Home → simulizi
→ ®HADITHI PICHA®
Mussabhai & YuYuShortstory
👙👙👙 DADA VUA👙👙👙
PICHA NO:_13
LIKE PAGE UWE WA KWANZA KUIPATA HII KILA SIKU.
https://www.facebook.com/YuYuTzHotStory
HAYA HAYAAA ZILE SIDIRIA AMBAZO KWA SASA NDO HABARI YA MUJINI TUNAZO
KAZI KWENU MASTISA DUU
UKIVAA MUGONGO WAZI KWA AJILI YA MTOKO NDO ZENYEWE HAZINA MIKANDA
NZURI KWA MABIBI HARUSI PIA
UKINUNUA LEO UTAUZIWA KWA BEI YA OFA
30000
WAHII KABLA OFA HAIJAISHA
TUPO DAR
MIKOANI TUNATUMA ILA BAADHI YA MIKOA TUNA MAWAKALA
mawasiliano
0711462866
0711462866 WhatsApp
TUNAUZA JUMLA PIA
Bonyeza link hapo chini kuangalia jinsi ya kuzivaa
👇👇👇👇
https://youtu.be/oWwe9rFZaxo
..........ilipoishia
Huku kwa kina Helena tayari Lucy alisharejea katika hali yake ya kibinadamu na wakati huohuo Sule alionekana anaondoka.Kwa kuwa helena alikuwa amepewa kazi ya kumzuia sule asiondoke bila kunywa kinywaji kile alichopewa na Shangazi,Basi alimfuata sule akiwa na kile kinywaji kujaribu kama hilo litawezekana.....
Endelea......NAOMBA LIKE YAKO MTU WANGU.
Basi Helena aliutumia tena usichana wake kumshawishi Sule anywe kinywaji kile.Basi helena alimfuata sule mpaka alipo kisha akamwambia"sule naomba unisamehe mimi pamoja na shangazi yangu,Na pia shangazi kasema haina haja ya wewe kuondoka kwani umeshakuwa mtu wa karibu katika familia yetu".Sule alimtazama kwa umakini kisha akajiuliza,"Mmmmmh!! inawezekana vipi shangazi anifume na wote hawa na bado aniambie nimekuwa mwana familia!!?" Sule kwa akili yake fupi aliwaza kisha akagundua kuwa shangazi alikuwa anamchora pengine anamuitia polisi.Helena hakuishia hapo alizidi kuingea"Aaaamh! na pia kama umeamua kuondoka basi chukua kinywaji hiki kunywa ili uendako usinisahau".Sule alipokea kikombe kile kikiwa na kinywaji ndani tayari kabisa kwa kunywa.
Sule alishangaa kuona helena anabembeleza sana ili anywe kinywaji hicho.Sule machale yalimcheza akamrudishie helena kile kikombe na hakutaka kunywa kabisa"Helena pleas siwezi kunywa kinywaji hiki"........"Sule inamaana hunipendi kabisa babaaa!! mbona yale yashapita jamouny"........Sule taaratibu maneno ya mtoto wa kike yalianza kumuingia lakini nafsi yake ikawa na mashaka kwani mazingira anayopewa hicho kinywaji yalimpa hofu sule alijiuliza"Sasa kwa nini wasinipe wakati ule nilipokuja saizi nataka kuondoka ndio wanipe!! hapana hapa kuna kamchezo"Sule aliangalia kwa mbali alimuona Lucy na shangazi yake wakitazama jinsi anavyopewa kinywaji kile na bidada helena,Na hapo ndipo Sule alipoghairi kabisa swala la yeye kunywa hicho kinywaji.
HUKU NYUMBANI ALIPO MAMA YAKE SULE MAMBO YALIKUWA HIVI,
Mama yake sule baada ya kuona anakabidhiwa nyaraka na hati miliki za mali zao alianza kuingiwa na tamaa.Alitoa nje na kuanza kuzitazama gari zilivyopark pamoja na nyumba ilivyo nzuri,Aliangalia huku akionekana kama kuna jambo analitafakari kichwani.Mama yake sule aliingia ndani kisha akachukua simu yake na kuanza kutafuta namba,Alipofika kwenye namba ya Bi kidako aliitazama huku akionekana kujishauri kuipiga,Lakini aliikaza roho na kupiga.
"Haloo!! shikamoo bibi!!?"
📲marhaba mwanangu habari zenu huko
"Hatujambo kabisa vipi kuhusu swala la sule?"
📲Sule niko naye hapa ndio nafanya mpango jinsi ya kumfanya arudi
"Ooooooh!! ahsante sana kumbe tayari uko naye sasa tutampata vipi"
📲Atakuja usiku huu huu haitafika saa nne
"Sasa bibi naomba unisaidie kitu"Mama yake sule aliongea huku akipepesa macho kuangalia kama yuko mwenyewe.Aligundua kuwa yuko mwenyewe na ndipo alipomwambia maneno haya bi kidako.
📲 sema tuu mwanangu
"Aaaamh!! unajua mi sitaki kabisa kuishi na huyu mwanaume na nataka ufanye jambo hapo"
📲 kwa hiyo wataka tufanye nini?
"Kesho anasafiri sasa nataka akienda huko iwe ndio mwisho kuiona tanzania na ukikubali kunifanyia hivyo nitakupatia milioni 20 kama zawadi na nitakujengea nyumba nzuri hapa mjini kama utataka ila kama utataka huko huko pia sawa"
📲Sawa lakini ni ngumu sana ila nitajitahidi lakini uwe makini sana kwani ni hatari,Nitafanya hivyo lakini nakusihi tena kuwa makini na naomba akishaondoka tuu ukuje huku na pia chakula cha wanao kimekwisha uje nacho.
"Yaani nitashukuru sana kama hilo jambo litafanikiwa sasa mimi kesho nakuja huko lakini hakikisha sule aje huku leo ili kesho tufanye hii niliyokuambia"
Yaani hapa wamekutana Mganga ana tamaa na mama yake sule ndio balaa.Walikubaliana kisha mama yake sule alikata simu,Wakati anageuka tuu alikutana uso kwa uso na kijana wake Wedi,Mama alishtuka sana alionekana kama ana wasiwasi kutokana na kile alichokuwa anazungumza kwenye simu.Alivuta pumzi kisha akaongea"Hujambo mwanangu??"......Wedi alimjibu"Yaani mama una bahati nilikuwa nije nikufumbe macho sema umewahi kugeuka"Wedi aliongea kisha akanyanyua funguo ya gari juu huku akimwambia mama yake"Supriseee!!!!!"......"Mama alishangaa sana"Whaaat!!"....Wedi alimwambia"Njoo uone huku nje.Mama alivyotoka nje alishangaa kukuta gari 2 zimepark nje moja ina plat namba imeandikwa MAMA na nyingine imeandikwa BABA.
Wakati huo mzee alikuwa ndani anajiandaa andaa kwa ajili ya safari yake.Mama alipigwa butwaa kwani ni jambo linaloshtua sana kitendo cha watoto kuwapa magari sio kitendo kidogo.Wakati wanashangaa mara sudi alitoka ndani akiwa amemziba baba yake macho mzee alikuwa anaongea ongea huku anacheka"Halafu nyie watoto mna masihala mjue huuhuuhu!! angalia usinigongeze mlangoni oohooo!!"Sudi aliwaambia"Shiiiiiii!!"Yaani wanyamaze kisha akampeleka mpaka pale mbele ya gari na kumwambia "Ebu papasa hapo" Mzee alipoligusa tuu lile gari na Sudi akamuachia macho,Basi mzee aliangalia kisha Sudi akamkabdhi ufunguo huku akisema"Tumefurahi sana kitendo cha nyie kuona umuhimu wetu hasa hasa mama kwani bila yeye nahisi usingewaza kutufanyia hivi baba yetu,Na tumeona tufanye hivi kabla haujasafiri baba yetu".Basi ilikuwa ni furaha kubwa kwenye familia ile,Kwanza walipiga picha nyingi mno mavinywaji nyalitolewa ndani walikunywa na mpaka basi.
Upande wa pili kule Sule aligomea kabisa kunywa kinywaji cha Helena.Sule alimwambia"Mbona unaning'ang'aniza sana kwanza sitaki hicho kinywaji hata wewe pia sikutaki tena"Sule aliongea kwa hasira kisha akawa anaondoka.Shangazi yake Helena alikuwa kwa mbali anatazama,Alivyoona sule amekataa alisema "Ahaaaaa!! unajifanya mjuaji eeeeh!! ngoja nikuonyeshe adabu" Aliongea huku akiingia ndani...........Nini kitafuata?? usikose sehemu inayofuata.
PATA SIMULIZI 4 TOFAUTI KWA SIKU UWAPO KATIKA GROUP LA KIJANJA KULE WHATSAPP.STORY ZOTE NI HOT NA UNAZIPATA MAPEMA YAANI ZIKIWA ZAMOTO KABISA KAZI KWAKO,JIUNGE NA WENZAKO KWA TSH 3000/-TUU ZA KITZ
Kwa wewe unayehitaji kuungwa group nicheki kupitia 0678641147 au 0688911112 whatsapp ni kuhusu simulizi tuu mambo mengine nicheki fb inbobo
KAMA HUJALIKE PAGE FANYA IVO SASA ILI UWEZE KUPATA VITU MUBASHARA.
#MussaBhai & #YuYuTz_ ®Newvission_2017
®HADITHI PICHA® Mussabhai & YuYuShortstory 👙👙👙 DADA VUA👙👙👙 PICHA NO:_13 LIKE PAGE UWE WA KWANZA KUIPATA HII KILA SIKU. https://www.facebook.com/YuYuTzHotStory HAYA HAYAAA ZILE SIDIRIA AMBAZO KWA SASA NDO HABARI YA MUJINI TUNAZO KAZI KWENU MASTISA DUU UKIVAA MUGONGO WAZI KWA AJILI YA MTOKO NDO ZENYEWE HAZINA MIKANDA NZURI KWA MABIBI HARUSI PIA UKINUNUA LEO UTAUZIWA KWA BEI YA OFA 30000 WAHII KABLA OFA HAIJAISHA TUPO DAR MIKOANI TUNATUMA ILA BAADHI YA MIKOA TUNA MAWAKALA mawasiliano 0711462866 0711462866 WhatsApp TUNAUZA JUMLA PIA Bonyeza link hapo chini kuangalia jinsi ya kuzivaa 👇👇👇👇 https://youtu.be/oWwe9rFZaxo ..........ilipoishia Huku kwa kina Helena tayari Lucy alisharejea katika hali yake ya kibinadamu na wakati huohuo Sule alionekana anaondoka.Kwa kuwa helena alikuwa amepewa kazi ya kumzuia sule asiondoke bila kunywa kinywaji kile alichopewa na Shangazi,Basi alimfuata sule akiwa na kile kinywaji kujaribu kama hilo litawezekana..... Endelea......NAOMBA LIKE YAKO MTU WANGU. Basi Helena aliutumia tena usichana wake kumshawishi Sule anywe kinywaji kile.Basi helena alimfuata sule mpaka alipo kisha akamwambia"sule naomba unisamehe mimi pamoja na shangazi yangu,Na pia shangazi kasema haina haja ya wewe kuondoka kwani umeshakuwa mtu wa karibu katika familia yetu".Sule alimtazama kwa umakini kisha akajiuliza,"Mmmmmh!! inawezekana vipi shangazi anifume na wote hawa na bado aniambie nimekuwa mwana familia!!?" Sule kwa akili yake fupi aliwaza kisha akagundua kuwa shangazi alikuwa anamchora pengine anamuitia polisi.Helena hakuishia hapo alizidi kuingea"Aaaamh! na pia kama umeamua kuondoka basi chukua kinywaji hiki kunywa ili uendako usinisahau".Sule alipokea kikombe kile kikiwa na kinywaji ndani tayari kabisa kwa kunywa. Sule alishangaa kuona helena anabembeleza sana ili anywe kinywaji hicho.Sule machale yalimcheza akamrudishie helena kile kikombe na hakutaka kunywa kabisa"Helena pleas siwezi kunywa kinywaji hiki"........"Sule inamaana hunipendi kabisa babaaa!! mbona yale yashapita jamouny"........Sule taaratibu maneno ya mtoto wa kike yalianza kumuingia lakini nafsi yake ikawa na mashaka kwani mazingira anayopewa hicho kinywaji yalimpa hofu sule alijiuliza"Sasa kwa nini wasinipe wakati ule nilipokuja saizi nataka kuondoka ndio wanipe!! hapana hapa kuna kamchezo"Sule aliangalia kwa mbali alimuona Lucy na shangazi yake wakitazama jinsi anavyopewa kinywaji kile na bidada helena,Na hapo ndipo Sule alipoghairi kabisa swala la yeye kunywa hicho kinywaji. HUKU NYUMBANI ALIPO MAMA YAKE SULE MAMBO YALIKUWA HIVI, Mama yake sule baada ya kuona anakabidhiwa nyaraka na hati miliki za mali zao alianza kuingiwa na tamaa.Alitoa nje na kuanza kuzitazama gari zilivyopark pamoja na nyumba ilivyo nzuri,Aliangalia huku akionekana kama kuna jambo analitafakari kichwani.Mama yake sule aliingia ndani kisha akachukua simu yake na kuanza kutafuta namba,Alipofika kwenye namba ya Bi kidako aliitazama huku akionekana kujishauri kuipiga,Lakini aliikaza roho na kupiga. "Haloo!! shikamoo bibi!!?" 📲marhaba mwanangu habari zenu huko "Hatujambo kabisa vipi kuhusu swala la sule?" 📲Sule niko naye hapa ndio nafanya mpango jinsi ya kumfanya arudi "Ooooooh!! ahsante sana kumbe tayari uko naye sasa tutampata vipi" 📲Atakuja usiku huu huu haitafika saa nne "Sasa bibi naomba unisaidie kitu"Mama yake sule aliongea huku akipepesa macho kuangalia kama yuko mwenyewe.Aligundua kuwa yuko mwenyewe na ndipo alipomwambia maneno haya bi kidako. 📲 sema tuu mwanangu "Aaaamh!! unajua mi sitaki kabisa kuishi na huyu mwanaume na nataka ufanye jambo hapo" 📲 kwa hiyo wataka tufanye nini? "Kesho anasafiri sasa nataka akienda huko iwe ndio mwisho kuiona tanzania na ukikubali kunifanyia hivyo nitakupatia milioni 20 kama zawadi na nitakujengea nyumba nzuri hapa mjini kama utataka ila kama utataka huko huko pia sawa" 📲Sawa lakini ni ngumu sana ila nitajitahidi lakini uwe makini sana kwani ni hatari,Nitafanya hivyo lakini nakusihi tena kuwa makini na naomba akishaondoka tuu ukuje huku na pia chakula cha wanao kimekwisha uje nacho. "Yaani nitashukuru sana kama hilo jambo litafanikiwa sasa mimi kesho nakuja huko lakini hakikisha sule aje huku leo ili kesho tufanye hii niliyokuambia" Yaani hapa wamekutana Mganga ana tamaa na mama yake sule ndio balaa.Walikubaliana kisha mama yake sule alikata simu,Wakati anageuka tuu alikutana uso kwa uso na kijana wake Wedi,Mama alishtuka sana alionekana kama ana wasiwasi kutokana na kile alichokuwa anazungumza kwenye simu.Alivuta pumzi kisha akaongea"Hujambo mwanangu??"......Wedi alimjibu"Yaani mama una bahati nilikuwa nije nikufumbe macho sema umewahi kugeuka"Wedi aliongea kisha akanyanyua funguo ya gari juu huku akimwambia mama yake"Supriseee!!!!!"......"Mama alishangaa sana"Whaaat!!"....Wedi alimwambia"Njoo uone huku nje.Mama alivyotoka nje alishangaa kukuta gari 2 zimepark nje moja ina plat namba imeandikwa MAMA na nyingine imeandikwa BABA. Wakati huo mzee alikuwa ndani anajiandaa andaa kwa ajili ya safari yake.Mama alipigwa butwaa kwani ni jambo linaloshtua sana kitendo cha watoto kuwapa magari sio kitendo kidogo.Wakati wanashangaa mara sudi alitoka ndani akiwa amemziba baba yake macho mzee alikuwa anaongea ongea huku anacheka"Halafu nyie watoto mna masihala mjue huuhuuhu!! angalia usinigongeze mlangoni oohooo!!"Sudi aliwaambia"Shiiiiiii!!"Yaani wanyamaze kisha akampeleka mpaka pale mbele ya gari na kumwambia "Ebu papasa hapo" Mzee alipoligusa tuu lile gari na Sudi akamuachia macho,Basi mzee aliangalia kisha Sudi akamkabdhi ufunguo huku akisema"Tumefurahi sana kitendo cha nyie kuona umuhimu wetu hasa hasa mama kwani bila yeye nahisi usingewaza kutufanyia hivi baba yetu,Na tumeona tufanye hivi kabla haujasafiri baba yetu".Basi ilikuwa ni furaha kubwa kwenye familia ile,Kwanza walipiga picha nyingi mno mavinywaji nyalitolewa ndani walikunywa na mpaka basi. Upande wa pili kule Sule aligomea kabisa kunywa kinywaji cha Helena.Sule alimwambia"Mbona unaning'ang'aniza sana kwanza sitaki hicho kinywaji hata wewe pia sikutaki tena"Sule aliongea kwa hasira kisha akawa anaondoka.Shangazi yake Helena alikuwa kwa mbali anatazama,Alivyoona sule amekataa alisema "Ahaaaaa!! unajifanya mjuaji eeeeh!! ngoja nikuonyeshe adabu" Aliongea huku akiingia ndani...........Nini kitafuata?? usikose sehemu inayofuata. PATA SIMULIZI 4 TOFAUTI KWA SIKU UWAPO KATIKA GROUP LA KIJANJA KULE WHATSAPP.STORY ZOTE NI HOT NA UNAZIPATA MAPEMA YAANI ZIKIWA ZAMOTO KABISA KAZI KWAKO,JIUNGE NA WENZAKO KWA TSH 3000/-TUU ZA KITZ Kwa wewe unayehitaji kuungwa group nicheki kupitia 0678641147 au 0688911112 whatsapp ni kuhusu simulizi tuu mambo mengine nicheki fb inbobo KAMA HUJALIKE PAGE FANYA IVO SASA ILI UWEZE KUPATA VITU MUBASHARA. #MussaBhai & #YuYuTz_ ®Newvission_2017
Artikel Terkait
MUUZA MAZIW EP 07 “aaaaahh!! Jamani wifi wao!!” Aliongea kwa furaha baada ya kumuona mgeni aliyekuwa akigonga ni penina. “asante wifi , shikamoo!” Penina aliongea na kisha kumkumbatia wifi yake kwa furaha. “ marhaba wifi ,vipi masomo?” Aliongea huku akiipokea mizigo aliyo ibeba “naendelea vizuri tu wifi” “haya mungu akusaidie” Aliongea lisa na kuelakea sebuleni , aliiiweka mizigo pembeni ya kochi na kasha kuelekea sehemuk ilipo friji. Penina, penina akaamua kuichukua mizigo ili aipeleke chumbani. “hapana wifi, hapana , hiyo iache hapo hapo nitaiingiza mwenyewe,, wewe kwanza kunywa juisi upumzike.“ Aliongea lisa huku akiwa ameshikilia jagi lenye juisi pamoja na glasi, alifanya hivyo kwa sababu chumba anachotakiwa kulala penina ndicho chumba ambacho amemficha muuza maziwa. “usipate tabu wifi wangu kunywa juisi upumzike, nipo kwa ajili yako “ Aliongea lisa huku akiibeba mizigo na kuelekea chumbani na kumuacha penina akinywa juisi taratibu. Alipoingia chumbani alimshutua muuza maziwa na kumweleza hali halisi. “kwahiyo nitatoka saa ngapi humu?” “ itabidi uvumilie mpaka usiku wifi akilala , mlango wa nje nitauacha wazi leo” Aliongea lisa “Sawa lakini vipi kuhusu chakula manaake niana njaa” “ usijali nitakuletea utakula humu humu , jitahidi usitoke nitajaribu kufanya mpango hata kamakabla ya usiku ikiwezekana” “poa” Muuza maziwa aliitikia “alafu nitaa……” Lisa alikatiza kauli yakebaada ya kusikia mlio wa kitasa kikifunguliwa. Haraka haraka muuuza maziwa aliingia kabatini na kisha lisa aliufunga mlango wa kabati hiyo kabla hata hajauachia mlango huo alisikia sauti nyuma yake. “wifi mbona unagombana na hilo kabati!?” Swali hilotoka kwa penina lilimfanya lisa ashikwe na kigugumizi cha ghafla huku akitoa maelezo ya kujikanyagakanyaga. “ah, mh, a-, u-n-a-j-u-a hi-li ka-ba-ti ni bo-vu” “limeharibika , ooh, mungu wangu!” Penina aliongea huku akilisogelea kabati hiloili kuiangalia sehemu ilipoaribika. “ah, hapana wifi usiiguse hapa nimeitegesha , iache hivyo hivyo mpaka atakapokuja fundi kulirekebisha” Aliongea Lisa haraka haraka. “okey”[sawa] Aliongea Penina huku akitikisa kichwa kuonyesha kwamba ameelewa. “nataka kuoga wifi” “na kweli manaake umechoka kweli kweli wifi yangu” Aliitikia Lisa haraka haraka kwani alijua huo ndio upenyo wa kumtoa muuza maziwa. Na kweli penina alipoingia bafuni lisa aliufungua mlango wa kabati haraka na kumtoa muuza maziwa , akala chakula haraka na kuanza safari ya kutoka nje ya nyumba hiyo , walipofika kwenye mlango wa kutokea muuza maziwa alimbusu lisa kwa mara ya mwisho , alipomaliza kufanya hivyo alitoka ndani ya chumba hicho na kutokeza koridoni ili atoke nje kabisa ya nyumba hiyo lakini kabla ya kufanya hivyo alisikia muungurumo wa gari, halikuwa gari lingine bali gari la Jerry mume wa Lisa. Hofu iliwaingia kwa ghafla na haraka haraaka walirudi tena chumbani kwa penina , ambapo kama kawaida alimfungia muuza maziwa kabatini, hawakuwa na njia nyingine tena bali hile waliyoipanga awali, muuza maziwa asubiri mpaka usiku wa manane Penina atakapo lala ndipo atoke kwani Lisa atauacha mlango wa kutokea wazi. Lisa alipomaliza kumfungia muuza maziwa katika kabati alitoka nje ya chumba hicho,akiwa koridoni aligongana ana kwa ana macho na mumewe. Wote wawili waliinamisha vichwa vyao chini. Kwani kila mmoja aliona aibu kwa kumsaliti mwenzake. Lisa kwa muuza maziwa na Jerry kwa sekritari wake. “Ah, mmh, wifi amekuja , kakaribu!” Aliongea Lisa kwa kujiumauma huku akiwa na wasi wasi. “ asante amekuja saa ngapi?” “sio muda mrefu” “aah yuko wapi sasa nimsalimie?” “yuko bafuni anaoga” “Okey” [sawa] Aliitikia na kisha kuelekea chumbani kwake. Lisa nae alimfuata mumewe nyuma hukubado akiwa na hofu juu ya kugundulika kwa uwepo wa muuza maziwa ndani ya nyumba hiyo. “Pole na kazi dear” Aliongea Lisa huku akijibaraguza kwa kumvua tai mume wake, macho yake bado yalikuwa na aibu sababu bado alikuwa na wasi wasi kwamba labda mumewe amegundua chochote. “ah, asante mpenzi” Aliitikia Jerry huku akitabasamu, lakina nae pia tabasamu lake liliishia mdomoni tu moyoni nafsi ilimsuta . Maovu aliyoyafanya na sikritari wake ofisini kwake yalikuwa bado yakionekana katika kichwa chake. Akavua nguo na kuingia bafuni kuoga lisa nae alimfuata na kujumuika nae kuoga . Alifanya hivyo ili Jerry hasihisi chochote. Walioga huku kila mmoja akiwa hana habari na mwenzake. Kwani wote wawili walikuwa wamechoka, walipomaliza kuoga wakavaa na kasha kwenda sebuleni. Huko wakamkuta Penina akianga lia tv. “mdogo wangu huyo!” Jerry aliongea kwa furaha huku wakicheka. “kaka!” Penina aliitikia na kisha kumkimbilia kaka yake. “waoo!!!” Waliongea kwa pamoja na kisha kukumbatiana kwa furaha. “habari za masomo!?” ITAENDELEA.. ... Read More
*Love bite* Sehemu Ya Kwanza (1) Ni siku ya jumapili iliyokuwa na kila aina ya mchanganyiko wa watu kutoka sehemu mbali mbali walionekana kwenye kumbi za starehe. Wengi ambao walikua wanapenda taarab basi walijazana travertine hotel kuwaangalia jahazi. Kwa wengine wanaopenda bongo flavour basi walikutana bills,maisha,masai..Dar live na kumbi zingine zilikuwa na wasanii pendwa waliokuwa wanaburudisha week end hiyo. JOTHAN alikua anapendelea sana mixing za ma dj mbali mbali. Hivyo jumapili hiyo aliamua kwenda coco beach usiku huo. Upepo mwanana uliokuwa ukipuliza huko coco beach na ukichanganya na big screen iliyokuwa inaenda sambamba na mixing za maana alizokuwa anazipiga dj huyo aliyezikonga roho za watu wengi waliokuwa pale, iilikuwa burudani tosha kwa waliohudhuria usiku ule. Jotham alipaki gari yake pembeni, alichagua kiti kilichukokuwa karibu na meza ya mwisho na kuagiza kinywaji alichokipendelea na kuendelea kufurahia mziki uliokuwa unaonyeshwa kwenye screen hiyo. Mara kwa mara madada poa walikuwa wanajipitisha pale alipo, lakini aliwachora tu na hakuwa na mpango nao. Baada ya dakika kadhaa, walitokea madada watatu waliokuwa wameingia pale coco beach na kuanza kutafuta mahali pa kukaa. Waliangaza meza nyingi zilikua na nafasi ya mtu mmoja au wawili tu na wao walikuwa na lengo la kukaa wote watatu kwenye meza moja. Baada ya kuangaza kwa muda, waliiona meza aliyokaa Jothan ikiwa na nafasi tatu za kukaa. Waliisogelea ile meza na walipokaribia tu kuifikia ile meza. Walishuhudia jamaa mmoja akiwa ameenda kukaa pale. “wewe kaka sogea sehemu yetu.” Aliongea mmoja kati ya wale wadada watatu baada tu ya kuifikia ile meza. “mbona hakuna alama yoyote kuwa mlikaa hapa. Hakuna vinywaji wala kitu chochote.” Aliongea yule jamaa huku akionyesha wazi kuvutiwa na ile sehemu iliyokuwa chemba lakini ikiwa inaonyesha vizuri ile tv. “ni vyema uwapishe kwa sababu waongeacho sio uongo.” Aliongea Jotham kumwambia yule jamaa. Hakuwa anapenda makelele ambayo alijua yatatokea baada ya mvutano huo wa kugombania ile sehemu. Yule jamaa akaamua kunyanyuka na kuwapisha wale warembo na yeye kwenda kukaa meza nyingine. “ahsante sana kaka, maana yule jamaa alitaka atubanie wakati sisi tumehangaika kutafuta meza tutakayokaa wote watatu”. Aliongea yule dada aliyeonekana kama kiongozi wao. Mavazi waliyovaa yalitosha kumshawishi mvulana yeyote rijali na kufanya iwe lazima macho ya matamanio kumtoka. Uzuri wa mabinti hao likuwa unashinda lakini huyo aliyekuwa kiongozi wao aliwazidi wenzake kwa kila kitu. Macho ya Jotham yaliona kila kitu kutoka kwa binti huyo mbichi. Chuchu zilitokeza kwa kujichora kwenye gauni ile nyepesi ambayo haikuwa na nguo nyingine ndani. “sikiliza oda zao, ziingize kwenye bili yangu” aliongea Jotham baada ya kumuita muhudumu aliyekuwa anamuhudumia toka afike pale. “ahsante.” Waliitikia wale madada baada ya kupewa ofa hiyo. Waliagiza vyakula na vinyaji walivyopendelea. Walipiga story za kawaida huku wakigongeana glass za vinywaji na kucheka. Jotham alikuwa kimya wakati wote huku akiwa bize kuangalia na kusikiliza mixing ambazo ndizo zilizomleta pale. Baada ya masaa kadhaa, alimuita muhudumu na kulipia bili yake. “ahsante kwa ofa yako.” Aliongea yule kiongozi wao baada ya Jotham kuwaaga. Jotham aliingia kwenye gari yake aina ya opah na kuondoka eneo hilo. Njiani alimkumbuka yule dada lakini aliishia kucheka tu kwakua hakuwa na hisia zozote za mapenzi juu yake. Zaidi alimtamani kuwa nae japo kwa usiku mmoja kwa jinsi alivyotoka. Hakika alikuwa na kila aina ya uchochezi wa kufanya ngono. Alifika kwake usiku mnene na kwenda kulala fofofo kutokana na usingizi uliojaa wakati huo. Asubuhi aliamka na uchovu tele na kwenda kuoga ili kujaribu kuupunguza uchovu aliokuwa nao. Alipomaliza kuoga. Alijiandaa tayari kwa kwenda kazini. Alisumbuka sana kuwasha gari lake lakini halikuwaka. Alipoangalia mafuta, aligundua kuwa wese lilikuwa limekata. Kwa kuhofia kuchelewa zaidi kazini, aliamua kwenda kituoni na kupanda daladala. Alifika kazini huku macho yake yakiwa mekundu yaliyoashiria kuwa bado alikuwa na usingizi. “mshikaji bora ukapate supu, maana hiyo harufu ya pombe uliyamka nayo ni noma. Utaongea vipi na bosi?” alishauri mmoja wa wafanyakazi wenzake aliyekuwa karibu naye. “poa, ngoja nielekee canteen basi.” Aliongea Jothan na kwenda canteen kupata supu ya mbuzi na chapati. Baada ya kunywa chai, alirudi na kuendelea na kazi. Saa nane ndio muda waliokuwa wanatoka kazini. Alienda kupata chakula cha mchana canteen na kuondoka zake kuelekea kituo cha daladala ambacho hakikuwa mbali na ofisini kwao. Alisubiri daladala kwa muda na kupanda gari iliyokuwa inaelekea mwenge kwa malengo ya kushuka kinondoni anapoishi. Usingizi ulichukua nafasi yake baada ya kupanda tu lile gari lililokuwa likisubiri abiria kwa dakika kadhaa pale kituoni Baada ya muda mrefu kidogo kupita, aliamka na kuangalia gari lilikuwa limefika wapi. Wakati akiwa anaanga angaza, macho yake yaligongana na yule mrembo aliyekuwa naye kwenye meza moja siku ya jana yake. Wote walikumbukana na kila mmoja akamuachia mwenzake tabasamu. Hapo alifanikiwa kumuona vizuri huyo msichana mwenye kila sifa ya uzuri. Usingizi uliendelea kumzonga Jotham na kujikuta anapitiwa na usingizi bila kuongea chochote na yule msichana. Gari lilifika mpaka mwenge na kupitiliza kituo alichokua anashuka Jothan. Aliamshwa na konda baada gari kushusha abiria wote. “tuko wapi hapa.” Aliuliza Jothan baada ya kuamka na kuangalia nje ambapo kulikua tofauti na mazingira anayoishi. “tumeshafika mwenge kaka.” Alijibu yule konda. Jothan aliangalia huku na kule na hakuona abiria yeyote aliyekuwa kwenye lile gari zaidi yake. Hakusikitika kupitishwa kituo, bali alisikitika sana kutochukua namba wala kujua jina la yule msichana aliyevutika naye zaidi baada ya kuonana nae kwa mara ya pili. Hakua na budi Jotham, zaidi ya kubaki ndani ya daladala na kugeuza nalo. Alipofika kinondoni kwa manyanya alishuka na kufuata njia ilyoelekea shule ya kambangwa secondary school na kupita chuo cha tumaini na kuingia nyumbani kwake ambapo hapakuwa mbali na pale. Hakuwa na hela nyingi sana, ila uwezo wa kula anachokitaka na kubadilisha nguo alikuwa nao. Alifika nyumbani na kujilaza kitandani kwake. Aliamka sa tatu usiku na kutoka kwenda sheli kununua mafuta kwenye kidumu kisha akaenda bar ya jirani na kupata chipsi kuku kisha akarudi nyumbani na kufungua tv na kuangalia yaliyomo. Saa tano usiku alianza kunyemelewa na usingizi,. Alizima tv yake na kwenda kulala. Alijikuta yupo na msichana yule mzuri kwenye fukwe za bahari wakipanga maswala yao ya kuoana. Alitoa pete na kumvisha mwanamke huyo mwenye kila aina ya sifa zilizompeleka Jotham kudata juu yake. Alikurupuka asubuhi na kugundua kuwa hali ile haikuwa halisi, bali alikua anaota.. aliangalia Alarm yake ambayo ilikuwa inalia wakati huo na kuizima. Alijiandaa na kupanda gari yake ambayo alishainunulia mafuta na kwenda nayo kazini kama kawaida. Baada ya mwezi mmoja kupita, Jothan alipata uamisho kikazi kwa miezi sita huko Morogoro. Alilaani ila hakua na jinsi kukubaliana na matakwa ya kazi. Ile ndoto ya kukutana tena na yule msichana iliyeyuka kwakua alijua kabisa kuwa kukaa kwake huko marogoro utakuwa mwisho wa kukutana tena na yule msichana kwa miezi mingi. Siku ya safari ilipofika. Alijiandaa na kupitiwa na gari la ofini kwao na kusafiri pamoja na wenzake waliopata uhamisho huo wa muda huko morogoro. Alifanya kazi huko kwa miezi mitatu na kupelekwa Arusha kwa ajili ya kumalizia miezi hiyo mitatu iliyobakia. Nia na madhumuni ni kuwafundisha kazi wafanyakazi wa mikoa hiyo kwakua ofisi yao ilikua imefungua matawi mapya katika mikoa hiyo. Zikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kurudi Dar, Jothan alipita barabara moja na kumkuta msichana mzuri akiwa ameshika tenga anauza maua. Moyo ulimlipuka ghafla na kujikuta anamsogelea yule dada bila kujitambua. “unauzaje maua” aliuliza Jothan huku akimuangalia binti yule mzuri ambaye alikua anatabasamu baada ya kumuona yeye pale. “shilingi elfu moja kwa kila moja.” Aliongea yule dada bila kumuangalia Jothan usoni. “nikitaka yote utaniuzia shilingi ngapi?” aliuliza Jothan huku akizidi kumtathmini binti yule huku akionyesha kufurahi na muonekano mzuri aliokuwa nao msichana huyo. “nisaidie kuhesabu, kisha nitajie idadi ili nikuuzie kwa bei ya jumla.” Aliongea yule dada na kumfanya Jothan kushangaa. Alijiuliza maswli ya haraka . labda hyule msichana hajui kusoma au alikua anamtega. “kwanini usiniambi tu, maana siyo mengi yaliyobaki.” Aliongea Jothan kwa sauti ya upole. “mi sioni kaka yangu.” Aliongea yule dada na kumfanya Jothan kupigwa na butwaa. “kweli???” aliuliza Jothan huku akiwa haamini alichoambiwa na yule dada. Kwa kumuonyeshea kuwa haoni, yule dada alivua miwani na kumuonyesha macho yake ambayo yalikuwa na watoto ndani. Aliingiwa na roho ya imani Jothan na kukiri moyoni kuwa yule dada alikua nahitaji msaada kwakua tatizo lake linatibika ila matibabu yake yalikuwa ghali sana. “unaishi mbali na hapa?” aliuliza Jothan baada ya kutoa noti ya shilingi elfu kumi na kuyachukua maua sita yaliyobakia. “si mbali na hapa, ni mtaa watatu hapo mbele.” Aliongea yule dada mwenye asili ya kichaga lakini asiyekuwa na lafudhi hiyo wala meno yake kuharibika. Ngozi yake ilikubali baridi na kuwa nyeupe yenye mvuto. “unaonaje kama nikikusindikiza?” aliuliza Jothan. “sawa” Alijibu yule dada na safari ya kuelekea kwao ilianza. Mwendo wa kuupapasa kwa fimbo ndio uliomfanya Jothan kuamini kuwa ni kweli huyo dada alikua kipofu. Alikaribishwa mpaka ndani na kukutana na mama yake huyo binti. “karibu baba,”alikaribisha mama yake yule dada na kuwapisha. “huyo ndio mama yangu wa peke, sina msaada mwengine zaidi yake.” Aliongea yule dada huku anatabasamu. Hakua anamuona Jothan ambaye wakati huo alikua anaumia juu ya msichana huyu ambaye alionyesha hali aliyokuwa nayo ameizoea. Aliaga baada ya kuongea na kupiga stori mbili tati ikiwemo maisha yao kwa ujumla. Alirudi kwenye nyumba waliyopangiwa na kumpa story rafiki yake anayekaa naye kwenye nyumba hiyo. “kwa hiyo unataka ufanyaje ndugu yangu,” aliuliza rafiki yake huyo baada ya kumpa mkanda mzima. “nitajitahidi kwa uwezo wangu wote ili BAHATI apone kabisa.” Aliongea Jothan na kumuonyesha rafiki yake ni jinsi gani ameguswa na mdada huyo. “kwa hiyo unampango wa kumchukua na kwenda naye Dar?” aliuliza rafiki yake huyo huku wakiendelea kula bisi zilizokuwa kwenye meza yao. “exactly” alijibu Jothan kiingereza kuonyesha msisitizo. Asubuhi ya siku ya pili, Jothan aliamka na kwenda tena kwa kina Bahati. Kabla hajafika, tayari alishamuana dada huyo mwenye juhudi na kazi yake akiwa barabarani kama kawaida yake akiuza maua. “mambo Bahati.” Alisalimia Jothan Kwakua sauti ya Jotham alikua ameshaijua, alimng`amua na kuachia tabasamu mwanana lililomuacha hoi Jotham. “safi” alijibu Bahati. Waliongea mengi na kubwa zaidi ni juu ya Jothan kumsaidia Bahati swala lake la macho. Bahati alifuraha sana na wote wakaenda kwa mama yake na kumpa taarifa zile njema. “nitashukuru sana mwanangu..mungu akuzidishie.” Aliongea mama yake Bahati na zoezi la kujiandaa kwa ajili ya safari ya Dar-es-salaam lilianza mara moja kwa kufua nguo zake chafu na kupanga zingine kwenye mabegi. “tutakupitia kesho saa kumi na mbili asubuhi.” Aliongea Jothan na kuaga. Bahati alipanga kila kitu chake akisaidiwa na mama yake tayari kwa safari ya kesho yake ambayo ilikuwa na matumaini makubwa kwake. Alisali na kumuomba mungu afike Dar salama na lengo la kufanyiwa upasuaji lifanikiwe kwa nguvu zake mungu wa viumbe vyote. Asubuhi na mapema gari ya kina Jothan ilimpitia Bahati na safari ya kuitafuta Dar-es-salaam ilianza. Njiani walipiga story na kucheka kama vile walikuwa wamezoeana muda mrefu au walikuwa wameshakutana kabla. Uchangamfu wa Bahati uliwapendeza watu wote waliokuwemo kwenye lile basi. Bahati alipendelea kukaa dirishani kwa ajili ya upepo. Lakini Jothan aliamini kuwa Bahati alikua anatamani pia kuona vilivyokuwa nje. Saa nane mchana walifika mombo na kupaki gari lao kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Waliokwenda haja walienda ilimradi safari ikiendelea pasiwe na usumbufu kati yao. “unapendelea chakula gani?” aliongea Jothan baada ya kuingia naye Bahati kwenye mgahawa huo. “kama kuna wali huwa napenda hata ikiwa na mboga yoyote.” Aliongea Bahati. Jothan alimuagizia wali na nyama ya kuku. “ahsante kwa chakula.” Aliongea Bahati baada ya kumaliza kula kile chakula. Baada ya hapo safari iliendelea na kufika ubungo saa kumi na mbili jioni. Safari ya kuwapeleka makwao ilianza na Jothan na Bahati walishuka kinodoni na kuingia ndani. Kutokana na uchovu wa safari, Jothan alimpeleka Bahati chumba atakachokuwa analala na kutoka nje kununua chakula watakachokula usiku huo. Baada ya kiza kutawla, Jothan alimpelekea chakula Bahati na kumuonyesha choo na bafu ambavyo vyote vilikua mule ndani kwenye kile chumba. Baada ya mapumziko ya siku mbili, Jothan alimpeleka Bahati kwenye hospitali kubwa ya macho CCBRT kwa ajili ya upasuaji. Vipimo vilileta majibu mazuri kuwa kulikowa na uwezekano mkubwa wa kutolewa hivyo vitoto vya jicho na Bahati kona tena. Tarehe ya upasuaji ilipangwa kwa ajili ya upasuaji huo na Jothan alimpeleka Bahati ili apate huduma hiyo ambayo kama itafanikiwa itakuwa imempa maisha mengine kabisa mrembo huyo ambaye alikuwa haoni toka alipozaliwa.. Muenendo mbaya wa utendaji kazi huko marogoro ndio uliomfanya Jothan kurudishwa tena mkoani humo. Alisikitika kumuacha mgeni wake katika hospitali kabla hajashuhudia matokeo ya upasuaji huo, lakini hakuwa na jinsi kwakua aliuachia uongozi jukumu la kumuangalia mgonjwa wake huyo. Miezi sita ilikatika akiwa huko Morogoro huku mawasiliano yakikosekana kati yake na Bahati. Hata alipouuliza uongozi wa kampuni yao walimwambia kuwa walikuwa wamempa kiasi cha hela baada ya kupona na tokea wamkabidhi hawakupata mawasiliano naye. Mawazo yalimsonga Jothan na hakujua kwanini Bahati aliamua kufanya vile. Baada ya uchumi wa kampuni hiyo kutengamaa na kupata uongozi uliokuwa ukipiga kazi kama ipasavyo, Jothan alirudi Dar kuendelea na majukumu yake ya kila siku. Alipofika nyumbani kwake palikuwa pamefungwa kama alivyo paacha. Aliingia ndani na kuikagua nyumba yake kwa macho kisha akaenda kulala kutokana na uchovu aliokuwa nao. Usiku wa jumamosi, aliamua kwenda club kwakua ni muda mwingi alikosa kwenda. Hivyo aliamua kwenda kupata mixing za ma dj wakubwa ambao wanajua kubadilisha nyimbo na kumfanya mtu aburudike na mpangilio wa nyimbo wanazoziweka kulingana na wakati. Wakati akiwa anaburudika na kinywaji chake huku akipata burudani nyingine akiwa kwenye kiti, mzuka alkampanda na kujikuta anaingia kati na kuucheza wimbo ulimvutia zaidi. Style alizocheza ziliwavutia wengi hadi baadhi ya wasichana walimfuata na kucheza nae. Aliifurahia sana hiyo siku na kurudi nyumbani akiwa na hamu ya kwenda tena siku ya jumapili. Kwakua alikua na likizo ya mwezi mzima kazini, hakuona tabu kulala mchana ili usiku akeshe tena kutokana na kuwa mziki ni starehe kubwa anayoipenda japokuwa siyo muimbaji. Siku hiyo alifika mapema na kutulia kwenye meza kwanza za nyuma na kuendelea kupata kinywaji na nyama choma kwa wingi. Wasichana wengi walimshobokea na kuomba ofa za bia. Kwakua Jothan alikuwa akiingia sehemu yoyote ya starehe huwa anakua amependeza mfukoni, basi hakuona shida kumwaga ofa mbali mbali kwa wanaomuomba bila kujali jinsia. Wakati disco likizidi kuchanganya. Kwa mbali kwenye mwanga hafifu Jothan alimuona msichana aliyemfananisha. Hakujiuliza mara mbili, alinyanyuka na kumfuata pale pale kwenye meza yao. Kadri alivyozidi kumsogelea, ndipo sura ya yule binti iliyozidi kumjia kichwani. Alimsogelea na kumuangalia kwa ukaribu zaidi. “kaka,tukusaidie nini?” aliuliza yule dada baada ya kumuona Jothan akiwa mbele ya meza yao amesimama na kumuangalia kupita kiasi. “sijui ndio wewe au nakufananisha?” aliongea Jothan huku akiwa haamini baada ya kumuona yule binti aliyekuwa kapendeza kupita kiasi. “kaka hizo swaga za kizamani kweli, za kuaza kufananishana mara sijui nilikuona wapi, achana na sisi bro” aliongea yule dada na kuwafanya wenzake kucheka. Kutokana na hadhi aliyokuwa nayo Jothan, alifedheheka kiasi na kumfanya akubali matokeo. Aliwaacha wale mabinti huku wakiwa wanamjadili na yeye kurudi kwenye siti yake. Ladha ya club ilipotea na kuamua kurudi nyumbani kwake. Alijitupa kitandani na kuwaza sana. Kwa jinsi alivyotekoa kufurahi kumuona tena yule msichana na majibu aliyopewa hata kabla hajajitambulisha yalimtia simanzi. “naweza kusema kuwa hawezi kunifahahamu, lakini hata sauti kashindwa kuitambua?… au kwa sababu sauti yangu ilikuwa ya kilevi?” Alijiuliza Jothan maswali mengi bila ya kuwa na majibu. Asubuhi ya siku ya pili alienda kupata supu maeneo ya karibu na kwao. Aliporudi alijitupa kitandani na usingizi ukamchukua mpaka saa kumi jioni. Njaa ilikuwa ina muuma sana. Aliamua kutoka na gari lake na kwenda kwenye Bar kubwa iliyokuwa msasani kwa ajili ya kupata chakula ambacho siku hiyo kilikuwa kinapikwa kwa ustadi mkubwa. Aliagiza oda yake na kuletewa baada ya muda kama wa dakika tano. Kabla hajaanza kula, kwa mbali aliisikia sauti ya yule mmsichana aliyekutana naye Club usiku wa jana yake. Alinyanyuka na kwenda kwenye ile meza ambayo alimkuta akiwa na rifiki yake mmoja wa kike. “samahani, wewe sio BAHATI!!!?” Aliuliza Jothan huku akiwa na uhakika asilimia zote kwakua alikua anafahamu fika kuwa yule ndiye mwenyewe kutokana na sauti yake na muanekano wake ingawaje kwa sasa alikuwa anavutia zaidi. “ndio mimi, umenijuaje?” aliuliza yule dada na Jothan aliachia tabasamu huku akitikisa kichwa chake. “ina maana Bahati hata sauti yangu huikumbuki?” aliuliza Jothan huku akiwa haamini kumuona Bahati akiwa na macho mazuri tena yaliyoongezewa uzuri na kope za bandia alizo bandika. “ningekuwa nakujua nisingekuuliza umenijuaje?” alijibu yule dada na kuendelea kuifyonza juice yake iliyosindikizwa na chpsi pamoja na nyama choma waliyokuwa wanakula yeye na rafiki yake. “nitakushangaa sana ukisema kuwa sauti ya Jothan hauikumbuki.” Aliongea Jothan na kubaki kumuangalia Bahati aliyepigilia mapigo ya ki sister duu. “WHO A JOTHAN BY THE WAY????” Aliuliza yule dada na kumfanya Jothan aondoke bila kuaga. Alienda counter na kulipia oda yake bila kuigusa na kuondoka zake. Hakuamini kuwa Bahati angewaza kuongea yale maneno mbele yake tena kwa nyodo wakati ni yeye ndie aliyemleta mjini na kumpa msaada wa kuyatibu macho yake baada ya yeye kuikubali hali ya ukipofu kutokana na kuwa kulikuwa na uhaba wa pesa nyumbani kwao. Jothan ilibaki kidogo tu agonge wakate anaendesha kutokana na mawazo yaliyochanganyikana na hasira kwa kile alichofanyiwa na Bahati.. Alijilaumu sana kwenda kula chakula pale na kuambulia maumivu. Alijuta kukutana tena na Bahati ingawaje mwanzoni alikuwa na hamu ya kuonana nae. Alifika nyumbani na kujilaza. ”who a Jonathan by the way??” Aliirudia ile kauli ya Bahati na kujikuta anashindwa kuamini kuwa yule ndie bahati halisi aliyemtamkia maneno yale. ITAENDELEA ... Read More
