RIWAYA: DAMU YA MWANANGU DAR ES SALAA SEHEMU YA TANO(05) *****ILIPOISHIA****** akachukua koroboi akaiwasha kisha akatoka nje kuelekea kule nyuma ya nyumba,, aone je? ni kitu gani kimedondoka! alipofika akamulika kwenye lile kaburi,,,akashtuka! macho yakamtoka ,,alipotazama juu ya kaburi hilo,,akaona ule mfuko alioutupa kule kwenye milima ya Nzoka,,uliokuwa na viungo vya mwili wa mwanae,,,ukiwa juu ya kaburi hilo!! akatupa koroboi na kutimua mbio akarudi ndani ya nyumba yake,,,akafunga mlango! punde si punde akasikia kishindo cha kitu kikitua juu ya meza!!!! alipotazama kwa makini akaona ni uleule mfuko!!! akafungua mlango haraka akatimua mbio,,,,kabla hajafika mbali,,mara ghafla!! KIZAAZAA!!!!!! ****ENDELEA***** ule,,mfuko ukajitokeza mbele yake! Nyamwela akazidi kuchanganyikiwa! akatimua mbio kimya kimya bila kupiga kelele,,akaingia ndani ya nyumba yake,,akachukua baiskeli yake akatoka nje na kuondoka zake,,, akaelekea kijiji cha tatu ni kkule alipokuwa anaishi marehemu Muna! akiwa njiani,,ghafla akaanza kuhisi harufu ya damu!mbichi inanuka,,,hofu ikazidi kuongezeka,,akajikuta anashuka kutoka juu ya baiskeli,,na kuitupa kando akaanza kutimua mbio kwa miguu....punde si punde,,,akahisi kama mikono yake imelowana,,,alipojaribu kutazama kwa makini,,hakuweza kutambua kutokana na giza lililokuwa limetanda usiku huo....akanusa mikono yake,,,akahisi ni harufu ya damu inanuka mikononi mwake! Nyamwela akazidi kuchanganyikiwa! sasa hivi akatimua mbio huku akipiga mayowe.. ******************************** Kutokana na hofu aliyokuwanayo alikimbia usiku kucha,,hatimae pakakucha,,,alipotahamaki,,,akaona yupo katika eneo ambalo hajawahi kufika tangu azaliwe,, wasiwasi ulitawala juu yake,,alitembea huku akigeuza shingo yake kuangaza huku na kule...kwa mbali akaona kijiji kimoja kikiwa bondeni,,yani upande wa chini,,,kwa sababu yeye alikuwa upande wajuu alikiona vyema kiji hicho! akaamua kukifuata,,,akatembea kwa hatua za harakaharaka,,na baada ya lisaa limoja na dakika kadhaa akawa amefika katika kijiji hicho! akastaajabu kuona watu wanamshangaa,,,hakujali akaendelea kutembea huku macho yake yakiangaza angaza huku na kule! katika pitapita zake akaona nyumba ambayo haijamalizika ujenzi,,,lakini imeezekwa kwa bati. akazipiga hatua kuifuata nyumba hiyo. kumbe hiyo nyumba ilikuwa ni ya marehemu rafiki yake,,ni yule aliyemfunga kamba kule porini na kumchinja...hakuwahi kumwambia Nyamwela kuwa anajenga nyumba mpya katika katika mashariki ya mbali... Nyamwela akaendelea kuifuata nyumba hiyo,,,akajisemea moyoni,,"hapa ndipo patakuwa makazi yangu,,endapo atatokea mmiliki wa nyumba hii nitamuomba nibaki hapa kwa muda mpaka siku atakayohamia! siku zilizidi kusonga,,,Nyamwela akawa anaishi hapo,,kama makazi yake ya kudumu! ****BAADA YA MWAKA MMOJA KUPITA***** Nyamwela hakuona dalili ya mtu yeyote kujitokeza na kudai kuwa ni mmiliki wa nyumba hiyo,,,akaamua kuweka milango na madirisha ,,akaifanya kuwa nyumba yake,,, maisha yakaendelea,,Nyamwela alikuwa na fani ya uchongaji wa vitanda viti na vitu vinavyotengenezwa kwa mbao! akaamua kuifanya kama kazi yake rasmi,,,akapata wateja wengi hatimae akawa ni mtu maarufu katika kijiji hicho kwa utengenezaji wa vitu vya mbao! Nyamwela akaamua kuoa mwanamke mwingine,,,na maisha yakaendelea,,, siku moja akiwa katika shughuri zake,,,akaonekana mwanamke mmoja akiwa anatembea kando ya barabara,,mwanamke huyo alikuwa kabeba mfuko kichwani! Nyamwela akashtuka! ni baada ya kumuona mwanamke huyo kabeba mfuko wa plastiki ,,,mfuko huo unafanana na ule mfuko ambao aliweka viungo vya mwanae,, macho yakamtoka! akamtazama mwanamke huyo kwa sekunde kadhaa kisha akaendelea na kazi zake. ghafla akanyanyua uso wake kumtazama tena yule mwanamk hakuweza kumuona tena! Nyamwela akaanza kuingiwa na wasiwasi,,,punde si punde akaanza kuhisi harufu ya damu! akahisi mikono yake imelowana,,,alipotazama akaona damu zimetapakaa mikononi mwake!akatimua mbio pasipokujua ni wapi anaelekea,,,akahisi kuchoka akapunguza kasi ya kukimbia,,alipotazama mikono yake hakuiona tena ile damu! Nyamwela akahisi kuchanganyikiwa akaamua kurudi kule kazini kwake,,, alipokaribia kufika,,kwa mbali akaona damu ikiwa imetapakaa kwenye meza anayoitumia kufanyia kazi zake,,,akasita kuendelea kutembea..punnde si punde ile damu ikatoweka na meza ikawa safi,,,ghafla ikasikika sauti ya mtoto mchanga akilia ! sauti hiyo aliisikia nyamwela peke yake,,,,akaanza kuingiwa na hofu,,,akageuza singo yake kutazama huku na kule,,lakini hakuweza kumuona mtoto anayetoa sauti hiyo, sauti hiyo ilizidi kuongezeka,,,hatimae ikwa inasikika ndani ya masikio ya Nyamwela! akatimua mbio kurudi nyumbani,,alikimbia mfululizo bila kusimama hatimae akafika nyumbani kwake,,akafungua mlango kwa pupa akaingia ndani!..akapitiliza mpaka chumbani,,,,akakuta mkewe kalala huku anatokwa na damu nyingi shingoni! akamuita huku akimtikisa,,,ghafla akabadilika,,,akaonekana mtoto aliyekatwa kichwa na mikono! Nyamwela akapiga kelele ghafla mtoto huyo akatoweka!!! mke wa Nyamwela akashtushwa na kelele hizo,,akafumbua macho!! TAHARUKI!!!!!! ITAENDELEA.........

at 3:52 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top