Home → ushauri
→ NIKIFANYA MAPENZI NACHUBUKA NA KUTOKWA NA DAMU NYINGI KAMA HEDHI

Mimi ni mwanamke wa miaka 32. Ninatatizo ambalo nimeshindwa kupata tiba yake hata bada ya kwenda kumuona Daktari. Mimi na mpenzi wangu tumekuwa pamoja kwa muda wa miaka miwili.
Mwanzo tulikuwa tukitumia Condom tunapofanya mapenzi lakini mimi nilikuwa napatwa na maumivu makali sana na wakati mwingine kutokwa na damu kama vile niko kwenye siku zangu za Hedhi.
Baada ya muda nikaja kugundua kuwa nilikuwa nachanika kidogo kidogo ukeni, basi tukakubaliana kuacha kutumia Condoms. Pamoja na kuacha kutumia Condom bado hali hiyo iliendelea kila ninapofanya mapenzi na Boyfriend wangu.
Nilipokwenda kwa Daktari, nilishauriwa niwe nabana sehemu zangu za siri kama vile navuta pumzi, nikajaribu kufuata ushauri huo lakini wapi! Sasa nimeanza kupatwa na mawazo je kuchanika huku chini kunaweza kunisababishia Cancer, labda sitoweza kushika mimba na kuendelea kuchanika zaidi na zaidi.
Naomba ushauri wenu.
USHAURI
1.Inawezekana mwanamume wako hauju kula, anatumia mwili wako kupiga punyeto(MASTABATORY SEX)!!! Jaribu kuongea naye ajifunze kula kutokana na mahitaji ya mwili wako!
2. Yawezekana hupati maandalizi ya kutosha na kusababisha uke wako kuwa mkavu, kiasi kwamba mume wako au mpenzi wako huyo anapofanya mapenzi na wewe anatumia nguvu nyingi kuingiza uume na kusabisha michubuko, na damu kutoka,
3.Jaribu kuhakikisha kuwa unakuwa katika mudi ya kufanya ngono ili uke uwe na maji maji ya kutosha ikishindakana jaribu kutumumia vilainishi ya uke then jaribu uone kama utatokwa damu
4.Pia yawezekana cervix yako iko jirani kiasi kwamba mumeo anapofanya mapenzi na wewe anaigusa na kusababisha damu kuvuja na machubuko kwenye cervix.
Nenda kwa daktari bingwa wa magojwa ya wanawake na sio alie kushauri uwe unabana uke huyo si dhani kama ana elimu husika katika suala hilo.
NIKIFANYA MAPENZI NACHUBUKA NA KUTOKWA NA DAMU NYINGI KAMA HEDHI  Mimi ni mwanamke wa miaka 32. Ninatatizo ambalo nimeshindwa kupata tiba yake hata bada ya kwenda kumuona Daktari. Mimi na mpenzi wangu tumekuwa pamoja kwa muda wa miaka miwili. Mwanzo tulikuwa tukitumia Condom tunapofanya mapenzi lakini mimi nilikuwa napatwa na maumivu makali sana na wakati mwingine kutokwa na damu kama vile niko kwenye siku zangu za Hedhi. Baada ya muda nikaja kugundua kuwa nilikuwa nachanika kidogo kidogo ukeni, basi tukakubaliana kuacha kutumia Condoms. Pamoja na kuacha kutumia Condom bado hali hiyo iliendelea kila ninapofanya mapenzi na Boyfriend wangu. Nilipokwenda kwa Daktari, nilishauriwa niwe nabana sehemu zangu za siri kama vile navuta pumzi, nikajaribu kufuata ushauri huo lakini wapi! Sasa nimeanza kupatwa na mawazo je kuchanika huku chini kunaweza kunisababishia Cancer, labda sitoweza kushika mimba na kuendelea kuchanika zaidi na zaidi. Naomba ushauri wenu. USHAURI 1.Inawezekana mwanamume wako hauju kula, anatumia mwili wako kupiga punyeto(MASTABATORY SEX)!!! Jaribu kuongea naye ajifunze kula kutokana na mahitaji ya mwili wako! 2. Yawezekana hupati maandalizi ya kutosha na kusababisha uke wako kuwa mkavu, kiasi kwamba mume wako au mpenzi wako huyo anapofanya mapenzi na wewe anatumia nguvu nyingi kuingiza uume na kusabisha michubuko, na damu kutoka, 3.Jaribu kuhakikisha kuwa unakuwa katika mudi ya kufanya ngono ili uke uwe na maji maji ya kutosha ikishindakana jaribu kutumumia vilainishi ya uke then jaribu uone kama utatokwa damu 4.Pia yawezekana cervix yako iko jirani kiasi kwamba mumeo anapofanya mapenzi na wewe anaigusa na kusababisha damu kuvuja na machubuko kwenye cervix. Nenda kwa daktari bingwa wa magojwa ya wanawake na sio alie kushauri uwe unabana uke huyo si dhani kama ana elimu husika katika suala hilo.
Artikel Terkait
NI JINSI GANI UNAMWOMBA MPENZIO MSAMAHA, JE NI KWA KUMPA ZAWADI? Msamaha una nafasi kubwa sana katika mapenzi. Hamna mtu aliyemkamilifu ndiyo maana neno samahani lipo. Ila neno hili linaweza kutumika sahihi au isiwe sahihi. Hivyo ni vizuri ukawa makini katika matumizi ya neno hili. Kuna baadhi ya watu hawawezi kabisa kutamka hilo neno na badala yake hutumia maneno yafuatayo (mbadala) kama ; yaishe,basi samahani,umeshinda,sorry(kama njia yakupunguza makali na wakati lugha iliyokua ikitumika ni kiswahili). Jinsi yakutumia samahani kiusahihi Unapotoa samahani kutoka katika kilindi cha moyo wako ina maana sana zaidi ya chochote. Samahani itumike tu pale unapotenda kosa moja kwa mara ya kwanza, hapo ni rahisi kusamehewa na kuaminiwa zaidi.Heshima, pendo na mapenzi yatakuwa kama awali na utaheshimika nakuonekana unajali. Hakikisha hauombi samahani zaidi ya mara moja kwa kosa moja ndo mana wanasema, “kosa sio kosa ila ukirudia kosa ndio kosa’’. Kama ulikua haufahamu ni vizuri ujifunze na ikiwezekana rudisha kumbukumbu zako katika matukio yanayohitaji msamaha kwenda kwa mpenzi wako na ulinganishe na hatua ulizozifanya. Kiri kosa ndiyo msamaha wako uweze kukubalika.Usiombe msamaha huku unasema lakinii…… ila……. Siamini kama haya yangetoa……… aina hizi za midokezo inapotumika katika kuomba msamaha ujue unataka kuonesha ulichokifanya sio kosa… Its simple, admit your mistake for the heartest forgiviness .Utapelekea upande wa pili (uliokosewa kukuamini tena na ni rahisi kusamehe na kusahau) tofauti na kuwa na maneno meeengi yakujitetea ilihali umetenda kosa. Sasa nije kwenye suala la zawadi, Jamani zawadi isiwe ndiyo silaha ya kudai msamaha. Zawadi inatumika wakati wowote kuimarisha mapenzi kwa kuonesha unamjali mwenzi wako nakumfanya ahisi faraja wakati wote na uwepo wake katika maisha yako. Epuka tabia ya kutoa sana zawadi wakati unamplease mpenzi wako.Kwa wakati mwingine utamjengea fikra za kosa pindi tu unapomletea zawadi. Hivyo asiifurahie ile zawadi na badala yake atakua na shauku kufahamu msamaha wa siku hiyo ni wa kitu gani au umetenda kosa gani tena. Wakati mwingine zawadi inapotumika katika kuomba msamaha itakua ni kama KUMBUKUMBU YA KOSA ulilomfanyia mwenzi wako, hivyo kumfanya akumbuke mara kwa mara kosa ulilolifanya. Kuwa makini sana katika njia za kuomba msamaha. Njia nzuri ya kuomba msamaha na ukubaliwe kwa upesi Kubali kosa pale ambapo umetenda,(note; Usikiri kosa kwa sababu tu unampenda na hutaki kumpoteza ,au hutaki malumbano. Ukifanya hivo ndo unaweza haribu uhusiano wako kabisa) Badili mazingira ya maongezi yaani tofauti na eneo la nyumbani/mlilozoea kukaa Omba msamaha wakati hasira zimepungua na ukiwa sio mlevi (hasa kwa wale wenye hasira au wanywaji wa pombe) Usilazimishe kusamehewa ,yaani mwenzako anapokua haridhii tumia njia nyingine mfano kumshirikisha mtu wenu wa karibu saana (kwa wote wawili) ila hapa uwe makini kwa sababu sio wote wanapenda siri zao za uhusiano kujulikana na wengine.Hapa itategemea na jinsi mlivyo Anayeomba msamaha ahakikishe sio mtu wa kukumbuka makosa ya mwenzie yaliyofanyika kipindi cha nyuma.Hapa na maanisha wale wenye tabia yakusamehe wenzao ila niwakukumbuka, endapo atakosewa kwa kitu kingine hata kwa bahati mbaya.Mfano akikosewa huwa ni mtu wakusema; ''hiyo ni kawaida yako'' that means anashikilia vitu moyoni.Itamuwia vigumu mwenzako kukubalia msamaha kwa urahisi, kutokana na tabia yakumshikilia bango kwa kumkumbusha yaliyopita endapo yeye atakukosea. Ni vizuri kujitahidi katika kufanya mambo mazuri kwenye uhusiano wako.Usitegemee zawadi kuwa ni kitu kizuri katika kuomba msamaha. Timiza malengo yako,jiheshimu,kuwa mwaminifu na kumthamini mwenzio na kumpenda kwa dhati. Bila kusahau kusikilizana na kufanya maamuzi kwa pamoja. ... Read More
ULISHAWAHI KUKUTANA NA MTU MWENYE UPENDO WA KWELI??? Ipo siku utakutana na mtu tofauti na ulivyozoea kuona au kusikia. Haitakuwa kwa sababu ya tabasamu lao au ucheshi wao au kwa jinsi ya kuongea kwao au kusema majina yao. Ni kwa sababu ya njia itakayo kufanya wewe ujisikie tofauti. hutaogopa kupenda na kupendwa. Siku moja utakutana na Upendo utakaoufurahia. Hutaweza kufikiria mara mbili. Hutaweza kuwa na wasiwasi kwamba anakupenda au hakupendi. ‘Utafahamu tu. Kwa mtu huyu hutaweza kuficha tabia yako. hutaficha madhaifu yako na usumbufu wako. hutakuwa na mawazo ya itakuwaje kama ata kupandia kichwani. hutakuwa na maswali ya kujua muhimu wake na hutakuwa na labda. Wakati ukikutana na mtu huyu hutaingiwa na woga. hutaweza kufikiri fikiri kitu chochote. hutaweza kufikiria upendo wake kwako. Na wakati anaposema hawezi kwenda mahali , utafahamu kuwa ni kweli. Wakati huo hutasikia kukosa kitu ndani ya moyo wako, hutasikia upweke, hutaweza kusikia chochote kinyume na upendo uliopo. Ipo siku , mtu fulani atabadilisha maisha yako. kwa sababu atakuonyesha upendo wa kweli ni upi na maana ya upendo ni nini, unaonekanaje. Atakuonyesha kuwa upendo hauna mwisho. na hutamkimbia , na hutaweza kutaka faida zaidi. hutapigwa na wala kupata maumivu yasio na msingi. Ipo siku Hutaogopa kupata maumivu. Hutaogopa kuacha tena. kwa kupoteza kipande cha moyo wako na roho yako. hutaogopa tena kutoa na kutoa upendo wako . Siku moja utapumua kwa urahisi kwa kufahamu kuwa huyo mtu hataondoka . Utapumua vizuri kwa kujua kwamba upendo huo utadumu. Huyo mtu hatakutelekeza na wala hataweza kukukimbia. Utafahamu toka moyoni mwako kwamba upendo huo hautakuumiza. Utaweza kuishi, kucheka, kulia na kupumua kwa urahisi ukiwa pembeni ya mtu huyo. Utajifahamu na kujiona vizuri. Utaweza kumuonyesha makovu, na vidonda ulivyonavyo na kwa kuwa vimepona. Utaweza kumuonyesha mtu huyo moyo wako wote kwa kujua kuwa hawezi kukuacha. Ipo siku utajikuta unaamka mikononi mwake, ukiwa karibu yake kwa upendo , katika maisha yako. hutakuwa na wasiwasi . hutaogopa. hutasikia uzito wa kupumua tena. Utahisi upendo ndani yako. mwisho utagundua Upendo halisi. Washirikishe wengi. ... Read More
Hatua 5 za kuzungumza na mpenzi wako aliyekasirika Kwenye mapenzi kuna nyakati za kutofautiana, kukasirishana. Katika hali ya kawada kipindi hiki huwa ni za hatari kwa sababu husababisha nyufa kubwa za uhusiano na kulifanya penzi kukosa ladha. Sote tunajua, watu hupigana, huachana, hujeruhiana, hutukanana, hudhalilishana wakiwa na hasira. Hata hivyo si wote wanaojua wafanye nini wanapojikuta wameingia kwenye hatua hiyo mbaya. Msomaji wangu, hebu jaribu kukumbuka ugomvi mmoja uliotokea kati yako na mpenzi wako na ikiwezekana jikumbushe mlivyoanza! Utabaini kuwa mlianza kama utani na mkajikuta mmefura kwa hasira, mkatwangana makonde, mkatamkiana maneno makali ya kuudhi na pengine mkaamua kuachana. Yote hii ni kwa sababu mlikosa elimu ya mazungumzo. Ingekuwa mmoja wenu hasa yule aliyekuwa wa pili kukasirika anafahamu hatua za kuzungumza na mtu aliyekasirika angechukua jukumu la kutuliza machafuko na kuleta amani kwenye mapenzi. Tazama hatua tano za kuzungumza na mpenzi aliyekasirika. MPUNGUZE MHEMKO Hasira hujaza kifua, huathiri mzunguko wa damu na ufahamu. Mtu aliyekasirika huwa vigumu kwake kusikiliza au kutazama mambo kwa jicho la tatu. Mwenye hasira huwa hafikirii matokea yajayo badala yake hutazama zaidi tukio na jinsi ya kupata ushindi iwe kwa maneno au kwa mapambano. Katika hali ya namna hiyo, mtu mwingine akija na busara za kutaka kumgeuza haraka haraka hawezi kumuelewa. Muhimu hapo ni kuacha kumwadama, kujibizana naye, kumshawishi asikilize badala yake mpe nafasi ya kusema atakavyo, abwate ajuavyo huku wewe ukimuitikia na kumkubalia lawama zake. “Basi mpenzi mwenye makosa ni mimi.” Kauli za aina hii zitampunguza hasira kwani atajiona msindi. MSOME SAIKOLOJIA YAKE Kwa kuwa unamfahamu mpenzi wako kwa kina itakuwa rahisi kwako kumtambua kuwa amepunguza hasira na kurudi katika hali yake ya kawaida. Ukisha fahamu hilo chukua jukumu la kumsoma kisaikojia ili kujua kama yuko kwenye hali nzuri ya kusikiliza yale uliyotaka kumwambia wakati alipokuwa na hasira. Zoezi hili linaweza kuchukua saa kadhaa na wakati mwingine hata siku mbili. Lengo ni nini? Ni kupata matokeo sahihi ya kuondoa chuki za mwenza wako na kumfundisha madhara ya kukasirika kwenye uhusiano wenu wa kimapenzi. “J, nakupenda sana, lakini juzi uliniumiza, uliniambia mimi malaya kwa kosa ambalo sikufanya?” Bila shaka muda huo atakusikiliza zaidi kuliko ungebishana naye alipokuwa na hasira. MRUHUSU AKUJIBU Pamoja na kumsoma kisaikojia na kumwambia kinagaubaga makosa yake, usimzuie kujitetea, mpe nafasi ya kuzungumzia kilichomkasirisha. “Unaona bado unanitukana, sasa naamini siku ile ulikuwa umedhamilia.” Usisiseme hivyo, mwache ajibu hoja hata kama atakuwa anakukandamiza na kuzidi kujijengea ushindi. Mvumilie aoshe ubongo wake. EPUKA MARUMBANO Kama nilivyosema kwenye hapo juu, wapenzi wengine huwa wagumu kuelewa, ni watu wa kuficha udhaifu wao na kutopenda kuonekana wamekosea. Watu wa namna hii unapowarejeshea mazungumzo wanaweza kujikuta wanahamaki tena. “Kwa hiyo ulikuwa unasemaje…nilifanya ndiyo,… wewe unaamuaje?” Mkifika kwenye alama hiyo usikubali kurumabana naye mwache aseme halafu wewe ingia kwenye hatua ya tano. MUOMBE MSAMAHA Hata kama atakuwa yeye ndiye mwenye makosa na amekataa kukiri, usijali, chukua jukumu la kumuomba msamaha na kueleza tena nia yako ya kumazungumzo ilikuwa ni kuelewana si kugombana. Kumbuka hata kama amekiri kosa, bado unatakiwa kumuomba radhi kwa kurejea yaliyopita. “Mpenzi inawezekana nikawa nimekuudhi kwa niliyosema, nakuomba sana tusameheane.” Bila shaka kwa haya machache msomaji wangu utakuwa umejifunza na kuchukua hatua za kuzuia migogoro mikubwa inayotokana na hasira za mpenzi wako. Leo niishie hapa, nikushukuu kwa kunisoma. Kaa mkao wa kura, kile kitabu bora cha mapenzi nchini TITANIC, TOLEO LA NNE, kitakuwa mtaani hivi karibuni. Usikose nakala yako. ... Read More
Mimba kuharibika na Sababu zake  Tatizo la kuharibika kwa mimba limekuwa tatizo kubwa, na limekuwa likiwatesa wengi, kama we ni mongoni mwa watu hao nakusihi usome makala haya ili kuepukana na matatizo haya. Somo hili ni mahususi kwa sababu waawake wengi wamekuwa wakaiharibikiwa na mimba bila kujua sababu. Na zifuatazo ndizo sababu za kuharibika kwa mimba. 1.Mama anapokuwa na matatizo uvimbe (fibroid), huweza kuwa na madhara na kusababisha mimba kuharibika mara kwa mara. 2. Uzito mkubwa (unene) Nayo huweza kuchangia tatizo hilo kinachohitajika ni kuwa na uzito unastahili kulingana na mhusika mwenyewe. Pia inasadikika kuwa uwepo wa manyama uzembe tumboni ni chanzo pia kwa kuharibika kwa mimba kwani, mtoto hukaa kwa shinda. 3. Historia ya kuharibika mimba mara kwa mara Mama aliepata kukumbwa na hali hii ya kuharibika kwa mimba 'miscarriage' zaidi ya mara 2 anauwezo mkubwa wa kuharibika kwa mimba yake kila anaposhika. 4. Utoaji mimba Mwanamke anapotoa mimba mara kwa mara kizazi huweza kuchangia kizazi chake kushindwa kuhimili kubeba mimba zinazokuja mbeleni kwa miezi tisa, hivyo epuka kutoa mimba. 5. Matumizi ya Pombe,Sigara Wanawake wanaotumia vilevi hivyo nao huwa katika hatari ya k?kumbwa na tatizo hili, hivyo ni vyema kuepuka matumizi ya vitu hivyo. 6. Magonjwa sugu Mama anapokuwa anazongwa na magonjwa sugu kama kisukari , moyo nk huweza kuwa chanzo cha tatizo hili pia. ... Read More
MWANAUME ANAPOSEMA HATAKI KUKUOA: MWAMINI  Naandika hii makala kwa sababu nimekutana na maswali mengi ambayo yanaumiza wanawake wengi. Swali linakuwa hivi. Nimekuwa na huyu mwanaume kwa muda mrefu na tumekuwa tukishirikiana mambo mengi. Sijawahi kuwa na hisia kama nilizo nazo kwa mwanaume huyu kwa mtu yeyote. Na nilijua tutakuwa pamoja maisha yetu yote. Tatizo ni kwamba anasema hataki kunioa? Nitafanyaje ili aweze kujua kuwa nampenda na tunaendana vizuri pamoja na tunatakiwa tuoane? Wanaume wengi huwa wanaogopa kuweka ahadi kama hawana uhakika na upendo walio nao kwa mwanamke. Semeni ukweli wanaume. Je ameongelea kuhusu maisha ya baadae? Kuna mpango gani? Ni rahisi kubadilisha mwanaume? Unawezaje kumlazimisha akuoe? Kitu gani cha kufanya kama amesema hawezi kukuoa? Kama amesema hatakuoa, Mwamini . Elewa. Najua tayari jibu umepata kwenye maandiko yangu ya juu, lakini napenda kurudia, huwezi kumlazimisha mwanaume akuoe kama amesema hataki kukuoa. Hataweza. Sasa basi sisemi kama haiwezekani kweli. Kuna wanaume ambao husema hawatakuoa na hubadili mawazo yao na kuamua kuoa mwanamke ambaye alikuwa hapendi kumuoa. Lipo hilo. Mwanaume anayesema hatakuoa na wakati anaishi na wewe, mara nyingi anakupotezea muda na atakwenda kuoa mtu mwingine anayempenda kuliko wewe. Tuangalie kwa nini iko hivyo. Ina maana gani anapokuwa anaongea kuhusu kuchukia ndoa Aina ya mwanaume ambaye atakuambia hatakuoa ni yule ambaye anachukizwa na taasisi ya ndoa au sheria yake. Mwanaume huyo hafikirii kama wazo la kuoa ni zuri kwa kila mtu- anaona hata wanandoa ambao wako pamoja hawaonyeshi kama wana upendo wa kutosha, hawana upendo wa kweli ( anaweza kuwa haamini hata kama kuna upendo) Anafikiria hata kama ataona, mbona ndoa nyingi hazifiki mwisho, au mbona ugomvi ndani ya ndoa hauishi. Vyovyote vile , kwa sababu zozote zile, lakini mwanaume huyu anaonyesha kuchukia taasisi ya ndoa, na hataki kuingia huko, ndio maana hataki kuoa. Kama utasikia akisema hivyo mwamini. Haonyeshi kama atatafuta mwingine ambaye ataweza kubadili mawazo yake kuhusu kuoa.hata kama mnakaa pamoja na mnapendana sana , lakini hatafunga ndoa. Ina Maana Gani Anaposema Muda Wa kuoa Bado. Huyu ni aina nyingine tena.Anasema muda bado, anakuwa na sababu nyingi.Kama hali yake ya maisha haijakaa sawa, hajajenga nyumba, hana gari, na sababu kibao. Mwanaume huyu hana tatizo katika kuoa , Ila wakati bado , hataweza kuoa wakati unaotaka wewe, hata kwa sababu zipi hataweza. Unachotakiwa kufanya ni kumwamini anachokisema. Sababu zake hazina msingi. Kitu cha msingi ni Ukweli anaokuambia.Inaumiza lakini ndio ukweli.Inavunja moyo lakini ndio ukweli, Amini hilo na itaokoa muda wa kwako kusubiri.Na wakati huo huo utakuwa unafanya maamuzi ya kusubiri, kukubali jinsi ilivyo. Lakini kumbuka kuwa ndoa ni kitu cha muhimu sana. Wanaume wanaosema hawataoa huongea ukweli.Kama anakuambia hatakuoa Amini tu. Wanaume wanajua ni mwanamke wa aina gani atakayeishi nae maisha yake yote, uwe makini asije akawa anakutumia huku ana mipango yake .Yapo mambo wanaume huyapenda kwa mwanamke, vile vile yapo mambo ambayo wanawake wanapenda kwa mwanaume. Kama unaona unamlazimisha jambo fulani hataki , kuwa makini. ... Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments: