Home → ushauri
→ Faida ya Vazi la Khanga Moko Katika Kudumisha Ndoa....

Mpenzi msomaji wangu, katika kuifanya ndoa iwe imara, niliwahi kuzungumzia mavazi sahihi ya mke kumvalia mumewe wakiwa chumbani. Lakini pia nikasema kwamba, kama kwenye nyumba mnaishi wawili tu, sioni shida mke kuvaa anavyotaka.
Pia nikasema kuwa, hakuna kitu kibaya kama mke wa mtu kuvaa nguo zisizo za heshima kwenye nyumba ya kupanga kiasi cha kuwatega wapangaji wa kiume.
Nilisema hayo baada ya kubaini kuwa, wapo wanawake ambao wameolewa lakini hawaoni hatari kuvaa kimitego bila kujali kuwa, kufanya hivyo ni kuiweka rehani ndoa.
Kuna hili vazi la kanga moja ambalo baadhi ya wanawake wamekuwa wakipenda kulivaa hasa maeneo ya mjini, bila kujali ni mchana au usiku, kwenye nyumba ya kupanga au binafsi.
Hapo ndipo penye shida na leo nimeona nilizungumzie ili wale wenye tabia hiyo waache mara moja kama wanazitaka ndoa zao.
Niseme tu kwamba, ukiwa na mumeo chumbani wala sioni tatizo kumvalia kanga moja, wakubwa wanajua faida ya vazi hili katika kuidumisha ndoa.
Pia ikiwa mnaishi peke yenu, siyo hatari hata kidogo kuvaa kanga moja, akazurura nayo sebuleni, jikoni na sehemu nyingine za nyumba yenu. Nasema hivyo kwa sababu, kuvaa minguo kibao mbele ya mumeo naweza kusema ni ushamba, labda kama kuna baridi sana, unaumwa au hauko vizuri na mwenza wako. Kinyume chake unaweza kuvaa vazi hilo na ikawa ni chachu ya mambo yetu yalee.
Shida inakuja pale utakapovaa vazi hilo kisha kutoka na kwenda bafuni kuoga, mbaya zaidi uwe umejaaliwa umbile tata kisha kwenye nyumba unayoishi kuna wanaume kibao. Unadhani katika mazingira hayo ndoa yako itakuwa salama kweli?
Unadhani wapangaji wenzako watakuheshimu? Sidhani kama itakuwa hivyo. Kwa kuvaa kanga moja ni wazi utapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakware na wengi watakuona unatangaza biashara. Mumeo naye hawezi kufurahia hilo, labda awe ni miongoni mwa wale malimbukeni.
Unachotakiwa kujua ni kwamba, kuvaa kanga moja hasa kwa mke wa mtu na kukatiza mbele za wanaume bila aibu ni kujichoresha. Utadharaulika na hata mumeo hawezi kupata heshima inayostahili kwani ataonekana kaoa mke mcharuko.
Labda niseme tu kwamba, unatakiwa kuwa makini sana na mavazi yako. Tambua uvaeje ukiwa na mumeo tu chumbani, uvaeje ukitoka kwenye geti la nyumba yenu na uvaeje ukiwa ndani ya nyumba huku ukiwa na familia.
Wapo wanaokosea, unakuta mke wa mtu ana watoto tena wakubwa tu lakini akiwa ndani kwake anaona sawa kuvaa kanga moja na akawa anazunguka huku na kule. Hii siyo sawa! Ni kweli wanao hawawezi kukutamani lakini unawafundisha nini kwa kuvaa hivyo?
Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapoingia kwenye ndoa unatakiwa kujitofautisha kabisa na wale ambao wako ‘singo’. Kanga moja ni vazi la kumvalia mumeo tena hasa chumbani.
Usijidhalilishe kuvaa nguo ambayo itakufanya utafsirike tofauti, udharaulike na kuonekana unatangaza biashara wak
Faida ya Vazi la Khanga Moko Katika Kudumisha Ndoa....  Mpenzi msomaji wangu, katika kuifanya ndoa iwe imara, niliwahi kuzungumzia mavazi sahihi ya mke kumvalia mumewe wakiwa chumbani. Lakini pia nikasema kwamba, kama kwenye nyumba mnaishi wawili tu, sioni shida mke kuvaa anavyotaka. Pia nikasema kuwa, hakuna kitu kibaya kama mke wa mtu kuvaa nguo zisizo za heshima kwenye nyumba ya kupanga kiasi cha kuwatega wapangaji wa kiume. Nilisema hayo baada ya kubaini kuwa, wapo wanawake ambao wameolewa lakini hawaoni hatari kuvaa kimitego bila kujali kuwa, kufanya hivyo ni kuiweka rehani ndoa. Kuna hili vazi la kanga moja ambalo baadhi ya wanawake wamekuwa wakipenda kulivaa hasa maeneo ya mjini, bila kujali ni mchana au usiku, kwenye nyumba ya kupanga au binafsi. Hapo ndipo penye shida na leo nimeona nilizungumzie ili wale wenye tabia hiyo waache mara moja kama wanazitaka ndoa zao. Niseme tu kwamba, ukiwa na mumeo chumbani wala sioni tatizo kumvalia kanga moja, wakubwa wanajua faida ya vazi hili katika kuidumisha ndoa. Pia ikiwa mnaishi peke yenu, siyo hatari hata kidogo kuvaa kanga moja, akazurura nayo sebuleni, jikoni na sehemu nyingine za nyumba yenu. Nasema hivyo kwa sababu, kuvaa minguo kibao mbele ya mumeo naweza kusema ni ushamba, labda kama kuna baridi sana, unaumwa au hauko vizuri na mwenza wako. Kinyume chake unaweza kuvaa vazi hilo na ikawa ni chachu ya mambo yetu yalee. Shida inakuja pale utakapovaa vazi hilo kisha kutoka na kwenda bafuni kuoga, mbaya zaidi uwe umejaaliwa umbile tata kisha kwenye nyumba unayoishi kuna wanaume kibao. Unadhani katika mazingira hayo ndoa yako itakuwa salama kweli? Unadhani wapangaji wenzako watakuheshimu? Sidhani kama itakuwa hivyo. Kwa kuvaa kanga moja ni wazi utapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakware na wengi watakuona unatangaza biashara. Mumeo naye hawezi kufurahia hilo, labda awe ni miongoni mwa wale malimbukeni. Unachotakiwa kujua ni kwamba, kuvaa kanga moja hasa kwa mke wa mtu na kukatiza mbele za wanaume bila aibu ni kujichoresha. Utadharaulika na hata mumeo hawezi kupata heshima inayostahili kwani ataonekana kaoa mke mcharuko. Labda niseme tu kwamba, unatakiwa kuwa makini sana na mavazi yako. Tambua uvaeje ukiwa na mumeo tu chumbani, uvaeje ukitoka kwenye geti la nyumba yenu na uvaeje ukiwa ndani ya nyumba huku ukiwa na familia. Wapo wanaokosea, unakuta mke wa mtu ana watoto tena wakubwa tu lakini akiwa ndani kwake anaona sawa kuvaa kanga moja na akawa anazunguka huku na kule. Hii siyo sawa! Ni kweli wanao hawawezi kukutamani lakini unawafundisha nini kwa kuvaa hivyo? Naomba nihitimishe kwa kusema kwamba, unapoingia kwenye ndoa unatakiwa kujitofautisha kabisa na wale ambao wako ‘singo’. Kanga moja ni vazi la kumvalia mumeo tena hasa chumbani. Usijidhalilishe kuvaa nguo ambayo itakufanya utafsirike tofauti, udharaulike na kuonekana unatangaza biashara wak
Artikel Terkait
SEHEMU 4 za Mwili Usizopaswa Kumshika Mkeo Nyakati Hizi 18+  Ingawa kuna mtazamo uliojengeka katika jamii kuwa ukishamuoa mwanamke na mkawa mwili mmoja basi una kila haki ya kumshika sehemu yoyote uipendayo hasa wakati unahitaji kufanya nae tendo la ndoa. Lakini utafiti na uzoefu uliokusanywa na wataalam wa mahusiano na ndoa waliofanya mahojiano na wanawake kama kuna sehemu wazisopenda kuguswa na waume zao na nyakati husika, umetoa picha na mtazamo ambao wanaume wanapaswa kuufahamu mapema kabla hawajaingia katika hatari ya kuwa kero au kuwakwaza wake zao. Kama tunavyofahamu, wanawake ni viumbe wenya mlango mmoja wa ziada wa fahamu kuwapita wanaume. Hii nitaizungumzia siku nyingine. Lakini mlango huu wa ziada ndio huwapa hisia ya ziada pamoja na kuwafanya kujali sana vitu ambavyo mwanaume hasa mwenye haja ya kufanya tendo anaweza asizingatie sana anataka kukidhi haja yake. Ukifuatilia sehemu hizi za mwili wa mwanamke nitakazozitaja na nyakati zake, utabaini kuwa ni rahisi sana kufahamu kwani mwanamke katika nyakati hizo anaweza kuonesha kusita sana wakati anataka kuguswa. 1. Chuchu wakati miili yao inaendelea na shughuli nyingine za ndani Idadi kubwa ya wanawake huwa hawapendi kuguswa na wanaume chuchu zao wakati wananyonyesha au wakati wako katika hedhi. Hiki ni kipindi ambacho kama mwanamke ananyonyesha na mwanaume anataka kumgusa sehemu hiyo basi maziwa yanaweza kutoka kwa kasi na kumfanya ajisikie hayuko ‘confortable’ kuendelea na zoezi la kushiriki tendo. 2. Kwapani wanapokuwa wanatoka jasho kabla ya kuoga Wanaume wengine huwa na hisia za matamanio zaidi wanapoyaona makwapa ya wake zao. Hii ni hali ya kisaikolojia inayojengeka kwa baadhi japo sio wengi. Kuna wanaume wakiona kwapa la mwanamke basi matamanio yao huongezeka mara dufu. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hujisikia vibaya na kukosa amani pale wanaume zao wanajaribu kuwashika kwapani wakati ambapo wametokwa jasho. 3. Sehemu za siri kabla ya kuoga Hili ni eneo ambalo wanawake wengi wameonesha kulalamikia waume zao. Kwa mazoea wanaume wengi huwa kama wanawabaka wake zao bila kufahamu, hasa pale wanapotoka safari zao wakiwa na matamanio. Lakini wanawake wengi wameeleza wazi kuwa hupoteza hali ya kuwa ‘comfortable’ pale wanapoguswa na wanaume zao sehemu za siri wakati bado hawajaoga. Wanaume wengi hujikuta wakishiriki tendo la ndoa na wake zao ghafla baada ya kukamilisha kazi kadhaa za ndani wakati wanawaangalia. Wanaume wanaweza kuwa wanafurahia zaidi tendo hilo lakini wanawake pamoja na kwamba hufurahia pia lakini mlango wao wa ziada wa fahamu huwafanya kukosa amani kwa kiasi fulani wakati wa tendo ukilinganisha na nyakati ambazo wanajiamini ni wasafi. 4. Nywele zao dakika chache baada ya kutoka saloon kujiremba Ingawa unaamini kuwa mkeo alienda saloon kujiremba kwa ajili ya kukuvutia wewe, usithubutu kutaka kuzivuruga nywele zake dakika chache baada ya kutoka kwa mtaalam wa kutengeneza nywele, hata kama pesa aliyotumia ulimpa wewe. Hiki ni kama kituko hivi, lakini ndio ukweli. Wanawake hutumia muda mrefu sana kwenye vibanda au saloon za gharama kwa ajili ya kujiremba ili waongeze mvuto. Lakini, hugeuka kuwa walinzi wa vichwa vyao angalau kwa saa kadhaa. Msifie uwezavyo, lakini nywele zake usizivuruge mapema mtaharibiana ‘mood’. Haya ni kati ya mambo machache ambayo wanaume huyaona madogo sana na kufuatilia yale wanayoamini ni makubwa zaidi. Lakini mambo haya ni kati ya machache yanayokwangua taratibu kuta za hisia za mwanamke kwa mmewe. ... Read More
MWANAUME ANAPOSEMA HATAKI KUKUOA: MWAMINI  Naandika hii makala kwa sababu nimekutana na maswali mengi ambayo yanaumiza wanawake wengi. Swali linakuwa hivi. Nimekuwa na huyu mwanaume kwa muda mrefu na tumekuwa tukishirikiana mambo mengi. Sijawahi kuwa na hisia kama nilizo nazo kwa mwanaume huyu kwa mtu yeyote. Na nilijua tutakuwa pamoja maisha yetu yote. Tatizo ni kwamba anasema hataki kunioa? Nitafanyaje ili aweze kujua kuwa nampenda na tunaendana vizuri pamoja na tunatakiwa tuoane? Wanaume wengi huwa wanaogopa kuweka ahadi kama hawana uhakika na upendo walio nao kwa mwanamke. Semeni ukweli wanaume. Je ameongelea kuhusu maisha ya baadae? Kuna mpango gani? Ni rahisi kubadilisha mwanaume? Unawezaje kumlazimisha akuoe? Kitu gani cha kufanya kama amesema hawezi kukuoa? Kama amesema hatakuoa, Mwamini . Elewa. Najua tayari jibu umepata kwenye maandiko yangu ya juu, lakini napenda kurudia, huwezi kumlazimisha mwanaume akuoe kama amesema hataki kukuoa. Hataweza. Sasa basi sisemi kama haiwezekani kweli. Kuna wanaume ambao husema hawatakuoa na hubadili mawazo yao na kuamua kuoa mwanamke ambaye alikuwa hapendi kumuoa. Lipo hilo. Mwanaume anayesema hatakuoa na wakati anaishi na wewe, mara nyingi anakupotezea muda na atakwenda kuoa mtu mwingine anayempenda kuliko wewe. Tuangalie kwa nini iko hivyo. Ina maana gani anapokuwa anaongea kuhusu kuchukia ndoa Aina ya mwanaume ambaye atakuambia hatakuoa ni yule ambaye anachukizwa na taasisi ya ndoa au sheria yake. Mwanaume huyo hafikirii kama wazo la kuoa ni zuri kwa kila mtu- anaona hata wanandoa ambao wako pamoja hawaonyeshi kama wana upendo wa kutosha, hawana upendo wa kweli ( anaweza kuwa haamini hata kama kuna upendo) Anafikiria hata kama ataona, mbona ndoa nyingi hazifiki mwisho, au mbona ugomvi ndani ya ndoa hauishi. Vyovyote vile , kwa sababu zozote zile, lakini mwanaume huyu anaonyesha kuchukia taasisi ya ndoa, na hataki kuingia huko, ndio maana hataki kuoa. Kama utasikia akisema hivyo mwamini. Haonyeshi kama atatafuta mwingine ambaye ataweza kubadili mawazo yake kuhusu kuoa.hata kama mnakaa pamoja na mnapendana sana , lakini hatafunga ndoa. Ina Maana Gani Anaposema Muda Wa kuoa Bado. Huyu ni aina nyingine tena.Anasema muda bado, anakuwa na sababu nyingi.Kama hali yake ya maisha haijakaa sawa, hajajenga nyumba, hana gari, na sababu kibao. Mwanaume huyu hana tatizo katika kuoa , Ila wakati bado , hataweza kuoa wakati unaotaka wewe, hata kwa sababu zipi hataweza. Unachotakiwa kufanya ni kumwamini anachokisema. Sababu zake hazina msingi. Kitu cha msingi ni Ukweli anaokuambia.Inaumiza lakini ndio ukweli.Inavunja moyo lakini ndio ukweli, Amini hilo na itaokoa muda wa kwako kusubiri.Na wakati huo huo utakuwa unafanya maamuzi ya kusubiri, kukubali jinsi ilivyo. Lakini kumbuka kuwa ndoa ni kitu cha muhimu sana. Wanaume wanaosema hawataoa huongea ukweli.Kama anakuambia hatakuoa Amini tu. Wanaume wanajua ni mwanamke wa aina gani atakayeishi nae maisha yake yote, uwe makini asije akawa anakutumia huku ana mipango yake .Yapo mambo wanaume huyapenda kwa mwanamke, vile vile yapo mambo ambayo wanawake wanapenda kwa mwanaume. Kama unaona unamlazimisha jambo fulani hataki , kuwa makini. ... Read More
JIFUNZE KUMTAMBUA MTU MWENYE MAPENZI YA DHATI NA WEWE: Unajua unaweza kuwa na mahusiano na mtu unayempenda sana ila yeye hakupendi kama vile umpendavyo lakini anashindwa kukwambia kuwa "sikupendi". Unawakati mzuri sana wa kumtambua mtu ambaye hakupendi na pia kumtambua anayekupenda. Vilevile kukubaliana na hali halisi. Watu wengi hawapendi kutambua kwamba mtu anayempenda yeye hampendi, kwasababu ni maumivu makubwa sana moyoni. Unapokuwa kwenye mahusiano na mtu huyo nae inamuwia vigumu kukwambia "sikupendi" hufanya hivi katika kuzihurumia hisia zako juu yake. MTU AMBAYE HAKUPENDI KWA DHATI: ==> Anapokuwa nawe inamuwia vigumu sana kukwambia neno NAKUPENDA mara kwa mara, utajikuta wewe ndio unakuwa mtumwa kwake kwa kumwambia nakupenda kila mara. Majibu yake baada ya neno hilo, mara nyingi atakwambia asante kwa kunipenda basi, na akikuhurumia sana atakwambia nakupenda pia ili kukuridhisha wewe na moyo wako. ==> Utajikuta una mawazo sana juu yake na kujiuliza "hivi kweli mtu huyu ananipenda?" Utajaribu kumuuliza, "je unanipenda?" Jibu lake kwanza litafikiriwa sana, sababu ya kufanya hivyo ni kwa vile anatambua kwamba hakupendi sasa kukwambia ukweli wa swali lako anahisi utaumia, kwahiyo baada ya swali hilo anaweza kukuuliza swali na wewe "kwani unaonaje?" kwavile unampenda sana utamjibu, "naona kuwa unanipenda" naye atakwambia "basi ndio hivyo". Mara nyingine baada ya wewe kumuuliza swali kuwa je anakupenda kweli, atakujibu "ukweli unaujua ila kwanini unapenda kuniuliza swali hilo kila mara?" kama umeshaingiza dosari juu ya upendo wake utajikuta unamuuliza "ukweli upi?" naye atakujibu "kuwa nakupenda", hapo utajikuta umepata furaha kugundua kuwa anakupenda kumbe mwenzio amekuhurumia tu. ==> Huwa hajali mambo yako unayomwambia, ukimueleza muda huu badae anajifanya kusahau ili tu akupotezee mueleleo. ==> Unapopanga kukutana nae huwa ni mtu asiyeishiwa na sababu za kushindwa kufika, huwa na aibu ya kukutambulisha kwa watu. Unaweza kufika nae mahali akakwambia kuwa "kuna watu wanafahamiana na mama/baba mahali hapa kwahiyo tusiongozane karibu", hapo anaweza yeye akatangulia mbele au kukuacha wewe utangulie. ==> Hufanya tabasamu la kuigiza au kicheko cha kejeli ili wewe uridhike kwamba anafurahishwa na uwepo wako kwake. ===> Wakati mwingine inampasa mtu kujitambua na kumpa uhuru huyo umpendaye aweze kuamua mwenyewe labda kuendelea na wewe au kumfata anayempenda yeye. Cha muhimu ni kuwa using'ang'anie mahusiano ambayo yanayoumiza moyo kwani yanaweza pasua moyo wako kwa mawazo. MTU ANAYEKUPENDA KWA DHATI: ==> Hachoki kukwambia NAKUPENDA, kwani anajisikia raha sana pale atamkapo neno hilo juu yako kwahiyo unaweza ukawa kama wimbo wake kwako. ==> Anajivunia kuwa na wewe na atapenda kukupa sifa nzuri kila mara, yani Hachoki kukusifia. Atakushauri pale unapokosea ili uwe katika njia nzuri. Unaponuna atajua cha kufanya ili wewe ufurahi na kurudi kwenye hali ya kawaida. ==> Hachoki kukuombea mema na kukutakia mafanikio. ==> Atapenda kukueleza ukweli kila mara ili uweze kujenga uaminifu na imani juu yake. ==> Wewe utakuwa ni mtu muhimu sana katika maisha yake, atakuthamini na kukujali. Tatizo lako litakuwa sawa na tatizo lake, atakupa ushauri bila kuchoka. ==> Kabla ya kumuuliza swali kuwa "je unanipenda?" atakuwa ameshakujibu tena kwa hisia nzito kuwa "nakupenda sana mpenzi wangu". ==> Hatokuonea aibu kukutambulisha kwa watu kuwa wewe ndiye mpenzi wake, kwakuwa wewe ndiye furaha yake. ====> Thamani yako ni kubwa sana kwake, anakuona mpya kila siku na hachoki kuvutiwa na wewe. Anakupenda kwa kumaanisha na si kukupenda kimazoea tu. Neno NAKUPENDA litamtoka moyoni na ataridhihirisha kwa kinywa chake. Mtambue mtu huyu kuwa anakupenda kwa dhati. NB: Hakuna aliyekamilika, kila mtu ana kasoro na mapungufu yake. Si vyema kutumia mapungufu ya mwenzio kama fimbo katika mapenzi, cha muhimu ni kumuelimisha na kumuelekeza ili muweze kwenda sambamba. Nadhani baadhi ya maswali ya wadau yatakuwa yamejibiwa na hiyo mada. Kama kuna nyongeza au swali lolote kuhusiana na hiyo mada tuambiane hapa na kupatiana majibu hapa hapa wadau. ... Read More
*SIMULIZI DARASA* *STORY FUPI* *USIMDHARAU USIYEMJUA* Msichana mmoja alikuwa amempenda kijana mmoja mtanashati na mcha Mungu.. Malengo yao ilikua waje kuoana baada ya muda. Kijana huyu alijitoa sana kwa binti huyu hadi wenzie wakamuona mjinga, lakini ukweli ni kuwa alimpenda msichana yule kwa dhati. Alimtafutia kazi alipomaliza chuo, alimshauri kuhusu mipango ya maisha na alikua akimuombea kila alipopata nafasiya kuomba. Siku moja binti alikua anasherehekea siku yake ya kuzaliwa…hivyo akaalika marafiki zake, na watu wengine muhimu akiwemo mpenzi wake. Wageni wote walifika kwa wakati isipokua yule kijana alichelewa kidogo… Hivyo msichana akatumia muda ule ambao mpenzi wake hajafika kuwaeleza wageni namna yule kijana alivyokua wa muhimu kwake.. Akamsifia sana, akasema atamvalisha pete ya uchumba soon, na akasema siku hiyo ya birthday yake anategemea zawadi kubwa sana kutoka kwa huyo mpenzi wa nafsi yake. Baadae kijana akaingia na kuketi high table.. Muda wa zawadi ulipofika watu wakamtunza binti zawadi mbalimbali na kijana akawa wa mwisho… Hivyo wageni wote wakawa na hamu ya kutaka kujua zawadi aliyoleta hasa baada ya yule msichana kumsifia sana. Kijana akaamka na kutoa mfuko.. kila mtu akataka kujua kilichokua ndani ya mfuko..mara kijana akafungua mfuko na kutoa mkate..!! Lahaula… watu wote wakastaajabu.. mkate??? Lakini kabla hajasema lolote kuhusu ule mkate, yule msichana akaanza kulia.. akapandwa hasira kwa kuwa mpenzi wake amemuaibisha..!! Akiwa analia kwa kwikwi, akamkwida shati na kumvua tai yake, akamwagia juisi, kisha akauchukua ule mkate na kuutupa.!! Maskini..yule kijana akaukimbilia ule mkate na kuuokota.. Kisha akarudi high table na kusema “baby nakushukuru kwa yote..Huenda umenidharau kwa kuwa nimekuletea zawadi hii ndogo kwenye siku yako muhimu kama hii. Lakini kama ungetambua thamani ya zawadi hii, usingefanya haya..” Kisha akafungua ule mkate na kutoa vitu viwili alivyoficha ndani ya mkate.. Kwanza akatoa ufunguo wa gari, ambalo alikuwa amemnunulia mpenzi wake na alitaka amkabidhi siku hiyo ya birthday. Kisha akatoa pete ya uchumba na kusema “Nilimuomba Mungu anipe mwanamke atakayenipenda katika hali yoyote. Nilipanga leo nikuvalishe pete hii ili kuelekea ndoto yetu ya ndoa.. ..Lakini kwa kuwa uliangalia nje, uliona mkate, badala ya pete hii ya thamani iliyokua ndani.. Naamini mwanamke niliyemuomba kwa Mungu bado sijampata.. Nashukuru kwa yote uliyonifanyia, nimekusamehe, nawe naomba unisamehe kama nimekukwaza..” Kisha akachukua mkate wake, huyoo akaondoka. Msichana akaomba msamaha lakini ilikua too late.. MORAL OF THE STORY..! Usidharau kitu/mtu kwa kumtizama nje.. Mungu huangalia thamani ya kitu ndani lakini Wanadamu huangalia nje.. Thamani ya kitu/mtu ipo ndani na si rahisi kuonekana.. Usiwe mwepesi wa kuhukumu kwa kutizama umbo la nje.. Wale wanaokudharau leo na kukuona mkate, ipo siku watagundua haukua mkate wa kawaida… kuna vingi vya thamani ndani yako. Wote wanaokudharau leo ipo siku watakusalimia kwa heshima..!! 🌹TUELIMISHANE MEMA🌹 Subra ndio inayotakiwa katika maisha. *akida* ... Read More
Utajuaje Kama Mahusiano Uliyonayo Yatadumu.  Dalili 8 zitakuonyesha kama upo kwenye mahusiano ya kudumu au hapana. Afya. Wote tunafikiria kuhusu hili. hasa kwa kadri tunavyoendelea kukua , tunatembelea madaktari, tunakula vizuri wakati mwingine. Tunatafuta dalili na wakati mwingine matokeo yake yanatuambia kuwa hali zetu sio nzuri. Lakini tunapofikiria afya, tunafanya hivyo katika miili yetu tu. mara nyingi tunasahau kufikiria kuhusu afya ya mahusiano na mapenzi. Tunaangalia zaidi afya ya mwili katika maisha ,lakini kuwa na afya nzuri katika mahusiano ni vitu vinavyoungana. Kwa kurahisisha , mahusiano mabaya hayadumu. au ingawa yanaweza kukaa kwa muda fulani.Na kama yakidumu , atakuwepo mtu wa kuumia. Lakini ni nini hasa afya ya mahusiano? Tutajuaje kama mahusiano yetu yatadumu? Utajuaje kama uko na mtu sio sahihi, mtu ambaye mtaishia kwenye kona fulani tu? Hakuna kipimo halisi cha kujua. Hakuna kipima joto kinaweza kupima kiasi cha muda wa mahusiano kuwa ni ya moto au baridi. Kwa bahati kuna hizi dalili 8 ambazo zinaweza kukusaidia kujua afya iliopo kwenye mahusiano yako. 1.Mchumba wako atakuwa na imani na wewe , na wewe utakuwa na imani naye.  Hataongea kwa ajili yake bali ataongea kwa ajili yenu wote. atakukumbusha pale unapokuwa umesahau au unapokuwa na mashaka kwa jinsi ulivyo. Ana maono ya wazi ya muhimu kwako. atalea hali hio na utaiona. Vilevile na upande wako utakuwa kama yeye. hutamsema vibaya kwa marafiki, hutalalamika kitu bali utaongea mbele yake. Utamwamini kuwa yuko kamili , mtu anayeweza kutatua matatizo na kusimama kwa miguu yake. Hata kama haujamsaidia kitu. 2.Unamwamini. Unamwamini katika ukweli wake wote. ahadi zake ni za kweli. utamkubali alivyo. Anahusika katika majukumu yake. 3.Unakubali mambo yake yaliopita na yeye anakubali ya kwako. Jinsi alivyokuwa, alikuwa na wanawake wangapi, wanaume wangapi. hutajali. utamkubali alivyo ili mkue pamoja. hutafikiria kitu chochote kilichopita, bali utakuwa na hamu ya kutaka kujua jinsi gani huyo mtu alivyo. Mahusiano yako yatakuwa yamekusanya, Msamaha na kuachilia yaliopita. 4.Unashukuru kwa vitu vizuri mlivyonavyo Unakubaliana na vitu vidogo vidogo anavyovifanya kwako. unakuwa na matumaini, husubiri kupata kazi, kwa ajili ya mshahara, kwa ajili ya mambo mengine. unashukuru kwa kile mlichonacho sasa na mwenza wako. Mnafuraha wakati huu. hana mchezo wa kijinga. anatengeneza pesa ya kutosha. anafanya kitu akipendacho. Utakuwa unalenga safari sio mwisho wa ndoa, mtoto, sherehe, vitu vinatokea kwa kawaida. 5.Mawasiliano ni ya wazi na ya kueleweka kwa kila mmoja. Hakuna wa kusubiri ni nani atamtafuta mwenzake. kila mtu anakuwa na jukumu la kufanya hivyo. Na kama itatokea mmoja hakuhusika , hakuna lawama, kwa kuwa mnaelewa . utavaa moyo wake. hutahangaika kuyatawala mahusiano kwa sababu hamfanyi mchezo wa kuigiza. 6.Maisha yenu ya sex yataendelea kuwa mazuri na ya kupendeza. Kwa sababu ya urafiki ambao mnao, maisha yenu ya mahusiano yatakuwa rahisi na ya kimapenzi. Ya ukaribu zaidi. sex itakuwa sio kipaumbele chenu bali ni matokeo ya upendo mlionao. mahitaji yenu ya kimwili yatatosheka kwa pamoja. 7.Utamuheshimu na yeye Atakuheshimu wewe. Kila mtu anaheshimu mipaka ya mwenzake na mnaweza kuhimizana katika kutimiza malengo yenu. kama unapenda kucheza , atakuhimiza kufanya hivyo. hutahitaji kukamilisha hisia zako zote. atakuwa na mahusiano mazuri na watu wengine pia. Ni mtu muhimu kwako. anakufanya ujisikie vizuri. 8.Malengo yenu yanafanana. Hutajaribu kumbadilisha. au kujaribu kuomba kuishi na yeye. hutahitaji awe mtu wa kutengeneza kitu chako. ni mtu ambaye ulimtaka awe wako. thamani yake ni muhimu katika maswali hata. Unataka watoto? Unapenda kusafiri? Una hamu ya kupata uzoefu fulani? unakubaliana katika mambo ya pesa? Una furaha unapokuwa naye? Unataka kuishi naye na kuwa naye chumba kimoja? Afya ya mahusiano yako ni muhimu katika maisha ya ndoa utakayoingia. Lakini hakuna kipimo cha kupimia uzima huo. Ni wewe tu na mwenza wako mnajua kama mahusiano yatadumu au yataishia kwenye kona. yatakuwa na matunda au hapana. Mttajua kama ni mazuri au sio. hizo dalili nane zikusaidie kufahamu kama ni ya afya au sio, yatadumu au hayatadumu. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: