikono yake imelowana,,akasita kukimbia akatazama mikono yake,,akaona damu zilizoganda kwenye mikono yake! punde si punde damu hizo zikatoweka kimiujiza,,akajisemea moyoni,,"hii ni ndoto au naona kweli??
kqmq ni ndoto,,mbona nipo macho sijasinzia!?
alijiuliza.maswali yasiyokuwa na majibu...
Upande mwingine,,lilionekana gari kubwa aina ya SCANIA likiwa katika safari,,,gari hilo lilipita katika barabara aliyokuwepo Nyamwela,,ghafla mvua ikaanza kunyesha,,,Mvua hiyo ilizidi kuongezeka kila baada ya dakika kadhaa,,hatimae ikawa mvua kubwa,,ikiambatana na upepo mkali....baada ya dakika kadhaa kupita,,,gari hilo likawa linapita eneo alilokuwepo Nyamwela!
Dereva huyo akastaajabu kumuona mtu akiwa kasimama chini ya mti mkubwa huku mvua ikimnyeshea,,,
akaingiwa na huruma,,akapunguza mwendo wa gari,, hatimae likasimama,,akapiga honi,,akachomoza mkono wake nje akifanya ishara ya kumuita Nyamwela!
Nyamwela hakuweza kusikia sauti ya honi,,wala kutazama upande wa barabarani,,,muda wote alikuwa kainamisha uso wake
chini,,
dereva wa lile gari,,akajisemea moyoni,,"bila shaka mtu huyu yupo katika dimbwi zito la mawazo! akaamua kuliwasha gari na kuliondosha taratibu,,
wakati gari hilo linaondoka,,Nyamwela akashtuka! akahisi kama kasikia mlio wa gari! akanyanyua uso wake! akaliona gari hilo likiondoka,,akakurupuka na kutimua mbio kuja barabarani,,akalikimbilia gari hilo kwa nyuma huku akiita kwa sauti kali na kunyoosha mkono wake kuomba msaada...
yule dereva akamuona Nyamwela,,kupitia kioo cha pembeni!
akaamua kusimamisha gari hilo! Nyamwela akalifuata kuomba msaada wa lifti.....lakini alipotazama upande wa dereva,,,akashtuka,macho yakamtoka! akashangaa kumuona Muna akiwa kaketi kando ya dereva huyo,,huku kashikilia tumbo,,na damu nyingi zikimtoka,,,Muna alikuwa akimtazama Nyamwela kwa macho ya masikitiko huku akilia kwa uchungu!
Nyamwela akaogopa sana! akazipiga hatua kurudi nyuma,, alipotazama tena ule upande aliokuwa kaketi Muna,,akastaajabu kutokumuona Muna,, kiti kilikuwa tupu! Nyamwela akatimua mbio na kutokomea kusikojulikana!
Dereva akabaki na mshangao,,akijiuliza,,"mbona mtu huyu anaonekana kuwa na hofu kubwa,,kwani kaona nini ndani ya gari hili,,mbona kakimbia?
baada ya sekunde kadhaa kupita dereva huyo akaliwasha gari na safari ikaendelea..
wakati huo huo, upande mwingine alionekana Nyamwela akiwa amejikunyata chini ya mti uliokuwa na matawi mengi,,maji ya mvua yalipita kiadi katika matawi hayo,,lakini baridi lilikuw akali kupita kiasi,,kutokqna na upepo uliokuwa unavuma kwa kasi...mvua iliendelea kunyesha mfululizo ikiambatana na ngurumo za radi,,hatimae giza likaanza kutanda kabisa...hali hiyo ilimfanya Nyamwela azidi kuogopa....kwa mbali akamuona mtu akizipiga hatua kuja upande aliokuwa amesimama,,mtu huyo alipokaribia eneo hilo,,Nyamwela.akashtuka kumuona Muna akiwa akasiamam mbele yake,,punde si punde Muna akatoweka kimiujiza,,,Nyamwela akaanza kuoiga mayowe huku akitazama huku na kule,,,ghafla radi ikapiga kwenye ule mti aliokuwa amesimama chini yake,,mti huo ukapasuka katikati..na kumdondokea Nyamwela,,ukamkandamiza akafa papohapo!
********MWISHO*********
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: