MKASA WA KUSISIMUA: DAH DUNIA HAINA HURUMA - SEHEMU YA PILI #inasikitisha pole sana Danny Ilipoishia........ Katika chumba kile Danny alitokewa na watu wawili wenye mavazi ya kung'aa mfano wa malaika aliingiwa hofu ila alistaajabu kuona sura zao, alikua ni Marehemu baba yake na marehemu mama yake, walimwambia, "USIOGOPE VUMILIA YATAKWISHA" walimuhusia mambo mengi wakamtia moyo, Danny aliwaambia, "Nimechoka naumia sana bora na mimi nife jamani nichukueni tuondoke wote" walimwambia, "USIOGOPE vumilia tu hutokufa, hatuwezi kuondoka na wewe hadi utimize ndoto zako" Danny hakutaka kukubali aliwaambia, "Lazima niondoke na nyie" aliinuka akamrukia mama yake kumkumbatia ila alipomgusa tu alizinduka na kujikuta yupo pale pale chumbani peke yake akiugulia maumivu makali akajua huenda ilikua ni ndoto tu ila ujumbe uliomjia ulimuacha na matumaini mapya maana walimsistiza ASIOGOPE YATAKWISHA. Danny aliishi katika maisha ya mateso vilevile akivumilia. Hatimaye miaka michache baadaye alimaliza darasa la saba kwa bahati mbaya alifeli, Danny aliumia sana akaona sasa ndoto zake zimeyeyuka rasmi, atakua mgeni wa nani bila elimu katika dunia hii ya karaha? Alijiuliza machozi yakimtoka. Mama mdogo wake na baba mdogo wake walimcheka sana na kumwambia, "HIVI KWA UTAHIRA WAKO ULIFIKIRI NA WEWE UTAFAULU KWELI??" Basi wakamwambia, "Bora umefeli umetupunguzia gharama za kukusomesha sasa inabidi ukafanye kazi mjini" alikuja dada mmoja ambae ameolewa mjini na kuwaambia kuwa anashida na kijana wa kazi kuuza dukani, hivyo akawaambia angependa kumchukua Danny kama wapo tayari nae atamlipa vizuri maana anamjua ni Mtoto asiye na sifa mbaya kijijini pale. Mama yake mdogo Danny na baba yake mdogo mzee Koyanza waliridhia kwa shariti kuu moja kuwa Danny afanye kazi ila asilimia 90 ya mshahara wake utumwe kijijini kwa kigezo eti watamtunzia. Dada yule alikubali shariti lile, Danny hakuwa na cha kukanusha au kuuliza, nguvu hiyo aitoe wapi? Alikua anapigiwa hesabu ya kuuzwa kama mbuzi au mtumwa kipindi cha ukoloni na suala la yeye kwenda wala hawakuhitaji idhini yake, Danny yeye alifurahia taarifa ile maana ilikua mwanzo wa neema aliona angalau sasa ataondoka matesoni. Danny alifikishwa mjini na kukabidhiwa biashara ya duka nyumbani kwa bosi, biashara aliikuta ni ndogo ila alipoingia ndani ya miezi 6 ilikua kwa kasi zaidi ya mara 5, dada yule alistaajabu ni nyota ya namna gani anayo Danny. Pamoja na mafanikio yote hayo, Danny aliishi akiambulia chakula tu na fedha kiduchu mno kiasi cha Shilingi 10, 000 kwa mwezi ingine ikitumwa kijijini kwa mzee Koyanza. Jamii ya watu wa mjini waliokua wanalijua duka alilokua anauza Danny walistaajabu, wamama wa uswahilini wakaanza kumuingia Danny ili kupata chochote ila alikataa hata walipowatuma mabinti zao wamtege Danny alikataa na kuweka msimamo kuwa anaheshimu biashara ya boss wake. Walipoona amekua mbishi waliamua kuja kumchongea uongo, wamama watatu wakaleta kesi kwa boss wake wakiwa na mabinti zao wakilalamika kuwa Danny anawatongozaga na kuwahonga ela. Wamama wale wakamuonya boss kuwa biashara yake itakufa kama akiendelea kumuacha Danny auze. Maskini Danny alijaribu kukanusha na kujitetea ila hakusikilizwa, boss wake alikasirika mno akamvaa na kumshushia kipigo kikali akamwambia, "Kama unafikiri ungeweza kuniharibia biashara nisijue basi umefeli, ntakuua mbwa wewe tena ngoja nkurudishe kijijini kwenu mana huna adabu mshenzi wewe" aliongea boss huku akimpiga Danny bila huruma. Usiku ule baada ya kipigo Danny alikuwa chumbani kwake akilia kwa uchungu na maumivu makali sana. Mke wa bosi alimfuata kwa siri na kumuuliza, "Danny kwa nini mdogo wangu mbona nlikuamini sana?!" Danny akitokwa na machozi alimwambia, "Dada tokea umenileta sijawahi kutongoza hata siku 1 wala sijawahi kuhonga hata senti 1 nmekua muaminifu mno kwa kazi yangu ndio maana biashara yenu imekua, ila nasikitika nimesingiziwa hamjataka kunisikiliza mmenipiga kiasi hiki daaah Mwenyezi Mungu atanilipia" Danny alimjibu dada yule kwa huzuni kuu iliyouchoma moyo wake huku akimuonesha makovu ya kipigo alichopata kutoka kwa mume wa dada yule yaani boss. Dada yule mke wa boss alijiskia kufadhaika sana moyoni, akamuuliza Danny, "Kwahiyo ndio mmefikia muafaka gani?!" Danny akamjibu, "Boss kasema nijiandae kesho anakupa nauli unisafirishe kijijini" Dada akajibu, "Ok". Kesho yake Dada yule alipewa nauli ya kumsafirisha Danny, wakaongozana mpaka Ubungo stendi ya mkoa. Wakati wanaelekea ndani kukata tiketi Danny alimsimamisha yule dada na kumwambia, "Dada kwani nauli umepewa kiasi gani?!". Dada yule akamjibu," Nimepewa elfu 80, kwa ajili ya kukukatia tiketi na ingine nkupe uende nayo kijijini." Danny alimwambia dada yule, "Nakusihi dada unipe hiyo ela ukirudi waambie umeshanipakiza naenda kijijini ila kiukweli mimi siwezi kurudi kule kijijini kwetu kwa baba mdogo mzee Koyanza na mama mdogo ntateseka sana bora nipambane huku huku Dar na vijana wenzangu naamini sitoshindwa kuishi fursa zipo nyingi " Alimsimulia maisha ya mateso aliyopitia hadi pale alipofikia dada yule alistaajabu na kuingiwa roho ya huruma, alitoa zile hela akampatia akampa na namba yake ya simu akamwambia akiwa na shida yoyote ambipu ataangalia namna ya kumsaidia. Wakaagana dada akapanda daladala kurudi nyumbani je nini kilifuata katika maisha mapya ya Danny? Tukutane sehemu ya 3 wiki ijayo USIKOSE Kama mateso anayopitia Danny yamekugusa kwa namna moja au usipite bila kutoa neno la POLE KWA DANNY kisha SHARE mkasa huu uwafikie wote katika jamii wanaonyanyasa na kuwatesa watoto yatima na masikini. Nakutakia Jumapili Njema, Mungu Akubariki

at 10:54 PM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top