Home → simulizi
→ JAMANI BABA
Sehemu 10
ILIPOISHIA
“Oooh ! Sasa?”
“Kuhusu kukutana nje ya hapa nyumbani?”
“Ee, ndiyo .”
“Nije wapi sasa ? Halafu leo naomba unikate kiu
kwelikweli mpenzi wangu.”
SEPA NAYO SASA . ..
“Hilo wala si ombi ni jukumu langu mimi kama
mpenzi wako , mimi kama mkata kiu wako na
mimi kama mumeo mtarajiwa, ” alisema
Masilinde huku mapigo ya moyo yakimwenda
kwa kasi ya ajabu kwani alikuwa bado hajaamini
kama amefika mahali binti mbichi kabisa ,
aliyeumbwa akaumbika kama Mwaija anafikia
hatua ya kuomba kukatwa kiu na yeye .
“Sasa sikia , ulizia watu Kwasandarusi ni wapi ,
watakuonesha mimi utanikuta nimekaa nje .”
“Sawa baby ,” alijibu bila woga Mwaija .Mwaija
alifunga nyumba huku sauti ya mama yake
ikisikika masikioni mwake . ..“ Mimi nakwenda
msibani tena, naomba usitoke nyumbani Mwaija .”
“Sawa mama .”
“We sema sawa mama halafu nirudi nikute
haupo.”
“Haitatokea mama. ”
“Sawa .”
“Aah! Sasa nikianza kuogopa maneno ya mama
nitalala na kiu yangu, ye’ ikifika usiku atakatwa
kiu, mimi je ?” alijipa moyo Mwaija huku akianza
safari ya kuelekea Kwasandarusi.. .
“Eti we mtoto, hujambo ?”
“Sijambo, shikamoo.”
“Marahabaa . Eti Kwasandarusi wapi ?”
“Pale penye mikokoteni nje ,” alijibu mtoto mmoja
aliyekuwa akicheza mtaani .
“Haya asante ee?” alishukuru Mwaija .
Mwaija alitembea kuelekea Kwasandarusi , kwa
mbali alimwona mama yake wa kambo amekaa
nje kwenye fomu ...
“Nikifika nitamwonesha maajabu ,
nitamkumbatia, ” alisema moyoni Mwaija .
“Kweli , alipofika, wakati Masilinde anasimama ili
kumkaribisha, Mwaija akamvaa na kumkumbatia
kisha mabusu mfululizo yakafuatia ...
“Mmm.. .mwaaa ... mmmmmwaaa ... mmmmwaaa!”
Masilinde tayari alishafika kitandani kihisia
japokuwa mabusu yale yaliwashangaza wengi
kwani waliowaona walibaini tofauti kubwa ya
umri kati ya Masilinde aliyeonekana kama ana
miaka 50 na Mwaija aliyeonekana ana miaka
kama 20 tu!
“Yule si kama mtoto wake?” alisema mzee
mmoja akiwa jirani na eneo la waliposimama
wawili hao .. .
“Yahe siku hizi ukifuata umri utaachwa! We
angalia wapi umelenga ,” alisema mwenzake
wakiwakodolea macho akina Masilinde.
“Nikwambie kitu my love,” alianza kusema
Mwaija.
“Nambie tu. ”“ Mama alinionya kuhusu kutoka
nyumbani.”
“Kwa hiyo?”
“Kwa hiyo twende haraka , kila kitu kiende
haraka ili niwahi kurudi kabla hajarudi. ”
“Sawa . Sasa unaona lile geti la mwisho pale?”
“Ndiyo.”
“Ile ni gesti , inaitwa Kichapo! Nenda pale ingia
mimi nakuja nikukute imesimama mapokezi ,
sawa?”
“Sawa ,” alisema Mwaija akiwa ameshaanza
kutembea kuelekea kwenye gesti hiyo ya
Kichapo.
“Hodi. ..hodi wenyewe,” Mwaija alibisha hodi
baada ya kuhisi ukimya umetawala .
“Karibu, ” sauti ya mwanaume ilisikika kutokea
ndani.
Mwaija alisimama mapokezi. ..
“Kuna mtu kaniambia nije nimsubiri hapa
mapokezi,” alisema Mwaija akiwa
anaogopaogopa...
“Nani, au Masilinde?” mtu wa mapokezi
alimuuliza.
“Mh ! Mi simjui jina . ”
“Sasa we utakujaje na mtu humjui jina ?”
“Hayakuhusu ,” alikuja juu Mwaija .. .
“Halafu pamoja na kuja kumsubiri mtu, we mtoto
umeumbika kweli ungekuwa na mtu kama mimi
ungefaidi. Ningekununulia simu ya maana, viatu
vizuri , yaani ungependa mwenyewe, ” alisema
yule mtu wa mapokezi.
“Sina shida navyo,” alijibu Mwaija , safari hii
akionesha hasira za waziwazi .
Mtu wa mapokezi aliposikia mlio wa viatu
alijikausha akijua aliyemtuma Mwaija kumsubiri
hapo anaingia ...
“Karibu sana. ”
“Asante . Kuna chumba ?”
“Kipo. ”
“Naomba. ”
Masilinde alichukua chumba akazama ndani na
Mwaija. ..
“Eti baby, we unaitwa nani?” aliuliza Mwaija mara
baada ya kukaa tu.
“Kwani vipi dear, hujui jina langu ?”
“Silijui . Nani ataniambia na kwa ajili ya nini ?”
Masilinde alipiga hesabu za haraka akagundua
kuwa, kuuliza kwa Mwaija kumekuja kwa
kuambiwa na mhudumu wa gesti hiyo. ..
“Huyu haiwezekani tumeingia chumbani kukaa
tu, anaulina naitwa nani? Lazima kaambiwa jina
langu na yule kijana. Na kama ni kweli kwa
kamwambia kwa sababu gani na ili iweje ?”
alijiuliza Masilinde.. .
“Mimi naitwa Mathayo, ” Masilinde alilitaja jina
lake la kwanza ambalo alijua muhudumu wa
gesti halijui.
“Ooo! Maana yule kaka kaniuliza umekuja
kumsubiri nani? Nikasema simjui jina , akasema
au Masilinde nini ? Sasa nikawa najiuliza
inawezekana ukawa unajulikana kwa jina hadi
gesti?”
“Simjui mimi na ni mara yangu ya kwanza
kuingia humu . Kumbe mzuri kidogo, si tutakuwa
tunakujakuja hapa mara mojamoja?” aliuliza
Masilinde...“ Wewe tu baby wangu,” alisema
Mwaija huku bila soni wala haya akianza kumvua
nguo Masilinde ili akatwe kiu . itaendeleaaa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: