❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤ KAMA SIO FURAHA NA AMANI HAPAKUWA NA SABABU YA MAHUSIANO! Kuwa na mahusiano na mtu mwenye nia na wewe, Namuongelea mtu ambaye analo pendo lililojaa huruma juu yako, Mtu ambaye anajuwa kusoma PAJI YA USO WAKO kama hauko Sawa atapambana kukurejesha katika Furaha, Simzungumzii mtu ambaye anakupenda kwa sababu fulani, Kwamba wewe ni mzuri wa mwili na sura nzuri ama ni vile ambavyo unamuwezea kwa kitanda, Namaanisha mtu ambaye anataka kujuwa kila taarifa muhimu kuhusu wewe, Mtu anayetaka kusoma kila neno ulilomuandikia, Mtu anayetaka kusikia kila neno la wimbo uupendao ili aweze kupokea ujumbe kwa hisia... Mtu anaetaka kutafuta kila kovu mwilini mwako na kujuwa kila moja limetokana na nini! Ukimpata MTU MWENYE HISIA NAWE huyo ndiye atatamani mchangie kila ambacho kinaleta furaha lakini dhiki ikija awe nawe kwa huruma, Mtafute MTU anaependa kujifunza kila haja yako ya moyo na kuzishiriki kwa wakati... Haina maana kuwa katika mahusiano ambayo muda mwingi unautumia KUTATUA MIGOGORO! Itengeneze njia yako kuelekea katika MAHUSIANO rafiki ambayo yatakutenga na UPWEKE ili ufurahie maana ya MAHUSIANO. * ❤❤❤❤❤❤❤❤❤❤ Dr Luv🤓🤓🤓

at 9:31 AM

Bagikan ke

Lintaskan

0 comments:

Copyright © 2025 Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top