HOUSE GIRL DIARY; NAITWA RAYA NI HOUSE GIRL MSTAAFU—SEHEMU YA TATU (ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI; Raya anarekodi Video ikimuonyesha yule Mama akimtesa mtoto wake wa kambo, akimpiga na kumfanyisha kazi. Anamkabidhi Baba Jack ili aone kinachoendelea. Je nini kitatokea ENDELEA.. Kama hujasoma sehemu ya pipi basi bonyeza hapa; Iddi Makengo Dada alimuona namna Baba anavyobadilika, namna ambavyo uso wake alikua anaukunja, ghafla nilimuona Baba machozi yanamtoka, nikitegemea kama atapandwa na hasira kama nillivyokua mimi na kuanza kumtandika Dada makofi niliona anamgeukia taratibu, alimuangalia kwa uchungu kama vile alikua anataka kusema kitu lakini maneno hayatoki. “Ni…ni nini hiki?” Alijitahidi kuuliza, wakati huo Dada alikua kimya akiangalia chini kwa aibu. “Nisamehe mume wangu ni hasira tu, huyu mtoto wakati mwingine ananiudhi nalazimika kumpiga…” Alijitetea. Mimi bado nilikua nashangaa ni kwanini Dada hakua amelala chini akitokwa damu kwa kipigo. “Hasira ndiyo unwe unampiga mtoto namna hii, hizi ni hasira gani?” Hapa Baba aliuliza kwa hasira kidogo, nilipata faraja labda atamtandika makofi lakini haikutokea. Dada alianza kulia, “Hata mimi sijui mume wangu, sijui hata nini kilinitokea siku hiyo nikampiga mtoto, mimi sina mkono wakupiga kabisa, wewe mwenyewe unanijua labda ni hii mimba…nikiwa katika hali hii nakua tofauti sana…” “Muongo, ni kila siku anampiga, hata haya anayoita mapele ni yeye. Hata chakula anamnyima, anamtukana, anamfanyisha makazi kama Mbwa, huyu si mwanamke ni shetani!” Niliongea huku nikinyanyuka kwa hasira, Baba alikua kama zezeta flani hivi, baada ya kutajiwa neno mimba ni kama alisahau kuwa yule mwanamke alikua ni shetani. Nilikua nasikia mambo ya limbwata lakini nilikua sijawahi kuona mtu kalogwa akalogeka. Kwa namna ile video ilivyokua mtu yeyote mwanye akili timamu hata kama asingekua mzazi wa Jack angekasirika na asingemsikiliza yule mwanamke. “Una mimba mke wangu, ina miezi mi ngapi? Mbona hukuniambia?” Alisahau kabisa kuhusu Jack na kuanza kuulizia upuuzi mwingine ambao nilijua kabisa ni uongo. “Hakluna cha mimba wala nini, hivi wewe huoni kama anataka kukuchota akili!” Niliongea kwa hasira, pale nilikua kama mfanyakazi ila kwa wakati ule nilijua kazi sina hivyo ilikua ni lazima kumtetea Jack na kuhakikisha haki inatendeka. Nilipiga kelele na harakaharaka nilitaja karibu kila kitu ambacho mimi nilikishuhudia Dada akimfanyia Jack. “Mume wangu unaona, huyu binti ndiyo sababu ya kila kitu. Hataki kufanya kazi, nyumba ikakua chafu na kamjaza mwanao kiburi, mbona kabla ya kuja tulikua tunaishi salama. Jack namfundisha kazi na ananisaidia kufanya kazi za ndani, kwa hali yangu hii siwezi kufanya chochote, wewe mwenyewe unakumbuka kilichotokea kipindi kile. Unajua namna tulivyohangaikia huyu mtoto, hivi kweli kumfundisha mtoto wa kike kazi za nyumbani ni kosa? Au kumchapa akikosea ni kosa? Au kwakua mimi sina kazi nipo hapa nyumbani, au kwakua mimi ni Mama wa kambo ndiyo mnaniona kama shetani. Huyu binti anajazwa maneno na Mama yake, kila siku wanaongea na ndiyo wanataka kutuvuruga. Mimi siwezi, mimi siwezi kama umenichoka niambie tu niondoke zangu!” Aliongea huku akilia, kila kitu kilikua ni uigizaji, wakati anaongea alianza kunyanyuka, alinyanyuka huku akishika tumbo kama vile ana maumivu tumboni. “Nini? Kuna nini kimetokea, tumbo linauma?” Baba alimuuliza lakini hakujibu zaidi ya kumuambia niache kama umeamua kumsikiliza huyo baki naye mimi naondoka. Alinyanyuka kwa kupepesuka kisha taratibu alidondoka chini. Niliona kabisa kafanya makusudi kwani hakudondokea sakafuni, alipiga jicho pembeni kisha akapepesa macho na kudondokea kwenye sofa, akawa kama kakaa kiupende kisha ndiyo akafika chini. Baba alipaniki, alianza kuhaha, simu alitupa pembeni na kuacha kuangalia, watoto wake nao walikuja kulia na kumlilia Mama yao. Ilikua ni kama maigizo flani, Baba alianza kuongea habari za Hospitali ndipo alijifanya kufungua macho na kulazimisha kupelekwa chumbani. Aliniambia nimsaidie kumnyanyua lakini sikua tayari, nilimshika Jack mkono na kuondoka naye mapaka chumbani, nilimuacha Baba akihangaika kumnyanyua ili kumpeleka chumbani, alisahau kabisa ishu ya mwanae. **** Usiku mzima sikulala, nilijua nafukuzwa lakini suala la kumuacha Jack pale halikuingia akilini. Nilimuambia Jack nimpeleke kwa Bibi yake lakini alikataa katakata. “Watakuja tu kunichukua, hata nikisema nini hakuna mtu wa kunisikiliza. Wewe dada ondoka tu uniache hapa, nimeshazoea kila dada anayekuja anachoka na kuondoka mimi naendelea tu kubaki. Baba hawezi kuruhusu niondoke, alishagombana na Bibi mara nyingi lakini anasema ananipenda na hawezi kukaa mbali na mimi. Kumbe sikua mimi peke yangu niliyeona yale mateso na kukerwa nayo, kulikua na wafanyakazi wengine wawili nyuma ambao walishafukuzwa kwaajili ya Jack ndiyo maana alikata tamaa. Mmoja alisema kwa Bibi yake Jack na mwingine alimpa chakula na alikua anawasiliana na Mama yake Jack. Asubuhi Baba aliamka kama kawaida, ni kama kulikua hakuna kitu kilichotokea, Dada alijifanya kuamka na kumuamsha Jack kwaajili ya shule, alijidai kumuandaa na kujifanya hana kinyongo. Waliwaaandaa na kuwapeleka shule, alipoondoka tu Dada aliniambia nikusanye kila kilicho changu na kuondoka. Alinitukana sana kwa kutaka kuingilia nyumba yake akiniambia kuwa pale hawezi kuondoka. Alitaka kunipiga lakini kwakua sikuwa nikihitaji kazi tena na nilishajua siwezi kubaki tena pale kumlinda Jack niliamua kumtolea hasira. Baba alishaondoka kwenda kazini hivyo tulibaki wawili tu, pamoja na mwili wangu mdogo lakini nilipitia mengi, maisha ya kupigana mtaani nilishayazoea. Nilimsubiri aliponipiga kofi la kwanza na la pili. Nilimuacha anogewe ndiyo nikaanza kumtandika, hakuamini. Nilimtandika kama vile mtoto mdogo, nilimpiga sana akapiga kelele lakini hakukua na mtu wa kumsikia. Baada ya hapo nilichukua kilicho changu na kuondoka. Nilimuambia naondoka lakini nitarudi, nitarudi kwaajili ya Jack. Alinyamaza kimya bila kusema chochote. Kumbe mtu mwenyewe alikua mayai mayai halafu anajifanya kuonea watu. Niliondoka na kwenda kwa kijana mmoja, huyo alikua ni X wangu, tulizinguana kitambo kabla sijaacha kazi nilipokua nikifanya mwanzoni, yeye alikua ni Kondakta wa daladala hivyo mchana alikua kazini. Mlango wake nilikua naujua vizuri hivyo niliufungua hata bila funguo. Sikua na pakwenda kwani sikua na ndugu Dar, ingawa sikuachana naye vizuri lakini nisingelala mtaani. Jioni alirudi na kunikuta, hata hakukasirika, alianza kucheka na kunitania kama siwezi kuishi bila yeye. Nilimuambia ishu yangu, nikamuonyesha ile video katika simu yangu, hata yeye pamoja na Bangi zake hakuamini kama kuna mtu anaweza kufanya vile tena kwa mtoto mdogo kama yule. “Huyo mwanaume kashatengenezwa, cha kufanya hapo ni kwenda Polisi, mbona siku mbili huyo akikaa ndani anakaa sawa…” Aliongea huku akinigusa, najua alitaka mapenzi lakini sikua katika mood kabisa, ila aliongea jambo amaalo sikuliwaza kabisa hapo awali. “Baba yake anaweza asijali lakini sidhani kama Polisi hawatajali.” Niliwaza kufanya hivyo lakini ulikua ni usiku, niliamua kusubiri mpaka asubuhi. Lakini niliwaza kama itakua vizuri nikienda na Jack kwani nilijua kuwa wakiangalia makovu yake basi utakua ni ushahidi tosha na watamuonea huruma. Lakini ningempataje wakati yuko shuleni, niliamua kwenda nyumbani kwao kumsubiri wakati anatoka shule. Wakati wanashushwa na gari kabla ya kuingia ndani nimchukue na kuondoka naye. Mchana muda wa wao kutoka shule nilichukua Bajaji, nilimuambia Dereva kupaki karibu na geti kabisa, Gari la shule lilipokuja na kuwashusha nilishuka na mimi. Wote waliniona, wale wengine walikimbilia ndani lakini Jack ambaye alikua anaogopa alisimama na kuniambia niondoke kwani atapigwa. Sikumsikiliza wala sikusubiri kumuelezea. Nilimshika na kumvuruta mpaka kwenye Bajaji, nikamuingiza kwa lazima kisha nikamuambia Dereva tuondoke. Kwakua nilishamuambia kila kitu aliwahsa Bajaji mpaka kituoni. Kule nilienda mpaka mapokezi, hakukua na watu wengi, nilianza kuelezea kila kitu, nikawaonyesha na Video. Kila askari aliyeiona alikasirika, tulipewa askari wa kike ambaye alienda kumkagua Jack. Alikua ni Mama mtu mzima, wakati anamkagua alianza kutokwa na machozi ingawa alijizuia sana. Mwanzoni Jack alikataa kusema lakini baada ya kuhakikishiwa usalama wake lielezea kila kitu. Niliandikisha maelezo kisha tukapewa PF3 ili akatibiwe, askari mmoja alitupeleka hospitalini na gari yake binafsi. Baada ya hapo ilitolewa RB, Dada na Baba wote walikamatwa na kufikishwa kituoni. Wote walikua na kesi, haikua ni ya mtu mmoja tena. Polisi waliwasiliana na ndugu wengine kwaajili ya kumchukua Jack na kukaa na wale watoto wengine kwani wote hawakupewa dhamana. Mimi niliondoka lakini nilikua naenda Hospitalini kumuangalia Jack mara kwa mara. Alilazwa kupatiwa matibabu kwa muda wa wiki moja hivi, Mama yake alikuja na baadaye kukabidhiwa mtoto wake. Baba na Dada walikaa mahabusu kwa wiki moja na kutoka kwa dhamana lakini cha kushangaza hawakupelekwa mahakamani. Sijui nini kilitokea lakini binafsi naamini walitoa pesa nyingi kwani Baba Jack alikua na pesa na kacheo flani. Kesi iliisha chinichini na mimi sikuweza kufuatilia, baada tu ya Jack kurudi na kukabidhiwa kwa Mama yake kwangu hilo lilitosha hayo mengine yalikua hayanihusu. Hela yenyewe ya kula ilikua ni shida nisingeweza kufuatilia maisha ya wengine. Sasa hivi imepita kama miaka miwili hivi tangu hili tukio litokee, nipo hapahapa Dar lakini nimehama mtaa. Sifanyi tena kazi za ndani, nimefungua Genge langu ambalo nauza mbogamboga na matunda. Bado nawasiliana na Jack kupitia Mama yake na anaendelea vizuri, wanaishi maisha ya kawaida sana lakini yenye furaha. Katika kazi yangu hii ya kuuza Genge wateja wangu wengi ni wadada wakazi ‘House Girl’ mengi wanayokutana nayo katika nyumba za watu ni kubwa. Kwa wa mama ambao ndiyo mabosi wetu kumbukeni hata sisi ni wanadamu kama nyinyi. ***MWISHO MAMA KWANI BABA YETU NDIYO HUYU HUYU AU SISI NI MAYATIMA? Baba yao ndiyo alikua na kila kitu, mali zote zilikua za kwao lakini kila akisafiri walikua wakiishi kama mashetani, Shangazi zao na Baba zao wadogo waliungana kuwachukia, Mama yao alikua akinyanyaswa na kutukanwa. Kila siku walimuambia yeye ni mzigo na hawezi kuchukua mali za Kaka yao. Bibi yao ambaye alitegemewa kuwa upande wao naye walimjaza maneno. Walimuambia huyu mwanamke kama Kaka akimuacha watagawana mali na Kaka akifa basi atachukua mali zote. Kilichopo hapa ni kuhakikisha Kaka hawi na kitu chochote cha yeye kuchukua…. JE UNATAKA KUJUA KISA HIKI KINAHUSU NINI…Kama kisa kilichopita kilikutoa machozi hiki kitakupigisha mayowe… Lakini nacho kimetokea niseme kinaendelea kutokea, unaweza kuwa na mali nyingi na wanao wakaishi kama mashetani hata kabla hujafa. Kama unataka kuwa wa kwanza kukisoma basi hakikisha umelike ukurasa ... Read More
*MWAGIA HUMO HUMO EP 03* Sehemu Ya Tatu (3) Baada ya kusema vile aliingiza mkono mfukoni na kutoa pochi alihesabu noti tatu za kumi kumi na kunipa. “Mpelekee hizi mwambie nitakuja.” Nilizipokea na kufunga kazi zangu, pamoja na penzi letu kufa bado nilipelekwa na kurudishwa nyumbani na gari. Nilipofika nyumbani nilikwenda chumbani kwangu, kabla ya kufanya kitu chochote nilivua nguo zangu na kubakia mtupu kama nilivyozaliwa mbele ya kioo kikubwa na kujitazama upya kasoro katika mwili wangu. Nilituliza macho na kuyazungusha taratibu mwilini mwangu kuangalia nina kasoro gani inayonifanya kila kukicha nipoteze wanaume. Kila hatua niliyokuwa nikipiga katika kusafirisha macho yangu nilijigundua nina sifa kubwa sana ya kuitwa mwanamke mrembo tena mwenye kumtia hamu ya mapenzi mwanaume rijali. Umbile langu kwa mimi mwenyewe kama ningekuwa mwanaume na kukutana na mwanamke mwenye umbile kama langu ningemganda kama ruba, lakini kwangu ilikuwa na tofauti kubwa sana. Baada ya kujigundua sina kasoro mwilini nilijikuta nikilia huku nikisema kwa sauti ya chini. “Hali hii mpaka lini?” ”Hali ipi?” Sauti ya Bi Shuu iliuliza nyuma yangu ilionesha Bi Shuu alikuwa ameingia kitambo bila mwenyewe kujua. Niligeuka na kwenda kujitupa kifuani kwake huku nikilia kwa uchungu. “Vipi tena mwali?” “Bi Shuu huu mkosi.” “Wa nini?” “Na Mateja kanimwaga.” “Kwa nini unasema hivyo?” Nilimweleza yaliyotokea ofisini huku nikilia. “Ulimwambia namwita?” “Amesema atakuja wikiend.” “Basi kazi hiyo niachie mimi.” “Siamini kama atakusikiliza.” “Ngoja aje, nitajua mbichi na mbivu.” “Mmh, sina matumaini.” “Hebu kaoge nikupe michapo.” Nilikwenda kuoga ili nipate michapo ya Bi Shuu ambaye alinihakikishia kunipigania mpaka mwisho. Nini kitaendelea? Tukutane wiki ijayo. Mwisho wa wiki Mateja alikuja kuonana na Bi Shuu, alipofika waliingia kwa Bi Shuu. Nilikuwa na hamu ya kusikia alitaka kumuuliza nini juu yangu, nilijitahi kusikiliza dirisha la sebuleni la Bi Shuu lakini sauti walizokuwa wakizungumza zilikuwa za chini sikuweza kusikiliza waliyokuwa wakizungumza japo kuna muda nilisikia Mateja akisema. “Ilikuwa vigumu kuja kuyasema haya kwako, kwa vile mpaka anafikia umri alionao niliamini ni vigumu kubadilika.” “Mmh kama ni hivyo nina kazi nzito, naomba unipe muda vinaonesha chukuchuku havijaungwa.” “Hapana Bi Shuu nakuheshimu sana, lakini tumechelewa ungeniita mapema tungeweza kulipatia ufumbuzi. Sasa hivi nipo katika mipango ya harusi na kila kitu kipo katika hatua za mwisho,” kauli ile ilinikata maini. “Mmh, sawa nimekuelewa.” “Basi bibie wacha nikuache tutaonana,” nilimsikia Mateja akiaga ili aondoke. “Lakini naomba usimfukuze kazi mjukuu wangu.” “Bi Shuu suala la kazi haliingiliani na mapenzi, sitamgusa katika kazi hilo usihofu.” “Kama ni hivyo nashukuru, lakini Manka kapoteza dume la haja.” “Kila kitu mipango ya Mungu.” Nilimshuhudia Mateja akihesabu nyekundu tano na kumpatia Bi Shuu ambaye alishukuru nusra amlambe viguu Mateja kwa pesa aliyompa. “Asante bwana yangu,” Bi Shuu alishukuru. “Kawaida Bi Shuu ukiwa na shida mtume Manka usiogope.” Mateja aliaga ili aondoke, nilitoka haraka dirishani kwa Bi Shuu na kukimbilia chumbani haraka. Nilijikuta nikiangua kilio kutokana na niliyoyasikia nusu kwa Bi Shuu, niliamini nilikuwa nimechelewa kuyasikia ya mwanzo kuhusu tatizo langu. Niliamini kosa lilikuwa langu nilitakiwa nimueleze mapema Bi Shuu kuhusiana na mabadiliko ya Mateja. Kwa kauli ya Mateja kama ningewahi ningeweza kulikoa penzi langu. Nikiwa nimejiinamia kitandani nilikia nilishtushwa na mlango kugongwa. Nilijua ni Bi Shuu ambaye hakutakiwa kugonga, lakini sikutaka kumlazimisha nilipaza sauti yangu ya kilio. “Ingia mlango upo wazi.” Mlango ulifunguliwa macho yangu yalimshuhudia Mteja akiingia ndani mwangu baada ya miezi sita toka alipokata mawasiliano na mimi. Alikuwa wa kwanza kuniuliza baada ya kukutana na michirizi ya machozi kwenye mashavu yangu. “Vipi Manka unaumwa?” “Ndiyo,” nilidanganya kwa vile sikuwa na cha kumwambia. “Nini tena?” “Kichwa.” “Ooh, pole sana, umemeza dawa?” “Bado.” “Basi nyanyuka nikupeleke hospital.” “Kitapoa tu.” “Basi kama utazidiwa utakwenda hospitali.” Mateja alisema huku akinisogelea mkononi alikuwa ameshikilia pochi na kunikabidhi elfu hamsini huku akisema. “Kama utazidiwa zitakusaidia kwenda hospital.” Nilitaka kuzikataa zile pesa kwa vile shida yangu haikuwa pesa bali yeye mwenyewe. Nilitaka kumuuliza tatizo langu nini lakini niliamini nilikuwa nimechelewa nilitakiwa kuuliza mapema na si muda ule ambao alinionesha mpenzi wake mbele ya macho yangu. Nilipokea zile pesa Mateja aligeuka na kuondoka akiniacha nilikilia kilio cha kwikwi, baada ya kuondoka Bi Shuu aliingia na kunisimamia kama jini la kutumwa mkono kiunoni. “Manka kwenu hakuna unyago?” Lilikuwa swali la kwanza bila kujali kilio changu. “Unyago! Ndio nini?” “Mafunzo ya msichana kujitambua na jinsi ya kumridhisha mwanaume kitabia na kimapenzi?” “Sikuwahi kuyasikia.” “Mmh, ndiyo maana.” “Una maana gani kusema hivyo?” “Umepoteza wapenzi kwa kutojua mwanamke anatakiwa kumridhisha vipi mwanaume.” “Kwani kuna kitu gani amekueleza Mateja?” “Tutazungumza na kulifanyia kazi.” Baada ya kusema vile alitoka na kuniacha na mawazo kibao juu ya maswali yake na kitu alichoambiwa na Mateja. Nilijiuliza kutopata mafunzo ya usichana yanahusiana vipi na kukataliwa na wanaume. Nilijikuta nikijizoazoa hadi kwa Bi Shuu kutaka kujua Mateja kamwambia nini. Nilipofika nilimkuta akizurudia kuzihesabu pesa alizopewa na Mateja, aliponiona aliziweka pembeni na kunitupia macho. “Mmh, mwali una jipya gani?” “Bi Shuu naomba unieleze ulichopelezwa na Mateja juu yangu?” “Nitakueleza kwa vitendo si la maneno.” “Matendo! Una maana gani?” “Nimepata sababu ya wewe kukorofishana na wanaume, inaonesha wazi hukupitia mafunzo ya usichana. Nina kazi na wewe, mi ndo Bi Shuu bwana kila mwali aliyepitia mikononi mwangu kila aliyeonja hakutema. Najua wanakutema kwa vile unawalisha vya chukuchuku.” “Vya chukuchuku! Una maana gani?” “Utajua baada ya kuviunga kisha uwaonjeshe kama hukuolewa narudi kijijini kwetu japo toka nitoke kwetu kumebakia magofu. Lakini nakuhakikishia nakutia mikononi mwangu halafu nisikie, eti bwana bwana kaniacha,” Bi Shuu alishikilia pua na kusemea puani. “Nakwambia najua kuviunga vya chunguni mpaka vya mwilini, wala hujachelewa sasa hivi mtu akigusa amenasa.” “Utafanyaje?” “Nataka uombe likizo ya mwezi mmoja tena nitakuombea mimi kwa Mateja ili niviunge viwe vitamu.” “Vitamu! Vipi hivyo?” “Nataka ukiguswa usisimke, ujue mwiko upo katika chungu au upo juu ya mfuniko, kumpa mwanaume mpaka asuse. Usilale kama gogo uoneshe basi upo safarini na si kukapua macho kama kibaka akimvizia mtu.” “Mmh, mbona umeniacha njia panda.” “Leo nataka kumbadili Mchaga awe kama Mmakonde.” Mmh, kila alilozungumza kwangu lilikuwa geni, nilisubiri niungwe ili niwe mtamu kwa mwanaume. Niliendelea na kazi yangu huku moyo ukiniuma kulipoteza penzi la Mateja, na mpenzi wake kutaka sifa kila muda wa chakula cha mchana lazima ampitie na wakitoka walikumbatiana na kuzidi kuniumiza. Lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo. Wiki moja baadaye Bi Shuu alinituma nimwite Mateja, kama kawaida nilimfikishia ujumbe wake, naye hakuwa na hiyana alikubali wito. Ilikuwa ajabu katikati ya wiki Mateja kukubali kwenda kumsikiliza Bi Shuu, tena aliniomba nikitoka kazini niongozane nae. Baada ya muda wa kazi niliongozana na Mateja hadi nyumbani, tulipofika aliingia kwa Bi Shuu na kuniacha nikiingia chumbani kwangu. Nilijikuta nikijawa na mawazo juu ya wito ule Bi Shuu alikuwa na kitu gani ambacho alichomuitia Mateja. Niliamini kabisa kama kutaka kumrudisha kwangu itakuwa ngumu kutokana na kila kitu kujionesha juu ya Mateja na mpenzi wake mpya. Nilipofika ndani hata hamu ya kuvua nguo iliniisha na kujikuta nikitoka na kujipitisha jirishani ili nisikie alichoitiwa na Bi Shuu. Lakini sauti ya Bi Shuu ilinishtua kwa kuniita, moyo ulinishtuka kutaka kujua naitiwa nini? Niliingia sebuleni na kumkuta Mateja amekaa kwenye kochi akiwa ametulia. Bi Shuu aliponiona aliniambia. “Manka kwenye friji yako kuna soda?” “Mmh, jana nilimalizia nilikuwa na mpango wa kuweka leo.” “Basi nifuatie dukani.” “Bi Shuu si lazima achana nayo,” Mateja aliingilia kati. “Hapana babu lazima unywe soda.” Siku zote Mateja hakuwa na makuu alimkubalia Bi Shuu, baada ya kupewa pesa nilipitia chupa na kwenda dukani haraka ili niwahi mazungumzo yao. Nilipofika dukani nusra nipasuke kwa hasira baada ya kukuta wateja wengi kwenye duka la Mpemba. Sikutaka kusubiri nilikimbilia kwenye grosary iliyokuwa mbali kidogo. Nilinunua soda haraka haraka na kurudi hadi karibu na nyumba na kuanza kunyata hadi dirishani ili nisikilize wanazungumza nini. Nilipofika dirishani nilimsikia Mateja akisema. “Hakuna tatizo Bi Shuu kila kitu kitakwenda kama unavyotaka.” “Kama hivyo nitashukuru.” Baada ya mazungumzo yale palipita ukimya mfupi huku sauti za nyayo zikielekea mlangoni, nilichepua mwendo hadi mlangoni na kukutana uso kwa uso na Bi Shuu. “Vipi mwali mbona umechelewa?” “Dukani kwa Mpemba kumejaa watu ilibidi nisogee mbele kwenye grosary.” Bi Shuu aliipokea soda na kuingia nayo ndani, nilibakia mlangoni nikijiuliza niingie au niende chumbani kwangu. Kupata jibu la nifanye nini lilinifanya nisimame kwa muda pembeni ya mlango. Kabla sijapata jibu nilishtushwa na sauti ya Mateja. “Manka kumbe upo hapa?” “Ndi..ndi..yo,” maskini nilipata kugugumizi cha ghafla. “Wacha niondoke zangu.” “Haya, karibu,” nilijibu kwa aibu huku nikiangalia chini. Mateja kweli alinichoka bila kuongeza neno alinitipa na kuelekea kwenye gari lake, Bi Shuu alimsindikiza mpaka kwenye gari. Nilibakia nikimsindikiza kwa macho. Baada ya Mateja kuondoka Bi Shuu alirejea, alipofika alinishangaa kunikuta nimetawaliwa na simanzi usoni mwangu. “Vipi mwali?” “Aah, kawaida tu.” “Acha kujitia ukiwa, kila kitu kina wakati wake na wakati ndio unakuja.” “Kwani Mateja kasemaje?” “Aseme nini?” “Kwa hiyo amekubali?” “Akubali nini?” “Kwani ulimuitia nini?” “Kuhusu likizo yako.” “Kasemaje?” “Amekubali.” “Naanza lini?” “Sijajua lakini amekubali.” “Mmh, haya.” Niliachana na Bi Shuu na kwenda chumbani kwangu kujiandaa na kujimwagia maji ili nipumzike. ********* Siku ya pili nikiwa ofisini niliitwa na Mateja kunitaarifu kukubaliwa likizo yangu ambayo ingeanza wiki itakayofuata kwa kukamilisha kazi zangu zote muhimu. Nilipewa pesa ya likizo na kujiandaa kwenda kwenye unyago wa kiutu uzima ili niugwe niwe mtamu mwanaume akigusa anate. Baada ya kumalizia kazi za ofisi kwa wiki niliyopewa, niliruhusiwa kurudi nyumbani kuanza likizo. Nilirudi nyumbani na kumkuta Bi Shuu ambaye kabla ya kuweka makalio chini aliniuliza. “Mmh, umepewa likizo?” “Nimepewa.” “Basi kazi yote niachie mimi.” Siku ile nilipumzika bila kugusiwa kitu chochote, lakini alfajiri niliamshwa na kupelekwa kuogeshwa maji baridi kisha nilifungwa upande wa kanga bila nguo ingine ndani. Aliniongoza hadi katika chumba kimoja cha ndani kilichokuwa kitupu. Chini kwenye sakafu kulikuwa na maji kuonesha amemwagwa, baada ya kuingizwa mule ndani wakati huo kibaridi kilikuwa kikinichanyata. Bi Shuu alifunga mlango kwa nje na kuniacha nimesimama nikijiuliza ameleta mule ndani nifanye nini? Ajabu muda ulikatika nikiwa nimesimama, miguu ilichoka na kujiuliza mbona harudi ameniweka mule ndani ili iwe nini. Kukaa chini nilishindwa kutokana chini kuwa na maji na muda ule ubaridi kilikuwa kikali sana. Niliposhika mlango ulikuwa umefungwa kwa nje nilijaribu kuita kwani nilikuwa nimechoka kusimama zaidi ya saa moja. Hakukuwa na jibu la mtu yoyote. Nilijawa na mawazo juu ya kuwekwa chenye chumba chenye maji kisha kusimamishwa kwa muda mrefu. Nilijiuliza unyago wenyewe kama ndio ule kwangu niliamini nitashindwa. Niliamua kukaa kwenye maji huku kibaridi kikizidi kunichonyota, kutokana na uchovu nilijiegemeza kwenye ukuta na usingizi ulinipitia. Nilishtushwa na maji ya baridi niliyomwagiwa ndoo nzima, Bi Shuu alikuwa mbele yangu akiwa amekunja uso kwa hasira na kunifokea kwa sauti ya juu. “Haya ndiyo yanakufanya ukose wanaume kila kukicha, mwanamke mvivu kama nini, kukuacha muda mfupi umeshindwa kuvumilia na kuuchapa usingizi kwenye maji.” “Samahani Bi Shuu.” “Haya fanya usafi haraka,” alisema huku akinitupia tambara kukausha maji. Nilichukua tambara na kuanza kufanya usafi kwa kukamilia maji kwenye ndoo mpaka nilipokausha, Bi Shuu alirudi na mkeka ambao aliutandika kisha alitoka na kurudi na chai. Tulikunywa chai kisha aliniacha nipumzike kwa kuniacha na kipande cha kanga tu. Jioni ilipofika Bi Shuu aliingia ndani na kuniketisha kitako na kuanza kuniuliza maswali. “Manka kitu gani wakati wa mapenzi hukipendi?” “Mmh, vingi lakini tabia ya wanaume kunisumbua wakati wa kilimo huna sikupendi.” “Mmh, kingine?” “Ni hilo hilo tu.” “Nimekuelewa, kuna vitu vingi vya kike vimekupita kushoto, siku hizi wanaume hawapendi mwanamke anayelala kama gogo, husisimki wala hutingishiki.” “Bi Shuu nitikisike vipi au nisisimke vipi?” “Ndiyo maana leo umo humu ndani, ukitoka utajua unasisimka vipi na unatikisika vipi?” “Mmh, haya.” Mmh, hukuwepo ila malaika wako alikuwepo, sikujua alichonipa Bi Shuu kilikuwa adhabu au mateso. Niliwekwa mikao ambayo haikuwa tofauti na ile niliyokuwa nikiwakatalia wanaume, kila nilipotegea nilitandikwa bakora ya mgongo iliyotua sawia kwenye mgongo mtupu. Kila siku nilikuwa nikifanyishwa mazoezi yagumu ya viungo ambayo yalikuwa mateso mazito, kuna kipindi nilifikiria kumwambia bora aniache nilivyo kuliko mateso yale. Lakini Bi Shuu alikuwa mkali kama pilipili hakutaka mchezo hata kidogo hata nilipochoka bado alinilazimisha huku akisema. “Kushinda kuchoka ndiyo siri ya kumkata kiu mwanaume.” Nilibebeshwa mzigo kichwani nikiwa mtupu na kuanza kuchomwa na sindano kiunoni kitu kilichinifanya nishtuke kwa kuchezesha kiuno. Haikuishia hapo nililazwa chini na kubebesha mzigo kiunoni na kuendelea kuchomwa na kitu cha ncha ambacho kilinifanya nijinyonge nyonge bila kupenda. Niliendelea na mazoezi makali chini ya kungwi wangu Bi Shuu huku akinipa mbinu nyingi za kumchanganya kimapenzi mwanaume. Kuna mambo mengine siwezi kuyasema gazetini lakini Bi Shuu koma. Toka nizaliwe sikuwahi kukutana na mwanamke Shankupe kama yeye. Mtoto wa kike nilifundishwa maneno ya kusema mtu akiwa juu ya mnazi wangu, pumzi za kutoa wakati mwiko upo ndani ya chungu na akianza kugeuza maini nilitakiwa nilegee vipi huku macho na pumzi nizifanye vipi. Najua mwenzangu mie mwenye viuno kama vimefungwa mbao na wakati wa mapishi unatulia unasubiri mtu amwage mzigo akimaliza anyanyuke. Lakini ukikutana na bibi huyu lazima bwana akutaje jina. Mwezi mmoja mtoto wa kike nilipikwa nikapikika, baada ya mafunzo mazito Bi Shuu kwa ushambenga wake alinitafutia mwanaume ili kutaka kunipima baada ya mazoezi. Sikukataa kwa vile nilijua kile ndicho kipimo, mtoto wa kike nilijiandaa kuonesha kilichoniweka ndani kwa mwezi mzima. Cha ajabu Bi Shuu alitaka mchezo ule nichezee chumbani kwake, mmh, makubwa madogo yana nafuu. Sikutaka kumbishia kwa vile nilikuwa na usongo na mafunzo ya Bi Shuu ambayo yalinifanya nijiamini na kumtamani mwanaume nimtoe kamasi nyembamba. Baada ya kijana aliyechaguliwa na Bi Shuu kufika alikaribishwa chumbani kwa Bi Shuu, nilijikuta nikiwa na usongo na yule kijana ambaye alikuwa mmoja wa vijana walioninanga sijui kucheza nilipokutana naye siku ya kwanza. Baada ya kuingia ndani nilimpokea juu juu na kumtoa nguo maungoni kama kuku aliyechinjwa na kunyonyolewa manyoya. Baada ya kumuandaa mtoto wa kike huku mwili ukinisisimka baada ya kukiona kijiti cha kupokezana kwenye mbio fupi. Mtoto wa kike nikiwa nataka kufanya mtihani wangu wa kwanza kwa umakini mkubwa huku nikipitia hatua moja baada ya nyingine. Nilimlamba mwili mzima kama mama mbuzi akimsafisha mwanaye baada ya kumzaa, nilijua kutumia ulimi wangu. Nilipofika kwenye shina la mnazi mtoto wa kike nilitulia kwa muda huku vidole laini na ulimi ukifanya kazi yake. Mara nilimuona kijana wa watu akitetemeka kama amekunywa coka ‘ngriiiiiiiiii’, maskini kumbe alikuwa akilia chozi lisilo na msiba. Kijana wa watu naye akabadili upepo na kunirudishia mashambulizi. Mtoto wa kike nilipoguswa nililegea na kuzitoa pumzi huku jicho likipoteza kiini cheusi. Kwa mara ya kwanza niligundua kumbe mwili kila sehemu una raha yake kuishinda nyingine. Kama nilivyofundishwa na Bi Shuu kila nilipoguswa nilisema neno lake. Baada ya mshike mshike wa maandalizi cha chakula, hatimaye kiliiva na kutengwa mezani. Nilimpokea juujuu huku nilionesha jinsi gani mtoto wa kike nilivyoshikika, mtoto wa kike sikuwa na haraka nilifuata mwiko ulivyogeuza maini ili kumfanya mpigaji na mwimbaji wasitofautiane. Mtoto wa kike nilimaliza maneno yote mdomoni, sikuamini kutatalika kama bisi kwenye chungu cha moto. Mpaka mchezo unakwisha nilikuwa nipo hoi kwani niliamini vilikuwa vitamu kijana wa watu kila alipomaliza alileta sahani aongezewe. Nami nilimpakulia naye alijilia huku akigugumia kama dume la njiwa lenye wivu. Huku nikilia mara nne kwa utamu wa msiba. Lazima niseme ukweli kuna kipindi nilitaka kunyanyua mikono, maji yalikuwa shingoni, nyonga iligoma kutokana na kutokuwa na uzoefu wa kuyakata mawimbi. Bi Shuu alinieleza kumfurahisha mwanaume si nyonga tu, hata kujua kuyapangilia maneno hasa kumsifia hakuna mwanaume kama yeye pia anajua kumshikisha punda adabu kwa kumtandika bakora balabala. Baada ya nyonga kugoma na kukiona kiuno kikiwaka moto, nilitumia sauti kumsindikiza mwenzangu mpaka alipofika juu ya mnazi. Kijana wa watu hakuamini ilibidi aniulize. “Manka, kumbe mambo unayaweza mbona ulikuwa uninikatili, mambo haya ungenipa tokea zamani sasa hivi ungekuwa mke wangu.” “Nilikulisha vya chukuchuku lakini sasa vimeungwa ndio maana unaviona vitamu.” Kijana wa watu bila kutegemea alinipa elfu 50 kama asante ya kumpa penzi tamu ambalo alikiri hakuwahi kulipata kwa mwanaume yoyote. Baada ya kuondoka na kuniacha nimejilaza baada ya kuhisi uchovu kila kona ya mwili kutokana na mshike mshike wa kufanya majaribio ya vitendo. Bila ya kujigeuza usingizi mzito ulinipitia juu ya kitanda cha Bi Shuu. Nilishtuka baada ya masaa matatu nikiwa nausikia mwili mchovu kila kona, Bi Shuu aliniamsha na kukuta ameniandalia maji ya kuoga. Nilioga kupunza uchovu na kurudi ndani ambako chakula kilikuwa tayari. Tulikula pamoja kisha tulipumzika sebuleni, cha ajabu niligundua Bi Shuu akiniangalia kwa kuniibia kitu kilichonifanya nimuulize. “Bi Shuu vipi?” “Kuhusu nini?” “Naona kama unanivizia kunitazama kuna nini si uniambie.” “Mmh, kweli ulikuwa na usongo.” “Wa nini Bi Shuu?” “Kazi umeifanya vizuri japo kuna kipindi ulichemsha.” “Ulijuaje?” “Nilikuwepo muda wote toka unaanza mpaka unamaliza, kwenye maandalizi nakupa mia kwenye sauti na pumzi sabini kwenye mchezo wenyewe hamsini.” “Jamani Bi Shuu kujitahidi kote unanipa hamsini.” “Manka kwanza nashangaa mtu ulikuwa hujui lolote umeweza kupata hamsini wengi huwa chini ya hapo.” “Bi Shuu kama nina hamsini nimeweza kupewa zawadi nikipata mia itakuwaje?” “Mia kupata ni kazi kwa vile maungo yako yalikakamaa muda mrefu lakini utaweza kufika hata sabini kwa bidii yako.” “Mapungufu yangu ni nini?” “Kutumia nguvu nyingi ambazo hukufanya upumue kwa kasi sana kitu kinachokufanya uchoke sana, pia papala ya kukata nyonga. Mwanzo uliweza kwenda sawa lakini ulipoanza kuchoka alifanya bora liende. Lakini mwanzo ni mzuri. Kwa uwezo wako huo na kuonesha ulikuwa makini kwa kuyashika mafunzo, inaonesha nikikuongezea matirio kama kwenye mpira ni ujanja wa kuweza kumsoma mwanaume. Kila mwanaume ana amambile tofauti na mwenzake na wengine wana nguvu kama kirafu unatakiwa kufanya nini.” “Bi Shuu nitashukuru nimeteseka sana, kwa nini sikuyapata mafunzo haya mapema ili kuweza kumdhibiti Mateja,” Nilijikuta nikidondosha chozi kulikumbuka penzi la Mateja nililolipoteza kutokana na kutokujua sheria za kitandani na kunifanya niendeshe ovyo na kusababisha ajali za kutoelewa alama za kitandani. “Manka usiwe kama kipofu aliyefumbua macho na kumuona chura na kuamini hakuna kama chura chini ya jua, mbona kuwa wanaume zaidi ya Mateja” “Bi Shuu ni kweli usemayo lakini Mateja niliamini ni mwanaume sahihi kwangu.” “Ni kweli, lakini kisicho riziki hakiliki we jipange ukikolea utamu nakuhakikishia nitakutafutia bwana Mateja cha mtoto. Kwanza nataka niyafanyie kazi makosa madogo madogo ambayo yatakufanya kila atakaye gusa atangaze ndoa. Nataka umlize mwanaume kama mtoto mdogo, umeisha ona mtoto akinyang’anywa ziwa jinsi anavyolia?” “Ndiyo.” “Basi nataka mwanaume chozi limtoke, kuna vitu vidogo wanawake hawajui, vitu hivyo ukimfanyia mwanaume kama ameoa lazima aitelekeze nyumba yake. Mchele mmoja lakini unatofautiana katika mapishi, hii nyumba jasho la mwili wangu pale nilipompata mume wa mtu. Leo hii naishi kwangu nawe nataka uwe mara mbili yangu.” “Bi Shuu mbona wasichana hatuna vitu hivi?” “Siku hizi uzungu umetawala na kujikuta wakipoteza vitu vingi vya kumfurahisha mwanaume. Kumfurahisha mwanaume kitandani si kigezo pekee cha kuilinda nyumba yako. Kuna vitu vingi ambavyo vipo nje ya kitanda. “Kuna wasichana wengi wana nyonga laini kama unakula keki lakini wana mapungufu kama chujui la nazi ambayo hayawezi kumfanya atulie kwa kwenye ndoa yake. Kama tabia yako nzuri ulichanganya na machejo ya kitandani hata utakita hata ndege utanunuliwa japo mwenzio hana uwezo wa kununua baskeri.” “Mbona hujanifunda na hivyo?” “Siwezi kukuichanganya kimoja kimoja, kwanza tunatengeneza mtego akiingia anase, ukimaliza mafunzo ya mwili tunarudi tena kilingeni ili mumeo aone tofauti ya magumegume na mwanamke.” “Bi Shuu mbona nimechoka sana.” “Umelia mara ngapi?” “Mara nne.” “Mara ya mwisho ulilia mara ngapi ulipokutana na mwanaume kabla ya leo?” “Mara mbili sijawahi kulia zaidi ya hapo.” “Ndio maana, lazima uchoke umeukamua mwili sana na shughuli haikuwa ya kitoto kuna kipindi kidogo nisimamishe mpambano mlikuwa kama mnataka kutoana roho.” “Bi Shuu umejuaje?” “Nikuambie mara ngapi nilikuwa nafuatilia toka mwanzo mpaka mnamaliza” “Jamani Bi Shuu kumbe ulikuwa unanipiga chabo,” Mbona niliona aibu mtoto wa kike, jamani bibi huyu ana mambo kumbe mwenzie nahenyeka yeye anapiga chabo. “Sasa ningejuaje mapungufu yako.” “Mmh, makubwa madogo yana nafuu.” “Na hayo mengine lini maana muda wa kurudi kazini umekaribia.” “Wiki iliyobakia inatosha, kapumzike jioni kama kawa mpaka kieleweke.” “Wacha nikalale naona mwili sio wangu, kwenye pesa hiyo chukua nusu niachie nusu” “Asante mwali, nina imani sasa umeamini nilichokisema kinatimia” “Wee mwisho Bi Shuu je, ungenikamata ndio unavunja ungo naona kila aliyenionja angeniganda kama ruba.” Baada ya mazungumzo nilimuomba Bi Shuu nikapumzike mwili ulikuwa na uchovu, nilikwenda chumbani kwangu kulala kwa kulifungulia feni mpaka mwisho mtoto wa kike nilijiachia kitanda kizima. ******* Kama kawaida Bi Shuu aliniamsha kwenye chakula cha mchana na baada ya chakula cha mchana nilioga na kupanda tena kitandani. Sikuamini mwili kuchoka kiasi kile, Bi Shuu alinieleza ni kutokana na kuzoea kulala kama gogo kitandani lakini siku ile niliushughulisha mwili hata kumwaga machozi manne kitu ambacho hakikuwa kawaida yangu. Nilipogusa kitandani usingizi haukuchelewa kunichukua, Bi Shuu aliniamsha saa mbili za usiku nilikwenda kuoga kisha nilipata chakula cha usiku. Baada ya chakula nilipumzika kidogo na kuingizwa unyagoni kumalizia muda ulipobakia kwa kunipa mbinu za kummiliki mwanaume kwa sauti na matendo huku tabia ikiwa ndiyo uliyochukua sehemu kubwa. Katika mafunzo siku moja alinipa nipike chakula baada ya kupika tulikula wote, kesho yake alinipa nipike tena chakula kilekile, lakini hakunipa chumvi. Nilipomuuliza alisema nipike vile vile na muda wa kula nilishindwa kumuelewa baada ya kunieleza nipakue, nilipakua na kukila bila chumvi. Tulikula wote bila kujua chakula kile kwa nini tulikila bila chimvi. Sikutaka kumuuliza kwa vile hakikuwa kingi tulikuwa na kukimaliza wote. Baada ya chakula usiku Bi Shuu akiwa ameniweka chini aliniuliza. “Manka kuna tofauti gani ya chakula ulichopika jana na leo?” “Tofauti yake cha jana kina chomvi lakini cha leo hakina chimvi.” “Kipi chakula kizuri?” “Cha jana.” “Kwa sababu gani?” “kina chumvi lakini cha leo hakina chimvi.” “Mbona umekila.” “Nilishindwa kuelewa ulikuwa na maana gani.” “Lakini bila hivyo usingekula?” “Nisingekula.” “Unajua nilikuwa nina maana gani?” “Hata sijui” “Hii nakuonesha yaisha ya ndani ya ndoa, wanawake wengi wanawalisha wanaume chakula kisicho na chumvi. Wapo wanaokosa uvumilivu huvunja ndoa lakini wanaoburuzwa na mapenzi hula chakula kisicho na chumvi kila siku na kuishia kunung’unika moyoni.” “Lakini Bi Shuu kama mkewe hamuwekei chumvi anashindwa vipi kuchukua mwenyewe kuweka kwenye chakula” “Swadakta swali zuri, ndio maana kukuweka huku ndani vitu vingi huvifanya kwa mafumbo jibu lake huwa ndio maisha yako ndani ya mahusiano yako. Chakula na chumvi sikuwa na maana hiyo bali kukueleza matatizo ndani ya nyumba nyingi wanawake wengi ndoa zao uziondoa chumvi bila wao wenyewe kujua” “Kivipi?” “Nyumba nyingi mwanzo wa mapenzi huwa moto moto kama kumpokea mpenzio akirudi kumtengea chakula kula pamoja kuoga pamoja kuwa karibu yake kumpoza uchovu wa kutwa nzima ambao ndiyo tiba ya mwanaume kutoitafuta faraja nje ya ndoa yake. “Wengi baada ya muda baadhi ya vitu hundoka kabisa na ndoa kuendeshwa kimazoea, moyoni lazima utasema hivi nisivyofanya kuna nini kwani hawezi kufanya mwenyewe. Kuacha kuyafanya hayo ni sawa kuondoa chumvi kwenye mahusiano yako na kumfanya mpenzio kula chakula kisicho na chumvi. “Wengi huvumilia na kuumia moyoni lakini wasio na uvumilivu huitafuta chumvi hiyo nje ya ndoa. Hapo ndipo tatizo linapoanza na kuipoteza ndoa yako bila kujua tatizo ni wewe mwenyewe. Kuondoa baadhi ya vitu ndani ya ndoa yako kama kutompokea mumeo au kutokula na kuoga pamoja ni vitu vinavyo mwanaume huona vya kawaida lakini ni ufa mkubwa katika ndoa. “Penzi halizeeki bali mwili ndio unazeeka, vyote nilivyokueleza usikipunguze hata kimoja ukiingia katika ndoa yako. Nakuhakikishia bwana atakaye kuoa watu watasema umemuwekea libwata, limbwata mwali ni kumlea mumeo kama mtoto. Nina imani umenielewa” “Mmh, kweli nimekubali Mungu kakujalia kumtengeneza mwanamke, nina imani ungenieleza kwa maneno ningekuelewa nusu lakini kwa vitendo nimekuelewa zaidi. Asante Bi Shuu” “Nashukuru kuonesha ni muelewa na mtu mwenye usongo na mafunzo” “Lazima Bi Shuu niwe na usongo nimeteseka sana” Nilimalizia mafunzo huku akilekebisha mapungufu aliyoyaona kwenye mtihani wangu wa kwanza.” Nilikuwa sijawahi kula kungu mtoto wa kike nilikula kungu jicho ukiniangalia utanionea huruma. Nilimaliza mafunzo salama, kabla ya kuanza kazi alinitafutia tena mwanaume mwingine naye alikuwa mmoja wa wale walioninanga mwanzo. Nilikuwa na imani alikuja akijua ni yule Manka wa mwaga msigo babangu kisha uondoke. Mafunzo niliyopata ya mwisho mtoto wa kiume chozi lilimtoka, kwenye maandalizi tu alilia zaidi ya mara tatu. Mtindo huu nilifundishwa kama sitaki kutumika sana kwanza namchosha mwanaume mwenye maandalizi. Hata ulipoingia baharini nusra anifie maji baada ya kushikwa na pumu katikati ya safari, machejo yalimfanya aifukuze Land Curuser VX kwa bajaj. Ilibidi niingie kazi ya kumpepea asinifie, baada ya kurudi katika hali yake ya kawaida aliniangalia mara mbili. “Ni wewe Manka au naota” “Kwani vipi?” “Hata siamini, kumbe ulikuwa unafanya makusudi” “Ulikuwa vya chukuchuku sasa vimeungwa” ”Una maana gani?” “Si umeona mwenyewe si la kusimuliwa” “Nimekubali lazima nirudie” ”Mmh, cha kunifia kifuani hapa namefungulia injini moja katika injini nne si ungebadilika jina.” “Manka naomba nikuoe.” “Ni haraka sana vuta subra” “Lakini niwe mmoja wa watu wa mbele kufikiriwa.” “Hakuna tatizo” Yule kijana ambaye alikuwa kama mlevi aliniachia laki moja ya asante” Baada ya kuondoka Bi Shuu kama kawaida yake alitoa tathimini yake. “Mwali japo mpinzani wako hakuonesha upinzani lakini umejitahidi sana tena sana, sasa nina uwezo wa kukueleza kapambane na mtu yoyote. La muhimu kuzingatia niliyokueleza hakika kila atakayehusa lazima anate sasa hivi mwili wako ni asali yenye ulimbo” Maneno ya Bi Shuu yalinifanya nijiamini nimeanza kuiva kimapigano, kwa vile muda ulikuwa umekwisha jumatatu ilipofika nililipoti kazini kwangu. Nilimkuta aliyekuwa amenishikia, baada ya kunipokea alinielekeza kazi za kufanya na yeye kuendelea na majukumu mengine. Kuna kitu kimoja nilisahau kukueleza baada ya kukaa ndani kuchezwa nilipotoka nilitakata na kunawili mtoto wa kike. Nikiwa naendelea na kazi bosi wangu dear zilipendwa aliingia ofisini, ilionesha hakujua kama naanza kazi siku ile. Alipofika hakuniangalia alinisalimia. “Za saizi?” “Nzuri” “Ile kazi tayari?” “Ndiyo namalizia” ’Baada ya muda gani” ”Dakika kumi” “Ok, fanya haraka.” Baada ya kusema vile aliingia ofisini kwake, ilionesha hakujua kama nipo mimi. Baada ya kumaliza kazi niliyoikuta niliprinti na kumpelekea, alikuwa bado ameinama nilipofika mbele yake nilisema. “Bosi kazi tayari” Sauti yangu ilimshtua na kunyanyua macho, kwa mshangao wa ajabu alisema. “Ha! Manka umekuja saa ngapi?” “Toka asubuhi” “Ina maana nimekupita kwenye ofisi yako?” “Ndiyo bosi” “Ooh, samahani sana” “Kawaida tu bosi wala usijisikie vibaya,” mtoto wa kike nilikuwa nimekwenda kimitego na kumuomba Mungu Mateja ajichanganye sijui aonje kidogo. Niliapa ningefanya aliyofundishwa na mengine nisiyo yajua ili kuhakikisha anakutana na vitu vipya katika medani ya mapenzi. Mtoto jicho lilikuwa limelegea kidogo jicho lilionekana kwa kujipaka wanja chini na juu na kuongeza uzuri wangu. Japo nilijijua mi mzuri, lazima mzuri ujijue kabla hujasifiwa na watu, lakini mapungufu yangu Bi Shuu aliyamaliza mengi niliyokuwa nayo. Mateja ilionekana kama kuchanganyikiwa kuniona nimebadika nimependeza na ninavutia tena kimitego ya kike hasaa. “Manka ulikuwa unakula nini?” “Kwa nini bosi?” nilimuuliza kwa sauti laini huku nikimchanulia tabasamu ya kufa mtu huku jicho nalo likizungumza. “Hapana, umependeza na unavutia” “Nashukuru kwa hilo ila moja umesahau” “Lipi hilo?” “Sasa hivi si Manka chukuchuku ila Manka huyu kaungwa akaungika” “Una maana gani?” “Bosi nitakuomba kesho nikukaribishe chakula cha usiku” “Mmh, hakuna tatizo kwa vile wiki hii ni ya mwisho baada ya hapo nitakuwa katika maandalizi ya harusi.” “Hakuna tatizo kazi njema.” “Na wewe pia.” Baada ya kumkabidhi kazi yake nilirudi kuendelea na kazi yangu, moyoni niliapa kama kweli atakubali mwaliko wangu amekwisha.Muda wa mchana Mchumba wake alimuijia kama kawaida na kwenda naye kupata chakula cha mchana. Japo moyo uliniuma lakini sikuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokeo kutokana na makosa kuyafanya awali. Jioni niliporudi nilimueleza Bi Shuu mwaliko niliompa Mateja kuja kula chakula cha usiku. “Mwali akiingia amekwisha, hakikisha anaisahau ndoa yake” “Bi Shuu la kuuliza hilo” “Nakuaminia mtu wangu.” “Naiona kama kesho inachelewa” “Itafika punguza munkari, usije yakakamia maji” “Si hivyo Bi Shuu nakuhakikishia kuyafanya yote kwa umakini mkubwa labda asije.” ***** Siku ya pili nilikwenda ofisini na kuendelea na kazi bosi alipokuja alinisalimia. “Mrembo hujambo” “Sijambo bosi simshindi wifi” “Manka mbona umefika mbali salamu umeijibu sivyo” “Samahani bosi, za nyumbani” “Mmh, salama sijui zako.” “Nami namshukuru Mungu, haya nipo ndani” “Sawa bosi” Kabla ya kuingia ofisini aligeuka na kuniuliza. “Mwaliko wa usiku upo vile vile au kuna mabadiliko” “Hakuna mabadiliko” “Haya,” alisema huku akifungua mlango na kuingia ofisini kwake. Baada ya kuingia ofisi nilibaki nilikuwa siamini kama nimesikia vizuri kuulizia mwaliko, niliona dalili njema zimeanza asubuhi jioni ni kumalizia tu. Huwezi amini siku hiyo nilifanya kazi kwa furaha ya ajabu kama Mateja amenikubali nirudiane naye. Jioni kabla ya kuondoka aliniaga na kuniahidi angekuja usiku. “Kweli Mateja utakuja?” “Kama siji ningekuambia” “Karibu sana mpe..” Mungu wangu nilitaka kujisahau kumwita mpenzi wakati tuliisha achana long time a go. “Niite tu mpenzi wala usijisikie vibaya,” “Hapana bosi” “Haya baadae” Mateja aliondoka na kuniacha nikipanga vizuri vitu vyangu kabla ya kurudi nyumbani. ********* Nilkipofika nyumbani Bi Shuu aliniomba siku ile aandae chakula cha mgeni, sikuwa na hiyana mtoto wa kike nilimuacha afanye mambo yake. Nilikiandaa chumba changu na kukiweka katika hali ya usafi wa hali ya juu, kama kawaida Bi Shuu alinipatia mafusho ya manukato mazuri. Baada ya kuhakikisha chumba changu kinapendeza niliingia kuoga mtoto wa kike na kujifusha utuli huku nikipaka wanja wa sina mume ambao lazima mwanaume barabarani akusalimie. Baada ya kusimama mbele ya kioo kujitathimini, nilizidi kujisifia mtoto wa kike kwa upendeleo niliopewa na mwenyezi. Baada ya kuhakikisha nipo sawa, nilikunywa kungu na kuanza kujisikia nikisisimka mtoto wa kike kama mamba mwenye njaa. Nikiwa nimekaa mkao wa kula kumsubiri Mateja, mara aliingia Bi Shuu na kuniongezea mambo fulani ya muhimu pindi Mateja akiingia chumbani kwangu. “Mwali nilitaka kusahau kwa vile anajua anakuja kula chakula na kuondoka cha kufanya akiingia tu, ukimvamia kwa kumkumbatia huku akimbusu hakikisha mikono yako inafanya kazi ya haraka kumvua nguo bila kuchelewa mpatie upande wa kanga. Wakati huo mimi nitakuwa tayari nimepeleka maji ya kuoga bafuni niliyoyawekea viungo. Nani alikuambia wanawake wa Tanga ndio wanajua mahaba, nataka Mateja akiondoka kila kitakachokuja mbele yake akione shombo.” “Nimekuelewa Bi Shuu.” “Sio umenielewa bahati hairudi mara mbili, itumie kubadili matokeo.” “Matokeo ya nini Bi Shuu?” “Ukimaliza kilicho tupotezea muda nitakwambia.” “Nitafuata maelekezo yako.” Baada ya kutoa maelekezo Bi Shuu alirudi kumalizia kutengeneza maajumati ya mgeni rasmi. Majira ya saa moja na nusu gari la Mateja lilisimama mbele ya nyumba yetu, ajabu usongo wote niliokuwa nao uliyeyuka kama donge la mafuta katika kikaango cha moto. Nilijikuta nikijawa na hofu juu ya nilichokipanga kumpa Mateja kama ataingia katika mtego wangu. Nilijihisi kupoteza ujasiri niliokuwa nao kabla ya Mateja hajaja, niliikandamiza mikono yangu kifuani na kubana pumzi na kukaa kwa muda kuvuta ujasiri kisha niliitoa na kushusha pumzi nzito. Baada ya kujipa ujasiri nilijitengeneza haraka haraka ili kujiweka sawa japo nilikuwa nimejiweka kimitego ya kike hasa. Ndani nilivalia kufuri la bikini la rangi nyekundu juu nilivalia kanga nyepesi ukituliza macho unaona kila kitu cha ndani. Wakati huo chumba kilikuwa kikinukia utuli kila kona mimi mwenyewe nilikuwa kama Hululaini malaika wa daraja la juu. Jicho mtoto lilikuwa lemelegea kwa kungu huku mwili ukisisimka kama nyoka mwenye hasira aliyepandisha sumu kwa ajili ya kumgonga mtu. Wakati nikifanya matayarisho ya mwisho kabla ya kumpokea Mateja mbele ya kioo, Bi Shuu muda huo alikuwa amempokea. “Wawooo mwanaume huyo.” “Niambie kipenzi changu?” Sauti ya Mateja ilisikika. “Niseme nini mkeo nawe umetupa jongoo na mti wake.” “Bi Shuu kama ningetupa leo ningeonekana hapa?” “Mateja kula nisishibe heri nisipewe.” “Bi Shuu heri nusu shari kuliko shari kamili na kidogo si haba kuliko kukosa kabisa.” “Nitakuwezea wapi mtoto wa Kisukuma aliyejifanya Mzaramo kwa kujifanya unajua kuyageuza maneno.” “Vipi nimewakuta?” Mateja aliuliza mimi ndani kiroho paa! “Umewakuta wamejaa tele wewe tu,” mmh, maneno ya Bi Shuu yalijaa nahau na misemo na kuzidi kuniweka njia panda. Wakati nikijua hodi itapigwa wakati wowote nilipandisha tena pumzi na kuzishusha kisha nilijiandaa kumpokea. Mara mlango uligongwa. “Hodi ndani?” “Karibu,” nilimkaribisha huku nikikaa mkao wa chura kuruka. Mara mlango ulifunguliwa na Mateja aliingia, mtoto wa kike nilijizoazoa na kumkumbatia. “Ooh, karibu mpenzi.” “Asante za hapa?” “Nzuri.” Mtoto wa kike niliutambaza mdomo wangu na kutua kwenye mdomo wa Mateja ambaye alikuwa bado amepigwa na butwaa, nikihema kama mgonjwa wa pumu. Mateja alinipokea na kubadilishana mate, mikono yangu alipata nafasi ya kumvua shati. Baada ya kumvua shati nilimsukumia kitandani na kumlalia juu, kwa haraka nilimalizia na vilivyokuwa vimebaki chini kisha nilimpatia upande wa kanga. Kila nililolifanya siku ile kwa Mateja kilikuwa kigeni kwake niliamini alijua bado Manka wa mwaka 47 hohehahe asiyejua chochote. Niliamini muda huo Bishuu alikuwa ameisha peleka maji yaliyochanganywa na viungo bafuni. Nilimshika mkono Mateja na kutoka naye nje kumpeleka bafuni kuoga, Bi Shuu kweli alikuwa amepania mlangoni nilikuta kuna ndala mpya. Mateja alivaa na kuongozana naye hadi bafuni. “Karibu mpenzi uoge.” “Asante.” Nilimwacha Mateja bafuni na kurudi ndani kujiandaa kumlisha vilivyoungwa na Bi Shuu. Kabla sijaweka tako chini Bi Shuu aliingia bila hodi na kusema kwa sauti ya juu. “Wee mwana, ndio unafanya nini?” Kauli ile ilinishtua sana. Kutokana na makosa ya kuruka baadhi ya sehemu katika hadithi ya wiki iliyopita kufikia hatua ya kuwachanganya wasomaji. Leo tutaelezea kwa ufupi toka Mateja alipomuona Manka ofisini mpaka kufikia hatua ya kumsubiri chumbani. Baada ya Mateja kushtuka kumuona Manka jinsi alivyopendeza kwa muda ambao hakuwepo kazini alimsifia kuwa amependeza mara dufu. Naye Manka alitumia nafasi ile kumkaribisha Mateja chakula cha jioni kwake. Mateja alimkubalia na kumuahidi angefika jioni kwa ajili ya chakula. Manka aliporudi nyumbani alimueleza Bi Shuu kuwa Mateja amekubali kuja kula chakula cha jioni. Bi Shuu alimueleza asiipoteze nafasi ile adimu ahakikishe kama atakubali kuvila vilivyoungwa basi achanganyikiwe. Bi Shuu alimuomba kazi ya kupika chakula aifanye yeye ya kuandaa chakula cha ujanani kwake pale alipokuwa akimtengenezea mpenzi wake. Baada ya makubaliano na Bi Shuu Manka aliingia ndani kujiandaa kwa ajili ya kumpokea Mateja kwa kufanya usafi wa mwili na chumba huku akifusha udi na asumini kumwagia kitandani. Yalikuwa mafunzo tosha ya Bi Shuu ambayo Manka aliyafanyia kazi. Baada ya kila kitu kuwa tayari Manka alimsubiri kwa hamu Mateja mpaka alipofika. Baada ya kumuandalia maji na kumuacha aoge peke yake ndipo Bi Shuu alipomfuata na kumuuliza amefanya nini. Ili kujua kosa lake nina imani mpaka sasa tupo pamoja, haya tuserereke pamoja… Kauli ya Bi Shuu ilinishtua na kujiuliza nimefanya kosa gani tena. “Bi Shuu nimefanya nini?” “Manka haya ndiyo makosa mnayafanya sana wanawake wengi, kwa nini umuache aoge peke yake. Nenda kaoge naye ikiwezekana anza kumliza kilio cha raha bafuni.” Mmh, mtoto wa kike haraka nilitelemsha nguo ya ndani na kubakia na upande wa kanga nyepesi na kumuwahi Mateja kabla hajajipaka sabuni. Nilipokaribia bafuni Mateja alikohoa kumaanisha kuna mtu. “Mm..mm..mmh.” Nilisukuma mlango na kumkuta amejipaka sabuni usoni, alipofumbua macho aliniona nipo mbele yake. “Aah, kumbe wewe?” “Ulidhani nani?” “Nilifikiri kuna mtu kaingia kwa bahati mbaya.” “Nilikwenda kutoa nguo ili tuje tuoge wote,” nilidanganya. “Sasa mbona hukuniambia kama tunaoga wote uliondoka kimya kimya.” “Nilijua nakuwahi.” “Haya tuoge.” ITAENDELEA ... Read More
HOUSE GIRL DIARY; NAITWA RAYA NI HOUSE GIRL MSTAAFU! Nilikua mgeni katika ile nyumba, ingwa haikua mara yangu ya kwanza kufanya kazi za ndani lakini bado nilikua ninaogopa ogopa Dada (Mama mwenye nyumba) alionyesha mkali sana kwani ile kuingia tu alishanipa mashariti elfu kidogo. Nilishaambiwa sehemu ambazo siruhusiwi kukanyaga, vitu ambavyo siruhusiwi kugusa na majina ya kuwaita wote mule ndani. “Sitaki unite Mama unanizeesha unafikiri mimi naweza kuzaa kinyago kama wewe!” Hiyo ndiyo ilikua kauli yangu ya kwanza kukaribishwa nayo mara tu baada ya kumsalimia na kumuita Mama. Kweli hakua mtu mzima, lakini kwakua katika nyumba niliyoondoka nilikua nimezoea kumuita bosi wangu Mama nilijua ni heshima nayeye atapenda kuitwa hivyo. “Huko ulikotoka kwanini ulifukuzwa?” Aliniuliza kwa hasira, sijui hata nilimfanya nini lakini alionekana na kisirani chake tu. “Sikufukuzwa dada niliamua tu kuondoka, walikua …” “Eeeeh! Mimi si shoga yako kuanza kuniambia matatizo yako, nyamaza nishakuambia sitaki kukusikia, nenda jikoni huko! Unajua kupiga au niwakufundishwa kila kitu!” Alinikatisha kabla ya kujielezea kisha kuendelea kufoka. Nilimuambia najua akaniambia niingie jikoni kuanza kazi. Ulikua mchana kwani niliondokea kwa Shangazi yangu (si Shangazi kweli ni mtu ambaye alinilete tu mjini). Niliingia jikoni na kukuta lundo la vyombo, sikua na haja ya kuelekezwa, nilishakua House Girl mzoefu hivyo nilijua nini cha kufanya. Nilianza kuosha na ulipofika wakati wa kupika nilimuuliza tunapika nini. Nashukuru safari hii alinijibu vizuri hivyo nilichukua kile nilichelelekezwa na kumpikia. Kutokana na kelele za nyumba niliyotoka na uzungu wa Bosi wangu wa zamani nilikua najua kupiga si kitoto, ile milenda milenda yangu ya kijijini niliiacha huko huko hivyo nilipompikia tu na kuweka chakula mezani, alikifurahia ingawa hakusema chochote lakini hakulalamika, hiyo ilikua dalili njema kwangu. Katika nyumba niliyotoka baada ya kuwatengea chakula nilikua nasubiri mpaka wamalize kula, hii ni kwasababu kama kikitokea kitu cha kutumwa basi niwepo kuwasikiliza. Huwa nasimama pembeni kama wale madhouse girl wa kwenye TV kusubiria mpaka mabosi wangu wamalize kula ndiyo huingia jikoni na kujitengea chakula changu. Nilishazoea hivyo na kwakua ilikua ndiyo nyumba yangu ya kwanza nilijua labda mjini kote ndiyo hali ilivyo. “Unasubiri nini hapo si uende jikoni huko ukajipikie au wewe huli?” Aliniuliza kwa hasira, nilitaka kumjibu kumuelezea nilivyozoea lakini hakutaka kusikiliza, jicho alilonikata niliondoka kama chizi nikikimbia. Nilifika jikoni na kupakua chakula, nilikaa chini ili kula. Lakini kabla hata sijafikisha tonge mdomoni alikuja, alikua kasimama pembeni yangu. “Ndiyo unafanya nini?” Aliniuliza, macho yake yalikua katika chakula. “Nakula ma…dada…” Kidogo nisahau na kumuita Mama. “Pumbavu unakula nini? Yaani unakula chakula ambacho ninakula mimi! Hivi una akili kweli unataka kuwa sawa na mimi, nikulipe elfu thelathini na chakula ule kama mimi!” Aliongea kwa hasira, alikipiga teke chakula kisha kutoka, alirudi na ndoo ya dagaa na kunirushia. “Kuna ndoo ya dona iko hapo, pika ugali wako ule. “Aliongea kwa hasira huku anaondoka, alienda kwa sekunde kadhaa na kurejea. “Upike mwingi kuna mwenzako anatoka shule atakuja kula na wewe!” aliondoka na kuniacha pale. Nilianza kuchambua Dagaa ambao wengi walikua wameoza, unakutana na wadudu kabisa. “Haya mapya! Nimeruka mkojo nimekanyaga mavi!” Niliendelea kujiongelesha huku nikichambua dagaa ambao walishaanza kunitia kichefuchefu. Huko nilikotoka nilikua nanyanyaswa lakini angalau nilikua nakula chakula cha mabosi wangu hata kama nilikua nalia jikoni! *** Jioni jioni hivi kama saa kumi na nusu watoto wake walikuja, walikua watatu. Mmoja mkubwa kuliko wenzake Jackline na wengine wadogo Joan na John, hawa walilingana kwani walikua mapacha. Baada ya kubadilisha nguo niliambiwa niwatengee chakula, nilifanya hivyo kwa kuweka sahani tatu mezani. Lakini Jackline ambaye alikua na miaka kumi hakukaa mezani, alikuja jikoni ambapo nilikua naandaa chakula cha usiku. “Wewe ndiyo Dada mpya, shikamoo…” Alinisalimia tena kwani alishanisalimia wakati nawafungulia geti ili waingie. Niliitikia kwa wasiwasi kwani nilishaambiwa nisiongee na wanae hivyo niliogopa hata kumjibu salamu. “Chakula changu kiko wapi?” Aliuliza, huku akikaguakagua vyombo. “Chakula si nimeshawatengea sebuleni?” Niliuliza kwa mshangao, hasira zilinipanda kidogo kwani nilishajua kuwa kumbe mbali na kudili na Bosi kichomi basi ningedili na mtoto mdogo kama yule ambaye ana kisirani. “Baba amesafiri mimi siruhusiwi kula sebuleni nnatakiwa kula na wewe!” Sikumuelewa niliuliza mata mbilimbili ndipo kwa utulivu kabisa alinieleza kuwa yule hakuwa Mama yake mzazi bali ni Mama wa kambo hivyo kila Baba yake anaposafiri yeye haruhusiwi kula chakula sebuleni na wengine mpaka anaporejea. Chakula anachokula ni cha Dada wa kazi. Kusema kweli hilo lilikua jingine jipya, labda kwakua nilikua sijafanya kazi katika nyumba ambayo Bosi ana mtoto wa kambo. Niliwaza kile chakula ambacho nilipika kwaajili yangu, nikawaza wale dagaa kisha nikamuangalia yule mtoto na kumuambia. “Jack, si unaitwa Jack… “Nilimuuliza. “Ndiyo Dada!” Alijibu kwa upole. “Huwezi kula kile chakula, hata mimi kimenishinda, hembu ngoja nikutengee kingine, mbona kiko kingi tu watamwaga hawa!” Niliongea huku nikimtafutia sahani ili kumpakulia chakula lakini alikataa katakata, aliniambia nitapigwa sana kama nikila chakula kingine. Alinionea huruma mimi pia nakuniambia hata Dada mwingine alifukuzwa kazi kwakua alikua ananipakulia chakula cha wengine. Alionyesha kuogopa mpaka na mimi nikaogopa kwa namna alivyokua anaogopa. “Huyu ni mwanamke wa namna gani mbona yuko hivi!” Niliwaza nikimuangalia Jackline, alikua kachoka lakini alijitahidi kuonyesha yuko sawa, mara kwa mara alikua akitabasamu huku akijilazimisha kucheka. Aliniongelesha ongelesha kutaka urafiki, kweli nilimuonea huruma machozi yalinilengalenga. Kwangu ule ulikua ni mtihani mpya ambao sikujua nitaumalizaje. *** Siku mbili baadaye Baba mwenye nyumba alikuja, huyu yeye niliambiwa nimuite Baba na nilifanya hivyo bila kuuliza maswali. Alikua ni kijana tu wa makamo au sijui niseme mtu mzima mwenye muonekano wa kijana. Alikua mchangamfu na alipokuja kila mtu alikua na furaha, si Jackline au watoto wake wengine nyumba ilikua kama imemwagiwa gunia la furaha. Hakukua na kupika mara mbilimbili, hata mimi niliambiwa nikae kwenye meza kubwa, hakukua na kutumwa tumwa kwani Baba akiwepo wakati wa kula ni kula na wote alituchukulia kama wanae. Ilikua ni kama unaishi katika nyumba nyingine tofauti kabisa, Dada alikua mchangamfu akiongea kwa kucheka mara kadhaa akimkumbatia Jackline. Hata mimi alinitambulisha kwa bashasha akinisifia kwa ufanyaji kazi wangu. Kweli nilishangaa “Mbona sielewe, huyu Mama yako wa kambo mbona kama anabadilika sana kama si yeye?” Nilimuuliza Jackline, alijiibaiba kukaa jikoni wakati wenzake wakiangalia TV, Baba yake akiwepo alikua haruhusiwi kufanya kazi yoyote. “Nimeshamzoea, anaigiza tu Baba akiwepo?” “Kwahiyo Baba yako hajui chochote?” “Hapana, nilishamuambiaga zamani lakini hakuniamini, niliishia kupigwa tu. Nilimuambia Mama kwanza aliposema kwa Baba akaambiwa nina wivu hivyo kukatazwa hata kuja kuniona, ilileta ugomvi mkubwa siku hizi kila nikilalamika naambiwa nimetumwa na Mama kuja kumfitinisha Mama Mdogo…” “Mama yako wewe yuko wapi? Kwanini huendi kuishi na Mama yako?” Yuko kijijini, waligombanaga na Baba zamani, hawakuoana, Baba alinichukua nikiwa mdogo na kunileta hapa, mimi sijui mambo hayo ila Mama yangu naongea naye tu kwenye simu mara moja moja lakini simkumbuki hata sura, hata sijui mimi mambo yao.” Aliongea kana kwamba ni mtu mzima, alionyesha kupitia mambo mengi na hakukua na mtu wa kumsikiliza. Nilipokuja kufuatilia nilikuja kugundua kuwa Mama yake na Baba yake hawakua wapenzi, ni watu tu walikutana na mimba ilipotokea basi Mama yake alivyokua akidai matumizi kipindi hicho ashaoa aliamua kumnyang’anya mtoto kwa nguvu. Kwao ni Iringa hivyo alimnyang’anya na kumchukua kipindi akiwa na miaka minne na tangu wakati huo alikua akiwasiliana naye kwa simu tu. Ana Mama yeka mkubwa, Dada wa Mama yake ambaye yuko Dar lakini naye haruhusiwi kumuona kwani ndiyo alimuambia kuhusu manyanyaso na kumuambia Mama yake ambaye alipoongea na Baba yake ukawa ugomvi mkubwa. Sikua na la kuongea zaidi ya kunyamaza tu kwa namna alivyokua akiongea ni kama alishakata tamaa ya maisha muda mrefu, sikujua ni kwa namna gani naweza kumsaidia kwani hata mimi nilikua na matatizo yangu. Usiku wakati wa kulala sikuolazwa stoo kama kawaida, hapana, niliambiwa natakiwa kulala katika chumba kimoja na Jack. Ulikua ni utaratibu wao, Baba akiwapo na mimi nakua mtoto na lala chumba kimoja na Jack. Usiku baada tu ya kuingia Jack alizima taa, nilishangaa kwani hata kitandani nilikua sijafika, nilimuuliza kwanini anazima, nikihisi labda ni Mama yake hapendi. Nilisogea na kuwasha, alishtuka, ni kitu amcho hakukitegemea. Alikua anavua nguo ili kuvaa nguo za kulalia, nilipowasha taa tu alianza kujificha kama vile anaona aibu. Nilishangaa kwani mimi ni mwanamke mwenzake, “Dada zima taa, zima taaaa!” Alipiga kelele, alionyesha kushtuka akijificha, lakini badala ya kuficha hata sehemu za siri alikua anaficha mgongo wake. Nilitaka kuzima lakini kabla ya kufanya hivyo macho yangu yalitua katika mgongo wake, ulikua kama ramani ya Tanzania, ulijaa makovu mengi ya fimbo, mengine mabichi kabisa kama vidonda. Sikuzima, sasa nilijua sababu ya yeye kuzima taa hakutaka nione makovu. Nilisogeza macho mpaka kwenye mapaja na sehemu za siri huko ndipo kuliharibika zaidi. Hapo ndiyo nilijua ni kwanini mara kwa mara huwa anakunja uso hata akiegemea sehemu au kugusa mapaja yake. Nilimsogelea na kumkalisha chini, alianza kulia kabla ya kusema chochote. “Kwanini humuambii Baba yako, kwanini humuonyeshi haya makovu? Akiona atakuamini!” Niliongea kwa hasira, sikua na muda pale lakini kwa upendo aliokua nao yule Baba sidhani kama angeweza kumuona mwanae katika hali ile na kunyamaza kimya. “Namuambia Baba yako, hii kazi ishanishinda, ngoje nifukuzwe lakini niondoke na huyu Sherani!” Niliongea huku nikinyuka kwenda kumgongea Baba yake, tayari walishaingia chumbani kulala. Jack alinifuata akilia kunibemebeleza ili nisiende akiogopa kuwa atamuua lakini sikujali, nilijua ni uoga ambao mimi kama mtu mzima nisingeweza kuuruhusu. Ushahidi alikua nao na hakukua na haja ya kuendelea kuteseka hata siku moja katika nyumba ya Baba yake. Alinisihi sana lakini sikumsikiliza, nilitoka mpaka sebuleni, alinifuata akiwa vilevile uchi kasahau kuvaa nguo, analia, nilielekea mpaka mlangoni kwa wazazi wake. Bado alikua analia, huku akiongea kwa kunong’ona. “Dada Raya, Dada Raya usimuambie, usiongee chochote, mimi niko sawa niliumia Shuleni, sio Mama aliyenipiga, ni ukorofi wangu tu!” Alipiga kelele kuniomba nisiseme. ITAENDELEA… (Hiki ni kisa cha kweli ingawa majina yaliyotumika hapa hayahusiani na wahusika. Hii ni sehemu tu ya simulizi kutoka kwa wadada wakazi “House girls” ambazo nitakua nikiwaletea. Je unadhani kama Raya atagonga mlango na kumshitaki Mama wa kambo, je Baba Jack akiambiwa atachukua hatua gani, kesho si mbali sana tukutane kwa sehemu ya pili hapahapa kwenye ukurasa huu…” ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: