🅱 Professional Love: Riwaya: SAFARI YA MSITU WA SIRI SEHEMU YA SABA(7) ***Ilipoishia*** Nlianza kuingiwa na amani na nikapata matumaini ya kurudi salama nyumbani....mara kwambali naona watu wakikimbia ovyo kila mtu alipita njia yake......nilipotizama vizuri niliona kiumbe kile kimeingia kijijini kwetu... ****Endelea*** niliona wanakijiji wakikimbiahuku na huku kila mmoja alipita njia yake....niliingiwa na wasiwasi kuwa mama yanguatakuwa hatarini... nilitimua mbio kuelekea nyumbani..wakati nakimnia watu walinishanhaa..na kuniona kuwa nimechanganyikiwa...kwanini nikimbilie kule kwenye hatari wakati wao wanakimbia kwaajili ya kwenda kujificha ili waokoe usalama wa maisha yao"",, nilikimbia nikaingia mpaka ndani huku naita MAMA MAMA..... nilipotazama vizuri sikumuona mama nikaamua kutoka nje... nilisikitika sana kuona maiti nyingi za wanakijiji zikiwa zimetapakaa chini kama mchanga"" nilizitazama maiti zile ili niangalie kama miongoni mwa maiti zile huenda nikamuona mama yangu"" nilitazama maiti moja hadi nyingine kwa umakini zaidi...ndipo nikagundua kuwa hienda mama yangu bado Yuhai.....nikakimbia nisijue naelekea wapi....mara kwa mbali nilimuona mama nilifurahi sana nikaita mama kwa kupaza sauti lakini mama hakunisikia kutokana alichanganyikiwa juu ya kiumbe huyu wa ajabu kwa kuuwa watu... ****** nilipoona haisikii sauti yangu nikaamua kukimbia kuelekea ule upande aliokuwa mama...mara ghafla nilimuona kiumbe yule akimfuata mama alikuwa nyuma kama hatua kumi hivi...niliogopa sana...nikapaza sauti tena nikaita mama..mama..ghafla kiumbe kile kikaacha kumfaya mama kikasimama..kikageuza shingo kutazama ule upande niliopo...kiumbe yule alinitazama kisha akaendelea kumfuata mama...nilimuonea huruma mama yangu alikuwa anakimbia huku kanga zikimdondoka.... nikatoa mshale nikauweka kwenye upinde nikauvuta kwa nguvu zangu zote huku nikikumbuka mjomba paul alipokuwa akinifundisha jinsi ya kulenga kitu kikiwa mbali bila kukikosa...nilivuta kisha nikaachia mshale ule""" ulienda moja kwa moja mpaka kwenye mgongo wa kiumbe yule...kutokana na umri mdogo niliokuwa nao nilitumia guvu nyingi kuuvita upinde ule na baada ya kuachia mshale nilidondoka chini nikaishiwa nguvu... "" kiumbe yule alipiga kelele za umivu kwa mngurumo mkubwa sana mpaka nikaogopa....nilikodoa macho nikaona kaacha kumfuata mama yangu kisha akaanza kuja ule upande niliokuwepo...!!!! nilipoona hivyo nilinyanyuka pale chini nikaanza kutimua mbio kuelekea kwenye nyumba yetu..niliiparamia mlango nikaingia ndani na kujifungia.... nilisikitika sana kuona nyumba yetu iliezekwa kwa nyasi hivyo itakuwa rahisi kiumbe yule kuninasa....pia niliwaza kama akifika hapa atahadibu nyumba ili aninase hivyo nyumba itabomoka na tutakosa makazi ya kuishi..... ******** baada ya kuwaza hivyo niliamua kufungua dirisha ili nitoke nje...kutokana na dirisha kuwa juu sana nilishindwa....nikaamua kutoka nje kwa kupitia mlangoni....nilipotazama mbele yangu niliona kiumbe yule wa ajabu kakaribia kabisa hakuwa mbali na nyumba yetu...nilitimka mbio hata sijui naelekea wapi!!!!! wakati nakimbia niliwaza nikimbilie msituni nikajifiche...kiumbe yule wa ajabu atanifuata""hivyo mama yangu pamoja na wanakijiji watapata muda mzuri wa kutafuta maficho wajifiche pia nitakuwa nimeokoa maisha ya wanakijiji waliobakia.... ********* nilikimbia huku napumua pumzi ya kutweta na mapigo yangu ya moyo yaliongezeka kupiga kwa kasi..niligeuka nyuma kutazama yule kiumbe yupo umbali gani nilistahajabu sikumuona kiumbe yule...nilipoona hivyo nikaongeza kasi ya kukimbia...ghafla alijitokeza mbele yangu...nilitoa mshale haraka nikauweka kunako upinde na kuachia mshale ule...ulikwenda moja kwa moja mpaka kwenye jicho la upande wa kushoto mwa kiumbe huyo...alipiga kelele zenye mgurumo mkubwa mpaka ndege waliokuwepo juu ua mti walionekana wakiruka kukimbia mngurumo ule.. kisha kiumbe yule alikimbia na kutokomea...nilijipa moyo nikajisemea moyoni kumbe dawa yako ni mshale jitokeze tena uone....kisha nikatoa mshale mwingine nilipogusa kwa juu kwenye PODO ile ya kubebea mishale niliishiwa nguvu baada ya kuona ulibakia mshale mmoja pekee... kumbi kipindi nakimbia mishale mingine ilidondoka..... wakati bado nimesimama naangaza angaza macho huenda kiumbe yule labda atajitokeza...ghafla niliona JOKA kubwa likitokea kichakani mwiliwangu ulisisimuka kwa uwoga nikapiga hatua kurudi nyuma huku namshangaa nyoka yule kwa ukubwa alionao"" nilijikwaa kwenye kipande cha mti uliokuwepo chini nikadondoka..kumbe kipindi nadondoka ndio wakati kiumbe yule alikuwa akinirukia ili atenganishe kiwiliwili changu kati kwa kati...alijigonga kwenye mti mkubwa uliokuwa pembeni yangu...kisha mti ule ukavunjika na kudondoka chini.. nilinyanyuka pale chini na kianza kutimua mbio nilikimbia kwa kasi hata sikujua naelekea wapi"" nikaona kichaka nikakivaa kichaka kile bila kujali"" kichaka kile kilikuwa na miba mirefu lakini sikuwwza kusikia maumivu miba ilipotoboa ngozi yangu kwa wakati ule.. ****** niliingia katikati kisha nikatulia tuli"" nilikaa kama dakika kadhaa sikusikia kitu chochote upande wa nje....nikaangaza angaza macho huenda nitaona upenyo wa kuona nje...gjafla nilimuona kiumbe yule kajitokeza huku akiangaza angaza macho uake huku na kule...alionesha kukata tamaa..niliona anainua mkono wake uliojaa matawi ya mti mkavu..kisha akaupeleka mpaka usoni akashika ule mshale niliomlenga jichoni..akauchomoa...alipiga kelele safari hii mngurumo uliongezeka..niliogopa sana nikaona anavunja miti iliyokuwa karibu yake... nilijiuliza atakuwa amekasirika baada ya kunikosa eneo lile ndiyo maana anavunja miti.?? ITAENDELEA........ 🅱 Professional Love: Riwaya:SAFARI YA MSITU WA SIRI SEHEMU YA NANE(8) ***Ilipoishia*** nilijiuliza kiumbe yule atakuwa amekasirika baada ya kunikosa eneo lile ndiyo maana anavunja miti.?? ***Endelea*** niliogopa nikaanza kutokwa jasho...nilihisi joto kali sana wakati porini humo kulikuwa na upepo mwanana kutokana na miti mikubwa....nilijiuliza kiumbe huyu atatoka mda gani eneo hili ili niweze kuchoropoka hapa nikimbie nirudi nyumbani..."" kila nikichungulia sioni dalili yoyote ya kiumbe yule wa ajabu kuondoka eneo lile...niliishiwa nguvu nikakosa tumaini nilipochungulia nikaona amekaa...ingawa alikuwa amekaa lakini bado alionekana mrefu sana!!! mikono yake ilienea matawi yaliyoonekana kama yapo kwenye mti mkavu....kalikuwa na sura ya kutisha na macho yake yalikuwa mekundu...ukimtizama kwa harakaharaka unaweza ukasema ni mti..lakini alionekana kuwa na umbile la binadamu.. niliwaza sana nini cha kufanya pia nilikuwa nahisi njaa kali..nilihisi kunamtu tumbini mwangu ananikatakata na kiwembe kwa jisi tumbo lilivyokuwa likiuma njaa...nikapata wazo kuwa nilibakiza mshale mmoja hivyo niurushe upande mwingine mshale ule...yule kiumbe akisikia kitu kinapita katika matawi ya miti ataondoka na kwenda ule upande aliosikia matawi ya miti yakitikisika na kutoa sauti... nilichukuwa mshale ule mmoja uliobaki taratibu nikauweka vyema kunako upinde kisha nikauvuta upinde na kuachia mshale juu ya matawi ya miti...mshale ule ulipokuwa unakwenda kwa kasi ulipita kwenye matawi ya miti na matawi yalitoa sauti kama kunamtu anakimbia huku matawi yakigusa mwili wake... kiumbe yule aliposikia hivyo"" ghafla alisimama na kuanza kukimbia muelekea ule upande niliorusha mshale...nilipohakikisha kiumbe yule yupo mbali nilitoka huku nazipiga hatua za kunyata kutoka kwenye kichaka kile miba ilinichoma lakini sikusikia maumivu...acho yangu niliyakodoa kwa makink kuangalia ule upande ambao kiumbe yu alielekea... ******** Upande mwingine kule kijijini"" wanakijiji walionekana wakilia kwa huzuni kubwa ya kuwapoteza ndugu jamaa na marafiki"",, wanakijiji wengine waliendelea kujitokeza kutokea mafichoni"" mama yake David alikuwa akilia kwa uchungu juu ya mwanae David ......jamani mwangu Davi sijui kama nitakuona tena......kama utakuwa umekufa angalau tu japo nione maiti yako"""" uliniahidi utakuwa tegezi langu nitabaki na nani mie"" aliongea maneno hayo kwa uchungu huku akilia...kutokana na maradhi ya shinikizo la Damu ya kupanda yaliyokuwa yakimsumbua mama david na mawazo juu ya mwanae wa pekee..mama David alipoteza fahamu na kuanguka chini... hakuweza kupata msaada wowote alikuwa yeye peke yake mdani.... ******* kule porini David alinyata kwa hatua kama tatu hivi kisha akaanza kutimua mbio kwa kasi..alikimbia huku anatafuta njia ya kurudi nyumbani......alikimbia jasho lilimtoka aliona hata ule upinde hauna msaada tena kwake hivyo aliutupa... wakati anakimbia huku anaangalia kushoto kulia huenda akaweza kuona njia ya kurudi nyumbani....aligeuka nyuma kutazama labda kiumbe yule anamfuata...alipo geuza shingo kuangalia mbele ghafla alijingonga katikati ya paji la uso kwenye mti mkibwa uliokuwa mbele yake kisha akapasuka usoni akadondoka chini na kupoteza fahamu... ********* kule kijijini watu walilia sana kila nyumba kulikuwa na msiba...inasikitisha sana kiumbe huyu hata hana huruma kwa watoto wadogo...tazama mwanangu kafa eee Mungu ulie juu tunakuomba utuepushie mbali maafa haya uwiii""" alisikima mama mmoja akilia kwa uchungu huku kamkumbatia binti yake wa miaka mitatu akiwa ameuwawa kwa kukanyagwa na yule kiumbe wa ajabu na kupasuka kichwa kabisa...... Nyumbani kwa kinaDavid alionekana mama David bado yupo chini kapoteza fahamu...wakati akiwa katika hiyo hali ya kutokuwa na fahamu aliona vitu vingi alimuona mumewe enzi za uhai wake alimuona marehemu mama yake enzi za uhai wake kisha akamuona david akitafunwa na kiumbe yule wa ajabu alipiga kelele akimwambia yule kiumbe usimuuwe mwanangu...mara ghafla akastuka akapata fahamu.. ******* kule porini wakati huohuo aliozinduka mama David ndio wakati aliozinduka David....kisha David alibaki kalala hapo chini akitafakari ni nini kimemtokea..alihisi maumivu kwenye paji lake la uso alipojigusa sehemu ile aliona damu zikimtoka. UTATA UKAANZA.. ITAENDELEA......... usikose kufatilia muendelezo wa simulizi hii ya kusisimua na ya kutisha iliyojaa maajabu ndani yake. ASANTENI.. 🅱 Professional Love: Riwaya: SAFARI YA MSITU WA SIRI SEHEMU YA TISA(9) *** Ilipoishia*** kule porini wakati huohuo aliozinduka mama David ndio wakati aliozinduka David....kisha David alibaki kalala hapo chini akitafakari ni nini kimemtokea..alihisi maumivu kwenye paji lake la uso alipojigusa sehemu ile aliona damu zikimtoka. ****Endelea**** Ndipo kumbukumbu zikarejea alistuka sana...David alinyanyuka pale chini alipokuwa ameanguka na kupoteza fahamu kisha akaangaza macho huku na kule""" sehemu ile kimya kilitawala haikusikika sauti yoyote zaidi ya sauti za milio ya ndege wa porini....alianza kukimbia huku akiangalia mbele...huku macho yake yalikuwa yakitazama kwa tahadhali kubwa....alitafuta njia ya kuelekea nyumbani lakini hakufanikiwa kuipata....kutokana na njaa kali aliyokuwa naya David alipunguza kasi ya kukimbia na hatimae alianza kutembea lakini kwa tahadhali kubwa...."" ,, akili yake yote iliwaza nyumbani,, alikuwa akimfikiria sana mama yake...mama yangu sijui anaendeleaje? akiwa anatembea kwa mwendo wa kujivutavuta kama gari bovu...njaa ilimzidia hakuweza tena kuendelea kutembea alijisogeza chini ya mti mkubwa akaketi chini ya mti huo..kwa mbali aliona mti wa MKOMA"" alipotazama kwa makini juu ya mti ule aligundua kuwa mti ule ulikuwa unamatunda alinyanyuka pale chini kiufuata mti ule..aliupanda mpaka juu kisha akuchuma matunda na kuanza kula...alikula matunda yale kwa pupa alichuma moja baada ya jingine mfululizo alipohisi kuwa kashiba aliamua kupumzika huko huko juu ya mti""" mara ghafla mvua ikaanza kunyesha... kutokana na miti mikibwa kwenye pori hilo"",,,hivyo mvua ilinyesha kwa wingi mule porini....mvua hiyo iliambatana na upepo mkali sana na ngurumo za radi...David aliogopa sana alikumbatia tawi la mti huku mvua ikimnyeshea...mvua hiyo ilinyesha mfululizo bila kukata..na baada ya masaa mawili upita Bariri lilimzidia David hivyo hakuweza kuendelea kukaa kule juu ya mti aliamua kushuka mpaka chini alitafuta kichaka mara akakiona....alikimbia na kuingia ndani ya kichaka kile...kwa sababu matawi yalibanana kwenye kichaka kile hivyo basi,, maji hayakuweza kupenya kwa wingi kuingia ndani ya kichaka kile...ingawa yaliingia lakini siyo mengi kama ilivyokuwa kule juu ya mti""" ************ upande mwingine""" kule nyumbani mama David alipata wasiwasi sana baada ya kuzinduka...mvua ile iliyokuwa ikinyesha ilimfanya awe na hofu juu ya mwanae david""" kisha akachungulia ule upande ambao pori lilikuwepo alistahajabu kuona mvua kubwa huku ukungu umetanda porini kule...ukungu ule uliweza kufunika hata miti isionekane kabisa....mama David alizidi kuogopa kwa sababu alimuona mwanae alikibilia porini huku akifuatwa kwa nyuma na yule kiumbe wa ajabu....jamani mwanangu sijui utakuwa na hali gani huko ulipo Davi wangu...nakuonea huruma sana mwanangu kwa nini unapata mateso haya angali ukiwa bado kijana mdogo.. Eee Mungu baba muhepushe mwanangu najambo lolote baya litakalo mkuta huko porini....mama david aliyasema maneno hayo huku akilia kwa uchungu mkubwa...kisha akaanza kusali..alipo maliza tu kusali ghafla mvua ile ilianza kupungua na ikakata kabisa.... ******** kule porini david alionekana bado yupo ndani ya kichaka kile kutokana na baridi kali david alitetemeka sana huku midomo yake ikijipigapiga kama mtu anayetafuna kitu ndani ya mdomo!!!! ingawa mvua ilikuwa imeacha kunyesha lakini david bado aliendelea kuwemo ndani ya kichaka kile wakati huo ilikuwa majira ya jioni..kutokana na wingu kubwa lililokuwa limetanda juu ya anga wingu hilo lilifanya kuonekane jioni zaidi kuelekea giza kuanza kuingia...David alitoka mdani ya kichaka kile kwa lingo la kuitafuta njia ya kurudi nyumbani alipotoka tu!!!"",,, ghafla alikutana uso kwa uso na kiumbe yule wa ajabu... ITAENDELEA..... usikose kufatilia simulizi hii ya kusisimua iliyojaa maajabu ya kutisha.

at 10:25 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top