Home → simulizi
→ MKASA WA KUSISIMUA: HUYU NDIYE "MAMA WA KUIGWA".
inasikitisha sana
Rahema alifika nyumbani mbio mbio na kumkuta mama yake aliyekua migombani akipalilia viazi vyake, "Mamaaa, hodi hodi humu nyumbani" aliita Rehema, "Naaaam, karibu nan jirani?" aliuliza mama yake Rehema, "Ni mimi mwanao Rehema mama" alijibu Rehema. Mama aliacha shughuli zake shamban na kurudi haraka, alimkuta mwanawe kaja nyumbani kutoka mjini anakoishi na mmewe ila cha ajabu kaja kidharura katika hali inayoonesha hayupo sawa yani atokako hali si shwari.
"Haya nieleze mwanangu nini kimekusibu waja mbio mbio kwangu kwa dharura kama kasuku"aliuliza mama Rehema," Dah ndoa imenishinda mama nimechoka mwanaume hashikiki nimeamua kurudi nimechoka visa mimi bora nikae nyumbani mama "alieleza Rehema. Mama yake alimuangalia namna alivyokua kavaa kikahaba akamwambia," Mwanangu kwa nini unanidhalilisha hivi, mmeo alivokuja kukuoa kijijini alikuchukua ukiwa na tabia njema na maadili mema, nani amekubadilisha namna hii huko mjini, hebu tizama hata mavazi uliyovaa yasivyo na staha "Rehema alitaka kujitetea," Ndio mavazi ya mjini mama mume ananionea tu sijabadilika"aliongeza.
Mama yake akamwambia, "Tulipata habari kuhusu ndoa yako, mmeo alitupigia simu zaidi ya mara 7 katika nyakati tofauti tofauti akitueleza kuwa umebadilika sana hushikiki tena umeungana na makundi ya mashangingi, unashinda kwenye masalun unazurura mji mzima katika mabaa na gesti unagawa unyumba humheshimu tena, leo ndio tulikua twapanga kukaa kikao kuzungumzia tena suala lako sasa nashangaa mbio mbio umerudi kulikoni??! "
"Hapana mama ananisingizia, mme kajaa wivu yule" alijitetea Rehema huku akiigiza kulia, ghafla mama yake alipokea simu, alikua ni mume wa Rehema
anapiga mama akapokea, "Mama sijui nikwambieje ila hakika mwanao sijui ana mapepo gani, yaani leo amenitia aibu ambayo sitokaa niisahau, kafumaniwa na mme wa mtu gesti kakimbia anasakwa mji mzima na vijana ndugu wa mke mwenye mume, mimi pia nimemtafuta sijamuona ndio nmetoka kuripoti polisi".
Mama alistaajabu sana kumbe Rehema alifikia hatua ya kutembea na waume za watu, "Pole sana mkwe wangu usijali amini yupo salama tutafanya juu chini arudi nyumbani kesho mimi na baba yake tutakuja huko kumpa kiapo cha mwisho" Mama Rehema alijibu, "Haya mama nashukuru sana ila kiukweli Rehema nampenda sana nisingependa kumuacha chondechonde mje mnisaidie kumfunda upya atulie" Mume wa Rehema alijibu.
Baada ya kukata simu mama Rehema alimgeukia mwanaye kwa hasira akamtandika vibao kama 7 vizito, akamwambia, "Mshenzi sana mtoto wewe, unapata mwanaume anaekupenda kweli alafu unaleta nyodo na mashauzi, hivi umesahau alipokutoa kijijini umepauka kama kiroba cha korosho? Pamoja na umaskini wako na elimu ya la 7 akakuridhia leo wamdharau? Hivi unafikiri yeye alikua mwehu kukuhudumia unapendeza ndio uwape penzi wa nje? Huo uzuri wako nani angeuona kama sio matunzo yake, Mwanangu Chunguza kabla ya kuamua, waza kabla ya kutenda, uzuri wako utakufanya uringe na upate mwanaume unaemhitaji ila tabia yako ndio itakayoamua ni kwa muda gani huyo mwanaume atakua na wewe. Uzuri huvutia kila mwanaume, ila tabia ndio itakufanya udumu katika ndoa . Upendeleo hudanganya na uzuri ni batili...bali mwanamke amchae Mungu ndiye atakayesifiwa
Nakushauri rudi kamuombe mmeo msamaha tulia nae thamini upendo wake, hakika kama ameweza kukuvumilia mauchuro yote hayo uliyomtendea basi tambua hata ukiachana nae hutokaa umpate mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na moyo wa huruma na uvumilivu kama yeye, rudi kwako haraka kesho mimi na baba yako tutakuja huko mjini mnapokaa kuweka mambo sawa, shenzi sana wewe"mama Rehema alimaliza akaokota fimbo akamcharaza kama 15 za fasta miguuni zikaingia kweli kweli maana Rehema alikuwa kavaa kimini, "Na ukiharibu siku nyingine usikanyage hapa nje kwangu ntakuvunja miguu fisi wewe huna adabu" Mama Rehema alimfukuza huku akimuonya kwa ukali. Rehema alikimbia kwa aibu akilia ndala mkononi.
Funzo 😑
Ni wanawake wangapi wamesahau waume zao walipowatoa saivi wanajiona wazuri wanaleta nyodo na kuona waume zao sio wa hadhi yao wanawadharau na kuwasaliti kama Rehema?
Je! Wewe unaesoma mkasa huu ni mwanamke wa aina gani kwa mmeo, unathamini upendo wake au unachukulia kama udhaifu wake na kumsaliti kama Rehema?
Je! Wewe ni mshauri na mkufunzi wa aina gani au ndio mtetea maovu, jiulize ingekuaje kama mama Rehema angemtetea mwanae badala ya kumkemea na kumuadhibu
Ni wamama wangapi wana ujasiri wa mama yake Rehema, kusimamia ukweli kukemea maovu ya watoto wao katika jamii?
Ni wanaume wangapi wenye mapenzi ya kweli kama mume wa Rehema
wenye uwezo wa kumvumilia mke hata katika maswahiba makubwa na kuwa tayari kusamehe?
Tafadhali kama umeupenda mkasa huu toa japo neno moja la pongezi kwa MAMA YAKE REHEMA kwa ujasiri na msimamo alioonyesha kukemea maovu ya mwanae Rehema kisha SHARE post hii iwafikie wamama wote katika jamii.
MKASA WA KUSISIMUA: HUYU NDIYE "MAMA WA KUIGWA". inasikitisha sana Rahema alifika nyumbani mbio mbio na kumkuta mama yake aliyekua migombani akipalilia viazi vyake, "Mamaaa, hodi hodi humu nyumbani" aliita Rehema, "Naaaam, karibu nan jirani?" aliuliza mama yake Rehema, "Ni mimi mwanao Rehema mama" alijibu Rehema. Mama aliacha shughuli zake shamban na kurudi haraka, alimkuta mwanawe kaja nyumbani kutoka mjini anakoishi na mmewe ila cha ajabu kaja kidharura katika hali inayoonesha hayupo sawa yani atokako hali si shwari. "Haya nieleze mwanangu nini kimekusibu waja mbio mbio kwangu kwa dharura kama kasuku"aliuliza mama Rehema," Dah ndoa imenishinda mama nimechoka mwanaume hashikiki nimeamua kurudi nimechoka visa mimi bora nikae nyumbani mama "alieleza Rehema. Mama yake alimuangalia namna alivyokua kavaa kikahaba akamwambia," Mwanangu kwa nini unanidhalilisha hivi, mmeo alivokuja kukuoa kijijini alikuchukua ukiwa na tabia njema na maadili mema, nani amekubadilisha namna hii huko mjini, hebu tizama hata mavazi uliyovaa yasivyo na staha "Rehema alitaka kujitetea," Ndio mavazi ya mjini mama mume ananionea tu sijabadilika"aliongeza. Mama yake akamwambia, "Tulipata habari kuhusu ndoa yako, mmeo alitupigia simu zaidi ya mara 7 katika nyakati tofauti tofauti akitueleza kuwa umebadilika sana hushikiki tena umeungana na makundi ya mashangingi, unashinda kwenye masalun unazurura mji mzima katika mabaa na gesti unagawa unyumba humheshimu tena, leo ndio tulikua twapanga kukaa kikao kuzungumzia tena suala lako sasa nashangaa mbio mbio umerudi kulikoni??! " "Hapana mama ananisingizia, mme kajaa wivu yule" alijitetea Rehema huku akiigiza kulia, ghafla mama yake alipokea simu, alikua ni mume wa Rehema anapiga mama akapokea, "Mama sijui nikwambieje ila hakika mwanao sijui ana mapepo gani, yaani leo amenitia aibu ambayo sitokaa niisahau, kafumaniwa na mme wa mtu gesti kakimbia anasakwa mji mzima na vijana ndugu wa mke mwenye mume, mimi pia nimemtafuta sijamuona ndio nmetoka kuripoti polisi". Mama alistaajabu sana kumbe Rehema alifikia hatua ya kutembea na waume za watu, "Pole sana mkwe wangu usijali amini yupo salama tutafanya juu chini arudi nyumbani kesho mimi na baba yake tutakuja huko kumpa kiapo cha mwisho" Mama Rehema alijibu, "Haya mama nashukuru sana ila kiukweli Rehema nampenda sana nisingependa kumuacha chondechonde mje mnisaidie kumfunda upya atulie" Mume wa Rehema alijibu. Baada ya kukata simu mama Rehema alimgeukia mwanaye kwa hasira akamtandika vibao kama 7 vizito, akamwambia, "Mshenzi sana mtoto wewe, unapata mwanaume anaekupenda kweli alafu unaleta nyodo na mashauzi, hivi umesahau alipokutoa kijijini umepauka kama kiroba cha korosho? Pamoja na umaskini wako na elimu ya la 7 akakuridhia leo wamdharau? Hivi unafikiri yeye alikua mwehu kukuhudumia unapendeza ndio uwape penzi wa nje? Huo uzuri wako nani angeuona kama sio matunzo yake, Mwanangu Chunguza kabla ya kuamua, waza kabla ya kutenda, uzuri wako utakufanya uringe na upate mwanaume unaemhitaji ila tabia yako ndio itakayoamua ni kwa muda gani huyo mwanaume atakua na wewe. Uzuri huvutia kila mwanaume, ila tabia ndio itakufanya udumu katika ndoa . Upendeleo hudanganya na uzuri ni batili...bali mwanamke amchae Mungu ndiye atakayesifiwa Nakushauri rudi kamuombe mmeo msamaha tulia nae thamini upendo wake, hakika kama ameweza kukuvumilia mauchuro yote hayo uliyomtendea basi tambua hata ukiachana nae hutokaa umpate mwanaume mwenye mapenzi ya kweli na moyo wa huruma na uvumilivu kama yeye, rudi kwako haraka kesho mimi na baba yako tutakuja huko mjini mnapokaa kuweka mambo sawa, shenzi sana wewe"mama Rehema alimaliza akaokota fimbo akamcharaza kama 15 za fasta miguuni zikaingia kweli kweli maana Rehema alikuwa kavaa kimini, "Na ukiharibu siku nyingine usikanyage hapa nje kwangu ntakuvunja miguu fisi wewe huna adabu" Mama Rehema alimfukuza huku akimuonya kwa ukali. Rehema alikimbia kwa aibu akilia ndala mkononi. Funzo 😑 Ni wanawake wangapi wamesahau waume zao walipowatoa saivi wanajiona wazuri wanaleta nyodo na kuona waume zao sio wa hadhi yao wanawadharau na kuwasaliti kama Rehema? Je! Wewe unaesoma mkasa huu ni mwanamke wa aina gani kwa mmeo, unathamini upendo wake au unachukulia kama udhaifu wake na kumsaliti kama Rehema? Je! Wewe ni mshauri na mkufunzi wa aina gani au ndio mtetea maovu, jiulize ingekuaje kama mama Rehema angemtetea mwanae badala ya kumkemea na kumuadhibu Ni wamama wangapi wana ujasiri wa mama yake Rehema, kusimamia ukweli kukemea maovu ya watoto wao katika jamii? Ni wanaume wangapi wenye mapenzi ya kweli kama mume wa Rehema wenye uwezo wa kumvumilia mke hata katika maswahiba makubwa na kuwa tayari kusamehe? Tafadhali kama umeupenda mkasa huu toa japo neno moja la pongezi kwa MAMA YAKE REHEMA kwa ujasiri na msimamo alioonyesha kukemea maovu ya mwanae Rehema kisha SHARE post hii iwafikie wamama wote katika jamii.
Artikel Terkait
Story........ NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi na mbili (12) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp.... 0769673145 Ilipoishia.......... Penina na Frank walishangazwa Sana na maamuzi ya Nolan lakini hata hivyo Nolan hakutaka wamuulize swali lolote, alimwamuru dereva wa tax ile awashe gari na kuondoka. Kisha Nolan naye akaingia kwenye gari yake na kugeuza kuwafuata vijana wale wa the killer na wakati huo walikuwa tayari wameshaungana wote kwa maana ya kikosi kile cha kwanza kilichokuwa kikimtafuta Nolan na kile cha pili kilichokuwa kikimtafuta Frank. *********Endelea ********* Vikosi vile viwili ambavyo vilikuwa kwenye magari mawili viliweza kumuona Nolan akiwa anarudi kule alikotoka. Vikosi vile navyo haraka haraka vikageuza magari yao na kuanza kumfuata Nolan. Nolan aliweza kuwaona wakimfuatilia na ndio kitu ambacho Nolan alikitaka, lakini kilichomshangaza Nolan ni kwamba Sasa anafuatiliwa na magari mawili tofauti na mwanzo walipokuwa wakimfuatiliwa na gari moja. Lakini Nolan hakujali hilo, akaacha barabara na kukataa kushoto na kuingia kwenye njia moja ya vumbi ambayo haikuwa ikipita watu Mara kwa Mara. Nolan baada ya kuingia kwenye barabara ile akasimamisha gari na kushuka ndani ya gari lile. Na sekunde hiyo hiyo magari mawili ya vijana wale wa the killer wakawasili pale alipo Nolan na kusimamisha magari yao Kisha wote wakashuka kwenye magari yao ambao kwa pamoja walikuwa Nane. Vijana wale wa the killer walishaangaa baada ya kufika na kumkuta Nolan peke yake badala ya kuwakuta wote Nolan pamoja na Frank. Nolan alikuwa amesimama pembeni ya gari yake huku akiwatazama vijana wale waliokuwa wakimsogelea taratibu. "mwenzako yuko wapi?" kijana mmoja wa the killer akamuuliza Nolan huku akijaribu kumkamata Nolan kwenye shingo. Kijana yule alijikuta akipokea ngumi Nzito ya tumbo kutoka kwa Nolan ambayo ilimfanya adondoke chini kwa magoti. Wale vijana wengine walishtuka kuona mwenzao alivyotandikwa ngumi ya tumbo. Lakini hata hivyo bado vijana wale waliamini Nolan hawawezi kwasababu wako wengi na wote wana silaha. Vijana wale kwa pamoja wakaanza kumfuata Nolan, Nolan naye akapiga hatua kadhaa na kurudi nyuma na kuwasubiri. Vijana wale walipomkaribia Nolan kwa pamoja wakaanza kurusha ngumi na mateke kumvamia Nolan. Lakini Nolan alikuwa akiwakwepa tu bila kumgusa mtu yoyote, ndani ya dakika tano Nolan alikuwa akiwakwepa vijana wale waliokuwa wakimshambulia bila mafanikio. Lakini Nolan alizubaa kidogo na kujikuta akipokea ngumi Nzito ya uso kutoka kwa mmoja wa vijana wale. Lakini hata hivyo kijana yule aliyembahatisha Nolan ngumi ya uso ikawa ndio mwisho wake wa kuishi duniani, kwani Nolan alimkamata na kuanza kumshambulia kwa ngumi za haraka haraka na kummaliza kwa kumvunja shingo. Wale vijana wengine ndio walishtuka vibaya mno na kuona huyu mtu sio wa kawaida, wakaamua wamshambulie kwa silaha zao baada ya kuona hawatamuweza kwa mkono. Vijana wale walichomoa bunduki zao na kuziweka tayari kummaliza Nolan. Lakini Nolan alikuwa tayari ameshaingia kwenye gari na kuondoka kwa spidi kali na kuwaachia vumbi kali Vijana wale. Nolan aliamua kukimbia baada ya kuona vijana wale wakitoa bunduki zao, hivyo asingewaweza kwa sababu yeye hakuwa na silaha yoyote. Vijana wale nao hawakumuacha waliingia kwenye gari na kuanza kumfuatilia Nolan. Lakini mpaka pale Nolan alikuwa tayari ameshawapoteza vijana wale na yeye Sasa alikuwa ameshika njia ya kuelekea nyumbani. * Mzee Joel akiwa ameketi sebuleni kwake akisubiri majibu ya kuuwawa kwa Frank na Nolan simu yake ilianza kuita na alipoangalia mpigaji ni nani alikutana na Jina la Dickson, kijana ambaye mzee Joel ndio anataka amuoe mtoto wake Penina. Mara moja mzee Joel akaipokea simu ile. "mzee Joel habari yako?" akauliza Dick baada ya simu yake kupokelewa na mzee Joel. "salama kijana wangu habari ya huko"? Akajibu mzee Joel na kuuliza. " huku Safi tu, Sasa mimi nilikuwa nataka nije kumchukua Penina moja kwa moja nahitaji kuwa na familia Sasa. " akaongea Dick kumwambia mzee Joel. " kijana wangu usiwe na haraka tunaweka mambo Sawa na Muda wowote tutakuita uje umchukue mke wako. " akaongea mzee Joel kumpa moyo Dick. " unaweka mambo Sawa unaweka mpaka lini kama ni pesa nikekupa za kutosha mbona unanizungusha zungusha tu au nikuongezee pesa zingine? " akaongea Dick huku akionesha kuchoshwa na namna mzee Joel anavyomzungusha. "kijana wangu tafadhali naomba utulie Penina ni wako usiogope." mzee Joel akamwambia Dick. "nitulie nitulie mpaka lini nakuja Tanzania kujua Kwanini unanichelewesha kumuoa Penina na wakati nimeshakupa pesa nyingi Sana." akaongea Dick na kukataa simu. Mzee Joel alihisi kuchanganyikiwa hakujua afanye nini ili aweze kumuunganisha Penina na Dick. Na wakati huo huo mlango ulifunguliwa na akaingia Nolan huku akiwa amechafuka kwa vumbi. "Wewe mbwa mbona unaingia ndani kwangu bila hodi?" mzee Joel akamuuliza Nolan huku akiwa amevimba kwa hasira. "mzee tulia huu mchezo umeutaka mwenyewe lazima Frank amuoe Penina." akaongea Nolan maneno hayo ambayo yalizidi kumpandisha hasira mzee Joel na kujikuta akimrushia Nolan glass ya maji iliyokuwa kwenye Meza. Nolan aliigonga ngumi glass ile na kuipasua pasua. "ukiniletea upuuzi na wewe nitakupasua pasua kama hiyo glass." Nolan akamwambia baba yake mzee Joel na kuelekea chumbani kwake. * Frank na Penina baada ya kufika uwanja wa ndege walifuata taratibu zote na hatimaye wakafanikiwa kuingia ndani ya ndege na dakika chache baadae walikuwa angani wakielekea South Africa. "kama tukifanikiwa kufunga ndoa nitafurahi Sana yaani furaha nitakayokuwa nayo sidhani kama itaelezeka." aliongea Penina huku akiwa amejiegemeza kwenye kifua cha Frank. "usijali mpenzi kila kitu ambacho kinatokea kimepangwa na Mungu na vitakavyotokea mbele ni Mungu pia anajua, hakuna mwanadamu asiyependa furaha." akaongea Frank kwa upole kumuambia Penina. "ni kweli mpenzi wangu." akajibu Penina na safari ikaendelea kwa masaa kadhaa na hatimaye wakawasili South Africa Katika jiji la Johannesburg na kuchukua chumba Katika hoteli moja ya kifahari. Baada ya kupumzika kwa dakika kadhaa Penina na Frank waliwasiliana na Nolan na kumjulisha jinsi safari yao ilivyokuwa. Nolan aliwataka wakae kwa amani na wasiwe na hofu yoyote yeye anaweka mambo Sawa na yakiwa tayari bas atawajulisha. * Vijana wa the killer bado walikuwa wakimtafuta Nolan na Sasa waliwasili nyumbani kwa kina Nolan na kukutana na mzee Joel ambaye aliweza kuwaambia Nolan yupo ndani na akawaelekeza chumba chake wakammalizie huko. Vijana wale taratibu walianza kuelekea Katika chumba cha Nolan, lakini kwa bahati mbaya ama nzuri Nolan aliwaona. "mmeamua kunifuata mpaka nyumbani nyie mmeisha." akajisemea Nolan Kisha akatoka chumbani kwake akiwa kifua wazi na kukutana na vijana wale sebuleni. Kilikuwa kitendo cha kushtukiza vijana wale hawakutarajia kukutana na Nolan sehemu Ile. Kitambo waseme waweke silaha zao tayari Nolan alianza kuwashambulia, na baada ya dakika chache Nolan aliwaweka vijana wale wote chini kwa kuwavunja vunja sehemu za miili yao. Mzee Joel ndio hakuamini baada ya kuingia ndani na kukuta vijana wote wamelazwa chini alafu kidogo hivi akatokeza Nolan akiwa amepigilia suti nyeusi Kisha akamwambia baba yake ambaye ni mzee Joel, "naenda kwenye kikao cha harusi ya Penina na Frank na kama utahitaji kadi unijulishe nikuletee ya kwako." ....... Itaendelea. ... Read More
*LOVE BITE EP 03* ILIPOISHIA………. Mawazo yalirudi tena kwenye ile picha na kuamua kuificha bila kuichoma moto kama alivyotaka mwanzo kufanya. Badala yake alienda sehemu ambayo kulikuwa na hati ya nyumba yake na kuiweka ile picha katikati. Ni kweli Prisza alikuwa anampenda na hawakuwahi kuachana. Ni muingiliano tu wa maisha ndi uliowatenganisha. Moyo wake aliona kama si haki kuichoma ile picha kwakua bado alikua na nafasi ndani ya moyo wake japokuwa kuonana na msichana huyo ni ngumu sana. Hata alipomaliza chuo alijitahidi kumtafuta bila mafanikio. Mpaka muda huu anajitegemea ni kipindi kirefu cha miaka sita tuko walipokutana na Prisca kwa mara ya mwisho. Mawazo ya msichana huyo wa kwanza katika maisha yake yalimchanganya kichwa na hakuwa na jinsi zaidi ya kukubali matokea na kuanzisha ukurasa mwengine wa maisha yake kwenye mapenzi na shani Baada ya usafi huo wa kabati lake, aliamua kujilaza kitandani na usingizi ukamchukua. SONGA NAYO………… Siku ya pili yake Jothan alienda kazini kama kawaida. Alifanya kazi zake na baada ya kurudi kazini alimkuta Shani amejaa tele nyumbani kwake. “karibu mume wangu “ alikaribisha Shani na kumfuata Jothan na kumpokea mizigo yake. “ahsante.” Aliongea Jothan na kumkabidhi mizigo yake Shani. “una oga kwanza au unakula ndio uende kuoga?” aliuliza Shani baada ya kurudi pale alipokuwa Jothan. “vyovyote tu mke wangu. Maana nahisi joto na hata njaa pia ninayo.” Aliongea Jothan na kumfanya Shani atabasamu. “kaoge kwanza, maana ukiwa vizuri hata chakula kitashuka barabara.” Alishauri Shani na mawazo yake yakapitishwa moja kwa moja na Jothan. Alipotoka kuoga Jothan, alirudi mezani na kukuta Shani ameshaandaa mapocho pocho ya kila aina yaliyochafua meza. “unajua mke wangu, hata niwe na njaa vipi, kama wewe upo nyumbani basi hudiriki kuitunza hiyo njaa kwa sababu unajua sana kupika mke wangu. Muda mwengine naomba nipate na njaa ya ajabu ili nikifakamie kisawasawa chakula chako.” Aliongea Jothan na Shani akabaki anatabasamu na kumuangalia Jothan kwa mapozi. Mapenzi moto moto kutoka kwa Shani yalizidi kupamba moto. Muda wote Shani alijitahidi kumuweka Jothan kwenye kundi la wanaoyafurahia mapenzi. Jothan alijisikia raha kutokana na Shani kila wakati kutokana na mauzo anayoyapata kuwa na msichana High classic. Walitamani kila saa wawe karibu na kulishana ndio style iliyowavutia watu wengi waliowashuhudia wawili hao walionyesha kupendana sana. Siku moja Jothan akiwa anatoka kazini, ghafla aliona gari likiwa limepaki pembeni na kuna msichana akihangaika kulishughulikia lile gari. Jothan alipaki gari lake pembeni na kushuka kwa ajili ya kutoa msaada. Alipomfika eneo la tukio, yule dada aligeuka kumuangalia Jothan na wote wakajikuta wanapigwa na butwaa. “JOTHAN!!” aliita yule dada kwa sauti kubwa iliyoambata na mshangao mkuu. “PRISCA!!” hata jothan naye alilitaja jina la yule msichana na kumfanya Prisca kujiachia na kupitisha mikono yake mgongoni mwa Jothan kupitia kweye makwapa yake kama ishara ya kumkumbatia. Jothan naye akampokeaa vizuri kwa kuzungusha mikono yake kwenye kiuno namba 6 cha Prisca. Baada ya kusalimiana, wakaona haitoshi. Waliacha gari zao pale pale na kutafuta sehemu tulivu na kukaa kwa ajili ya kupigiana story mbili tatu kutokana na kukumbukana kupita kiasi. “ ahsante mungu kwa kunikutanisha na kipenzi changu jamani,.. jothan milima haikutani ila binaadamu tunakutana. Leo hii kauli hiyo ndio naikubali kwa asilimia zote.” Aliongea yule dada huku akionyesha furaha ya wazi juu ya Jothan ambaye wakati huo alikua na tabasamu la usoni lakini kichwani alikua kwenye msongo wa mawazo. Anampenda Prisca lakini kwa sasa Shani amechukua nafasi kubwa kwenye moyo wake kutokana na kumpa kila anachokihitaji tena kwa wakati. Alikiri kuwa kwa sasa Prisca alizidi uzuri na kumfunika hata Shani. Maana Shani alikuwa ameridhika na kuzidi kuwa mnene kiasi japokuwa sio kigezo cha kupunguza uzuri wake. Ila Prisca alikuwa mwembaba lakini aliyekuwa na figa iliyojichonga kama glasi ya wine. Kwenye kiuno alikuwa mnene na kufaya hipsi zake kuonekana sana. Pia kijungu cha wastani kilichotupiwa huko nyuma ndio kilizidi kumpa maksi zaidi na kumfanya azidi kuonekana special na wanaume wote wanaojua viwango vya wanawake wazuri na wenye mvuto katika muonekano wa macho ya marijali. Kiuno kilichoingia ndani na muinuko wa kibinda ndio kilitengeneza namba 6. kiuno hicho mungu kawapendelea wasichana wachache sana. Hata wachina wameshindwa kutengeneza dawa ya kutengeneza kiuno hicho. Sura ya mviringo iliyokuwa na macho yenye kilevi bila ya kunywa kileo chochote ndio kilikuwa kivutio kingine. Ukiachana na weupe halisi ambao ulikuwa kiasi na kufanana na maji ya kunde, pia vijisima vidogo mashavuni vilivyojitokeza kila akifanya tendo lolote liliousumbua mdomo wake vilimfanya mtu yeyote kutamani kumuangalia usoni. Uso uliombwa na haya mbele ya mwanaume ndio ulikuwa kivutio hasa kwa mvulana mwenye kutafuta mtu wa kuweka ndani na kuoa kabisa. Mambo yote hayo ndiyo aliyokutana nayo Jothan baada ya kukutana na Prisca kwa mara nyingine baada ya muda mrefu. Hata yeye mwenye alikutana na majaribu hayo aliyoyafananisha na majaribu ayapatayo mwanamke mjane baada ya kusikia sauti ya mwanaume tajiri aliyekuja kumfariji na kwa kumuahidi kumuoa na kuwa tayari kuwalea watoto wake. Alijikaza kiume na kujaribu kuyaficha madhaifu yake yaliyomkumba na kujifanya yupo kawaida. “Hata mimi nimefurahi kukuona, za miaka?” aliongea Jothan na kumuangalia Prisca ambaye alikua na furaha wakati wote huo toka wameonana. “vipi, leo maaskari hawaji??” aliuliza Prisca na kucheka. “leo hakuna mwanafunzi hapa..au wewe mwanafunzi?..maana siku ile nilikataa kuwa mimi ni mwanafunzi halafu wewe ukajitambulisha kuwa mwanafunzi.” Aliongea Jothan na kufanya kicheko kitawale kwa sekunde kadhaa kati yao. “tumetoka mbali sana Jothan, leo naona kabisa kuwa mungu katufanya tusahau kipindi chote ambacho hatukua pamoja.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kuwa bado alikuwa na mawazo ya mapenzi juu ya Jothan. “hata mimi naona kama vile hatukuonana siku mbili kwa jinsi siku ya leo ilivyofukia mashimo ya miaka mingi niliyoishi bila kuiona sura yako.” Aliongea Jothan na kumuangalia Prisca aliyekuwa na kila kitu cha kutalii umuangalipo usoni. “nikuulize swali Jothan?” Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kushangaa kidogo baada ya kuombwa ruhusa ya kuulizwa kitu. Alifikiria kwa nukta kadhaa kisha akaruhusu kusikia kitu alichotaka kuuliza Prisca. “umeshaanzisha uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mwengine zaidi yangu?” Aliuliza Prisca swali hilo huku akiwa kawaida na kuonyesha wazi kuwa lile swali linahitaji majibu sahihi na yenye utashi juu yake. Jothan hakuamini kama swali lile lingekuja mapema kabla hajaliandalia maandalizi yoyote ya kujibu. Ubongo wake ulikimbia kwa kasi kutafuta jibu la kumpa kati ya ukweli au kumuongopea kwakua wakati huo swala la kumuepuka au kumpotezea msichana huyo aliyeonja penzi lake toka hajakuwa sister du kama hivi sasa. Elimu ya msichana huyo na maisha mazuri anayoishi pia vilikuja kwenye ubongo wake na kufanya machaguo kuwa mengi. Yaani kama ni mtihani, basi lile swali lilikuwa katika mfumo wa matiple choice tena lililokuwa na mfumo wa A,B,C,D,E na F.. “sina.” Alijibu Jothan huku moyo wake ukimuuma kumkana Shani. “wooh… ni wazi hii couple Mwenyezimungu amekuwa akiismamia kwa kipindi kirefu. Unajua kuwa hata mimi nilikuwa naamini kuwa kuna siku tutakuja kuonana tena. Ndio maana sikuona uzito wowote kuwakataa wanaume wengi huku nikiwa sijui ni lini tutakutana. Roho ingeniuma sana ungeniambia kuwa kuna mwengine umeshampa moyo wako.” Aliongea Prisca bila kujua kuwa huo ndio ulikuwa ukweli wenyewe. Maneno hayo yalimfanya Jothan ajione kuwa hakuwa na makosa kumuongopea kwa sababu angemwambia ukweli chochote kingeweza kutokea na kusababisha maongezi ya amani kati yake na Prisca kutoweka. “unataka kuniambia kuwa mpaka hivi sasa hauna mtu mwengine aliyerithi mikoba yangu?” aliuliza Jothan kimitego. “hakuna… yaani toka uliponiacha sijaguswa na mtu mwengine. Yaani hata kama ungekuwa umenifunga luku basi zingesoma unit zile zile ulizoziacha.” Aliongea Prisca na kumfanya Jothan kutabasamu. Waliongea mengi na kila mmoja alifurahia uwepo wa mwenzake pale. Waliachana baada ya kumrekebishia Prisca gari lake na kila mmoja kupata mawasiiliano yote ya mwenzake. Waliachana na ahadi ya kukutana naye tena walikubaliana kuwa watapeana taarifa kwenye simu. Siku hiyo iliwekwa kwenye Diary ya Jothan ambaye alikuwa anatemba nayo kwenye mkoba wake wa kazini. Usingizi ulikuja ukiambata na ndoto iliyojirudia kuanzia mwanzo hadi pale walipoachana. Aliamka asubuhi na kukuta Shani ameshamuandalia maji ya moto kwa kuwa asubuhi hiyo ilikuwa na kiubaridi kidogo. Alipoamka tu aliletewa nguo za bafuni pamoja na mswaki ambao ulisha wekwa dawa kabisa. Alipokuwa bafuni mawazo yaligeuka upande wa pili na kumfanya amuwaze pia Shani kwa jinsi alivyokuwa akitimiza wajibu wote kama mke bora anavyotakiwa kufanya. Kila aliloliwaza kutendewa na msichana basi Shani alikuwa wa kwanza kufanya hata kabla hajaambiwa fanya. Hayo na mengine mengi ndio yalimfunga Jothan na kuyatuliza macho yake kwa wasichana wengine na kumfanya kuwa mtiifu kwa kurudi nyumbani mapema. Na kama anataka kupata moja moto maja baridi basi hutoka na mpenzi wake huyo ambaye alimfanya kuinjoy kwa kuwa sehemu nyigi walizoingia hakukua na mtu mwenye demu mkali kama wake. Alimaliza kuoga huku kichwani hakujua jibu nini kati ya A au B. kuna wakati alitamani kuyaweka kuwa yote ni majibu. Kuna wakati alitamani arushe shilingi ila alishindwa kumjua nani amuweke mwenge na nani amuweke bichwa. Prisca ndio msichana waliyebikiriana kwakua yeye hakuwahi kufanya mapenzi kabla kutokana na ulinzi thabiti wa wazazi wake alipokuwa anasoma. Na Prisca ndiyo yeye aliyekata utepe. Shani ndio mpenzi wake wa ukubwani ambaye anamuonjesha matamu ya ndoa hata kabla hajafikia maamuzi ya kuoa. Hata sasa anaanza kuonekana na kitambi kidogo kwa sababu ya raha azipatazo kwa mpenzi wake huyo. Japokuwa walikuwa wapenzi kwa kipindi kirefu, lakini hawakuwahi kukaa pamoja hata wiki moja kwa sababu kila mmoja alikuwa anaishi na wazazi wake. Ila Shani na yeye wamekuwa wakilala pamoja mara tatu kwa wiki. “itakavyokuwa ndio hivyo hivyo.” Aliongea Jothan baada ya kuona anaisumbua akili yake bila majibu sahihi. Siku waliyo ahidiana kukutana kati ya Jothan na Prisca iliwadia huku kila mmoja akiwa amewasili bila kukosa huku wakiwa wamejitupia vitu vya thamani kila mmoja. Make up na mpangilio wa nguo alizovaa Prisca zilimfanya kuonekana katika muonekano mwengine wa kuvutia zaidi. Jothan hakuamini kuwa ndiye yeye alikuwa analala kwenye kifua cha yule msichana zamani. Pia hakuamini kuwa huyo msichana ndiye aliyekuwa akilipigania penzi lake miaka yote japokuwa walikuwa hawajaonana miaka mingi. Walikutana huku kila mmoja akiwa ameshuka kwenye gari lake na kwenda kwenye hotel moja yenye hadhi hapa Dar. Walipata chakula cha mchana na baadae wakaenda kwenye swimming pool kuogelea. Hamadi !, Macho yalimtoka Jothan baada ya Prisca kuvua nguo zake na kubaki na nguo ya ndani huku juu kukiwa na sidiria ndogo iliyobana maziwa yake na kuyafanya yapande juu na kuonekana sehemu kubwa ya maziwa iliyoteganishwa na msitari mmoja kati kati kuwa wazi. Jothan hakuona ubaya kuvua nguo na yeye na kubaki na boxer na kujumuika naye kwenye swimming pool huku wakiwa peke yao eneo hilo lililokuwa na mabwawa mengi ya kuogelea. Waliogelea na kujikuta michezo yote wanacheza. Kuanzia bembea, mpira wa pete na mwisho wakamaliza na mchezo usio hitaji kocha wala mashabiki japo kuwa unapendwa na watu wengi hapa duniani. Ukiwa mtoto unaambiwa kuwa mchezo huo ni mmbaya lakini ukikuwa bila kufundishwa unajikuta unacheza huku ukijilaumu kwa nini hukuanza kucheza toka mwanzo. Hawakujua walitumia muda gani kwakua taa za ile hotel ziliwaka muda wote na kufanya mtu asitambue wakati kama hajaangalia saa. Mndinyo wa kitanda murua cha hotel hiyo ndio sababu iliyowafanya kudumu muda mrefu huku kila mmoja akiwa ame miss raha za mwenzake. Mechi hiyo ya marudiano ilikuwa kali na kila mmoja alikiri kuwa walihitaji kuwa karibu na kucheza kila mara. Baada ya muda, Jothan aligutuka kuwa hiyo siku ndio siku Shani alikuwa analala kwake. Aliamka fasta na kutupa macho yake kwenye saa ya ukutani “MUNGU WANGU…. SAA SABA USIKU?” Alishtuka kimoyo moyo na kutaja alichokiona kwenye saa. Aliamka ili aenda kuoga kwa ajila ya kwenda nyumbani kwake. “vipi darling, unaenda wapi tena… mwenzio nahitaji kimoja tu cha mwisho.” Alidakwa mkono kimahaba na Prisca aliyekuwa ameyarembua macho yake na kuonyesha ishara zote za kuhitaji kipindi cha pili baada ya mapumziko. “najisikia uchovu ndio maana nilikua nataka kwenda kuoga.” Aliongea Jothan huku akiwa na wasiwasi mkubwa juu ya Shani kugundua usaliti alioufanya siku ile. “twende wote babie, tukirudi mpango mzima au…” aliongea Prisca na kumfanya Jothan azidi kuchoka. “poa.. twende.” Alikubali kishingo upande na wote wakaenda kuoga na uchokozi alioufaya Prisca huko bafuni ikiwafanya mchezo huo kuanzia huko huko bafuni na kumalizikia kitandani wakiwa hoi na usingizi wa muda wote waliokuwa wakicheza cheza ulikuja na kuwafanya wapate usingizi mnono. Saa nne asubuhi ndio waliachia kitanda na kwenda kuoga. Walipofungua mlango walikutana na wahudumu waliokuwa wakigonga kwa ajili ya kufanya usafi. Walieda kupata supu kutokana na kupotelewa na nguvu nyingi masaa kadhaa yaliyopita. Baada ya hapo. Walijiandaa na kila mmoja akapanda kwenye gari lake huku Prisca akionyesha wazi kuwa aliufurahia uzinduzi wa uhusiano yao uliofanyika kwenye kitanda cha hotel ya SERENA. Jaothan akiwa kwenye gari lake, aliiona simu yake aliyoiacha makusudi kwa ajili usumbufu pindi awapo na Prisca. Alikuta missed call zaidi ya kumi na tano na sms sita zote zikiwa za Shani na zikionyesha kuwa na wasi wasi juu ya usalama wake. Alihuzunika sana kwa kosa alilolifanya japokuwa hakupanga kulala nje. Maisha ya kuendesha mioyo miwili hakuwahi kuishi na tayari kwa siku hiyo aliona adha yake na kutamani kuchuja na kuwa na mmoja tu. Ni nani ambaye angestahili kubaki na ni nani atoke ndio swali lililokosa majibu kwakua wote alikuwa anawakubali kwa wakati wao. Alivyolala na Prisca alikuwa kama alikuwa anamfungua kwa mara ya kwanza hali iliyomfanya aamini kuwa hakutumika muda mrefu. Aliona sio sawa kumuacha msichana huyo mwenye ndoto naye nyigi za maisha yao toka walipokuwa wanasoma. Na Shani hakustahili kutendewa unyama wowote kwakua hata yeye hajawahi kumfanyia unyama wowote zaidi ya kumfariji anapokuwa ana huzuni na daima aliisimamia furaha yake hata ikibidi kuenda kinyume na matakwa ya dini kwa kukubali kuishi nae bila ndoa. Akiangalia kila mmoja alionyesha kumpenda kwa wakati wake na hawakuwa tayari kumuachia. Ila yeye swali la NIMPENDE NANI lilimsumbua kuliko hata DIAMOND. Aliamua kuwasha gari lake na kuelekea nyumbani. “oooh.. ahsante mungu. Umekumbwa na nini kipenzi changu?.” Aliongea Shani baada ya kuupokea mkoba wa Jothan. Hali hiyo ilimshangaza Jothan kwakua hakutegemea mapokezi kama yale. “samahani mke wangu, sikukupa taarifa kuwa ofisini kuliandaliwa warsha na nikaenda kwa kudhani itaisha siku hiyo. Hata hivyo simu yangu niliisahau kwenye gari na kunifanya nisizione missed call zako mapema.” Aljiuma uma Jothan mbele ya Shani ambaye wakati huo ndio kwanza alikuwa anamvua viatu baada ya kukaa kwenye moja ya masofa yaliyokuwa pale sebuleni. “sawa mpenzi wangu. Nimefarijika tu wewe kurudi salama.. maana nilikuwa na wasi wasi juu ya uzima wako tu.” Aliongea Shani na kumuonyesha Jothan jinsi anavyomjali. “samahani sana mpenzi wangu, nitajaribu kukupigia simu kwa kila siku nitakayochelewa kurudi nyumbani.” Aliongea Jothan na kukiri kuwa amefanya makosa makubwa ambayo hata yeye mwenyewe hakuyategemea. Siku hiyo ilipita kwa Jothan kulala muda mrefu kutokana na uchovu wa jana yake. Asubuhi aliamka na kukuta ameandaliwa nguo za kuvaa kwa ajili ya kwenda kazini zikiwa zimepigwa pasi kabisa. Aliwekewa maji ya uvugu vugu kwa ajili ya kuoga kisha kifungua kinywa matata kilikuwa tayari mezani kinamsubiria yeye tu. “ashante mke wangu.” Alishukuru Jothan baada ya kumaliza kunywa chai. “usijali mume wangu, nakutakia safari njema. Take care honey.” Aliongea Shani na kumfungulia mlango wa gari Jothan. Jothan alifika kazini mapema na kufanya kazi zake kama kawaida. Saa nane alitoka kazini na kurudi nyumbani. Alikuta ameandaliwa chakula cha mchana mezani lakini Shani hakuwepo kwakua ilikuwa ni siku ya kwenda kwao. Alijihisi mpweke na alitamani Shani angekuwepo kwake moja kwa moja. Alikata shauri baada ya kula chakula na kuamua kumtafuta mpenzi wake kwenye simu. “hallow” alipokea Shani kwa mapozi. “I miss u babie, unaweza kuja tutoke baadae kidogo tukale mbuzi maeneo ya Facebook pub?” aliongea Jothan. “noo babie, leo nimeenda kwa mama. Sio vizuri kuonyesha tabia mbaya mbele yake ya kurudi usiku. We vumilia babie. Kesho tutakuwa wote.” Aliongea Shani kwa pozi zilizomfanya Jothan kushindwa kukata simu hata kama maneno ya msingi ya kuongea nae yameisha. “basi sawa. Sijui lini utanipeleka kwa mama.” Aliongea Jothan huku anatabasamu. “si wewe mwenyewe tu hujaamua. Ukiamua hata leo nakuleta huku.” Aliongea Shani huku akionyesha wazi kuwa alikua anacheka. “nitakuja tu mine, si unajua mambo mazuri hayahitaji haraka.” Aliongea Jothan na kukata simu. Siku ya pili yake walitoka pamoja na kwenda kula bata maeneo hayo na kurudi mida ya saa tano usiku. Alipokuwa kazini, alisikia simu yake ikiita kwa mlio tofauti. Kabla hata hajasoma jina la mpgaji wa hiyo simu. Tayari alishamtambua kwakua aliihifadhi namba ya mtu huyo kwa mlio tofauti kwa makusudi. “haloo.” Aliipokea ile simu. “haloo babie, I miss u.” sauti nyororo ya kike ilisikika upande wa pili. “I miss u too Prisca, niambie.”aliongea Jothan huku akiangalia wafanya kazi wenzake waliokuwa bize wakifanya shughuli zao. “hata kunitafuta wangu,.. yaani kama uliniroga mwenzako siku ile. Yaani sijielewi mpaka hivi leo.” Aliongea Prisca kwa sauti ya mahaba. Jothan aliangalia na kuona soo kuendelea kuongea maneno yale mbele ya wafanyakazi wenzake. “sema nini babie, nitakupigia nikiwa free. Now nipo kazini halafu nina kazi nyingi.” Aliongea Jothan kwa sauti ya chini. “sawa wangu, baadae.” Aliitkia Prisca na kukata simu. Jothan alifanya kazi zake na kurudi nyumbani kwake. Baada ya kupata chakula cha mchana, alijitupa kitandani na kuchukua simu yake na kumpigia Prisca. “haya lete maneno.” Aliongea Jothan baada ya Prisca kupokea simu. “nina hamu ya kuonana na wewe babie… sihitaji kuwa mbali na wewe hata kwa dakika moja kwa jinsi nillivyozimika mbaya.” Aliongea Prisca kwa sauti iliyomshinda mwana dada wa kipindi cha ala za roho kinachoruka usiku kwenye kituo cha clouds fm. Sauti ilipenya vizuri kwenye masikio ya Jothan na kuhisi labda Prisca alichanganya sauti ya Loveness love (Diva) na wema sepetu. “tupange week end, sababu katikati ya wiki ni majanga.” Aliongea Jothan. “poa, ijumaa si ulisema unatoka mapema. Unaonaje kama tukikutana siku hiyo.” Aliongea Prisca na wazo lake likapitishwa moja kwa moja na Jothan. Siku ya ijumaa ilipofika. Jathan alimpa taarifa Prisca na wakakutana maeneo ya Peacock hotel iliyopo maeneo ya mnazi mmoja. Jothan alifika na kumkuta Prisca alishafika muda mrefu kidogo na tayari alishaagiza kinywaji na alikua anakunywa taratibu. Alipofika, alipokelewa kwa kukumbatiwa na Prisca na kupewa mabusu matatu matakatifu kwenye mashavu yake na moja likiwa sawia mdomoni mwake. Baada ya salamu hiyo adhimu. Walimuita muhudumu aliyekuja haraka na kumpa oda yao. “tuchukue chumba sasa hivi au baadae?” aliuliza Prisca baada ya kumaliza kula. “hapana, leo sijisikii vizuri kabisa na sipo tayari kushiriki tendo lolote Prisca.” Aliongea Jothan na kumfanya Prisca apigwa na butwaa. Maana alijiandaa kabisa kupata mechi nyingine siku hiyo. “kwanini babie….unaumwa???” aliuliza Prisca kwa mshangao. “siumwi, ila mayo wangu unanisuta kila siku nikiongea na wewe kwenye simu au nikikutana na wewe. Najihisi sifanyi fair kwa nikitendacho.” Aliongea Jothan huku sura yake ikionyesha wazi kuwa hakuwa na furaha ingawaje aliingia kwa muonekano wa mtu aliyefurahia uwepo wao pale. “jamani, tatizo ni nini wangu, mbona una nifumba fumbo ambalo sijui nitalifumbua vipi?…naomba uniambie ukweli kuliko kuniweka mwenzako kwenye uzio wa alama ya kuuliza.” Aliongea Prisca huku akionyesha wazi kubadilika kutoka katika hali ya furaha aliyokuwa nayo mwanzo na kuungana na Jothan. “Prisca, hivi bado unanipenda?” aliuliza swali Jothan lililomfanya Prisca apigwe na bumbuwazi kwakua hakulitegemea lile swali. “nakupenda sana tena zaidi ya niwezavyo kuelezea kwa ulimi wangu. Ndio maana nikaweza kukaa kipindi kirefu bila ya kuwa na mtu mwengine japokuwa ni wengi walikuwa wanakuja kunitongoza na bado sikuona umuhimu wa kuanzisha mapenzi mapya kabla mapenzi yako wewe na mimi kufa.” Aliongea Prisca na kumuangalia Jothan aliyekuwa makini kumsikiliza. “hata mimi nakupenda Prisca, ila mimi ni msaliti na sio mwema kwako hata kidogo. Cha kwanza nimekuwa muongo kwa kukuongopea toka siku ya kwanza tulipokutana kwa mara ya pili ukubwani. Cha pili sistahili kuwa wako kwakua tayari nimeshakuharibia mipango na malengo yako kwa kipindi krefu Prisca.” Aliongea Jothan huku akionyesha wazi kuwa alikuwa katia wakati mgumu kufunguka yale yaliyomjaa moyoni. “sikueliwi Jothan.. naomba nidadavulie uyasemayo.” Aliongea Prisca huku akionyesha kuchaganyikiwa. “kwanza naomba unisameha Prisca kwa haya nitakayokuambia. … nilifanya makosa makubwa siku ile kwa kutokuambia ukweli kuwa tayari nina msichana na ninaishi naye. Nampenda sana ingawaje sikuweza kutoka kwenye mitego yako siku ile kwakua wewe ndio wa kwanza kukaa moyoni mwangu na chembe chembe za upendo juu yako ndizo zilizonisukuma mpaka kukuongopea na kukuambia kuwa sina mtu. Siwezi kuweka mafahari wawili kwenya zizi moja. Na kumuacha Shani ni kitu kisichowezekana kwakua ananionyesha mapenzi zaidi ya niliyowahi kufikiria mapenzi kuwa hivyo. Maamuzi yangu ni kwamba. Kuanzia leo sahau kuwa na mimi ni mpenzi wako…. Niwie radhi kwa hili.” Aliongea Jothan huku machozi yakimlenga lenga. Hakika ni uamuzi mgumu aliouchukua kwakua aliamini ilikuwa ni mtihani mkubwa katika mapokezi ya mlengwa. Alipoinua macho yake kumtazama Prisca, tayari mashavu ya prisca yalishalowana kwa machozi huku macho yakiwa mekundu. Kilio cha kwiki kilianza kusikika na kumfanya Jothan kuingiwa na imani baada ya kumtaza mpenzi wake huyo anaye amua kumuacha bila kosa lolote. ITAENDELEA ... Read More
Story...... NI WEWE TU PENINA Sehemu ya kumi (10) By GIVAN IVAN Phone & whatsapp...... 0769673145 Ilipoishia...... Baada ya dakika kadhaa Frank na Penina waliwasili nyumbani kwa Frank. Wakashuka kwenye bajaji na kuelekea kwenye nyumba ya kina Frank. Walipoufikia mlango Frank alijificha nyuma ya Penina na kumtaka Penina abishe hodi ili wawafanyie surprise Wazazi wake Frank. ***********Endelea ********* Mlango ulifunguliwa na mama yake Frank na kukutana uso kwa uso na Penina. "ooh mwanangu hujambo?" akauliza mama yake Frank. "sijambo mama shikamoo." akasalimia Penina "marahaba karibu ndani." mama yake Frank akamkaribisha Penina. "Asante mama ila nataka nikufanyie surprise." Penina akamwambia mama yake Frank. "hii ipi tena mwanangu usije ukaniue kwa presha." akaongea mama yake Frank, na Muda huo huo baba yake Frank naye akajitokeza sehemu pale na kuungana na mama yake Frank. Penina alisogea pembeni na hapo hapo Frank akajitokeza mbele ya Wazazi wake. Mama yake Frank alijikuta akishindwa kuongea na kumrukia Frank kwa furaha isiyo na kifani. Frank pamoja na Wazazi waliingia ndani huku wakiwa na furaha tele kwa kumuona tena Frank ambaye alitoweka kwa siku kadhaa. Lakini kila mmoja alikuwa na hamu ya kutaka kujua ni nini kilimtokea Frank. Frank ilibidi awaeleze kilichomtokea mwanzo mpaka mwisho. Kila mtu alihuzunika kwa hicho kilichomtokea Frank. Lakini pia Penina aliwaeleza pia kilichomkuta kaka yake Nolan na Mpaka Muda ule kaka yake alikuwa bado yupo hospitalini. Lakini hata hivyo furaha ilirejea upya usoni mwa Penina pamoja na Wazazi wake Frank baada ya kumuona Frank kwa Mara nyingine tena. Frank alienda kuoga na kubadilisha nguo Zake zile zilizochakaa na kuvaa nguo zingine nzuri ambazo ziliendana vizuri na yeye. Frank aliondoka na Penina na kuelekea moja kwa moja mpaka Katika hospital aliyopo Nolan kwa ajili ya kumjulia hali. * Lakini kumbe Katika hospital ile, Nolan baada ya kujua kuwa baba yake ndio alimfanyia mchezo ule. Nolan hakubaki tena pale hospitalini alitoroka bila hata kuruhusiwa na daktari na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwao. Penina na Frank baada ya kufika hospitalini pale. Walistaajabu kuambiwa kuwa Nolan hayupo pale hospitalini na hawajui alipoelekea. Penina na Frank waliondoka na kuelekea nyumbani kwa kina Penina wakihisi labda Nolan ameelekea huko. Na kweli baada ya kufika nyumbani kwa kina Penina walimkuta Nolan akiwa ameketi nje ya geti lao huku akionekana kuwa na mawazo tele. "Nolan vip ndugu yangu mbona mawazo tele?" alikuwa Frank akimuuliza Nolan baada ya kumkaribia. Nolan alinyanyua kichwa chake na hakuamini baada ya kumshuhudia Frank akiwa amesimama mbele ya macho yake akiwa pamoja na Frank. "oooh Frank ni wewe?" akauliza Nolan kama vile haamini, Kisha akanyanyuka na kumkumbatia Frank kwa furaha Sana. "nimefurahi Sana kukuona tena Frank, hakika wewe ndio furaha ya mdogo wangu Penina karibu tena Frank." akaongea Nolan kumuambia Frank. Na hapo hapo Nolan akamtaka Frank amueleze ni nini kilichomkuta mpaka akatoweka Muda wote ule. Frank Bila kusita alimuelezea Nolan mkasa mzima uliomkuta wa kutekwa na watu asiowafahamu. Nolan alimhurumia akampa moyo na kumtaka ajikaze kwasababu wana vita nzito mbele yao. Lakini pia Nolan akawaelezea jinsi baba yake mzee Joel alivyomtumia watu waje wamuue kwasababu ya kutetea penzi La Penina na Frank. "ina maana baba anataka akuue?" Penina akamuuliza Nolan kwa mshangao. "ndio nadhani ndio nia yake kwasababu ameona mimi ndio niliyeamua kusimama na kulitetea penzi lenu." akaongea Nolan kwa huzuni Sana. Penina pia alihuzunika Sana mpaka machozi yakaanza kutiririka usoni mwake baada ya kugundua baba yake ndio alipanga njama ya kummaliza Nolan. "lakini msijali kuweni na amani mimi nawakikishia lazima mtaoana na kuwa mume na mke." akaongea Nolan kwa kujiamini. "tunashukuru kusikia hivyo hata sisi tutakuwa pamoja na wewe kwa lolote lile." akaongea Frank naye kwa kujiamini. "Sasa sikilizeni niwaambie, nataka niwasafirishe muende mkakae nchi nyingine kwa miezi miwili alafu mimi nitabakia hapa Tanzania nikifanya taratibu za nyie kufunga ndoa na kila kitu kikiwa tayari nitawajulisha na mtarejea Tanzania kwa ajili ya kufunga ndoa yenu." akaongea Nolan kumwambia Frank na Penina. Bila kipingamizi chochote Penina na Frank walikubaliana na wazo la Nolan na kilichotakiwa ni kwenda kujiandaa na kuondoka. "ngoja bas nikajiandae Mara moja." akaongea Penina, lakini Nolan akamzuia na kumwambia. "usiingie ndani tena, sitaki uonane na baba kuanzia Sasa kila kitu utakachahitaji nitakutimizia mimi, katafuteni hoteli yoyote mkae hapo mkijianda na kama na pesa au kitu chochote mtaniambia mimi." aliongea Nolan kwa msisitizo. "ok tumekuelewa tupo pamoja." akajibu Frank Kisha wakaondoka pamoja na Penina. Nolan alinyanyuka pale chini akagonga geti na kufunguliwa na mlinzi na bila kusema kitu Nolan akaelekea moja kwa moja mpaka sebuleni ambapo alimkuta baba yake mzee Joel akiwa ameketi huku akionekana kuwa na mawazo. "Niko sambamba na wewe kwa chochote kile utakachokifanya, sitajali kama wewe ni baba yangu au nani wangu lakini nachotaka utambue Frank lazima amuoe Penina." akaongea Nolan kumwambia baba yake Kisha akaondoka na kuelekea chumbani kwake bila kusikiliza baba yake atasema nini. "wewe lazima nikuue wewe hata kama mimi ni baba yako huwezi kuniingilia Katika mambo yangu." akajisemea mzee Joel na kutoka nje kwa kasi mpaka kwenye gari Lake. Mlinzi alifungua geti na moja kwa moja mzee Joel akatoka kwa kasi mpaka Katika hospital waliyolazwa wakina Zaza. Mzee Joel alishuka kwa kasi kwenye gari Lake na kuelekea mpaka Katika chumba walicholazwa wakina Zaza. "Zaza mlifanya nini mbona mmeniangusha kias hiki?" akaongea mzee Joel kwa jazba. "mzee Joel yule mwanao ni hatari Sana hebu ona tulivyovunjwa vunjwa." akaongea Zaza huku akionesha jinsi walivyopigwa na Nolan . "ni bora mlivyopigwa kuliko hichi kingine kilichoibuka." akaongea mzee Joel na kushika kiuno. "nini tena mzee wangu?" akahoji Zaza huku akiwa anajinyanyua pale kitandani alipokuwa amelala. "Frank amerudi" akajibu mzee Joel na kuwafanya wakina Zaza washangae. "yaani kwa kweli mmeniangusha Sana alafu isitoshe Nolan ameshaanza kuota mapembe na kama nyie mmemshindwa bas itabidi nitafute wababe wengine zaidi yenu na nyie lazima nitawaua pesa niliyowapa ni nyingi Sana lakini hakuna cha maana mlichokifanya pumbavu nyie. " akaongea mzee Joel kwa hasira Kisha akageuka na kuondoka. * Penina na Frank waliwasili kwenye hoteli moja ya kifahari na kufanya taratibu zote na kuchukua chumba kwenye hoteli Ile na kulipia kukaa hapo kwa siku tatu. Lakini Frank aliwapa taarifa Wazazi wake ya jinsi mipango inavyofanyika hivyo akawataka wasiwe na hofu yoyote kuhusu yeye.* Upande wa Nolan yeye alipanga lazima amfundishe adhabu baba yake kwa namna yoyote ile. "Wewe ni baba yangu ndio sikatai, umenitunza vizuri, umenipa elimu ya kutosha Sawa, lakini kwa unyama huu unaotaka kuufanya hakika sitakuacha lazima nitaenda sambamba na wewe." alijisemea Nolan akiwa chumbani kwake akipanga mipango yake. Lakini pia Nolan aliapa kama asipofanikisha ndoa ya Frank na Penina bas atajiua. ............. Itaendelea ... Read More
NILIPOTEZA WATOTO WANGU WANNE (Mkasa wa maisha ya ndoa ya Naomi) Sehemu ya kwanza(01) Naitwa Naomi Charles,katika maisha yangu sikuwahi kuamini haswa mambo yanayohusiana na nguvu za giza,kitu pekee nilichojua ni kwamba hivi vitu huwa vipo midomoni mwa watu tu,lakini kadri nilivyozidi kukua na kuingia katika maisha ya ndoa hapo ndipo nilipokuja kushuhudia kwa macho yangu kwamba haya mambo si ya kwenye midomo ya watu,bali yanafanyika na kuishi katika jamii mwa watu. Ndugu yangu amini nakuambia,kama kuna mwanga basi elewa hata giza lipo,na siku zote lengo la kuwepo mwanga ni kwasababu ya kukimbiza giza,kusingekuwa kuna ulinzi wa Mungu endapo kama mambo ya giza yasingekuwepo,nilichokuja kuamini ni kwamba siku zote uwepo wa mwanga wa Mungu wa wanadamu ni kwasababu ya kukimbiza giza linalowanyemelea wanadamu. Niliwahi kusoma vitabu na kama vile "Dollo,Mama yangu anakula nyama za watu" na kitabu cha "Jini lilivyonilelea mwanangu kimiujiza",waliandika na kusema hiyo ni mikasa ya ukweli lakini bado nilisema kwamba huu ni utashi tu wa utunzi wa watu. Ni miaka takribani 15 imepita tangu niamue kuachana na safari ya ndoa na John mume ambae nilipenda kumuita J...Alinioa ndoa ya halali kabisa,nakumbuka kipindi naonana nae alikuwa na miaka 40 wakati huo mimi nilikuwa na miaka 28,alikuwa ameniacha mbali ki umri lakini haikuwa sababu ya penzi letu kufa. Lakini kuna mambo mawili ambayo yalinishangaza kwake,alikuwa na umri mkubwa sana na majukumu ya kumuingizia pesa lakini cha ajabu bado alikuwa anaishi na Mama yake mzazi,cha pili ni kwamba aliniambia kwamba alipokuwa na umri wa miaka 30 alipataga mke ambae walipanga kuoana lakini aliamua tu kuishi nae nyumbani kwao kama mke wake,baada ya miaka mitano kupita John aliniambia mwanamke yule aliamua kukatish safari ya mahusiano na yeye,alibahatika kuzaa nae watoto wawili lakini wote walifariki. John hakuniambia ni sababu ipi iliyomfanya hasa aachane na yule mwanamke. Nakumbuka baada ya ndoa yangu mimi na John nilimshawishi na kumwambia kwamba mimi staki tuendelee kukaa pale na mama yake,tuondoke tukaanzishe maisha yetu na kama Mama tutaendelea kumjali maana si kwamba amezeeka kufikia kipimo cha kuweza kukaa nae na kumlea. John alinikubalia na kusema tutahama lakini tukae kae kwanza pale kwao wakati anajipanga. Miezi miwili ilipita tangu ndoa,hatimae nilishika ujauzito tukiwa bado tunakaa na palepale kwa Mama yake,ambae ni mama mkwe wangu,wote walifurahi baada ya kuona mimi nimekamata ujauzito. Wanasema kulea Mimba sio kazi bali kulea mtoto,miezi tisa si mingi kama ukiwa na subira,hatimae nilishusha mtoto wa kiume,furaha kubwa ilitawala baina ya familia zetu pamoja na mimi na mume wangu,ilikuwa ni furaha isiyo na kifani,wajirani na marafiki wa kutembelea hawakukosekana,taratibu kazi ya kulea mtoto ilianza. Hatimae miezi sita ilipita,mtoto alizidi kuchangamka,kilichobaki kinaniumiza ni kwamba kila nikimuambia mume wangu tuhame kwa mama yake tukaanzishe maisha yetu alikuwa ananijibu bado hajajipanga,likikuwa linaniumiza sana kichwa swala hili na nilijikuta nakata tamaa ya kuwa namuuliza mara kwa mara. Katika safari yangu ya ndoa sintakuja kuusahau usiku,usiku ambao vindumbwe ndumbwe na maajabu vilianza katika maisha yangu,nakumbuka nilikuwa nimelala mimi na mume wangu pamoja na mtoto wangu huyo wa miezi sita,ambae tulimpa jina la Grey,niliota tumezunguukwa na wanawake wanne mimi na mume wangu kwenye kitanda ambacho tulikuwa tumelala,wanawake hao walikuwa wamevalia shuka nyeupe ambazo wamejifunga rubega,nilitaka kupiga kelele lakini moja ya wanawake wale aliniziba mdomo kisha mmoja wao akanyoosha mikono yake na kumchukua mwanangu,nilikodoa macho na kutamani kupiga kelele lakini nilishindwa kwasababu nilishikwa,nilimkazia macho yule mwanamke aliemchukua mwanangu na ndipo niliposhikwa na bumbuwazi baada ya kugundua kwamba ni mama mkwe wangu.Alianza kuondoka na mwanangu huku akifuatiwa na wale wanawake watatu waliobaki,nilianza kupiga kelele za kumlilia mwanangu mpaka nalia huku nikiinuka kitandani kuwafuata,ghafla nilishtushwa na mume wangu huku akiniambia"we Naomi unaenda wapi huko na kupiga kelele na wakati mtoto huyu hapa,umepatwa na nini".Nilianza kuhema huku nikimwangalia mwanangu kama yuko salama,wakati huo nikawa namwaga jasho. Hazikupita sekunde nyingi,mwanangu alianza kulia huku akitoa povu jeupe mdomoni.Nilijikuta naanza kuchanganyikiwa akili.... JE NINI KITAENDELEA Je Grey atapona...? Je ndoto aliyoota Naomi inauhalisia wowote katika maisha yao..? tukutane sehemu ya pili kesho jioni panapo majaaliwa. Ruksa kushare,pia toa maoni yako ili watu wajifunze zaidi. NILIPOTEZA WATOTO WANGU WANNE-(02) (Mkasa wa maisha ya ndoa ya Naomi) Ilipoishia. Hazikupita sekunde nyingi,mwanangu alianza kulia huku akitoa povu jeupe mdomoni.Nilijikuta naanza kuchanganyikiwa akili.... Sasa endelea... Nilijikuta nalia tu huku nikiita"Greeeey....Greeey",wakati huo sasa mume wangu nae ndipo alipomtazama mtoto wetu na kugundua kwamba mdomoni anatoka povu,nilimuona ameshtuka ghafla na kuinuka kutoka kitandani huku akiuliza"Naomi,mtoto amekuwa na nini,inamaana alikuwa anaumwa harafu hukuniambia mpaka amezidiwa hivi..?". Moja kwa moja Mume wangu alijua labda huenda nimemficha sikumwambia kama Grey alikuwa anaumwa kitu ambacho hapana. Grey alizidi kulia zaidi na wakati huo povu jeupe liliendelea kumtoka,wote tulikuwa tumechanganyikiwa hatujui tufanye nini,ndipo Mume wangu alienda sebureni na kuchukua maji haraka haraka kisha kumnywesha Grey,wakati anakunywa maji alitulia kwanza kulia lakini baada ya kumaliza tu kunywa maji kilio kiliendelea tena,nilimchukua na kuanza kumnyonyesha lakini alikataa ziwa,mara muda haukupita Bibi yake ambae ni mama yake na Mume wangu akawa ametugongea mlango"nyie kuna nini tena humu?,mbona mtoto analia hivi".Mume wangu alimfungulia mlango kisha akaingia ndani,alifika na kuanza kumtazama mtoto ambae alikuwa bado analia,mimi nilijikuta naacha kumtazama mwanangu badala yake nilianza kumtazama huyu mkwe wangu huku nikikumbuka nilichoota,nilitamani nijue zaidi hivi nilichoota kina uhalisia au ilikuwa ndoto tu. Ghafla nilimuona Mama mkwe wangu akimuweka mwanangu kitandani na kusema"huyu mtoto mbona ameumwa ghafla hivi kulikoni,au alianza toka mchana lakini hukutuambia,hebu mwangalieni na mwili wake ulivyobadilika na kuwa mwekundu"aliposema hivyo moyo ulinilipuka na kuacha kumtazama yeye kisha kumtazama mwanangu,sikuamini kuona mwili wa mwanangu aliekuwa mweupe umekuwa mwekundu rangi ya damu kabisa,kulia nako kukazidi,nilimchukua na kuanza kumbembeleza lakini haikusaidia kitu,matokeo yake na mimi nilijikuta naanza kulia huku nikisema"Baba Grey mwanangu anakufa,Mwanangu anakufaaa"Nililia sana wakati huo Baba Grey nae anawaza afanye nini. Mama mkwe alitoka ghafla kisha kuelekea sebureni,alikaa huko kwa dakika kadhaa kisha akarudi na maji kwenye kikombe akasema"Hebu mnyweshe haya maji nimeyachanganyia chumvi na sukari huenda yakamsaidia",kweli niliyachukua haraka haraka kisha nikamnywesha,kweli duniani kuna maajabu,kwani baada tu ya kumnywesha yale maji Grey aliacha kulia na kukubali kunyonya lakini mwili wake uliendelea kuwa mwekundu. Ilikuwa mida ya saa kumi usiku na ndipo Baba Grey alisema sasa tumpeleke Grey hospitali,kweli juhudi za kujiandaa kwenda hosipitali zilianza na hatimae safari ilitimia,tulifika kwenye Zahanati moja hivi iliyokuwa jirani na sisi na kumkuta daktari wa zamu,walitupokea kisha wakamuangalia mtoto kitendo kilichofanya daktari ashtuke baada ya kumuona ni jinsi gani Grey alivyokuwa mwekundu,harakati za vipimo na matibabu vilianza,juhudi zilifanyika na wapimaji wakati sisi tukiendelea kusubiri,majibu yalikuja ya kushangaza kwani tuliambiwa kwamba Grey hana ugonjwa wowote,hapo ndipo nilipoanza kuona kwamba huenda kweli kuna mauza uza. Tulipewa kitanda ili mwanangu alale kwa ajiri ya kukicha aendelee na matibabu zaidi,nilikaa na mwanangu pale kitandani wakati huo Baba Grey aliniacha huku akisema kwamba anaenda kutoa taarifa na kufanya mchakato wa chakula asubuhi ili aniletee.Nilibaki na mwanangu mle wodi ya watoto akiwa amelazwa,nilipomnyonyesha alikuwa akinyonya kama kawaida.lakini ghafla alianza kukataa ziwa,hali ya kulia ilizidi,alianza kulia toka saa kumi na moja na nusu ya alfajiri,wauguzi walikuja tena kwa ajiri ya vipimo lakini majibu ni yale yale kwamb hamna ugonjwa,walimpa dawa za kutuliza maumivu lakini hazikuzaa matunda.Hatimae ilipofika mida ya saa moja mwanangu Grey aliaga dunia...... JE NINI KITAENDELEA Je ni nini kipo nyuma ya pazia katika kifo hicho cha Grey. Usikose sehemu inayofuata kesho muda na wakati kama huu. NILIPOTEZA WATOTO WANGU WANNE-(03) (Mkasa wa maisha ya ndoa ya Naomi) Tulipoishia .... Hatimae ilipofika mida ya saa moja mwanangu Grey aliaga dunia...... Sasa endelea... Kilio changu kizito kilitawala ndani ya chumba kile katika wodi ya watoto,uchungu mzito wa uzazi na kuondokewa na mtoto ulitawala ndani ya moyo wangu,mawazo yangu yote nilijua na kufahamu kwamba mwanangu hajafa katika kifo salama,bali ameondolewa Duniani kwa kulazimishwa.Wauguzi na akina mama wengine ambao walikuwa wanauguza watoto zao walijitahidi sana kunituliza lakini ndio kama walikuwa wanazidisha maumivu moyoni mwangu. Mwisho mume wangu alikuja akiwa ameleta chai,alipofika kwenye chumba ambacho ndicho tulikuwa tumelazwa na mwanangu moja kwa moja alijua tayari mtoto wetu hayupo duniani,kwani alinikuta bado nalia lia japo sio kama mwanzo kwasababu Wamama wenzangu walikuwa wakijitahidi sana kunipoza na kunituliza,hapakuwa na kingine zaidi ya mchukua mtoto wetu Grey ambae alikuwa tayari ni marehemu kwa ajiri ya kuanza safari ya kurudi nyumbani kuweka msiba,tulichukua gari huku mimi njia nzima nikienda nalia. Grey alikuwa bado mdogo,alikuwa na miezi sita hivyo hata mazishi yake yalipangwa yafanyike siku hiyo hiyo,kila mara nilikuwa nauchungulia mwili wa mwanangu,sikuamini kama kweli amenitoka,nilikuwa nimemzoea,alikuwa na afya nzuri na mwenye kuchangamka,lakini kilichokuja kunitisha zaidi Grey baada ya kufariki mwili wake uliirudia hali yake kwa maana ya kwamba ile hali ya mwili kuwa mwekundu utafikiri kalowekwa kwenye damu ilitoweka.Nilibaki najiuliza huu ni ushirikina wa namna gani,sikutaka kumtuhumu mama mkwe moja kwa moja kwasababu sikuwa na ushahidi wowote,ndoto pekee huwezi ukaitumia kumuhukumu mtu,japo ilikuwa ni ndoto ya mashaka. Hatimae saa kumi ya jioni ilifika muda ambao ulipangwa kwa ajiri ya mwanangu Grey kuzikwa,watu mbalimbali,majirani ndugu na marafiki walikusanyika kwa ajiri ya kutoa heshima zao za mwisho kwa kichanga changu kile,pale nilijifunza kitu kimoja kwamba siku zote ukiishi na watu vizuri basi utakuwa mtu wa watu,mwanangu alikuwa ni mdogo na asiejulikana sana mbele za watu,lakini watu waliohudhuria walikuwa ni wengi kiasi kwamba ni msiba wa mtu mzima na umaarufu wake. Basi jioni iliisha kwa kumpumzisha mwanangu katika nyumba yake ya milele. Hatimae maisha ya upweke bila kulea bila kunyonyesha yalirudi,tulikaa wiki moja na baada ya hapo ndugu jamaa na marafiki waliokuwa wamekuja kututembelea nao waliondoka na hatimae tulibaki tukiishi watu wanne kama mwanzo yaani mimi,mume wangu,mama mkwe wangu pamoja na mdada wa kazi aliekuwa akiitwa Rhoda. Sikujiskia tena kuendelea kukaa na pale pamoja na mama mkwe wangu,hatimae niliamua kuanza kumsumbua mume wangu kwamba inatupasa tuhame pale tukaanzishe maisha yetu,lakini bado juhudi za mume wangu kujaribu kukataa ziliendelea,na mimi pia neno kuhama nililigeuza wimbo wa taifa mdomoni mwangu kila mara nilipokaa nae.Hatimae siku moja aliniambia kwamba amenielewa na atakaa kuongea na mama yake ili tuweze kuondoka na kwenda kuanzisha maisha yetu. Moja kati ya siku nyingine ambayo sintakuja kuisahau katika maisha yangu ni siku ambayo nilikuwa natokea chumbani naelekea sebureni,nilichungulia kidogo nikaona mtu na mama yake wamekaa wanaongea,yaani mume wangu na mama yake,kwakweli nilinyata taratibu taratibu mpaka karibu na ukuta wa kukatizia kuingia sebureni ili niweze kusikia wanazungumza nini,nilitamani sana kusikia wanazungumzia swala la mimi na mume wangu kuhama,nilikuwakuta wameshaanza mazungumzo ambayo sikujua wanaanzia wapi lakini tumbo lilikuja kushtuka baada ya kumsikia mama mkwe wangu akitoa kauli kwa mume wangu na kumwambia"Sawa kama mnataka kuhama hapa nyinyi hameni lakini ukumbuke kwamba bado una deni kubwa sana kwangu,bado hujakamilisha kile kinachohitajika kwahiyo wewe hama lakini ukae unajua kwamba deni langu ni lazma ulipe"Tumbo lilinikata na kuanza kujiuliza ni aina gani ya deni ambalo mime wangu anadaiwa na mama yake,nilitamani niendelee kusikia mazungumzo zaidi lakini nilimuona mama mkwe wangu akinyanyuka na kushika njia ya mlango kuelekea nje. JE NINI KITAENDELEA Je ni aina gani ya deni ambalo anadaiwa John na mama yake..? Usikose sehemu inayofuata hapa hapa kesho panapo majaaliwa. ... Read More
CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SITA (06) ILIPOISHIA SEHEMU YA TANO: Siku ya pili, vicent alitoka mapema nyumbani, aliwahi shule kabla hata ya rafiki zake. Hii yote ni kutokana hata usingizi haukupatikana,kutokana na mawazo aliyo nayo. Alikuta baadhi ya wanafunzi wapo darasani, Alifika akakaa kwenye kiti na kufungua begi,kuchukua kitabu na kuanza kusoma. Ila hata sijui nini kilimtuma kutazama mbele maaana alijikuta anatoa macho. ENDELEA....... Alijikuta Anatoa macho, baada ya kuona,marafiki zake nao wamewahi shule. Aiseeee vicent alichekaaaa sana, mpka akajishika tumbo. "hadi nyinyi mmewahi leo aaah kweli mtihani siyo poa".aliongea vicent huku anawatazama kwa zamu. "mimi mwenyewe sijaamini nilivyo kuona ndo maana nikasimama mlangoni nihakikishe ni wewe au hahhhhhah".aliongea Richard huku anaelekea kule alipo vicent.ila cha kushangaza suma akuchangia neno zaidi ya kuachia tabasamu na kutembea kwenda walipokuwa wenzake. "aiseeee kama tuliambizana yani"aliongea tena vicent. Hapo suma ndo na yeye akanyanyua,mdomo wake na kuongea. " hivi unajua kwanini nimeshindwa kuongea chochote?,nikwasababu naona uchuro hapo nje nimekutana na rich, hapa nakuona wewe, nikawa najiuliza hivi hawa waliambizana nini mimi wamenichunia ila nimewabamba".aliongea suma,huvu anavuta kiti anakaa. "hii ili iweje sasa imetokea tu"alijibu richard. "sisi hatuwezi kukufanyia hivyo kwasababu sote ni wamoja". Alisema vicent, suma hakuwa na neno. " oyaa tusomeni basi kabla muda wa kwenda mstalini aujafika"aliongea tena vicent. "poa mwanangu umeongea point" alijibu suma.basi kikapita kimyaa,kila mtu alifanya yakeee kwa muda huo. ******* Mwezi ulipita,hatimae miezi, na si vicent, wala niram aliye kumbuka kama walishawahi kuonana. Basi ilikuwa weekend, moja walionekana marafiki, watatu wakiwa wamesimama stendi ya mabasi,si wengine bali ni vicent, richard na suma wakiwa wamevalia nguo za nyumbani.ilibaki kama wiki mbili wafanye mtihani. Ilionyesha kuwa walikuwa wamelewa kwenye maongezi sasa sijui vicent, walikuwa wanasubiri usafiri maana vicent hakuwa na gari siku hiyo. Mara gaflaa walishtushwa na sauti, nyororo iliotokea,barabarani. "vicentiiiiiiiiiiiii" ilikuwa sauti ya niramu, aliekuwa ndani ya range nyekundu, huku akiwa amependa,kupindukia wanasemaga kadamshi, ile mbayaaaa. Wote macho yalikuwa mbele,ila hakuna mtu alieshtuka kama vicent, maana akutegemea kuonana na binti yule ana muwaza siku zote. Na ilikuwa muda Awajaonana. Kiukweli vicent, moyo ulikuwa unampenda mbio vibaya.ila alijikaza, huku nyuma suma pamoja na richard, aisee!! Macho yaliwatoka maana walishindwa kuelewa, wanae muona machoni mwao, ni jini au malaika. Vicent alijikongoja mpaka kwenye dirisha la gari, na kumsababishia niram. " mambo niram siamini kama ni wewe, kumbe unani nakumbuka? ".alijikuta anaongea mfululizo vicent huku akiuliza, swali humohumo. "poa vicent, nakukumbuka sana vp leo huna usafiri? Maana naona kama mpo wenyewe mnasubiri usafiri? ".aliuliza niram,huku macho akiwaelekezea wakina rich. "aaah ndiyo tunamsubiri dereva tax mmoja hivi,katuambia hayupo mbali".alijibu vicent huko akiangalia huku na kule kama anaetafuta kitu. "haah kwani mnaelekea wapili niwape lifti?maana mimi naelekea mbezi"aliuliza niram. Vicent akapiga mahesabu ya haraka,alafu akaongea. "aaah! Wale wanarudi nyuma ila mimi naenda kunduchi" alijibu vicent. Ila wadau ngoja niwaambie kitu, vicent ameongopa, kwasababu wenzie wanaenda kawe sawa yeye anaenda kunduchi, ila njia ni ileile wameachwa wakina suma, yeye angeendelea mbele, ila aliamua kusema vile ili aweze, kutupa ndoano Kiulaini. Tuendelee, basi niram akamwambia "basi twende nikupe lifti waage wenzio".vicent akachomoka na kuwafata, wenzie alimkuta suma anashauku si mchezo. " vipi yule ndo yule demu uliesema? Na anaelekea wapi ili atupe lift basi kama vipi" alijikuta anaongea maneno,mfululizo na swali juu. "hamna aendi huko kaniambia nimsindikize kariakoo".aliongea vicent huku anageuka nyuma, akagongana macho na niram,wote wakatabasamu. "duuuh mwana kwahiyo umetuacha? ".aliongea richard huku anakazia macho kwenye gari. "aaah aina jinsi ila chukueni hii mpande tax".alisema vicent huku anazamisha mkono mfukoni na kutoa noti tatu za elfu kumi akamkabidhi suma. Suma alizichukua na kuzitia mfukoni. "oyaaa Usikose kutupigia ukifika home"alisema rich. Na suma akadakia. "ndiyo utupe data zote maana duuuh! Mpaka nakuonea wivu".vicent hakutia neno aliishia kutabasamu huku Anaendelea kutembea, basi aliingia ndani ya gari, huku ukimya mwingi ulitawala.vicent akaona avunje ukimya, "basi nilijua utanisahau kabisa".aliongea Vicent Huku ametoa tabasamu hafifu usoni mwake, Huku macho yanatazama mbele. "Ooooh!!Hapana siwezi kukusahau,mtu muhimu Kama wewe Kwa ule Msaada wako ".aliongea Niram,huku anamwangalia Vicent, macho yakakutana, wote wakatabasamu, Niram akageuka mbele na kuendelea, kuushika usukani akizidi kukanyaga mafuta. "hahhhhah!! Ni kweli niram lakini Siyo wote wanao kumbuka fadhila".aliongea Vicent ,Huku kimoyomoyo akiomba wasifike haraka. "haaahhh sawa bwana Wala ujaongopa, ".aliongea niram,huku akizidi kuuchapa mwendo, na bahati nzuri hakukuwa na foleni. "niram nikuombe kitu Kama hutojali? ".aliuliza Vicent Huku amemgeukia kabisa, aliongea Kwa sauti nzito, tens yakubembeleza. "usijali Kama kipo Ndani ya uwezo wangu ntakupa".alijibu niram. Vicent hakaona asizubae Sana, akasema alilokusudia."nilikuwa naomba unisaidie namba yako ya simu ili niwe nawasiliana nawe hata kukujulia Hali,maana tushakuwa marafiki".aliongea Vicent,kwa umakini wa hali ya juu ili asije kukosea step,akamkwaza Niram. " Ooooh!! Wala usijali Kwa hilo".alisema niram, huku anamtajia namba zake. Vicent aliziandika kwenye simu yake. " asante sana".alishukuru vicent. "asante nawe kwa kushukuru".alijibu niram, mara ikawa kama vituo viwili vicent ashuke. "sasa niram mie nashuka hapo kituo kinachofuata utaniacha hapo" aliongea vicent, lakini kama ungemuona moyoni mwake, alichukia kupita kiasi, alitamani wazunguke mpaka alfajiri. Duuuuh kweli mapenzi siyo poa wadau. "haaah ni hapo oky sawa"alijibu niram, na alipofika, akakanyaga break, na kusimamamisha gari. "oooh!!asante sana umenifaa mungu akufikishe salama".aliongea vicent huku anafungua mlango wa gari na kushuka. "haya asante ufike salama pia".alijibu niram, akawasha gari na kuishia, vicent alibaki anampungia mkono, mpaka alipo ishia. Kiukweli ile siku aliiona ya bahati sana kwake, hakika alikuwa na furaha mno. Alifika kwao. Akagonga geti likafunguliwa, alikuta mlinzi akamsalimu, na kuingia ndani hakumkuta yeyote ndani zaidi ya house girl. Alimsalimia akajitupa kitandaniii , pwaaaaaaah!! Aliangalia sana juu vicent, hakika kuwa na namba ya niram,kwake ilikuwa ni furaha tupu. ********* Vanessa alikuwa mezani wakipata chakula cha usiku, maana leo ilikuwa weekend kwahiyooo alikuwa mwenyewe jikoni, ila leo mawazo yalipungua kwani mawasiliano yalikuwa kama zamani na hadi asubuhi ya siku hiyo, vicent alimuaga kuwa atatoka na wakina richard. Mara ghafla alishtukia, akizibwa macho. "mmmh juliana nini bwana,ebu acha mzaha njoo ule"aliongea vanessa. " mmmh dada kwahiyo wewe mtu wako wa karibu ni Vanessa tu? ".aliuliza kwa manung'uniko Clara. Mdogo wake wa nne akitoka huyo ndo juliana, kumbuka wakiume ni wawili kwenye familia yao na ndio wakwanza na wapili. "hamna mamy wote nawapenda ila nilijua yeye, kaa chini ule mdogo wangu".aliongea Vanessa kwa sauti ya kubembeleza,huku akimvuta akae. Basi mambo yakaisha,walikula kwa furaha, wazazi na kaka zao hawakuwepo, walibaki wenyewe. ********* Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani Mara ghafla simu ikaanza kuita...... Itaendelea CHOICE OF MY HEART (chaguo la moyo wangu) SEHEMU YA SABA (07) ILIPOISHIA SEHEMU YA SITA: Niram alikuwa chumbani kwake akijisomea, wakati huo alikuwa ameshakula, alikuwa kitandani miguu kuegemeza ukutani, muda wote alikuwa mtu mwenye tabasamu usoni, kilicho mfurahisha akijulikani Mara ghafla simu ikaanza kuita. endelea........ Mara gafla akaona simu inaanza kuita. Niram akaangalia mpigaji, akaona namba ngeni. " mmh! Atakuwa Nani huyu?".alijiuliza niram, alitafakari Sana maana sikawaida kupigiwa na namba ngeni, baada ya kutafakari kwa muda.akaamua kupokea. "hellow".aliitika niram. "hallow Niram huko poa?, Vicent hapa". Ilisikika sauti upande wa pili."oooh! Vicent nashukuru mungu niko poa sijui wewe ulifika salama? ".alijibu niram nakupachika swali. "nilifika salama niram hofu ilikuwa kwako".alisema vicent. "namimi nashukuru mungu nimefika salama".alijibu niram kwa sauti nyororo kabisa. ****** Vanessa alikuwa ndani kwake akaona mbona muda unaenda sana,na ajaona msg wala simu kupigwa kutoka kwa vicent. Alikaa akasubiri na kusubiri weeeeh lakini ikawa kimya. "mmmh!! Ina maana itakuwa ajarudi bado huko alipoenda"alijisemea mwenyewe, akaona muda unaenda lakini simu aipigwi. "mmh ngoja nipige"aliamua apige yeye, akachukua simu yake na kuipiga. Jibu alilokutana nalo ni NAMBA UNAYOPIGA INATUMIKA KWA SASA.. "mmmh saa tano hii au ndo amerudi hivyo anaongea na wenzie kuwa julisha kuwa amerudi?".alijiuliza jibu akakubaliana kuwa anawasiliana na rafiki zake. ****** Huku vicent akiwa anaongea, akaona kama kuna mlio wa simu nyengine kuingia akaiangalia , alipoona mpigaji kuwa ni Vanessa akaendelea kuongea. Simu iliita mpka ikakata. Waliongea mengi na baadae niram akaaga kuwa anahitaji kupumzika. Basi waliagana na simu ikakatwa. Baada ya hapo alipiga simu kwa Vanessa,huku Akiwa ameshaupanga uongo wa kumwambia. "hellow baby mbona kimya, na napiga unatumika?".aliongea vanessa mara baada ya kupokea simu. "aaah amna nilikuwa naongea na mzee maana mchana,hakuwa na nafasi ndo kunitafuta sasahivi".alijibu vicent kwa ujasiri wa hali ya juu,bila kubabaisha maneno. "oooh kumbe haya niambie mizunguko ilikuwaje? ".Aliuliza Vanessa huku alibadili mikao ya kila aina Hapo kitandani. "ilikuwa poa sema nimechoka sana".alijibu vicent huku akijifanya anapiga mihayo. "oooh basi pumnzika baba angu tutaongea kesho".aliongea Vanessa kwasauti fulani hivi ya madeko. "sawa mama ntakuchek kesho ulale salama"alimaliza kuongea vicent akakata simu. Alienda moja kwa moja bafuni akaoga, maana choo kilikuwa ndani kwake humohumo. Alipomaliza alitoka sebleni muda ulikuwa umeenea sana ila alikuwa bado ajala, alikuta msichana ameshaenda kulala,aliwasha taa ya sebuleni akachukua sahani jikoni nakuenda kula chakula. Mara ghafla akasikia mlango unafunguliwa alikuwa mama yake, "yani wewe Bwana mi nilivyorudi nikaambiwa upo ndani nikajua ushakula".aliongea mama yake vicent,huku anavuta kiti pale sehemu ya kulia chakula akakaa. "hapana mama uwezi amini yani nilipitiwa na usingizi nikalala ndo nimeshtuka sasa hivi".aliongopa vicent, aisee huyu jamaa hatari."ooooh pole baba ni uchovu tu huo"aliongea kwa huruma mama yake. "asante mama".alijibu vicent huku anafakamia wali kwa maini. Basi waliongea mengi mama mtu alinyanyuka, na kuenda kulala. "ukimaliza usisahau kuzima taa baba".aliongea mama yake. "sawa mama ntaizima".vicent alikula akashushia juisi, akaelekea kwenye swichi akazima taa na kuenda kulala. ******* Pilikapilika zilikuwa zinaendelea, katika nyumba ya kina niram.ilikuwa Jumapili kulikuwa na ugeni mkubwa kwao, kuna ndugu zao walikuja.basi yalipikwa masontojoo siyo ya kawaida. Zilisagwa juisi za matunda basi ilikuwa tafrani. Niram akutulia alikuwa bize vibaya. "niram ebu kuongezeae chumvi kwenye biriani kule".ilikuwa sauti ya mama yake. "sawa mama".alijibu huku anaacha alichokuwa anafanya na kwenda kuweka chumvi kwenye chakula. Kila kitu kilikuwa sawa sasa niram alikuwa chumbani anajiandaa akaoge. ******** Suma alipoona ajapigiwa jana, akaona isiwe kesi ngoja amchek yeye maana umbea ulikuwa unamuwasha mtoto wa kiume huyu. Akukubali kitu kimpite hivihivi,yani alikuwa tofauti na richard mwenzie hakuwa mpenda kufuatilia yasiyo muhusu. Basi aliweka vocha akampigia "oyaaa mwanangu unayumba"haliongea suma ."hamna nilichoka sana yani uwezi amini ".alijibu vicent. "eeeh ilikuwaje jana na yule mtoto mzuri?".aliongea suma huku akitegesha masikio vizuri kupata udaku "hahhhhah suma eeh nna kazi kama unataka kuhusu hiyo stori ntakupigia baadae " "ok poa basi usisahau ".alijibu suma huku anakata simu. Ila suma akakumbuka kitu ayaaaaaah!! Daaah!!.Nimesahau kumuuliza Kitu, yeye na haraka zake mpaka nimesahau".aliongea suma huku anamlaumu vicent,kwa uamuzi wa kukata simu haraka. "anyway nitamchek baadae".aliongea suma, mara kisimu chake kikaanza kuita."duuuh huyu somoe ana mpya gani nae mi leo nnampango wa kuonana na hadijaa".alijiseme suma kimoyomoyo ,huku anaangalia ile simu bila kuipokea. Labda niwafafanulie vijitabia vya huyu ismail au kwa ufupi ndo unaweza kumuita suma. Yani suma yupo tofauti na wenzake, suma kwanza ni mwingi wa habari,anapenda kujua mambo ya watu ni mwongeaji mno kuliko wenzake.ajatulia hata kidogo isimpitie sketi mbele yake lazima amfate tu, ila richard na vicent wapo tofauti sana na yeye, richard ana mahusiano na binti mmoja anasoma, shule tofauti na yao. Na ni huyohuyo tu ndo yupo nae. Lakini suma weeeeeeh!! Mwiko mkubwa tena uchuro, kutulia na mwanamke mmoja. Basi baada ya simu kukata akaizima na kuendelea na mambo mengine. ******* Ilikuwa ni mida ya jioni. Wageni wameshaondoka, nyumbani kwa kina niram. Na mama yake kama unavyomjua mtu wa pilikapilika usiseme, alikuwa ameshaenda kuzurura muda mrefu. Aaaaah ahhh!!,sijui muhindi gani huyu mwenye tabia za Kiswahili.ok tuachane nae tuendelee. Basi niram alikuwa amekaa sebuleni peke yake, maana mdada wa kazi hupendelea kukaa ndani kwake kama kazi ameshazimaliza. Basi alijikuta mpweke sana na alijikuta anatamani, kuongea na vicent,ili apate kampani na kupoteza muda kidogo. Hata sijui ni kwanini alimuwaza vicent kuwa ndio mtu pekee wa kumtoa upweke. Hata mimi sijui,ila tutajua hivi karibuni. Basi aliingalia simu kwa muda nakujifikiria ampigie au atulie asimpigie. Basi nafsi ya niram ikawa inashindana,moja inamwambia piga nyengine, inamwambia usipige ila akiwa katika mgongano wa kutoa maamuzi nini afanye, gafla akaona kitu moyo ukapiga paaaaah!!! .alishindwa kuamini alichokiita. Itaendelea.... ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: