Home → simulizi
→ JAMANI BABA
Sehemu 13
ILIPOISHIA
Mwaija alitoka, akarudi nyumbani huku miguu
ikimtetemeka. Alijua mama yake atamla nyama
siku hiyo. Alipofika, alisukuma mlango akaingia
ndani. ..
“Ukitaka salama yako Mwaija uniambie ukweli ni
mwanaume gani uliyekuwa naye pale gesti ? .
Usinidanganye maana mimi nilimwona kwa
macho yangu ,” alisema mama Mwaija .
ENDELEA ...
Mwaija alianza kutetemeka kwa mbali akiamini
mama yake atamtoa sikio kama si kiganja cha
mkono.. .
“Mama nisamehe sana .”
“Nikusamehe kwa sababu gani?”
“Nisamehe tu mama, najua nimekukera sana.”
“Nimekuuliza ulikuwa na nani?”
“Na mwanaume mmoja hivi .. .”
“Anaitwa nani?”
“Abdallah .”
“Anaishi wapi ?”
“Kule chini.”
“Mlikutana wapi mpaka mkakubaliana kuingia
gesti?”
“Siku ile ulinituma mayai dukani ndiyo nikakutana
naye akaomba namba yangu.”
“Ahaa ! Sasa kumbe wewe umekuja Dar kwa ajili
ya kufanya uhuni siyo?”
“Hapana mama ... ”
“Huyo Abdallah kijana mzee ?”
“Yuko kama baba wa hapa ndani .”
“Kwa hiyo kumbe wewe siku moja utaweza hata
kunisaliti mimi mama yako ?”
“Hapana mama , siwezi kufanya hivyo . ”
“Unaweza ,” alisema mama Mwaija huku
akimsogelea mwanaye amchape makofi mawili
matatu kabla hajampa ushauri wa kimapenzi,
mara alisikika mtu akiingia akajua ni mumewe na
yeye hakutaka mume wake ajue kuhusu habari
ya yeye kumkuta Mwaija gesti ...
“Vipi mbona kama hamna amani humu ndani ?”
aliuliza Masilinde akijifanya hajui chochote na
sura za wote wawili zilikuwa zikionekana kuwa
na tafrani ...
“Si huyu Mwaija .”
“Amefanya nini ?”
“Nimekwenda msibani, nimerudi hajafanya kazi
yoyote ile .”
“Kwa nini , ye anasemaje ?”
“Hala na kusema ndiyo maana nikawa namsema
hapa.”
“Ah! We Mwaija , umeanza uvivu wako siyo?”
“Hapana baba , nilikuwa nahisi kama kichwa
kinaniuma ndiyo maana .”
“Umekunywa dawa ?”
“Sijanywa .”
“Sasa mama Mwaija kumbe mtoto anaumwa
kichwa angefanyaje kazi ?” aliuliza Masilinde...
“Mimi siamini ndiyo maana nimemgombeza .”
Kurudi kwa Masilinde kidogo kulituliza hali ya
hewa kiasi kwamba mama Mwaija alikwenda
kufanya kazi zake za ndani huku akimtaka binti
yake akanunue dawa anywe , apumzike. ..
“Nenda kanunue dawa sawa , unywe halafu
upumzike,” alisema...
“Sawa mama .”
***
Usiku, muda wa kulala ulifika, Mwaija alitangulia
kwenda chumbani lakini alivizia baba yake
amekaa sebuleni akapita hapo akiwa na kanga
moja tu. Safari hii alimtingishia makusudi
wowowo lake ili kumpa ujumbe kwamba wako
pamoja. ..
“Daaa ! Huyu mtoto ni wa kupangishiwa nyumba,
kweli tena. Haiwezekani akawa ananifanyia hivi
wakati anajua sina uwezo kwa usiku huu .”
Moyoni Masilinde aliamua kwamba , mkewe
atakapoingia kulala amzukie chumbani Mwaija .
Kwa hiyo aliendelea kuwepo sebuleni huku
mkewe naye akiendelea kuwepo jikoni lengo lake
mumewe akiingia chumbani tu aende chumbani
kwa Mwaija kumpa semina ya mapenzi mapema.
Kila alipotokea sebuleni, alimwona mumewe
amekaa macho pima ...
“Mh ! Huyu naye halali ?” alisema moyoni mama
Mwaija.
Masilinde naye, kila aliposimama na kuchungulia
jikoni, alimwona mkewe bado jikoni .. .
“Mh ! Huyu leo vipi kwani? Wenzie tunataka cha
kulalia yeye anaweka ukuta , ” alisema moyoni
Masilinde.
Saa saba kamili usiku , mama Mwaija na
mumewe walikuwa bado hawajaingia chumbani .
Lakini mwisho wa yote , mama Mwaija alishindwa
yeye, akaenda kulala...
“Mimi nakwenda kulala,” alisema mwanamke
huyo.. .
“Sa. ..aaawa ,” Masilinde naye alisema huku
akisinzia. ..
“Wewe bado kwani ?” aliulizwa Masilinde...
“Naangalia taarifa ya habari ya ITVT ,” alijibu
Masilinde bila kutambua kwamba muda ulikuwa
umekwenda sana .
“Taarifa ya habari saa hizi mume wangu ?”
“Kwani kuna nini ?”
“Ipo ?”
“Si ndiyo nasachisachi hapa, ” alijibu Masilinde
huku akiminyaminya rimoti.
Mama Mwaija alikwenda kulala, Mwaija kule
chumbani alikuwa hoi kwa usingizi, alikuwa
akikoroma lakini mlango wa chumba chake
ulikuwa wazi kwani wakati anakwenda kulala
aliamini Masilinde anaweza kuzama ndani kama
alivyowahi kufanya .
Masilinde alipoona ukimya ndani mwake ni
asilimia mia moja , alisimama sebuleni,
akajinyoosha kisha akaanza kutembea polepole
kuelekea chumbani kwa Mwaija. Njiani alikuwa
akijiambia...
“Nitalala mwepesi sana leo . Mtoto haishi kiu ,
ukimwangalia tu kiu inapanda , jamani! Kuna watu
ni wanawake wengine ni wana wa wake .”
Alishika kitasa, akakizungusha , mlango
ukafunguka, akaanza kuzama ndani taratibu .. .
“Nasikia akikoroma , amelala muda mrefu sana, ”
alisema moyoni Masilinde na kuingia chumbani
humo ...
“We baba Mwaija , huko nako kwa mtoto unaingia
kufanya nini mume wangu jamani?”itaendeleaa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: