UNAFIKIRI NI KWA NINI WANAWAKE WANAHANGAIKA NA KUYALILIA MAPENZI KULIKO CHOCHOTE? Wacha niongee nawe... Unajuwa mwanamke alivyoumbwa Sio mwepesi wa kukubali jambo hata kama alilitarajia lakini Bado atakuwa na maswali mengi kichwani, Na imezoeleka wanaume kucheza na akili za wanawake wakati akiwa anamhitaji, Mwanaume akimpata mwanamke huiondoa ile kasi alokuwa nayo na kumuacha mwanamke akiwa ndo amejiachia kuwa nae, Kadri siku ziendavyo ndivyo mwanamke humpenda mwanaume wakati huo mwanaume aliisha maliza kazi yake na hilo ndilo linatesa mahusiano mengi, Kwa wanaume ambao huziheshimu hisia za Mwanamke na kuzisikiliza mahala zilipo mara nyingi humpa ZAWADI ya ajabu ambayo kwa mwanamke huyo ni hazina ya furaha yake, Mwanaume akituliza akili na kutozichanganya hisia zake hata zikasimama kwa mwanamke mmoja kwa hakika hufikisha burudani nzuri kwa mwanamke wake! Mwanamke yeyote hupenda apewe nafasi ya kujieleza Kadri anavyojisikia ili aweze kupata haja ya moyo wake, Mwanamke akisikilizwa na kupewa uhuru Mara nyingi hawanaga papara maana wameumbiwa kitu ambacho nakifananisha na YAI Kwani hawapendi kutingishwa kwa aina yoyote ile, Ni kosa kubwa kwa mwanaume kutojuwa hisia za Mwanamke wake na hilo ndilo linawasababisha wanawake watubebeshe lawama sisi wanaume, WANAWAKE kwa uhalisia wana aibu ni wachache wanaoweza kuzielezea hisia zao, Ni jukumu la mwanaume kuhakikisha anatafuta mahala zimejificha hisia za Mwanamke wake kwa kufanya hivyo UTAPONYA MAHUSIANO AMA NDOA YAKO Kwani hakuna mwanamke anapenda kutanga na njia ila wewe unaweza kumpa sababu hiyo Kwani VIGEZO NA MASHARTI HUZINGATII.

at 10:56 AM

Bagikan ke

0 comments:

Copyright © Braytonofficiallove
Designed by Siyamdezign | Edited By braytonofficiallove
braytonofficiallove | braytonofficiallove | braytonofficiallove
Powered By Blogger
Back to Top