*💘💘SASA NIMEFAHAMU*💘💘 *💘MANENO YATOAYO MACHOZI💘* 💘"Mama anaongea na mwanawe na kumpa *Usia"* 💘Mwanangu mpenzi: 💘Kuna siku utanikuta uzee, sitafanya mambo yangu kwa akili; 💘Yakitokea hayo nakuomba tafadhali nipe muda na *subira ili unifahamu !!* 💘Pale mikono yangu itakapotetemeka, na chakula changu kikaangukia kifuani pangu, na nisipoweza kuvaa nguo zangu; 💘Jifunge na *kusubiria, na kumbuka miaka imepita nilikuwa nakufunza ambayo leo siwezi kuyafanya!!* 💘Ikiwa leo si maridadi na sina harufu nzuri; usinilaumu.. kumbuka udogoni kwako nikijitahidi sana nikufanye uwe maridadi mwenye harufu nzuri!! 💘Usinicheke utakapoona ujinga wangu na kutofahamu mambo ya wakati wenu huu, lakini wewe kuwa jicho na akili yangu ili niyapate niliyoyakosa!! 💘Mimi ndiye niliyekufunza adabu na mimi ndiye niliyekufunza vipi ukabiliane na maisha; *💘Sasa inakuaje leo unanifundisha yaliyo wajibu na yasiyo wajibu?* 💘Usinichoke kwa udhaifu wa kumbukumbu yangu, na uchelewaji wa *maneno yangu na fikra zangu* wakati ninapozungumza nawe, kwani furaha yangu wakati huu ni kuwa pamoja nawe tu!! *💘Wewe nisaidie tu kupata ninachohitaji;* kwani bado najua ninachotaka!! 💘Miguu yangu ikikataa kunipeleka sehemu ninayotaka kwenda; *nihurumie* na kumbuka kwamba mimi nilikushika sana mkono ili uweze kutembea!! *💘Usione haya abadan kunishika mkono wangu leo;* kwani kesho utatafuta wa kukushika mkono wako!! 💘Katika umri wangu huu; elewa kuwa mimi siyaelekei maisha kama wewe; lakini kwa ufupi nangojea mauti; kwa hiyo *kuwa pamoja nami wala usinitupe!!* 💘Pale ukikumbuka makosa yangu; jua kuwa mimi nilikuwa sitaki ila maslahi yako!! 💘Na mimi napenda sana unayonifanyia hivi sasa kwa *kunisamehe matelezo yangu na kusitiri aibu zangu..* *💘💘NAWE MOLA AKUGHUFIRIE NA AKUSTIRI!!💘💘* 💘Bado *vicheko na tabasamu zako vinanipa furaha* kama ulivyokuwa mdogo... kwa hiyo usininyime suhuba yako!! 💘Nilikuwa nawe wakati *unazaliwa;* kuwa nami pale *nitakapofariki!!* *💘Maneno bora yaliyopitia katika maisha yangu, na hata nikiyarudia mara elfu moja sichoki kuyasoma..* "Mola wangu warehemu wazazi wangu kama walivyonilea nilipokuwa mdogo"(Rabbi Arhamu humma kama rabayan swakhira) *💘MANENO MAZITO KWA MWENYE AKILI💘* *💘💘SASA NIMEFAHAMU💘💘*

at 9:35 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top